05/12/2025
KUVIMBA AU KUFURA MIGUU (EDEMA )
Miguu kuvimba husababishwa na kutuama kwa maji kwenye chembe hai za miguu, huweza kusababishwa na matatizo katika mfumo wa mishipa ya damu, mirija ya mitoki au tatizo katika figo. Unaweza kuvimba miguu kwa sababu pia ya kukaa ama kusimama mda mrefu sehemu moja.
SABABU YA KUFURA MIGUU
Kuna aina mbili za visabaishi, aina ya kwanza ni kutokana na kuvia kwa maji na aina ya pili kutokana na michomo kwenye chembe hai maeneo ya miguu. Maelezo zaidi yanapatikana kwenye aya zinazofuata.
Kuvimba miguu kutokana na mkusanyiko wa maji kwenye tishu za miguu
A-Kufeli ghafla kufanya kazi kwa figo
B-Magonjwa ya kuta za moyo
C-Kufeli sugu kufanya kazi kwa figo
D-Kufanyika makovu kwenye ini
SABABU ZINGINEZO
1-Kufeli kwa moyo
2-Kuziba kwa mishipa ya ngiri
3-Kuharibika kwa mishipa midogo ya ndani ya figo
4-Dawa wa dawa za kutuliza maumivu kiholela
5-Ujauzito
6-Madawa k**a madawa ya kisukari na shinikizo la damu
7-Kusimama kwa mda mrefu, kukaa kwa mda mrefu k**a kwenye ndege na gari
8-Magonjwa ya mishipa ya damu
9-Mishipa ya damu ya vein kushindwa kurudisha damu kwenye moyo
LA ZIADA
Kuvimba miguu kutokana na magonjwa ya michomo kinga
X-Kuvunjika kwa mfupa
XMaambukizi kwenye ngozi
Gauti
X-Maambukizi kwenye vidonda vya miguuni
X-Maambukizi kwenye vijifuko vya maji katika maungio ya miguu
X-Misuguano ya mifupa katika maungio
X-Baridi yabisi
X-Jeraha kwenye maungio ya visigino
X-Mgandamizo kwenye miguu
TIBA
Unaweza tumia soksi maalumu za kugandamiza miguu yako .Soksi hizi husaidia miguu isiendelee kuvimba Zaidi na pia inapunguza uvimbe. Daktari wako atashauri matumizi ya hizi soksi na namna unavyowezazipata.
ZINGATIA
KINGA MIGUU NA MAJERAHA
Hakikisha eneo la miguu yako limekuwa safi na halijakauka, na usiliweke katika mazingira ya kupata jeraha.
PUNGUZA KIWANGO CHA CHUMVI
Fuata ushauri wa dakiktari kuhusu kiwango cha chumvi unachotakiwa kutumia. Chumvi huwa na tabia ya kuhifadhi maji kwenye mwili, hivyo ukila nyingi inaweza kusababisha hali ya kuvimba ikawa mbaya Zaidi.
KWA TIBA NA USHAURI WASILIANA NASI KWA +254721836774 DR ISMAIL