09/11/2025
H. PYLORI NA VIDONDA VYA
TUMBO
H. Pylori (Helicobacter Pylori) ni aina ya bakteria wanaopatikana tumboni mwa binaadamu, Bakteria hawa wanaweza kuuishi kwenye ute wa tumbo na kusababisha maambukizi yanayoweza kupelekea vidonda vya tumbo (peptic ulcers) na hata saratani ya tumbo kwa baadhi ya watu.
Dalili ya Maambukizi ya H.pyroli
Dalili za maambukizi ya H. Pylori zinaweza kutofautiana kati ya watu na wengine huweza kuwa na maambukizi bila kuonyesha dalili za kawaida ni pamoja na ;
Dalili kuu za H. pyroli.
1) Maumivu ya tumbo - Hasa unapokuwa na njaa au kati ya mlo
2) Kuhisi kiungulia - Hisia ya moto kwenye kifua au koo.
3) Kichefuchefu - wakati mwingine kunaweza kuwa na kutapika.
4) Kuvimba tumbo - Hisia ya kushiba haraka au tumbo kujaa gesi.
5) Kupungua uzito bila sababu - Kutokana na kupungua hamu ya kula .
6) Kukosa hamu ya kula -Unaweza kujisikia kutopenda kula.
7) Kinyesi Cheusi au kilicho na damu - Inaweza kuwa ni ishara ya vidonda vya tumbo.
Athari za H. Pylori
Maambukizi ya H. Prolific yanaweza kuwa na athari mbalimbali mwilini, hasa ikiwa hayatatibiwa kwa muda mrefu, Athari zake ni zinaweze kuwa za kawaida au mbaya zaidi, kulingana na kiwango cha maambukizi.
Athari za H. Pyroli
i) Vidonda vya tumbo Peptic Ulcers.
~ h.pyroli huharibu utando wa kinga na tumbo na utumbo mdogo hivyo kuruhusu asidi ya tumbo kudhuru kuta za tumbo na kusababisha vidonda.
- dalili: maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kiungulia na kutapika.
ii) Kuvimba kwa Tumbo (Gastritis)
~Bakteria hawa huweza kusababisha kuvimba kwa kuta za tumbo, hali inayojulikana k**a Gastritis.
- dalili: maumivu makali ya tumbo, kichefuchefu na hisia ya tumbo kujaa haraka.
iii) SARATANI ya tumbo (Stomach Cancer).
~maambukizi ya muda mrefu yanaweza kuongeza hatari ya kupata saratani ya tumbo hasa ikiwa kuna vidonda vya muda mrefu Gastritis sugu.
-dalili: Dalili za awali za saratani ya tumbo ni pamoja na kupungua uzito bila sababu, kukosa hamu ya kula, na maumivu ya tumbo yasiyo isha.
(iv) Upungufu wa damu (Anemia) ya upungufu wa chuma.
~H.pyroli inaweza kusababisha kutokwa na damu pole pole tumboni jambo linaloweza kusababisha Anaemia.
- dalili: uchovu mwingi, udhaifu ngozi kuwa na rangi hafifu (pale)
(V) Kudhoofisha kinga ya mwili.
Maambukizi ya muda mrefu yanaweza kuchochea mwili kutoa kemikali za vichocheo, ambazo zinaweza kudhoofisha kinga na kusababisha magonjwa mengine ya mfumo wa chakula.
Tutakusaidia kupata suluhisho la kudumu kuondoa H.Pyroli, Minyoo sugu walioshindikana, kutibu vidonda vya tumbo kikamilifu ,matatizo ya gesi tumboni.
Kwa mawasiliano wasiliana nami kwa
0765 163 943
Whatsapp tupo Daresalaam, utapata huduma mkoa wowote Tanzania na nchi jiraani delivery kwa daresalaam ipo.