Tahta shajara Herbalist &jinni Research Center

Tahta shajara Herbalist &jinni Research Center Tunashughulikia sana na wagonjwa walioathiriwa na mashetani wa kijinni na sihr au uchawi na hasad kwa kutumia Ruqya ya kisheria na madawa ya kisunna.

MJUE JINNUL ZAWABIR NA TIBA YAKEAsalam alaykum warahmatullahi wabarakatu  Hawa ni majini wakorofi sana.Na pia wana madha...
24/10/2021

MJUE JINNUL ZAWABIR NA TIBA YAKE
Asalam alaykum warahmatullahi wabarakatu Hawa ni majini wakorofi sana.Na pia wana madhara makubwa sana mwilini na pia miongoni mwa madhara yao humsababishia mgonjwa awe na saratani na maradhi ya mkanda wa jeshi.Huwaingia watu kwa haraka sana majini hususan wale ambao hupenda kukaa uchi baada ya kuoga.Na pia k**a atakuwa ni jinni mahaba wa kutoka ukoo huu huwa hapendi watu ambao wananuka jasho na akikaa karibu na mtu ambaye ana jasho atakuwa anatema tema mate ovyo ovyo.Siku za nyuma nilikuwa nimeelezea kwamba sio maradhi yote ambayo ukipimwa hospitalini tiba yake utaipata huko kwasababu maradhi yote hayo yanakuwaga yako sehemu mbili.ya kawaida na yale ya kusababishwa na majini wa kichawi.natumai kufikia hapo nimeeleweka.ijapokuwa kuna dalili ambazo zitakufahamisha ni jinni wa aina gani ambaye amekuvamia mwilini kwasababu kujua majini walioko ndani ya mwili kwa tabibu yeyote ni jambo la muhimu sana ili ajue anapambana na adui wa aina gani kwa dalilina kujua tiba yake kwasababu kila jinni ana tiba tofauti na mwingine.Na pia kuwajua majini kupitia ndoto ambazo mgonjwa anaota ni jambo ambalo ni la muhimu zaidi kwa tabibu
DALILI ZA KUMJUA JINNUL ZAWABIR AKIWA MWILINI
✔️Mwili kuwasha sana
✔️Mwili kuwa na vidonda vidonda vya upele
✔️ Mwili kupauka hata ukipaka mafuta
✔️Ngozi kumbambuka
✔️Mwili Kuvimba na kuwaka moto
✔️Ngozi kuvuka k**a gamba la nyoka
✔️Kuwa na majipu ya kila wakati
✔️ Rangi ya ngozi wakati mwingine kubadilika
✔️ Kukosa usingizi
✔️Kukosa utulivu wa moyo
TIBA YA KUMTOA JINNUL ZAWABIR
✔️ Mruturutu
✔️Kibiriti upele
✔️Shabu
✔️Karkam
✔️Mafuta ya ndimu
✔️Mafuta ya Thawm
✔️Mafuta ya nyonyo
MAANDALIZI NA MATUMIZI YA DAWA HIZO NI K**A YAFUATAYO
Hizi dawa zitatwangwa kisha zikilainika zichanganywe pamoja halafu mgonjwa atakuwa anafukiza mara mbili kwa siku.zoezi hilo atalifanya kwa siku 21 hadi 30 in sha Allah mgonjwa atapona
TIBA YA PILI NI DAWA ZA KULA
✔️Sanamaki
✔️Sidr
✔️Sufa nyekundu
✔️Haltit
✔️Pilipili manga
MAANDALIZI NA MATUMIZI YA DAWA HIZO
Dawa hizo zinatakiwa zikiwa ni za unga halafu zitachanganywa pamoja zote kisha ziwekwe kwenye asali lita moja.matumizi yake ni kijiko cha chakula kimoja kutwa mara 3 kwa siku 30 hadi 45 in sha Allah ni mujarab dawa hizo.Na mgonjwa afanyiwe Ruqya kwa ukamilifu wake siku 7.TUNATIBU NAYE ALLAH ANAPONYESHA.HII NI SABABU TU YA KUPONA KWAKO
Kwa wale ambao wanahitaji dawa hizo zikiwa tayari tunazo.unaweza ukaagiza na utafikiwa na mzigo wako popote ulipo
✔️+254756553838
✔️+254708995244

DAWA ZA KUFUKIZA KWA WALE WALIOSIBIWA NA MAJINI WABAYA MWILINI✔️Kibiriti upele✔️Sandarus✔️Haltit✔️Shubir✔️Kafur mayt✔️Ma...
23/10/2021

DAWA ZA KUFUKIZA KWA WALE WALIOSIBIWA NA MAJINI WABAYA MWILINI
✔️Kibiriti upele
✔️Sandarus
✔️Haltit
✔️Shubir
✔️Kafur mayt
✔️Mane mane
✔️Bakal hadi
✔️Mayatul sayla
✔️Mruturutu
✔️Misk ya unga
Zote dawa hizo zinatakiwa zikiwa zimetwangwa.kisha mgonjwa atakuwa anafukiza mara mbili kwa siku kwa siku 21 hadi 30
Kwa wale ambao wanahitaji dawa hizo zikiwa tayari za kufukiza wasiliana nasi kwa namba zifuatazo
✔️+254708995244 Whatsapp
✔️+254799659791 imo
✔️+254756553838 Whatsapp

DALILI ZA MTU ALIYESIBIWA NA MAJINI MWILINI MWAKEKUTOKA SEHEMU YA KWANZA✍️ Kukosa damu au kupungukiwa na damu au maji mw...
19/10/2021

DALILI ZA MTU ALIYESIBIWA NA MAJINI MWILINI MWAKE
KUTOKA SEHEMU YA KWANZA
✍️ Kukosa damu au kupungukiwa na damu au maji mwilini au kukonda ghafla
✍️Kuota ndoto ukiwa unakula
✍️Kuota ukiwa unafukuzwa na wanyama wakali
✍️Kuota ukiwa unapigana au unapigwa
✍️Kuota ukiwa umepandisha jinni
✍️Kuota ukiwa unapiga makelele
✍️Kuota ukiwa baharini unaogelea au unatembea
✍️Kuota ukiwa unavishwa pete au mkufu
✍️Kuota ndoto ukiwa unafukua kaburi
✍️Kuharibika kwa vitu vya moto kila wakati au kuwa na ndoto ukiwa unaona moto
✍️Ndoto ukiwa unamuona ngamia
✍️Ndoto za simba
✍️Kuota ukiwa unawaona mbwa au mbwa mwitu
✍️ Kuota majumba ya mizimu
✍️Kuota ukiwa unakabidhiwa mkuki au fimbo au mundu au wanyama k**a kondoo au ng'ombe na kitambaa cheupe au cheusi au chekundu
✍️Kuota ukiwa katikati ya watu kisha wanakuchagua kuwa kiongozi wao
✍️Kuota watu wakiwa wamevaa kanzu
✍️Kuota ukiwa unakunywa damu au unanyweshwa damu
✍️Kuota kuhusu vibuyu vya uganga ni dalili kuu nyingine kuwa unayo majini
✍️Kuota ukiwa unavaa bangili au mikufu
✍️Kuota ndoto za watu wamevaa mavazi meupe wamekusimamia
✍️Kuhisi k**a unaona vivuli vya watu
✍️Kuota ndoto za watu wanachunga ng'ombe
✍️Kuota ndoto ukiona mafuvu ya binadamu kila wakati
✍️Kuota unaona vishuguu
✍️Ndoto za nyimbo nyimbo na kufanyiwa mambo ya kienyeji
✍️ Kupenda sana kuwa mchafu kila wakati
✍️ Kupenda sana kukaa jalalani
✍️ Kupenda sana kukaa kweye ufuo wa bahari kila wakati
✍️Kupatwa na usingizi mzito tena wa ghafla ambapo hata ukiharibu kuamka huwezi.**hali hii husababishwa na jinnul al kabus na siku za nyuma nilikuwa nimeshaeleza**
✍️Kuanza kuwa na kifafa**hapa ifahamike kwamba kuna aina tatu ya kifafa k**a ifuatavyo
1.Kifafa cha kurogwa
2.Kifafa cha kawaida
3.kifafa ambacho kinasababishwa na majini mayti
✍️Kuwa majnun au kichaa.**ifahamike kwamba wale ambao wanakuwa vichaa wengi wanakuwaga wametumiwa majini waitwao jinnul Asahha
**Majini hawa wakati wanapoingia mwilini huamrishwa kukaa kwenye mishipa ya ubongo au ya fahamu na hapo ndipo matatizo haya yataanza.nitazidi kueleza na nilikuwa nimeelezea siku za nyuma wakati nilikuwa nazungumzia sihrul junoon.
Kwa wale ambao wanahitaji kufanyiwa visomo vya Ruqya tunafanya hivyo na pia tunayo madawa ya kupambana na sihr na hasad na majini wabaya .ijapokuwa nimeelezea dalili za majini wote kwa pamoja/Marohani na Mashetani
Kwa matibabu wasiliana nami kwa namba zifuatazo
✍️+254708995244 Whatsapp
✍️+254756553828 Whatsapp
✍️+254799649791 imo

DALILI ZA KUONESHA UMESIBIWA NA MAJINI MWILINIAsalam alaykum warahmatullahi wabarakatu, Dalili zake ni nyingi sana anbaz...
19/10/2021

DALILI ZA KUONESHA UMESIBIWA NA MAJINI MWILINI
Asalam alaykum warahmatullahi wabarakatu, Dalili zake ni nyingi sana anbazo ni za majini tofauti tofauti k**a vile tunavyozidi kueleza na dalili zenyewe ni k**a zifuatazo
✍️Kuumwa na kichwa cha upande mmoja
✍️Kifua kubana
✍️Kuhisi kichefuchefu unapomaliza tendo la ndoa
✍️Kuota ndoto ukiwa unafanya tendo la ndoa
✍️Mwili kuwa mzito hususan kwenye mabega
✍️Miguu kuwaka moto au kuhisi baridi wakati sio msimu wake
✍️Viungo vya mwili kufa ganzi
✍️Kuota ukiwa na mimba
✍️Mimba kutoka kila baada ya miezi mitatu au nane
✍️Kufunga hedhi au kutoka damu nyingi hadi kupitiliza siku za kisheria za hedhi
✍️Kuota ndoto ukiwa porini unafundishwa miti ya dawa
✍️Kuota ukiwa unapaa
✍️ Kuota ndoto za simba kila wakati
✍️Kuhisi k**a unafuatwa nyuma yako na ukiangalia huoni mtu yeyote
✍️Kuwa na wasi wasi kila wakati na kuhisi unakufa wakati wowote
✍️ Kupenda sana kukaa chooni
✍️Kusinzia ukiwa chooni
✍️Kuskia harufu ya manukato au harufu mbaya
✍️Kuchukia sauti ya adhana au mawaidha au Quran
✍️Kupiga miao kila wakati hususan wakati unaposwali au unaposoma kitabu cha Quran
✍️ Mapigo ya moyo kwenda mbio k**a vile mtu ana shinikizo la damu au presha
✍️Kukosa hamu ya tendo la ndoa
✍️ Ugomvi wa kila wakati hususan kwa wanandoa
✍️Kushindwa kufika kileleni wakati ufanyapo tendo la ndoa
✍️Kuishiwa na nguvu za kiume ufikapo kwa mkeo na ukiwa huko nje ulikuwa sawa
✍️Mke kumhitaji mme wake akiwa mbali lakini akifika anaanza kuwa na hasira naye
✍️Kuota mwanamke akiwa anazaa mtoto
✍️Ndoto za mwanamke kunyonyesha mtoto
✍️Unaota ukiwa umebeba mtoto
✍️Kuota ndoto za sherehe kila wakati
✍️Kuwa na hasira za ghafla ambazo hazina sababu yeyote
✍️ Kupenda sana ugomvi
✍️ Mwanamke ambaye bado hajaolewa kuchukia wanaume
✍️Kuchukia sana mwanamke anapoambiwa habari za ndoa au mapenzi
✍️Tumbo la kizazi kuuma sana kila wakati na kuvuta kwenye kitovu
✍️Kuskia sauti za watu wakiongea na wewe na watu ambao huwaoni
✍️Kuskia ukiitwa lakini ukienda huoni mtu
✍️ Kukosa usingizi nyakati za usiku
✍️Kuota ndoto za watu waliokufa
✍️Kuota ndoto ukiwa makaburini
✍️ Kizunguzungu kila wakati
✍️Macho kukosa aibu
✍️Kuhisi vitu vinatembea mwilini
✍️Kutojiskia kuongea na watu na kupenda sana kukaa ukiwa peke yako
✍️Kupata maradhi ya kujibadilisha badilisha
✍️Kuhisi uchungu wakati wa tendo la ndoa
Kuna sehemu ya pili pia kwasababu dalili ni nyingi sana na siwezi nikazimaliza zote
Kwa matibabu wasiliana nami kwa namba zifuatazo
✍️+254756553838 Whatsapp
✍️+254708995244 Whatsapp

MADHARA NA DALILI ZA JINNI CHEKETUAsalam alaykum warahmatullahi wabarakatu, hawa ni katika majini wakorofi sana,Na pia m...
18/10/2021

MADHARA NA DALILI ZA JINNI CHEKETU
Asalam alaykum warahmatullahi wabarakatu, hawa ni katika majini wakorofi sana,Na pia majini ambao ni makatili sana na hawana huruma,wachawi hupenda sana kutumia majini hawa katika kazi zao za kichawi kwasababu huwa wanawapenyeza sehemu ambazo wachawi hao hawawezi wakaingia na kufanya ushirikina wao.Kuwafahamu wanazo dalili zao ambazo nitazieleza hapa k**a ifuatavyo
✍️Jini huyu akishakuingia husababisha mambo yako kukwama.na hakuna jambo hata moja ambalo utaanzisha likamilike yote huishia njiani
✍️Jinni huyu huwasaidia wachawi kupita kwenye pembe za nyumba k**a vile nimetangulia kusema
✍️ Jini huyu pia humsababishia mtu kuteseka sana kwa maradhi mbalimbali ambayo yatasababisha asumbuke kila wakati kwa maradhi ambayo hayaishi
✍️ Humsababishia mtu heshima yake ishuke na kudharaulika kwa watu hata aseme jambo lipi kwake haliskilizwi hata k**a ana cheo cha aina gani lakini au hata elimu kiwango gani lakini hawezi akapata heshima hata kidogo
✍️Jini huyu pia hutembea na wachawi kwenda kumfanyia mtu uchawi na ana uwezo wa kujigeuza kwa sura yeyote ile.
✍️ Husababisha mtu kutuhumiwa na watu wengine na kuambiwa kwamba yeye ni mchawi popote aendapo
✍️Jinni huyu ni miongoni mwa majini ambao humpiga mtu hasad au nuksi kwasababu.mambo yake yatakuwa magumu sana ya kimaisha kila ufanyalo haliwi
✍️Pia jinni huyu husaidiana na wachawi kukupiga chale za wanga.natumai wale ambao wanafuatilia darasa zetu kwenye group tayari nilikuwa nimeshaeleza namna chale za wanga huwa zinapigwa
✍️ Husababisha kuharibu mahusiano kuchukiwa na mke, au ndugu au rafiki na hususan kwa wazazi mahusiano huwa mabaya sana
✍️ Husababisha madhara mengi sana mwilini kwasababu kila wakati unaweza ukawa unafanyiwa upasuaji kwa maradhi ambayo hayaishi au kuteswa kwa namna yoyote ile ili mradi hutakaa ukiwa na pesa zozote na hutafanya jambo lolote la maendeleo katika maisha yako maadamu huyu jinni yuko mwilini
✍️ Jinni huyu pia hutumika kushusha nyota za watu kwa kukutia giza
✍️Jinni huyu pia humdhibiti mtu katika mambo yake mengine hata akiweka ahadi huwa hazitimii kwasababu ya mambo yake kukwama
Kwa wale ambao wanahitaji kufanyiwa visomo vya Ruqya akiwa popote alipo tunafanya hivyo na tunatoa hasad na sihr kwa wale ambao wanaosumbuliwa na matatizo hayo na pia tunayo madawa ya kisunna ya kupambana na matatizo hayo na pia tunatibu maradhi mengine mengi
Kwa matibabu wasiliana nami kwa namba zifuatazo
✍️+254708995244 Whatsapp
✍️+254756553838 Whatsapp
✍️+254799659791 imo

MFAHAMU JINNUL MAQABIR NA DALILI ZAKEHawa majini asilimia kubwa wanakuwaga ni wa kutumwa na wachawi kuleta madhara ndani...
16/10/2021

MFAHAMU JINNUL MAQABIR NA DALILI ZAKE
Hawa majini asilimia kubwa wanakuwaga ni wa kutumwa na wachawi kuleta madhara ndani ya mwili wa binadamu.Ambapo majini hawa makazi yao ni makaburini ambayo yalishajaa na hayatumiki tena.ijapokuwa tabia za huyu jinni na jinni mayti zinakaribiana na hata kuingiwa na majini hao ni nadra sana labda yawe yametumwa na wachawi ili kuja kusababisha matatizo kwa mhusika.wakati tabibu anapomfanyia kisomo cha Ruqya mgonjwa ambaye amesibiwa na majini hawa huwa mara nyingi hawapandi.Ili kujulikana ni majini wa aina gani ambao wanaokusumbua mwilini ili uweze kupata tiba sahihi kwasababu kila jinni ana tabia na tiba yake tofauti na mwenzake.Hapa nitaeleza dalili zake kwa ufupi k**a ifuatavyo
DALILI ZA KUMFAHAMU JINNUL MAQABIR NI K**A ZIFUATAZO.
✍️Kuota ndoto za makaburini kila wakati au kuota ukiwa unazika au unazikwa
✍️Hupandwa na hasira za ghafla ambazo hazina sababu zozote
✍️Mtu kupenda sana kukaa akiwa peke yake na hataki maongezi
✍️ Kupenda sana kukaa kwenye giza ima nje au ndani ya nyumba
✍️ Kupenda sana kukaa makaburini kila wakati
✍️Mwili kukak**aa
✍️Kuhisi k**a umefungwa baadhi ya viungo vya mwili k**a miguu na mikono nk
✍️Wakati mwingine mtu hutokwa na mabaka mabaka au malenge lenge mekundu pamoja na kuwashwa
Kuna sababu kadhaa ambazo husababisha hadi jini huyu akivae k**a sio wa kutumwa.Na sababu hizo nitaeleza hapa kwa ufupi k**a ifuatavyo
SABABU AMBAZO HUPELEKEA HADI MAJINNI HAWA WANAMVAA MTU
✍️ Kupenda sana kuwa mchafu kila wakati
✍️Kukosa kufanya ibada
✍️Kupiga miruzi au makelele au kucheka ukiwa makaburini
✍️ Kupenda sana kuongea kwa sauti ya juu hususan nyakati za usiku
✍️ Kuanguka makaburini au kukalia makaburi au kujilaza makaburini
✍️Kukosa kusoma dhikr wakati unapoenda makaburini
✍️ Kutembelea makaburini ukiwa na janaba au hedhi au nifasi
TIBA YA KUMTOA JINNUL MAQABIR
Mgonjwa afanyiwe kisomo cha Ruqya kwa ukamilifu wake kwa siku 45 na pia atakuwa anatumia dawa za kisunna za kula na kufukiza na kunywa.Na awe anajiweka katika hali ya usafi kwa mda huo na kuendelea kwasababu ya kinga zaidi
Kwa wale ambao wanahitaji kufanyiwa kisomo cha Ruqya kutolewa majini wabaya mwilini na hasad na sihr wawasiliane nami kwa namba zifuatazo
✍️+254708995244 Whatsapp
✍️+254756553838 Whatsapp
✍️+254799659791 imo

MFAHAMU JINNIL UMMU MULDAM NA DALILI ZAKE NA TIBA YAKEHawa ni katika majini ambao ni hatari sana wakati wanapowavamia bi...
13/10/2021

MFAHAMU JINNIL UMMU MULDAM NA DALILI ZAKE NA TIBA YAKE
Hawa ni katika majini ambao ni hatari sana wakati wanapowavamia binadamu.Na jinni huyu mara nyingi hutumwa na wachawi kisha akishaingia mwilini hukalia kizazi.Na pia husababisha mwanaume akose hamu ya tendo la ndoa pindi tu afikapo kwa mkewe.dalili za kumfahamu jini huyu ni k**a zifuatazo
DALILI ZA KUMTAMBUA JINNI UMMU MULDAM
✍️Kushikwa ngiri wakati wa joto
✍️Mwanaume kuwahi kushusha manii haraka akiwepo kwenye tendo la ndoa
✍️Uume kusinyaa na kuanza kurudi ndani.na kuwa na baridi k**a kufa ganzi vile
✍️Mwanamke kukosa hedhi kwa miezi mitatu hadi miezi 4 mfululizo
✍️Kushikwa chango linalo zuia mkojo
✍️Mwanamke kuwa na maziwa k**a mja mzito
✍️Kichwa kuuma sana hususan wakati anapofanyiwa kisomo
✍️ Mgonjwa kutetema k**a anahisi baridi na hata kushindwa kuongea
✍️Mwili kuishiwa nguvu na hata kuona giza
✍️Tumbo la kizazi kuuma
Hizo ni dalili kwa uchache tu ijapokuwa kunazo dalili nyingi sana ambazo zinahusishwa na jinni ummul muldami.ifahamike kwamba wakati mgonjwa anapofanyiwa kisomo ni vigumu sana kupanda.ijapokuwa mgonjwa ataumwa na kichwa na maeneo ya kisogoni na halafu hujikuta midomo inatetema na kushindwa kuongea basi anaemfanyia tiba huyu mgonjwa atambue kwamba huyu ni ummu muldam.na ana madhara makubwa sana wakati anapoingia mwilini kwasababu inakuwa vigumu sana kwa mwanamke kupata mimba kwasababu k**a vile nilikuwa nimetangulia kusema ni kuwa huyu jinni hukaa kwenye kizazi kisha huzuia au hata kutoa mimba ambayo mwanamke amepata.jinni huyu humsababishia mwanaume kupata ugumba ijapokuwa kuna namna ya kuweza kumtoa jinni huyu mkorofi.na hapa nitaelezea dawa ambazo hutumika kusaidiana na kisomo cha Ruqya za kisunna k**a ifuatavyo
TIBA YA KISUNNA YA KUMTOA JINNI UMMUL MULDAMI
✍️Seena
✍️Sufa
✍️Khardal
✍️Hulba
✍️Zaatar
MAANDALIZI NA MATUMIZI YA HIZI DAWA NI K**A YAFUATAYO
Chukua dawa zote hizo kisha zichanganye pamoja.Na uhakikishe zoote ni za unga na ziwe kipimo kimoja.yaani grm 200 hadi grm 250 kisha utakuwa unatumia kwenye uji wa ulezi au mtama ambao haujawekwa chochote isipokuwa sukari mawe au Asali.Na utakuwa unatumia mara tatu kwa siku na tiba hii itaendelea kwa siku 45 hadi siku 90 In sha Allah jinni huyu atatoka kabisa
Kwa wale ambao wanahitaji kufanyiwa kisomo cha Ruqya wawasiliane nasi au k**a wanahitaji hizo dawa zikiwa zimeandaliwa tuko nazo na tunaziuza kwa bei ya chini
✍️+254756553838 Whatsapp
✍️+254708995244 Whatsapp
✍️+254799659791 imo
NA PIA TUNAMTUMIA DAWA POPOTE ALIPO MGONJWA

JE JINNI NEBIROS NI NANI?Huyu ni jinni ambaye ana uwezo wa kumshurutisha kufanya uovu mtu yeyote amtakaye na pia ana uwe...
10/10/2021

JE JINNI NEBIROS NI NANI?
Huyu ni jinni ambaye ana uwezo wa kumshurutisha kufanya uovu mtu yeyote amtakaye na pia ana uwezo wa kumletea mtu fahari kuu na pia jinni huyu ana uwezo wa kumuonesha mtu vitu bora k**a madini na mawe na mboga na wanyama.Ana uwezo wa kutabiri vitu ambavyo vitatokea kwasababu ndiye mkuu wa utabiri katika ulimwengu wa kijinni.Anazunguka zunguka huko na huko kila Sehemu kwa ajili ya kuangalia, kuchunguza na kukagua aina zote za maangamizi.Ana wasaidizi 3 ambao ni Ayperos na Haberus na Glassyalabolas.Jinni Nebiros yuko namba 24 katika orodha ya majini 72 aliokuwa akiwamiliki nabii suleyman as kwa kuwaamrisha kumfanyia kazi mbalimbali,Na jinni huyu hufahamika k**a inspekta jenerali wa jeshi katika Utawala wa iblis laana za Allah ziwe juu yake.Ana vichwa vitatu na sura k**a ya mbwa halafu ana miguu mitatu.hawa ni katika majini ambao ni viongozi ambao ni hatari sana kwa binadamu.
Kwa wale ambao wanaosumbuliwa na majini wabaya na sihr na Hasad tunayatoa matatizo hayo kwa visomo vya Ruqya na tunayatibu kwa madawa ya kisunna.na pia tunatibu maradhi mbalimbali
Kwa matibabu wasiliana nami kwa namba zifuatazo
✍️+254708995244 Whatsapp
✍️+254756553838 Whatsapp
✍️+254799659791 imo
Tunasafirisha dawa Sehemu yeyote alipo mgonjwa kwasababu uaminifu ndo ngao yetu

MFAHAMU JINNI SUBIANI NA TIBA YAKEAsalam alaykum warahmatullahi wabarakatu,Leo nataka nielezee ni nani jinni subiani.ifa...
10/10/2021

MFAHAMU JINNI SUBIANI NA TIBA YAKE
Asalam alaykum warahmatullahi wabarakatu,Leo nataka nielezee ni nani jinni subiani.ifahamike kwamba kuna tofauti kubwa sana kati ya jinni subiani na jinni ummu subiani na jinni Abuw subiani.Na majini hawa huwashinda walimu wengi sana kuwatoa kwasababu wana tabia ya kubadilika.ifahamike kwamba majini aina zote 660 wamegawanyika Sehemu 2.
1Kuna majini wazuri ambao ndo Maruhani
2,Na kuna majini wabaya ambao ndo mashetani
Majini hawa ni hatari sana kwa binadamu na wana dalili nyingi sana za kuweza kuwatambua nazo nitazielezea hapa k**a ifuatavyo
DALILI ZA SUBIANI
✍️Kuishiwa damu kila mara
✍️ Kuota ukiwa unafanya kitendo cha ndoa
✍️Kuwa na hasira za ovyo za mara kwa mara
✍️Kukosa nguvu za kiume
✍️Kuota ukiwa una mimba
✍️Kuchakaa wakati bado wewe ni kijana
✍️Kuambiwa na watu kwamba wewe ni mchawi
✍️Kuota ndoto ukiwa unazaa na unanyonyesha
✍️ Kuota ndoto ukiwa unabeba mtoto
✍️Mimba kutoka hasa ikiwa na miezi 3 hadi 8
✍️Kuumwa chango au ngiri mara kwa mara
✍️Kushindwa kumwaga manii ufikapo kileleni
✍️Kukosa hedhi
✍️Kuingia na kumwaga manii kwa haraka zaidi
✍️ Kupata hedhi kwa miezi 2 hadi 3
✍️Tumbo kuhisi joto
✍️Kutembea vitu mwilini
✍️Maradhi yasiyoisha ya mara kwa mara
✍️Wakati jinni huyu anapanda anakuwaga na fujo sana
✍️Mgonjwa huwa anagaa gaa wakati huyu jinni anapanda
✍️Hulia wakati mwingine na kupiga kelele
✍️Ni mkali sana na ana nguvu sana anaweza akshikwa na watu hadi 10 lakini lazima awatikise tu
✍️ Anaweza akafanya mtu kuwa k**a kichaa
✍️Majini hawa taaluma yao ya asili ni uganga.kwa hivyo hata akipanda anaweza akajifanya anafanya uganga.**Na hapa ndipo nilisema kwamba tabibu ambaye anafanyia mgonjwa kisomo lazima ambainishe k**a ni mkweli au ni muongo jambo ambalo sio kila mtu anaweza akalifanya
✍️Pia humuotesha mgonjwa akiwa porini akimfundisha miti ya dawa
✍️Ndoto zake nyingi ni za kula kula ovyoovyo
✍️Kuumwa kila wakati haswa ganzi na vichomi
✍️Mwili kuwaka moto na kukosa hamu ya chakula
✍️Mke kukataa tendo la ndoa
✍️Jinni huyu hutoa mimba kuanzia miezi 3 hadi 8
TIBA YA TATIZO HILI
✍️Mafuta ya figiri
✍️Mafuta ya kitunguu thawm
✍️Mafuta ya kitunguu maji
✍️Mafuta ya ngamia
✍️Mafuta ya nyangumi
✍️Mafuta ya ndimu
✍️Mafuta ya mchaichai
Kwa wale ambao wanahitaji kufanyiwa visomo vya Ruqya na wanahitaji dawa hizo zikiwa zimekamilika wawasiliane nasi kwa namba zifuatazo
✍️+254756553838 Whatsapp
✍️+254708995244 Whatsapp
✍️+254799659791 imo
Pia tunamtumia mtu pahali alipo na zitamfikia salama kwasababu uaminifu ndo ngao yetu

Address

Imara Daima
Nairobi South

Telephone

+254799659791

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tahta shajara Herbalist &jinni Research Center posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Tahta shajara Herbalist &jinni Research Center:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram