05/11/2025
UTANGULIZI
Watu wengi huona kuamka mapema ni kama tabia ya watu tu wenye nidhamu au mafanikio tu. Lakini kwa macho ya kiroho, kuamka mapema ni tendo la kisheria la nishati, ni kuungana na mawimbi ya kwanza ya uumbaji kabla dunia haijaanza kuzungumza.
Kabla jua kuchomoza, dunia huwa katika hali ya kimya cha nishati yani hakuna mawimbi ya hasira, presha, au mawazo ya watu milioni kadhaa wanaoamka na kukimbilia mijini/vibaruani
Ni kipindi ambacho nishati ya Muumba (Source Energy) hujipanga upya ili kuingiza mwanga mpya kwa siku inayofuata.
Ndiyo maana katika tamaduni zote za kale, kuamka mapema kulizingatiwa kuwa mlango wa mawasiliano na ulimwengu wa mwanga:
Wahindi walikiita “Brahma Muhurta” yani wakati wa Muumba.
Waislamu waliuita “Tahajjud” yani wakati wa dua zinazojibiwa.
Wamasai, Wachagga, na Wagogo wa zamani walitoka mapema kufanya matambiko au kupiga mluzi wa rohoni kuamsha nguvu ya dunia ndani mwao.
Kuamka mapema, basi, sio ibada ya dini fulani bali ni sheria ya nishati na vibration.
Ni namna ya kumiliki siku kabla dunia haijaanza kukuamulia wewe.
Ebu nijaribu hivi👇
🌅 1. WAKATI WA “FREQUENCY SAFI” (PRE-SUNRISE PERIOD)
Kipindi cha saa 9 usiku hadi saa 12 alfajiri (3:00–6:00 AM) ndicho kinachoitwa Brahma Muhurta.
Hapa anga linakuwa tulivu kabisa. Dunia inakuwa kama kanda tupu (blank CD) ... bado haijaandikwa mawazo ya wanadamu.
Yes natambua kwamba wakati ww unasema huu ni usiku,kuna maeneo ni mchana, sasa hapa ninacho zungumzia ni nisharti ile itakayo kuangazia katika Eneo lako mfano kwa wewe uliye Tanzania ama Africa ya mashariki tunaoshea muda mmoja..
Sasa Mtu anayeamka na kutulia muda huu wa saa9 usiku- Alfajiri anapata yafuatayo;
▪️Ufahamu wa ndani (inner knowing)
▪️Maono ya siku au maisha yake
▪️Utulivu wa kiroho unaoongeza nguvu ya kuvuta matukio mazuri
👉Kwa lugha ya vibration: huu ni wakati wa kuunganisha akili ndogo (mind) na akili kuu ya ulimwengu (Universal Mind).
Unapoamka muda huu, unakuwa unapanda mbegu ya nishati safi kabla jua halijaweka “signature” yake angani.
☀️ 2. BAADA YA JUA KUCHOMOZA
Kuanzia saa 12:30 hadi saa 2:00 asubuhi (6:30–8:00 AM), frequency ya dunia hubadilika.
Hapa jua linaanza kuchochea nguvu za “kutenda,” ubongo unakuwa hai zaidi, na mfumo wa mwili unaanza kutengeneza homoni za utendaji.
Hapa Mtu ambaye tayari amejiunganisha kabla ya jua, sasa anatembea akiwa ameshika frequency ya mwanga yani Anaitawala dunia yake
Lakini ambaye amelala hadi jua linanoga/limechomoza, anaamka akiwa amekutana na nishati iliyokwisha kuchanganywa na mitetemo ya watu wengi..hapa jua ndilo linakutawala
Ndiyo maana msemo wa kiroho unasema:
🗣️ “Kama hukupanda mapema, utakuta wengine wameshaokota nishati.”
Sio kwamba wamekuchukulia kitu, bali wao walijiunganisha na safu ya kwanza ya mwanga yani ile " 👉 pure light code .... kabla haijaguswa na vibration za woga, wasiwasi, hofu,malalamiko,na presha za dunia,yani za watu wengi nchini kwako ama katika mkoa wako,wila yako,kata yako,mtaa/kijijini kwenu
🌄 3. SASA SWALI NI: KWA NINI NI MUHIMU KUAMKA MAPEMA❓
Kuamka mapema si desturi tu, bali ni kanuni ya kimungu inayofungua mlango wa mawasiliano kati ya roho yako na nguvu kuu ya uumbaji.
Faida zake ni hizi:
1. Akili inakuwa wazi , hakuna kelele za mawazo ya dunia, hakuna mizigo ya mawazo ya jana, hivyo ubongo wako uko safi kupokea maono mapya.
2. Mwili unavuta prana safi , hewa ya asubuhi huwa na nishati ya uhai (prana) ambayo bado haijachanganyikana na vibrations za shughuli za binadamu.
3. Roho inapata mwanga wa kwanza (Divine Light Code) , huu ni mwanga safi wa kimungu unaotoka moja kwa moja kutoka kwenye chanzo, kabla ya polarity ya jua kubadilika saa 7 mchana.
4. Unaandika siku yako mwenyewe kabla dunia haijaanza kukuandikia.
Kwa maneno mengine👇
🗣️ Ukiamka kabla ya jua .. wewe ndiye unaongoza nishati.
Ukichelewa ...nishati ndiyo inakuongoza wewe.
4. KUONDOKA NYUMBANI UKIWA TAYARI KIROHO🌬️
Usiondoke tu kwa kukurupuka.
Kabla hujaondoka, amka ndani yako kwanza.
Tulia, pumua kwa makini, kisha sema kimoyomoyo:
🗣️“Leo nimeunda dunia yangu yenye amani, mafanikio na watu wema wanaonitafuta.”
Hapa ndipo wengi wanakosea ... wanaomba rehema au msaada kila siku kana kwamba hawajaundwa kikamilifu.
Lakini kumbuka:
Usiombe rehema za Mungu, bali tengeneza mwelekeo.
Wewe ni sehemu ya Muumba, sio kiumbe kinachoomba kuumbwa upya kila asubuhi.
Hapa ndipo siri ya manifestation ya kweli inapozaliwa.
Dunia hujibu frequency yako, sio maneno yako.
Angalia mfano huu:
Mtu anaamka amechelewa, hajafanya ibada ya kujiumbia dunia yake, halafu kazini kwake anasema “riziki atatoa Mungu.”
Lakini ukweli ni kwamba ... kama huna nguvu yoyote (iwe chanya au hasi), dunia haitakusikiliza.
Unatakiwa kusema kwa ujasiri:
🗣️ “Leo nimepata elfu 20.”
“Leo nimeingiza tayari laki moja katika kazi yangu.”
Kumbuka, wewe ni nishati, wewe ni roho ... ndiyo muumbaji halisi wa dunia yako.
Usitegemee huruma za Mungu kwa sababu Chanzo (Source) hakitumii hisia bali kanuni.
Ndiyo maana wale wanaotegemea huruma, hupokea kiwango kilekile au pungufu.. kisichotosha.
Usiombe pesa ije, usiitafute pesa, kwa sababu pesa pia ina vibration, ina miguu ya kithabiti ... itakukimbia.
👉 Bali ivute pesa kwa nguvu za uumbaji.
Pesa inavutwa na wenye nguvu, sio wenye maneno.
Haitakuonea huruma ... itaitikia tu frequency yako.
☀️ 5. KUHUSU SAA 7 MCHANA ...KILELE CHA FREQUENCY YA JUA
Kuanzia saa 6:45 hadi 8:00 mchana, jua linapita katikati ya anga.
Huu ndio wakati ambao nishati ya jua inafika kileleni, kisha inaanza kushuka polepole.
Waswahili walikuwa na hekima walisema:
“Ni muda wa treni kubadilisha behewa.” 😄
Ndiyo maana Wahindi wengi hupumzika kipindi hicho.
Wengine hurudi nyumbani kwa dakika chache, si kwa kula tu, bali kwa kusawazisha nguvu zao.
Katika baadhi ya maeneo ya India, hufanyika ibada iitwayo “Agni Meditation.”
Watu hukaa kimya, huhema taratibu, na kumshukuru Surya ... nguvu ya jua.
Wakinyosha mikono kuelekea jua, husema:
🗣️ “Surya Namah... “Naisalimu nguvu ya mwanga.” ☀️
Hii sio ibada ya jua, bali ni kutambua mzunguko wa nishati unaotembea kupitia mwanga wa jua.
Wakati huu, ubongo wa binadamu hubadilisha polarity ... upande wa kulia (hisia) na kushoto (mantiki) huanza kusawazika.
Ndiyo maana kufanya meditation, maombi ya shukrani, au kutulia kimya kipindi hiki huleta utulivu, umakini na nguvu mpya.
⏰ NINI MAANA YA “1:00 PM” NA “PM”❓
Kihistoria, “PM” humaanisha Post Meridiem ... baada ya jua kupita katikati ya anga.
Lakini siri ya kiroho ni kwamba
👉PM = Power Moment,
yaani kipindi cha kutuliza nguvu ya mwanga na kuanza mzunguko mpya wa nishati.
Waratibu wa muda waliweka saa 7 kama 1:00 PM kwa mujibu wa Elimu ya Namba (Numerology) ...namba 1 ikimaanisha mwanzo mpya wa kimfumo wa nguvu.
Wasiokuwa na maarifa haya hudhani ni “umasonic,” lakini ukweli ni kwamba ni hekima ya kale ya kozmiki.
Kwa lugha ya mwanga, saa 7 mchana jua huonekana likisema kwa sauti:
🗣️ ☀️“Nimewasha moto wa siku, sasa ni zamu yako kuutuliza na kuuongoza kwa hekima.”
Kwa hiyo huu ni muda bora wa:
▪️ Meditation ya kimya
▪️ Maombi ya shukrani
▪️Kurekebisha mawazo na mwelekeo wa siku
▪️ Kupumua na kuunganisha moyo na jua
🧘🏽♂️ MAZOEZI RAHISI YA SAA 7 MCHANA
Kama uko kazini au huwezi kurudi nyumbani, fanya hivi taratibu:
1. Kaa wima, fumba macho.
👉 Hii inasaidia mwili na akili kutulia, ubongo uanze kupokea mwanga.
2. Pumua ndani kwa sekunde 4, shikilia 4, kisha toa 4.
👉 Hii ni njia rahisi ya kusawazisha pumzi na mzunguko wa damu, huku ukirudisha nguvu ndani yako.
3. Fikiria mwanga wa jua unashuka kupitia kichwa hadi kifua.
👉 Huo ni mwanga wa uzima unaosafisha mawazo, huzuni na uchovu.
4. Sema kimoyomoyo:
🗣️ “Ninaungana na Chanzo cha mwanga, na ninasawazisha nguvu za leo.”
👉 Maneno haya yanaamsha kiungo cha roho yako na jua (Surya Connection).
5. Tabasamu taratibu na endelea na shughuli zako.
👉 Tabasamu ni alama ya kuruhusu mwanga ukae ndani yako.
⏳Ukweli ndugu yangu , Dakika tano tu za utulivu huu zinatosha kabisa kufufua nishati ya mwanga ndani yako na kuondoa uchovu wa mchana.
🌇 JIONI .... KIPINDI CHA TAFSIRI NA SHUKRANI
Baada ya jua kushuka, nishati ya dunia hubadilika kuwa tulivu.
Huu ni muda bora wa:
👉 Kujitafakari ...pima siku yako, angalia ulivyotumia nishati yako.
👉Kuandika mafanikio ya siku.. hata jambo dogo ni ushindi wa mwanga.
👉 Kufanya shukrani na kujiandaa kwa kesho ... shukrani hufunga mlango wa leo kwa amani na kufungua kesho kwa baraka mpya.
Kama uliianza siku kwa mwanga, na ukaimaliza kwa shukrani,
umekuwa mtu wa mzunguko kamili wa nuru , roho yako huingia usingizini ikiwa imetulia, tayari kuumba kesho yenye vibration ya mafanikio mapya
HITIMISHO
Jua sio tu chanzo cha mwanga ... ni kifaa cha kisheria cha ulimwengu, kinachosambaza mawimbi ya uhai na kuamsha roho za viumbe wote.
Kuamka kabla ya jua ni kuungana na nguvu ya uumbaji,
Kupumzika saa 7 mchana ni kuheshimu mzunguko wa uhai,
Kufunga siku kwa tafakari ni kuweka alama ya shukrani kwenye mwanga wa kesho.
Mafanikio ya kweli hayaji tu kwa kuomba dunia ikutendee..bali...
yanakuja pale unapounda dunia yako kwa frequency sahihi.
Kwa hivyo,
🗣️ Usisubiri dunia ikupe nguvu,
amka mapema, shika mwanga, na iandike dunia yako kwa vibration ya roho yako.
Nikwamba, Somo hili linaweza kutumika kama mwongozo wa “SIRI ZA JUA NA NGUVU YA KUAMKA MAPEMA” .. kwa wote wanaotaka kuishi kwa mwanga, uelewa, na mafanikio ya ndani na nje.
litaendelea.............