Dk.sule natural therapy

Dk.sule natural therapy tunatoa ushauri na tiba asilia

19/05/2022

Tiba ya kwikwi
Tiba ya Kwikwi
Habari ndugu yangu. Karibu Tiba asili, Kupitia post hii leo utajifunza tiba ya Kwikwi,
Kwikwi ni kitu gani?
Kwikwi (Kekefu) ni hali ya kushtuka na kusinyaa kwa ghafla kwa misuli mikuu ya upumuaji (diaphragm) ambako hujirudia rudia na kusababisha hewa kuingia kwa kasi kwenye mapafu. Hali Hii husababisha milango ya sauti katika koo (vocal cords or voice making cords) kufunga ghafla na kutoa sauti inayosikika wakati wa kwikwi. Kwikwi sio ugonjwa, kwikwi ni ya muda mfupi ambayo inapita, lakini kwikwi isiyokatika inaweza kuwa dalili ya tatizo lingine ambalo huenda likahitaji uchunguzi wa kitaalamu.
Sababu zinazopelekea tatizo la kwikwi
Kula haraka haraka au kula sana (kuvimbiwa)
Kula vyakula vyenye viungo sana (very spicy foods)
Kunywa vinywaji vyenye gesi(carbonated beverages) au vya baridi sana
Ulevi au kunywa pombe nyingi kwa mpigo
Upungufu wa maji na madini mwilini (dehydration)
Tumbo kujaa gesi, asidi (hyperacidity) au vidonda vya tumbo
Tiba ya kwikwi kwa kutumia kitunguu maji (anion):
Kitunguu maji(anion) ni Mujarrab sana kwa magonjwa mengi likiweo tatizo la kwikwi. Tiba ya kwikwi kupitia kitunguu maji ni k**a ifuatavyo:
Kata kata kisha ponda kitunguu maji kutumia kinu, blender, au chochote kile hadi kipondeke vizuri.
Weka chumvi na maji machache kisha changanya vizuri
Kamua na kisha chuja mchanganyiko wako upate juisi.
Weka kwenye Chombo safi kisha kunywa utapata matokeo mazuri hapo hapo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.
Tiba hii ni Mujarrabu sana hata kwa kwikwi ya aina gani. Kwa taaluma zinazohusu tiba kwa njia asili, endelea kufuatilia mada zetu pia usisahau kuwashirikisha wengine ili nao wapate faida hii,kwa kubonyeza vitufe vya mitandao ya kijamii hapo pembeni au chini. Pia Blog yetu inazo dawa za asili zenye ubora na tunasarisha kote Tanzania, bei zake ni nafuu na zina matokeo mazuri sana.

KISONONO NA DALILI ZAKE.Kisonono mara nyingi haisababishi dalili zozote. Wote wanaume na wanawake wanaweza kuwa na maumi...
14/05/2022

KISONONO NA DALILI ZAKE.
Kisonono mara nyingi haisababishi dalili zozote. Wote wanaume na wanawake wanaweza kuwa na maumivu k**a ya kuungua wakati wa kukojoa. Wanaume wanaweza kuwa na uchafu mweupe au wa njano unaotoka kwenye uume, maumivu wakati wa kumwaga manii au korodani iliyovimba. Wanawake wanaweza kuwa na uchafu mweupe au wa njano unaotoka kwenye uke, kutokwa damu ukeni baada ya kujamiiana au katikati ya vipindi vya hedhi na maumivu kwenye sehemu ya chini ya tumbo.
Ikiwa kuna maambukizi ya kisonono kwenye sehemu nyingine za mwili, dalili zinaweza kujumuisha koo kuuma, maumivu wakati wa kupata haja kubwa au uchafu kutoka kwenye njia ya haja kubwa. Ikiwa mtoto mchanga anapata maambukizi haya kutoka kwa mama yake wakati wa kuzaliwa, anaweza kuwa na maambukizi ya jicho (kikope) au maambukizi ya koo.
Vihatarishi vya ugonjwa wa kisonono
Kisonono mara nyingi husambazwa kwa njia ya kujamiiana bila kutumia kinga na mtu aliyeambukizwa. Pia, inawezekana kwa mtoto mchanga kupata ugonjwa huu kutoka kwa mama yake wakati wa kuzaliwa.
Watu wenye umri kati ya miaka 15 na 35 wana uwezekano mkubwa wa kupata kisonono. Imeandaliwa na dkt.sule natural therapy herbal

ASSALAAM A'ALAYKUMU WARAHMATULLAH WABARAKAATUH.leo wapendwa tutazungumzia kisonono.Kisonono ni nini?Kisonono ni maambuki...
12/05/2022

ASSALAAM A'ALAYKUMU WARAHMATULLAH WABARAKAATUH.leo wapendwa tutazungumzia kisonono.Kisonono ni nini?
Kisonono ni maambukizi ya bakteria wanaosambazwa kwa njia ya ngono na bakteria anayeitwa Neisseria gonorrhoeae. Hali hii wakati mwingine huitwa 'the clap'. Hii ni hali ya kawaida. Kisonono mara nyingi huambukiza urethra (mrija kati ya kibofu cha mkojo na ngozi) pamoja na shingo ya kizazi kwa wanawake.
Dalili za kawaida ni maumivu wakati wa kukojoa na uchafu kutoka kwenye mrija wa mkojo. Watu wengi wenye kisonono hawana dalili, na hugunduliwa kuwa na hali hii kwa vipimo vya uchunguzi (kupima watu ambao hawana dalili).
Kisonono hutibiwa kwa antibiotiki. Mpenzi wako lazima pia atibiwe. Hali hii ikitibiwa katika hatua za mwanzo, watu wengi hupona vizuri na huwa hawana matatizo endelevu. Maambukizi yasiyotibiwa yanaweza kusababisha madhara, ikiwa ni pamoja na utasa.. Itaendelea kesho dalili zake n.k

