16/10/2025
MAFUNZO YA SANAA KWA MAENDELEO YA VIJANA – MBEYA 2025
Katika kuadhimisha Wiki ya Vijana Kitaifa Tanzania 2025, Taasisi ya Kaa Kijanja, kwa kushirikiana na DSW Tanzania pamoja na Sekretarieti ya Mkoa wa Mbeya, iliandaa mafunzo kwa vijana wasanii 20 mkoa wa Mbeya, kuwawezesha kutumia sanaa na ubunifu kuwasilisha jumbe chanya kuhusu kupinga ukatili wa kijinsia (UWAKI), afya, na stadi za maisha kwa vijana.
Mafunzo yalifunguliwa rasmi tarehe 06 Oktoba 2025 na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya, Bi. Elukaga Mwalukasa, ambaye aliongoza warsha kuhusu kupinga ukatili wa kijinsia na kueleza namna wasanii na wabunifu wanavyoweza kuchangia katika utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA II 2024/25–2028/29).
Dkt. Mariam Mhanjim kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya alitoa mafunzo kuhusu huduma rafiki kwa vijana, afya ya uzazi, na stadi za maisha, huku
Dkt. Reinfridy Chombo (Hospitali ya Rufaa ya Mbeya) akiongoza mafunzo kuhusu afya ya akili kwa vijana, hasa wasanii.
Dkt. Chombo alisisitiza umuhimu wa vijana kudhibiti changamoto za maisha, kufanya kazi kwa bidii, na kuchangia katika maendeleo ya familia, jamii, na uchumi wa taifa.
Mratibu wa Vijana Mkoa wa Mbeya, Ndg. Francis Ngelela, aliwahimiza vijana kuendelea kuwa vielelezo vizuri kwenye jamii na kutumia sanaa zao kupinga mila kandamizi na tamaduni potofu zinazokwamisha maendeleo ya vijana.
Mafunzo yalifungwa rasmi na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Mbeya (Mratibu Msaidizi wa Polisi), ASP Veronica Ponera, aliyesisitiza umuhimu wa sanaa k**a chombo cha mabadiliko chanya katika jamii, hasa katika kutoa elimu na kukemea vitendo vya ukatili na unyanyasaji katika jamii.
Washiriki wote walipokea vyeti vya ushiriki na kutambuliwa rasmi k**a Vinara wa Mradi wa REST na Kampeni ya Kaa Kijanja 2025.
Mafunzo haya ni muendeleo wa utekelezaji wa mradi wa Reproductive Equity Strategic in Tanzania (REST II) wenye lengo la kujengea uwezo Vijana na taasisi za vijana kufikia malengo yao.