05/11/2025
Ni vigumu kuelezea kwa maneno kile ambacho mioyo yetu inapitia sasa Sauti zetu zimejaa maumivu, macho yetu yameona mambo ambayo hatujawahi kufikiria kuyaona katika nchi yetu tuliyokuwa tunaiita salama,
Tumepoteza ndugu zetu, Tumepoteza usingizi, tumepoteza amani na bado tunajaribu kuvuta pumzi moja zaidi kwa matumaini kuwa kesho itakuwa salama,
Leo tunalia, lakini pia tunaomba Mungu atuponye k**a Taifa, atupe faraja na atuongoze tuwe wamoja tena, Kwa waliojeruhiwa, kwa waliopoteza wapendwa wao na kwa kila aliye na hofu moyoni tunawaombea.
๐น๐ฟ Mungu ibariki Tanzania.
โ๏ธ โIkiwa watu wangu, walioko kwa jina langu, watajinyenyekeza, waombe, watafute uso wangu, na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia kutoka mbinguni, nami nitawasamehe dhambi zao na kuiponya nchi yao.โ
โ 2 Mambo ya Nyakati 7:14