DadasAfya

DadasAfya Tunaelimisha, tunahamasisha, na kusaidia wanawake katika afya ya mwili na akili.
� +255 787 677 932

Happy Birthday Dr Ahmad Badowe. Tunakutakia afya njema na mafanikio zaidi katika uongozi wako wa Dadas Afya, ukiendelea ...
09/03/2026

Happy Birthday Dr Ahmad Badowe. Tunakutakia afya njema na mafanikio zaidi katika uongozi wako wa Dadas Afya, ukiendelea kusimamia lengo la kuelimisha jamii, kuboresha ufahamu wa masuala ya afya, utatuzi wa changamoto na kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi za afya kwa wote.

Leo tunaadhimisha nguvu, hekima na mchango mkubwa wa wanawake katika jamii.Dadas Afya tunawatakia wanawake wote Heri ya ...
08/03/2026

Leo tunaadhimisha nguvu, hekima na mchango mkubwa wa wanawake katika jamii.

Dadas Afya tunawatakia wanawake wote Heri ya Siku ya Wanawake Duniani.

Mwanamke mwenye afya ni msingi wa familia imara na jamii yenye maendeleo. Endelea kujali afya yako, kuelimika na kuwa chachu ya mabadiliko chanya.

Happy International Women’s Day.

21/02/2026

BABA ANA MCHANGO MKUBWA KULIKO UNAVYODHANI

Afya ya uzazi sio jukumu la mama pekee.
Kitaalamu, mwanaume huchangia takribani nusu ya mafanikio ya ujauzito.

Mbegu dhaifu zinaweza kusababisha:
▪️ Mimba kuchelewa
▪️ Mimba kutoka mapema
▪️ Kiinitete kutokua vizuri

Lakini pia mazingira ya kihisia ndani ya ndoa yanaathiri homoni za mama.
Msongo, migogoro na kutokuwepo kwa ushirikiano hupunguza nafasi ya ujauzito kushika vizuri.

K**a unapanga kuitwa baba au mama, anza kuandaa mwili na tabia zako mapema.

👉 Afya ya uzazi ni jukumu la wawili
👉 Jiandae kabla ya mimba, sio baadae

📍 Tunapatikana Zanzibar na tunahudumia Tanzania nzima
📞 0787 677 932
📌





13/02/2026

FAIDA KWA MWANAMKE 🔥 | MSAADA KWA MWANAUME

K**a una tatizo la:
▪️ Uchafu ukeni unaorudia
▪️ Harufu mbaya
▪️ Ukavu au maumivu wakati wa tendo
▪️ Kushindwa kupata ujauzito

Usidhani ni tatizo la mwanamke peke yake.

⚠️ Ukweli ni huu:
Afya ya uzazi ni ya pande zote mbili.
Bila kutibu chanzo kwa usahihi, maambukizi hurudiana mara kwa mara.

✅ Mwanamke anapopona vizuri:
– Mahusiano yanaimarika
– Maumivu yanaisha
– Uwezekano wa kupata mimba huongezeka

✅ Mwanaume pia hulindwa dhidi ya maambukizi ya kurudia.

👉 Endelea kutazama / Swipe ujifunze zaidi
👉 Suluhisho lipo hapa

📍 Tunapatikana Zanzibar na tunahudumia Tanzania nzima
📞 0787 677 932
📌





Pata Mimba Ndani ya Siku 30–90 🤰🏽Ndiyo, inawezekana — k**a chanzo cha tatizo kimeeleweka mapema.Wanawake wengi wanachele...
02/02/2026

Pata Mimba Ndani ya Siku 30–90 🤰🏽
Ndiyo, inawezekana — k**a chanzo cha tatizo kimeeleweka mapema.

Wanawake wengi wanachelewa kupata ujauzito si kwa sababu hawawezi, bali kwa sababu👇
▪️ PID isiyotibiwa sahihi
▪️ Uchafu ukeni unaojirudia
▪️ Harufu mbaya ukeni
▪️ Fangasi kuharibu mfumo wa uzazi mara kwa mara

❌ Kumeza dawa nyingi bila uchunguzi hakuponyi tatizo
✅ Uchunguzi sahihi + tiba sahihi huleta matokeo

👉 Swipe ujifunze zaidi ➡️➡️
👉 Suluhisho lipo hapa

📍 Tunapatikana Zanzibar na tunahudumia Tanzania nzima
📞 Wasiliana nasi: 0787 677 932
📌





Mtu anaweza kuona uchafu ukeni akadhani ni UTI, akameza dawa nyingi bila mafanikio.Ukweli ni huu👇🔹 UTI huathiri njia ya ...
02/02/2026

Mtu anaweza kuona uchafu ukeni akadhani ni UTI, akameza dawa nyingi bila mafanikio.
Ukweli ni huu👇

🔹 UTI huathiri njia ya mkojo, si uke.
🔹 Mwanamke anaweza kuwa na UTI bila uchafu wowote.
🔹 Damu ya hedhi na damu baada ya kujifungua hutoka ukeni, si kwenye njia ya mkojo.

❌ Si kila uchafu ni UTI
❌ Si kila maumivu yanahitaji dawa za mkojo

👉 Elimu sahihi ndiyo tiba ya kwanza.
👉 Pima, elewa chanzo, ndipo utibiwe sahihi.

👉 Swipe ujifunze zaidi ➡️➡️

📍 Tunapatikana Zanzibar na mikoa yote ya Tanzania
📞 Piga: 0787 677 932
📌





01/02/2026

Umakini unaohitajika ili kujifungua salama 🤍

Kujifungua salama huanza kabla hata ya kupata ujauzito, si wakati wa uchungu pekee.
Ni mchakato unaohitaji umakini katika hatua zote:

Kabla ya kupata ujauzito:
• kupima afya ya uzazi mapema
• kurekebisha lishe na mtindo wa maisha
• kutibu maambukizi kabla ya mimba

Wakati wa ujauzito:
• kuhudhuria kliniki mara kwa mara
• kufuatilia ukuaji wa mtoto
• kuzingatia lishe, mapumziko na ushauri wa kitabibu
• kutambua dalili hatarishi mapema

Wakati wa kujifungua:
• kufuata maelekezo ya mtaalamu
• kupumua na kusukuma kwa usahihi
• kupata uangalizi wa karibu hadi baada ya kujifungua

📌 Kujifungua salama = maandalizi sahihi + elimu + ufuatiliaji wa kitabibu katika kila hatua.

👉 Swipe ujifunze kwa kina.

📍 Tunapatikana Zanzibar na mikoa yote ya Tanzania
📞 0787677932
📲

Wakati wa kujifungua, msamba (mfuko wa uzazi) hulazimika kuchanika au kuraruka ili mtoto apite.Hili ni tukio la kitabibu...
31/01/2026

Wakati wa kujifungua, msamba (mfuko wa uzazi) hulazimika kuchanika au kuraruka ili mtoto apite.
Hili ni tukio la kitabibu linalotokea kulingana na: • ukubwa wa mtoto
• kasi ya uchungu
• uimara wa tishu za uzazi
• namna mama anavyosukuma

📌 Ndiyo maana uangalizi wa kitaalamu wakati wa kujifungua ni muhimu ili kupunguza madhara na kusaidia uponaji salama baada ya kujifungua.

👉 Elimu sahihi humsaidia mama kujiandaa kimwili na kisaikolojia.

📍 Tunapatikana Zanzibar na mikoa yote ya Tanzania
📞 0787677932
📲

Baada ya mama kujifungua, wakati mwingine hupata maumivu makali ya tumbo yanayoambatana na mfinyo wa mfuko wa uzazi (ute...
30/01/2026

Baada ya mama kujifungua, wakati mwingine hupata maumivu makali ya tumbo yanayoambatana na mfinyo wa mfuko wa uzazi (uterus contraction).
Hii ni ishara ya mwili kurudi katika hali yake ya kawaida, si ugonjwa.

📌 Maumivu haya hutokea zaidi kwa waliowahi kujifungua mara zaidi ya moja.
📌 Ni sehemu ya mchakato wa kawaida wa uzazi, lakini yakizidi au kuambatana na dalili nyingine, usisite kushauriana na mtaalamu.

👉 Elimu sahihi huondoa hofu zisizo za lazima.

📍 Tunapatikana Zanzibar na mikoa yote ya Tanzania
📞 0787677932
📲

Kitambi kinaweza kuathiri uwezo wa kupata ujauzito — lakini si kwa kila mwanamke.Kwa wengine huathiri upandikizaji wa mi...
28/01/2026

Kitambi kinaweza kuathiri uwezo wa kupata ujauzito — lakini si kwa kila mwanamke.
Kwa wengine huathiri upandikizaji wa mimba, kwa wengine hakileti tatizo kabisa.
Tofauti ipo kwenye ukubwa na mahali kilipo.

📌 Usihukumu mwili wako bila uchunguzi.
📌 Pima mapema, elewa hali yako, chukua hatua sahihi.
📌 Elimu sahihi huondoa hofu zisizo na msingi.

👉 Swipe ujifunze namna kitambi kinavyoathiri uzazi na lini unapaswa kumuona mtaalamu.

📍 Tunapatikana Zanzibar na mikoa yote ya Tanzania
📞 0787677932
📲

DadasAfya

Una changamoto ya PCOS (kutopata ovulation mara kwa mara) na unatafuta ujauzito?PCOS si hukumu ya kutopata mimba — lakin...
27/01/2026

Una changamoto ya PCOS (kutopata ovulation mara kwa mara) na unatafuta ujauzito?
PCOS si hukumu ya kutopata mimba — lakini hakuna dawa ya miujiza ya haraka bila mpango sahihi wa kiafya.

Ukweli wa kitabibu:
👉🏽 PCOS huathiri homoni na mzunguko wa yai
👉🏽 Ujauzito hupatikana kwa udhibiti sahihi wa mwili, si papara
👉🏽 Kila mwanamke ana PCOS yake — tiba si sawa kwa wote

Mapendekezo muhimu:
✔️ Pima homoni na fanya ultrasound
✔️ Dhibiti uzito, lishe na sukari ya damu
✔️ Fuata mpango wa matibabu unaoeleweka kitabibu
✔️ Epuka kutumia dawa/supplements bila ushauri

📌 Elimu sahihi + ufuatiliaji = nafasi salama ya ujauzito.

👉 Swipe tukajifunze zaidi.

📍 Tunapatikana Zanzibar na mikoa yote ya Tanzania
📞 0787677932
📲

26/01/2026

“Mimba yangu ya mwisho hii… sitakuja kuzaa tena.”
Maneno haya husikika kwa wanawake wengi waliopitia shida nzito za mimba — presha ya mimba, kutokwa damu, upasuaji mgumu, kupoteza mimba au uchungu wa muda mrefu.

Ni hisia za kweli. Lakini pia ni muhimu kujua:
👉🏽 Si kila hofu ni mwisho wa safari ya uzazi
👉🏽 Changamoto nyingi za mimba zinaeleweka kitabibu na zinaweza kudhibitiwa kwa ufuatiliaji sahihi
👉🏽 Uamuzi wa kuzaa au kutozaa unahitaji taarifa sahihi, si hofu pekee

Mapendekezo ya kiafya:
✔️ Fanya tathmini ya afya kabla ya mimba (preconception check)
✔️ Zungumza na mtaalamu kuhusu historia yako ya mimba
✔️ Dhibiti magonjwa sugu mapema (presha, kisukari, upungufu wa damu)
✔️ Pata elimu sahihi kabla ya kufanya uamuzi mkubwa

📌 Uzazi salama unaanza na elimu + ufuatiliaji + maamuzi yenye taarifa.

📍 Tunapatikana Zanzibar na mikoa yote ya Tanzania
📞 0787677932
📲

Address

Zanzibar

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when DadasAfya posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram