Magonjwa ya Wanawake

  • Home
  • Magonjwa ya Wanawake

Magonjwa ya Wanawake You're health is our concern , Call us +255769600821 or +255655562181

FAHAMU UNDANI KUHUSU UGONJWA WA ACID REFLUX/TINDIKALI YA TUMBO (GERD-GastroEsophagaelRefluxDesease)+255655562181 , +2557...
14/11/2025

FAHAMU UNDANI KUHUSU UGONJWA WA ACID REFLUX/TINDIKALI YA TUMBO

(GERD-GastroEsophagaelRefluxDesease)

+255655562181 , +255769600821

• Ni tatizo linalotokea katika mfumo wa mmeng'enyo na kusababisha hitilafu ya chakula au maji kurudi katika koo la chakula (*Umio*) mara baada ya kuwa chakula Hiko kimeshamezwa au Ni kitendo cha kupanda kwa acid ( *tindikali* ) ya tumbo hadi kwenye Koo /Umio la chakula kwa muda mrefu na kusababisha kiungulia ( *HEARTBURN* ).

• Kiungulia hiki huanza muda mfupi baada kumaliza kula na kuisha baada ya masaa mawili.
• Pia dalili za tatizo hili kwa watoto hujionesha pale m tototo anapotapika kupita kiasi au kupaliwa mara kwa mara wakati wa kula chakula.

_*Dalili zingine ni kama*_

• Tumbo kuunguruma na Kukosa hamu ya kula chakula na kuhisi kichefuchefu.
• Mdomo kunuka kutokana na kurudi juu kwa chakula cha tumboni chenye tindikali.
• Kupata hali ya kuunguza kwenye kifua karibu na moyo, hali inayotokea Muda Mfupi baada tu ya kula na kupata shida wakati wa kumeza chakula.
• Kucheuwa Maji Maji Yenye Tindikali Ukiwa Usingizini Hasa Baada Ya Kulala Muda Mfupi Baada Ya Kula.
• Kukohoa au kupaliwa mara kwa mara ikiambatana na kuweweseka Kwa Kukosa Pumzi.
• Mdomo kuwa mchachu muda mwingi.
•Kuvimba Kwa Tezi za Shingoni Kama Vile Tonses na Goita.
• Mdomo kukauka.
• Meno kupoteza uimara na kuanza kumomonyoka kutokana na uwepo wa tindikali.
• Tumbo kujaa Gesi , Kupata Choo Kama Tope Kunakoambatana kujamba sana.
• Tumbo Kuunguruma Hasa Muda Mfupi Baaada Ya Kula.

• Tatizo la Acid / Tindikali Ya Tumbo Linatibika na Kupona Kabisa.

-📞"Wasiliana nasi kuhusu afya - Kupitia Simu Namba 0655562181 / 0769600821

°Au Kuchart Nasi Moja Kwa Moja Watssapp Bofya link hapo chini 👇👇
http://.wa.me/255655562181

- Pia Waweza Jiunga na Group letu la Afya la WhatsApp Kwa Kubonyeza Link Hii hapa 👉👉👉 https://chat.whatsapp.com/C4qdsFaTDTB7tUPplBak8Q

, & Usaidie na Wengine

19/10/2025

𝙎𝘼𝘽𝘼𝘽𝙐 𝙆𝙐𝙐 ( 𝙑𝙔𝘼𝙉𝙕𝙊 ) 𝙕𝙄𝙉𝘼𝙕𝙊 𝙎𝘼𝘽𝘼𝘽𝙄𝙎𝙃𝘼 𝘼𝘾𝙄𝘿 𝙍𝙀𝙁𝙇𝙐𝙓 / 𝙂𝙀𝙍𝘿.

Call & WhatsApp +255655 562 181 , +255769600821

1. Vyakula na vinywaji fulani
Vyakula vyenye mafuta mengi

• Chokoleti
• Kahawa, chai kali, soda
• Vitunguu na pilipili
• Nyanya na vyakula vyenye asidi nyingi
• Pombe
• ladha za kuongeza kwenye mboga na baadhi ya vyakula zinazo tokana na kemikali.

2. Tabia za kula.

• Kula chakula kingi kwa mara moja
• Kulala au kuinama muda mfupi baada ya kula
• Kula usiku sana
• Kutokula kwa ratiba maalum

3. Shinikizo tumboni (abdominal pressure)
Unene/uzito kupita kiasi

• Mimba
• Nguo zinazobana sana kiunoni

4. Sababu za kitabibu Kulegea kwa LES (valve ya umio wa chini)

• Hiatal hernia (sehemu ya tumbo inapanda juu ya diaphragm)
• Maambukizi ya H. pylori au vidonda vya tumbo
• Matumizi ya dawa kama aspirin, ibuprofen, au dawa za arthritis

5. Mtindo wa maisha.

• Uvutaji wa sigara (husababisha valve kulegea)
• Msongo wa mawazo (stress)
• Kukosa usingizi au kuchoka kupita kiasi

• Tatizo la Acid / Tindikali Ya Tumbo Linatibika na Kupona Kabisa.

-📞"Wasiliana nasi kuhusu afya - Kupitia Simu Namba 0655562181 / 0769600821

°Au Kuchart Nasi Moja Kwa Moja Watssapp Bofya link hapo chini 👇👇
http://.wa.me/255655562181

- Pia Waweza Jiunga na Group letu la Afya la WhatsApp Kwa Kubonyeza Link Hii hapa 👉👉👉 https://chat.whatsapp.com/C4qdsFaTDTB7tUPplBak8Q

, & Usaidie na Wengine

𝙆𝙒𝘼 𝙉𝙄𝙉𝙄 𝙈𝙒𝘼𝙉𝘼𝙈𝙆𝙀 𝙃𝙐𝙏𝙊𝙆𝘼 𝘿𝘼𝙈𝙐 𝙐𝙆𝙀𝙉𝙄 𝙒𝘼𝙆𝘼𝙏𝙄 𝙒𝘼 𝙏𝙀𝙉𝘿𝙊 𝙇𝘼 𝙉𝙀𝙏𝘼? Hizi hapa ndiyo Sababu kuu za Postcoital Bleeding-Kwa kawai...
17/10/2025

𝙆𝙒𝘼 𝙉𝙄𝙉𝙄 𝙈𝙒𝘼𝙉𝘼𝙈𝙆𝙀 𝙃𝙐𝙏𝙊𝙆𝘼 𝘿𝘼𝙈𝙐 𝙐𝙆𝙀𝙉𝙄 𝙒𝘼𝙆𝘼𝙏𝙄 𝙒𝘼 𝙏𝙀𝙉𝘿𝙊 𝙇𝘼 𝙉𝙀𝙏𝘼?

Hizi hapa ndiyo Sababu kuu za Postcoital Bleeding-

Kwa kawaida mtu mwenye hormonal imbalance anaweza kutokwa damu wakati wa tendo la ndoa (sex) kwa sababu kadhaa zinazohusiana na mabadiliko ya homoni, hasa estrogen na progesterone.

Hapa kuna maelezo ya kina:

🧠 1. Upungufu wa homoni ya estrogen
Estrogen husaidia kuweka kuta za uke zikiwa nene, zenye unyevu na zenye elastic.

Wakati kiwango chake kimeshuka (kama kwenye hormonal imbalance, stress, au baada ya uzazi), ukuta wa uke hukauka na kuwa mwembamba.

Hivyo, wakati wa sex ukuta huu mwembamba huweza kupasuka kirahisi na kusababisha damu kidogo au maumivu.

🩸 2. Mabadiliko ya homoni kwenye mzunguko wa hedhi.

Wakati mwingine mwili unapata mabadiliko ya ghafla ya homoni kabla au baada ya hedhi.

Hali hii inaweza kufanya mfuko wa mimba (uterus) kutoa damu kidogo wakati wa tendo la ndoa.

Kwa wanawake wenye hormonal imbalance, hii hutokea mara kwa mara bila ratiba maalum.

🌿 3. Uchochezi au uvimbe kwenye shingo ya kizazi (cervix).

Homonal imbalance inaweza kufanya tishu za shingo ya kizazi kuwa nyeti na kuvimba (cervical erosion).

Shingo ya kizazi ikiguswa wakati wa sex, damu hutoka kwa urahisi.

⚠️ 4. Sababu nyingine zinazochangia ni
Maambukizi ya uke au shingo ya kizazi (yeast, PID, trichomonas, n.k.)

Fibroids au polyps kwenye kizazi.

Matumizi ya vidonge vya kupanga mimba visivyo na uwiano wa homoni.

Stress na usingizi duni, ambavyo pia huharibu uwiano wa homoni.

𝐊𝐀𝐑𝐈𝐁𝐔 𝐍𝐈𝐊𝐔𝐒A𝐃𝐈𝐄 𝐏𝐈𝐆𝐀 & 𝐖𝐇𝐀𝐓𝐒𝐀𝐏𝐏

Call➖text&sms➖whatsapp👇

➖ Ili Kupata Ushauri na Msaada Zaidi Kuhusu Matatizo Mbali Mbali Kiafya - Mawasiliano - +255655562181 au +255769600821

➖ Jiunge na Group letu la Afya la WhatsApp Kwa Kubonyeza Link Hii hapa 👉👉👉 https://chat.whatsapp.com/C4qdsFaTDTB7tUPplBak8Q

➖ SHARE kwenye MA GROUP NA WATU MBALI MBALI UWASAIDIE WENGI WANAO TESEKA 🙏🙏🙏 kisha tuandikie maoni yako au ushauri hapo chini

𝐊𝐀𝐑𝐈𝐁𝐔 𝐀𝐒𝐀𝐍𝐓𝐄.

"VYAKULA 16 VINAVYOONGEZA KINGA YA MWILI"✒ Watu wengi tumekuwa tukijiuliza kinga ya mwili ni kitu gani na je ni nini tuf...
12/04/2025

"VYAKULA 16 VINAVYOONGEZA KINGA YA MWILI"

✒ Watu wengi tumekuwa tukijiuliza kinga ya mwili ni kitu gani na je ni nini tufanye ili kuiongeza hiyo kinga ndani ya miili yetu. Suala la kuimarisha na kuiongeza kinga ya mwili linapaswa kuwa ni jambo endelevu la kila siku.

✒ Hakuna dawa au chakula cha kula siku moja na kuponya tatizo la kushuka kinga ya mwili milele. Kinga ya mwili huongezeka ama kupungua kila siku kutegemea na umekula nini, umekunywa nini au hali ya ubongo wako kwa ujumla ipoje kwa siku hiyo, mathalani kama umeshinda una hasira hasira tu kutwa nzima lazima na kinga yako itapungua.

✒ Mwili ulibuniwa na Mungu uweze kujitibu wenyewe bila kuhitaji DAWA YOYOTE. Ulivyo ni vile unavyokula na kunywa. Shida ni kuwa watu wengi hatujuwi tule nini kwa ajili ya nini, mara nyingi tunakula ili tushibe.

✒ Fanya chakula kiwe ndiyo dawa zako na dawa zako ziwe ni chakula unachokula. Kinga yako inapokuwa na nguvu na ya kutosha huwezi kuugua ugonjwa wowote kirahisirahisi.

Vifuatavyo ni vyakula na mitishamba 16 inayoweza kukusaidia kuongeza kinga ya Mwili wako

👉 Vyakula vinavyoongeza Kinga ya mwili"

1. MTINDI (yoghurt).

✒ Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na matakwa yako, yogati pengine ndio chakula kinachoongoza kwa kuogeza kinga ya mwili wako

👉 2. MATUNDA.

✒ Yanapatikana sehemu yoyote duniani kwa bei unazozimudu, katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, mtu asiyekula matunda ana hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda.

✒ Unaweza kuamua pia moja ya mlo wako katika siku kama ni wa jioni au wa mchana au wa asubuhi uwe ni matunda tu na si kitu kingine zaidi. Jaza kwenye sahani yako ndizi, embe, papai, nanasi, tikiti maji, parachichi nk, sahani iwe na matunda tu kula hadi ushibe matunda tu.

👉 3. Tui la Nazi:

✒ Nazi ikiliwa na binadamu hugeuza aina hizo za mafuta kuwa tindikali ambayo kitaalamu huitwa ‘medium chain fatty acids’ au kwa kifupi (MCFA’s) ambazo huwa na uwezo wa kuiimarisha kinga ya mwili na hivyo kuupa mwili uwezo wa kuyashinda maradhi mbalimbali".

✒ Matumizi ya nazi kama tiba ya kuimarisha kinga ya mwili duniani yalishika kasi mwaka 1990 mara baada ya mtafiti wa tiba kutoka Iceland, Bw. Halldor Thormar, kubaini maajabu ya tiba hii. Waathirika wa UKIMWI toka sehemu mbalimbali duniani waliotumia nazi walitoa ushuhuda wao wa namna walivyopata nafuu mara baada ya kutumia nazi kama tiba.

✒ Dozi yake ni rahisi, kunywaji glasi nne za tui la nazi kila siku kwa muda wa kati ya miezi mitatu hadi minne, huweza kuondoa maradhi yote yanayosababishwa na kupungua kwa kinga ya mwili na pia hung’arisha ngozi na kuifanya kuwa nyororo.

✒ Kula nazi kwa wingi kadiri uwezavyo, kama kinga yako imepunguwa basi anza kunywa tui la nazi glasi nne kwa siku na utaona maajabu ndani ya miezi mitatu tu. Kama tayari una vidonda visivyopona basi paka mafuta ya nazi kila utokapo kuoga, na matokeo utayaona bayana.

👉 4. VITUNGUU SWAUMU".

✒ Hupatikana kwa wingi Tanzania! Japokuwa vitunguu swaumu vimekuwa vikitumika sana kwa ajili ya matibabu ya magonjwa mbalimbali toka enzi za mababu, wataalamu wameshauri pia vitunguu hivi ni chanzo muhimu kwa kinga ya binadamu. Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.

✒ Chukuwa kitunguu swaumu kimoja, Kigawanyishe katika punje punje, chukua punje 6 hivi, Menya punje moja baada ya nyingine. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisu, Meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala au fanya kutwa mara 2.

👉 5. Mlonge:

✒ Mlonge au Moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean. Mti huu umeripotiwa kutibu zaidi ya magonjwa 300 ikiwemo magonjwa mbalimbali sugu.

✒ Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa. Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.

✒ Mbegu za mlonge zimekuwa dili kubwa duniani kwa sasa, zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Marekani na China na kwa mjibu wa taarifa ni kuwa zinauzwa mpaka shilingi 45000 ya Tanzania kwa gramu 500. Walikuja pia wachina kuzinunua kwa wingi na walipokuwepo hapa Tanzania bei ya mbegu za mlonge ilifika mpaka 11000 kwa kg kwa bei ya jumla yaani kwa anayechukua kg 100 au 500 au 1000 na kwenda juu.

✒ Taarifa zisizo rasmi zinadai Wachina hawa walikimbia nchini baada ya serikali kuanza kufuatilia na kuwakamata wakwepaji kodi bandarini. Isingekuwa hivi mpaka leo mlonge ungekuwa umeshatoweka wote Tanzania.

✒ Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani. Kile ulikuwa hujuwi ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajili ya binadamu na wanyama.

👉 MLONGE UNA:

*Kalsiamu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe
*Potasiamu mara 15 zaidi ya ile ya kwenye ndizi
*Una vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti
*Una protini nyingi mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi (Yogurt)
*Una Klorofili (kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea) mara 4 zaidi ya ile ya kwenye nyasi au majani ya ngano (wheatgrass)
*Una madini chuma (iron) mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach
*Una vitamini A mpaka Z,
*Una Omega 3, 6, na 9
*Una asidi amino zile mhimu zaidi zinazohitajika na mwili
*Una kiasi cha kutosha cha madini ya Zinc ambayo ni madini mhimu katika kuongeza homoni za kiume na nguvu za kiume kwa ujumla

👉 MLONGE NDICHO CHAKULA CHENYE AFYA ZAIDI KULIKO CHAKULA KINGINE CHOCHOTE JUU YA ARDHI;

👉 6. Asali yenye Mdalasini

✒ Asali ni dawa kwa kila ugonjwa, zingatia tu unapata asali mbichi na nzuri ya asili kwani endapo utauziwa asali iliyochakachuliwa kuna hatari ya kuharibu afya yako zaidi. Katika kila lita moja ya asali ongeza vijiko vikubwa vya chakula 8 vya unga wa mdalasini na uchanganye vizuri kisha lamba kijiko kimoja cha chakula cha mchanganyiko huo kila siku kutwa mara tatu kwa mwezi mmoja hivi kinga yako ya mwili itarudi katika hali yake nzuri.

👉 7. UYOGA:

✒ Usishangae! Ndio.. hiki ni moja ya vyakula muhimu zaidi kuimarisha afya yako kwani huchangia kiasi kikubwa kuimarisha seli nyeupe za damu zinazofanya kazi ya kupambana na magonjwa mbalimbali!

👉 8. SUPU YA KUKU:

✒ Wengi watahisi ni gharama lakini si kubwa kuzidi gharama ya kumuona daktari! Unywaji wa supu ya kuku ya moto husaidia kuzuia kupungua kwa seli nyeupe za damu vilevile hupunguza uwezekano wa kupata matatizo yanayohusiana na mapafu na mfumo wa hewa kiujumla!

✒ Mhimu ni kuwa supu hii ya kuku hakikisha ni ya kuku wa kienyeji tu.

👉 8. Mafuta ya habbat soda

✒ Unaweza kutumia mafuta ya habbat soda kuimarisha kinga yako ya mwili kwa ujumla na hivyo kuongeza ulinzi wa mwili wako dhidi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo dhidi ya bakteria na virusi. Mafuta ya habbat soda ndiyo bidhaa pekee ya asili iwezayo kuimarisha kinga yako ya mwili kwa muda mfupi.

✒ Ukiacha hili la kuongeza kinga ya mwili, Habbat soda ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo.

👉 9. Ubuyu:

✒ Pata kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku (kumbuka uwe ubuyu halisi). Ubuyu una vitamini C nyingi zaidi kuliko ile ipatikanayo kwenye machungwa au maembe.

✒ Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa.

1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
4. Ina virutubisho vya kulinda mwili
5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.
6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
7. Huongeza nuru ya macho
8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

✒ Unywe kiasi gani? Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.

✒ Ili upate faida za juisi ya ubuyu, zinazoelezwa hapa, lazima upate ule ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.

👉 11.VIAZI VITAMU(mbatata):

✒ Unaweza kuhisi ngozi sio sehemu ya muhimu katika kinga ya binadamu lakini ukweli ni kwamba ngozi ni sehemu ya muhimu sana kwa mwili wa binadamu. Kwa kinga kamili ya mwili wa binadamu tunahitaji Vitamin A ambayo hupatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu

👉 12. KAROTI:

✒ Karoti zina ziada kubwa ya vitamin pengine kuliko tunda lolote lile hivyo jitahidi kujumuisha karoti kama kiungo kwenye chakula au unaweza kuitafuna ikiwa mbichi!

👉 13. SAMAKI:

✒ Husaidia seli nyeupe kuzalisha ctokins zinatohusika kuzuia baadhi ya magonjwa yanayosababishwa na virusi hasa yale yanayohusiana na mfumo wa hewa nk.

👉 14. MATIKITI:

✒ Wengi Hudharau lakini tunda hili ni muhimu sana katika afya ya kila siku ya binadamu kwani husaidia kuongeza kiasi cha maji mwilin, madini chuma na kuimarisha seli nyeupe za damu.

✒ Tunda linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.

👉 Faida 13 za tikiti maji kiafya

• Asilimia 92 yake ni maji
• Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
• Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili,
• Huponya majeraha,
• Hukinga uharibifu wa seli
• Huboresha afya ya meno na fizi
• Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema
• Hubadilisha protin kuwa nishati
• Chanzo cha madini ya potasiamu
• Husaidia kushusha na kuponya shinikizo la damu
• Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
• Huondoa sumu mwilini
• Huongeza nguvu za kiume hasa ukila pamoja na mbegu zake

👉 15. MAJI YA KUNYWA:

✒ Kama kuna Kitu cha kwanza kwa uhai wa binadamu basi ni maji. Bila kunwya maji ya kutosha bado utakuwa katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali. Angalau glasi 8 hadi 10 za maji kwa siku ni muhimu kwa afya yako!.

✒ Kila mtu ana kiasi cha maji anachohitaji kunywa kila siku kwa mjibu wa uzito wake.

👉 16. Mbegu za Maboga:

✒ Mbegu za maboga pia zina kiasi kingi cha madini ya Zinki (Zinc). Madini haya yana faida lukuki mwilini, ikiwa ni pamoja na kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha ukuaji na uundaji wa chembechembe hai za mwili, kuboresha usingizi, kuboresha ladha mdomoni na harufu, huboresha afya ya macho na ngozi, hurekebisha sukari na huboresha nguvu za kiume pia.

✒ Upungufu wa madini ya Zinc mwilini una uhusiano mkubwa sana na matatizo ya kuzaa watoto njiti, kuota chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo darasani kimasomo na matatizo mengine mengi ya kimwili na kiakili.

👉 Namna nzuri ya kula mbegu za maboga:

✒ Unaweza kula zikiwa kavu na ndiyo utapata faida nyingi zaidi ingawa mimi napenda kuzikaanga kidogo kama dakika 15 hivi na huwa nazichanganya na maji ya chumvi ya mawe ya baharini kidogo kwa mbali ili kupata radha.

✒ Unahitaji ujazo wa kiganja kimoja cha mkono wako cha mbegu za maboga kwa siku ujazo wa kama nusu kikombe cha chai hivi kwa siku.

✒ Vitu vinavyoharibu na kushusha kinga ya mwili

1. Msongo wa mawazo (stress)
2. Vilevi vyote
3. Lishe duni (chakula kichache)
4. Kutokufanya mazoezi ya viungo
5. Kutumia dawa za kupunguza maumivu kila mara bila ushauri wa kitaalamu.

🔅Mawasiliano :☎️ 0655562181 au 0769600821

Ku chart Nasi Moja Kwa Moja WhatsApp Bonyeza Hapa 👉🏿 https://wa.me/255655562181

"Ili Kuwa Karibu Nasi Saa 24 ( 24hrs ) Kwa Msaada na Ushauri Wa Magonjwa Mbali Mbali , Jiunge na Group Letu la Whatsaapp .. Bonyeza Link hii hapa >>>>> https://chat.whatsapp.com/KCYfdXeCyVI1fVufcFbaVf

SHARE post hii kwa ajili ya wengine

UKIWA NA DALILI HIZI USISEME UNA VIDONDA VYA TUMBO~ +255655562181 , +255769600821 ~• Kupatwa na kiungulia mara kwa mara ...
04/04/2025

UKIWA NA DALILI HIZI USISEME UNA VIDONDA VYA TUMBO

~ +255655562181 , +255769600821 ~

• Kupatwa na kiungulia mara kwa mara ambapo huambatana na koo la chakula kuwaka moto pia maumivu ya kifua na hali hii huzidi zaidi pale mtu anapolala kichwa kimeinama au kulalia tumbo.

• Kiungulia hiki huanza baada ya lisaa limoja na kuisha baada ya masaa mawili baada ya kula.

• Pia dalili za tatizo hili kwa watoto hujionesha pale mtoto anapotapika kupita kiasi au kupaliwa mara kwa mara wakati wa kula chakula ,Kikohozi kisichopona au kupaliwa na kukosa pumzi akiwa usingizini.

•Dalili zingine ni kama;

• Tumbo kuunguruma na Kukosa hamu ya kula chakula na kuhisi kichefuchefu.
• Kutokwa na makohozi kooni mara kwa marq.
• Kutoa mabaki ya chakula wakati was kupiga mswaki.
• Mdomo kunuka kutokana na kurudi juu kwa chakula cha tumboni chenye tindikali.
• Kupata hali ya kuunguza kwenye koo , kifua na karibu na moyo, hali inayotokea Muda Mfupi baada tu ya kula na kupata shida wakati wa kumeza chakula.
• Kucheuwa Maji Maji Yenye Tindikali Ukiwa Usingizini Hasa Baada Ya Kulala Muda Mfupi Baada Ya Kula.
• Kukohoa au kupaliwa mara kwa mara ikiambatana na kuweweseka Kwa Kukosa Pumzi.
• Mdomo kuwa mchachu muda mwingi hasa baada ya kutoka usingizini.
• Kupata usingizi kwa shida kutokana na maumivu ya tumbo na Koo.
• Kuvimba Kwa Tezi za Shingoni Kama Vile Tonses na Goita.
• Mdomo na koo kukauka.
• Meno kupoteza uimara na kuanza kumomonyoka kutokana na uwepo wa tindikali.
• Tumbo kujaa Gesi , Kupata Choo Kama Tope Kunakoambatana kujamba sana.
• Tumbo Kuunguruma Hasa Muda Mfupi Baaada Ya Kula.

• Hii inaitwa ACID REFLUX au GERD
( *GastroEsophagaelRefluxDesease* na siyo vidonda vya tumbo kama wengi wanavyodhani , Kwa sababu Ugonjwa huu unafanana sana na Vidonda vya Tumbo.
• Watu wengi wanao jitambulisha kuwa wana Vidonda vya tumbo baada ya vipimo vya Kumulika tumboni kufanyika na Kuonyrsha “Kuta ni Nyekundu. Lakini pia huonyesha Gesi imejaa tumboni”. Kitalamu wanaangukia kwenye GERD na Gastritis na Siyo Vidonda vya Tumbo.
:
ENDOSCOPY - Vipimo vya Kuingiziwa Kumulika ndani haviwezi kukwambia CHANZO CHA TATIZO halisi cha Tatizo na ndiyo maana wagonjwa wengi wamekuwa wakijitafsiri wana Madonda ya tumbo kwa sababu wameanzishiwa dawa za Kutibu dalili (Gesi na Kiungulia) bila Kuchunguzwa chanzo.

• Kibaya zaidi Watalamu wengi wamekuwa wakikimbilia kutibu H Pylori na kusahau kuna vyanzo Vingi Vinavyo sababisha Mtu kuwa na GERD na Gastritis.

• Katika mfumo wa chakula kuna bakteria rafiki ambao husaidia kumeng’enya chakula vizuri. Maisha ya Pombe, sigara, Vyakula vya kukaanga, Soda Na juisi Huathiri hawa bakteria na Kusababisha vimelea maadui kuota katika kuta na kushambulia ukuta wa Mfumo wa chakula. Kitalamu husababisha SIBO (Small Intestine Bakteria and Yeast Overgrowth) Hali hio Huvimbisha Mfumo wa chakula Gut Inflammation na Unaweza Kuibua mzio sugu, Kukosa usingizi, Mvurugiko wa homoni kwa sababu ya Kudhoofika kwa Mfumo wa Chakula.

“Uhai na Kifo vipo katika Mfumo wa Chakula”

•.Vyakula Vya Sukari na wanga kwa mtu kama uwezo wa mwili Kutumia wanga huo ni Mdogo. Husababisha wanga kukaa tumboni muda mrefu badala ya kuwa Dighested kwa wakati na kusababisha kuchachuka haraka na Kuongeza makali ya gesi na kiungulia.

• Hivyo katika matibabu Mgonjwa huwa tunampampatia Suluhisho kwa Kuondoa changamoto ziluzopo jwa kusafisha mfumo wake wote na kuufanyia repair ili kurudisha hali yake ya asili ndani ya muda mfupi Sana.

♐Tatizo la Acid / Tindikali Ya Tumbo Linatibika na Kupona Kabisa.

🕳 Kwa msaada zaidi :- Tafadhali Usisite Kuwasiliana Nasi Kuhusu Tiba Kwa Njia za Kisasa Kabisa na Ushauri wa Masuala Mbali Mbali Ya Afya.

𝐊𝐀𝐑𝐈𝐁𝐔 𝐍𝐈𝐊𝐔𝐒A𝐃𝐈𝐄 𝐏𝐈𝐆𝐀 & 𝐖𝐇𝐀𝐓𝐒𝐀𝐏𝐏

Call➖text&sms➖whatsapp👇

➖ Ili Kupata Ushauri Bure na Msaada Zaidi Kuhusu Matatizo Mbali Mbali Kiafya - Mawasiliano - +255655562181 au +255769600821

➖ Jiunge na Group letu la Afya la WhatsApp Kwa Kubonyeza Link Hii hapa 👉👉👉 https://chat.whatsapp.com/C4qdsFaTDTB7tUPplBak8Q

➖ SHARE kwenye MA GROUP NA WATU MBALI MBALI UWASAIDIE WENGI WANAO TESEKA 🙏🙏🙏 kisha tuandikie maoni yako au ushauri hapo chini

𝐊𝐀𝐑𝐈𝐁𝐔 𝐀𝐒𝐀𝐍𝐓𝐄.

TAFADHALI : USISAHAU KU SHARE.

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Magonjwa ya Wanawake posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Magonjwa ya Wanawake:

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram