12/10/2025
Franco Luambo Makiadi : Sauti ya Bara Linaloamka
Tarehe 12 Oktoba 1989, Afrika ilinyamaza kwa muda.
Kama vile Mto Kongo ulisimamisha mkondo wake kusikiliza kwa mara ya mwisho sauti nzito na ya kifalme ya "Franco Luambo Makiadi".
Siku hiyo, gwiji wa OK Jazz aliaga duniani, lakini kazi yake iliingia katika umilele.
"Franco Luambo Makiadi" hakuwa Msanii wa kawaida.
Alikuwa ni dhamiri ya muziki, mfasiri wa roho ya jamii ya Kibantu, na mjumbe wa kihistoria aliyeandika simulizi za watu wake kwa ala na sauti.
Gitaa lake mara laini, mara kali lilibeba huzuni na furaha za watu waliotafuta heshima na utu.
Kupitia midundo ya rumba ya Kongo, alichonga kumbukumbu ya pamoja, akisimulia mapenzi, usaliti, umaskini, umalaya, utajiri, umaskini, siasa, hekima za jadi na kejeli za maisha ya kila siku.
Kwa OK Jazz si bendi tu, bali taasisi alijenga urithi mkubwa, wenye mizizi ya Kiafrika na upeo wa kimataifa.
Alifanya Léopoldville icheze, Brazzaville ilie, Abidjan iote ndoto, Dar Es Salaam iamke, Nairobi ikubali, Brussels itambe na Paris itikisike.
Sauti yake nzito na ya kifalme ilibeba uzito wa mzee wa jadi wa kisasa, aliyeweza kuunganisha mitaa ya watu wa kawaida na kumbi za mabalozi.
Lakini nyuma ya midundo ya furaha, kulikuwa na macho ya kisiasa yaliyoamka.
"Franco Luambo Makiadi" alijua kuwa rumba si burudani tu bali ni silaha. Aliitumia kwa ustadi wa daktari na ufasaha wa mshairi.
Nyimbo zake, ndefu na wakati mwingine zilizopigwa marufuku, zilikuwa ni ramani za kijamii, mahakama za watu, vioo vya jamii inayobadilika.
Miaka thelathini na sita baada ya kifo chake, "Franco Luambo Makiadi" bado anasikika kwenye teksi za Kinshasa, kwenye redio za bara zima, kwenye kumbukumbu za walioko ughaibuni muziki wake bado unaishi, Unagusa, unafundisha, unaunganisha. Unakumbusha kuwa Afrika, hata ikiwa na majeraha, imezaa sauti zinazovuka mipaka na karne.
"Franco Luambo Makiadi " hajafa :
Amegeuka kuwa midundo !
Amegeuka kuwa maneno !
Amegeuka kuwa kumbukumbu.
Aendelee kupumzika kwa Amani.
L.W.L
Franco Luambo Makiadi : La voix d’un continent qui s’éveille
Le 12 octobre 1989, l’Afrique suspendit son souffle.
Comme si le fleuve Congo lui-même avait interrompu son cours pour écouter, une dernière fois, la voix grave et souveraine de Franco Luambo Makiadi.
Ce jour-là, le maître de l’OK Jazz quittait la scène terrestre, mais son œuvre entrait dans l’éternité.
Franco Luambo Makiadi n’était pas un artiste ordinaire.
Il était la conscience musicale d’un peuple, l’interprète de l’âme bantoue, le messager d’une histoire collective transmise par les cordes et les mots.
Sa guitare tantôt douce, tantôt tranchante portait les douleurs et les joies d’une société en quête de dignité.
À travers les rythmes de la rumba congolaise, il sculptait une mémoire partagée, racontant l’amour, la trahison, la pauvreté, la prostitution, la richesse, la politique, la sagesse ancestrale et les ironies du quotidien.
L’OK Jazz n’était pas une simple formation musicale : c’était une institution.
Franco y bâtit un héritage immense, enraciné dans l’Afrique profonde et ouvert sur le monde.
Il fit danser Léopoldville, pleurer Brazzaville, rêver Abidjan, éveiller Dar Es Salaam, convaincre Nairobi, rayonner à Bruxelles et faire vibrer Paris.
Sa voix grave et majestueuse portait le poids d’un ancien devenu moderne, capable de relier les ruelles populaires aux salons diplomatiques.
Mais derrière les rythmes festifs, veillaient des yeux politiques.
Franco savait que la rumba n’était pas qu’un divertissement : c’était une arme.
Il la maniait avec la précision d’un chirurgien et l’éloquence d’un poète.
Ses chansons, longues et parfois censurées, étaient des cartographies sociales, des tribunaux populaires, des miroirs tendus à une société en mutation.
Trente-six ans après sa disparition, Franco Luambo Makiadi résonne encore.
Dans les taxis de Kinshasa, sur les ondes du continent, dans les souvenirs de l’exil sa musique vit.
Elle touche, elle enseigne, elle rassemble.
Elle rappelle qu’une Afrique meurtrie peut enfanter des voix qui transcendent les frontières et les siècles.
Franco Luambo Makiadi n’est pas mort :
Il est devenu rythme.
Il est devenu verbe.
Il est devenu mémoire.
Qu’il repose en paix.
L.W.L