18/06/2025
Tafakari
Utumiaji wa bangi huongeza hatari maradufu ya kufa kutokana na ugonjwa wa moyo, kwa mujibu wa uchambuzi mpya wa utafiti wa kitabibu uliyohusisha watu milioni 200 wengi wao wakiwa kati ya umri wa miaka 19 na 59.
Mwandishi mkuu wa utafiti huo Émilie Jouanjus, profesa mshiriki wa famasia katika Chuo Kikuu cha Toulouse, Ufaransa anasema "Kilichoshangaza zaidi ni kwamba wagonjwa waliohusika waliolazwa hospitalini kwa shida hizi walikuwa bado vijana na bila historia ya ugonjwa wa moyo na mishipa au kutumia tumbaku."
Na kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa Jumanne kwenye jarida la Moyo (The journal Heart) ni kwamba ikilinganishwa na wasiotumia bangi na wale waliotumia pia walikuwa na hatari kubwa ya asilimia 29 ya mshtuko wa moyo na hatari kubwa ya asilimia 20 ya kufikwa na kiharusi.
Dokta Lynn Silver, profesa katika sekta ya tiba kutoka Chuo Kikuu cha California, San Francisco anasema "Hii ni moja ya tafiti kubwa zaidi hadi sasa juu ya uhusiano kati ya bangi na ugonjwa wa moyo, na inazua maswali mazito juu ya dhana kwamba bangi inachagiza hatari ndogo ya moyo na mishipa."
Utafiti huo haukuwauliza watu jinsi walivyotumia bangi k**a vile kuvuta sigara, kunyunyiza na kutumia k**a chakula, lakini hata hivyo kulingana na data zinaonesha kuna uwezekano kwamba bangi ilitumika kwa namna ya kuvutwa katika visa vingi. Utafiti unapingwa na utafiti lakini bado una nafasi ya kutoa maoni yako.