 #1Mafuta ya MISKI Yatokanayo na Mnyama AL GHAZALIFAIDA ZA MNYAMA AL GHAZALI:1.Faida ya kwanza ya mnyama huyu ni nyama2....
11/05/2022

#1
Mafuta ya MISKI Yatokanayo na Mnyama AL GHAZALI

FAIDA ZA MNYAMA AL GHAZALI:
1.Faida ya kwanza ya mnyama huyu ni nyama
2.Faida ya pili hutoa mafuta ya misk

Sasa basi leo tutazungumzia juu ya faida na matumizi ya misk

FAIDA NA MATUMIZI YA MISKI:
Hali yake ina ujoto na uyabisi katika daraja la pili. Ina ladha na harufu tofauti na mafuta mengine mazuri. Inatokana na mnyama anaeitwa kwa kiarabu AL GHAZALI.

Namna ya kutofautisha Misk halisi na feki ni kwa kuonja ladha yake na kunusa harufu yake. Pia njia nyingine ni kwa kusomea aya za Ruqya kwenye misk halisi halafu ajipake mwenye matatizo ya majini, italeta athari na k**a ni misk feki haiwezi kuleta athari.

Vile vile misk feki haiwezi kutibu maradhi ya kimwili k**a vile maradhi ya ngozi.

MATUMIZI YA MISK KATIKA TIBA:
1) UBONGO NA MISHIPA YA FAHAMU: Kuna tiba iitwayo kitaalamu Aromatherapy. Maana yake ni kupata dawa kwa njia ya kunusa au kupata harufu yake k**a vile kufukiza udi, misk huchangamsha ubongo na kuipa nguvu mishipa ya fahamu.

Utakuwa unanusa misk mara kwa mara au upate mvuke wake. Kwa kupata mvuke wake chukua bakuli halafu uweke ndani yake maji ya moto yaliyochemka halafu uweke ndani yake matone kadhaa ya misk. Sogeza bakuli karibu ya usoni mwako ili upate kuvuta mvuke wake.

Hali k**a hii, mvuke wa misk utakuingia kupitia puani au mdomoni. Tiba hii inaitwa Aromatherapy. Ni nzuri kwa watu wenye kifafa, dege dege, kuumwa na kichwa, kizunguzungu, kutopata usingizi na kuondosha kichefuchefu. Pia huongeza kumbu kumbu.

2) RHEUMATISM: Ni dawa ya kuondosha maumivu ya miguu, ganzi na viungo. Ule ujoto wa misk huondosha maumivu ya mishipa, viungo, miguu, mgongo na kiuno.

3) MZUNGUKO WA DAMU: Husaidia mzunguko wa damu na kuondosha presha.

4)Kwa mwanamke inazidisha hisia na hamu ya tendo la ndoa. Pia ukipaka katika uke huufanya uke kubana k**a vile bado bikra

5) HUONDOSHA HARUFU MBAYA: Kwa kuondosha harufu mbaya sehemu za siri (nyeti),makwapani au miguuni, jipake misk.

6) FANGASI SEHEMU ZA SIRI: Huondosha sehemu za siri mwashowasho na mapele.

MATUMIZI YA MISK KWA KUMDHOOFISHA AU KUMFUKUZA JINI WA MAHABA:
Kwanza kabisa misk isomewe aya za Ruqya, kisha mgonjwa mwenyewe ajipake kila siku asubuhi na jioni viungo 32 vya mwili wake.

-Tundu mbili za pua.
-Tundu mbili za masikio.
-Kope mbili za macho.
-Mdomoni k**a vile mfano wa lipstiki.
-Chuchu mbili (mwanamke anaenyonyesha asipake)
-Sehemu za siri mbele na nyuma.
-Kitovuni.
-Mbele mwa kucha zote za vidole 20 vya mikono na miguu.

JE UNAPENDA KUONGEZA UWEZO WAKO WA KUMBUKUMBU?
Mafuta ya Misk hufungua mishipa ya fahamu na ubongo kwa kiwango kikubwa sana na kuupa ubongo uwezo mkubwa wa kufikiri.

Kwa maelezo ya jinsi ya kutumia na uchanganyaji tuwasiliane Insha allah tutasaidiana. nitumie meseji INBOX nitakujibu au whatsapp namba +255788333946 imeandaliwa na dkt.sule natural therapy.

Assalaam alaykum warahmatullah wabarakaatuh pia mnakaribishwa kulike account yatu ya facebook
11/05/2022

Assalaam alaykum warahmatullah wabarakaatuh pia mnakaribishwa kulike account yatu ya facebook

tunatoa ushauri na tiba asilia

Address

Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dk.sule natural therapy posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Dk.sule natural therapy:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram