Tras Medical Laboratories Tz

Tras Medical Laboratories Tz Kwa vipimo vya Maabara | tunakupatia majibu ya uhakika na katika ubora wa hali ya juu | Gharama naf

MFUMO KINGA IMARA NI MUHIMU SANA.🔵Hizi ni baadhi ya hatua unazoweza kufanya boresha kinga yako ya mwili :1️⃣Hakikisha un...
18/03/2020

MFUMO KINGA IMARA NI MUHIMU SANA.

🔵Hizi ni baadhi ya hatua unazoweza kufanya boresha kinga yako ya mwili :

1️⃣Hakikisha unapata usingizi wa kutosha
-Ukosefu wa usingizi Hufanya kinga ya mwili kuwa dhaifu

2️⃣Fanya Mazoezi.

3️⃣Jitahidi kupunguza mkazo wa mawazo na stress
4️⃣Kama ni mlevi, punguza kiwango cha pombe unazokunywa

5️⃣Kula lishe bora yenye mbogamboga na matunda mengi
- Upungufu wa virutubisho k**a zinc, selenium, iron, copper, folic acid, vitamins A, B6, C, na E huathiri namna mwili unavyopambana na vimelea

17/03/2020
Fahamu kuhusu virusi vya Corona na ugonjwa wa COVID-19Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyosababisha maradhi kwa wanya...
17/03/2020

Fahamu kuhusu virusi vya Corona na ugonjwa wa COVID-19

Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyosababisha maradhi kwa wanyama na binadamu. Kwa binadamu, jamii kadhaa za virusi vya Corona vinafahamika kusababisha maambukizi kwenye njia ya hewa na mfumo wa upumuaji. Maradhi yaliyowahi kusababisha madhara makubwa kutokana na virusi vya Corona ni pamoja na MERS na SARS yaliyozuka mwanzoni mwa miaka ya 2000. Kirusi cha Corona kilichogundulika hivi karibuni kinasababisha ugonjwa unaofahamika k**a COVID-19.

COVID-19 ni nini?

COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona. Virusi hivyo vipya havikuwa vikifahamika hapo kabla na sayansi ya tiba. Na vilianzia nchini China mwezi Disemba mwaka 2019.

Dalili za Corona ni zipi?

Dalili kuu za Corona ni pamoja na Homa kali, Uchovu na Kikohozi kikavu na zinatokea taratibu. Dalili kubwa na inayoweza kutia hofu, ni mtu kukosa pumzi. Lakini isikutishe, ni mtu 1 pekee kati ya watu 6 walioambukizwa virusi vya Corona hufikia dalili hiyo ya hatari. Na asilimia 80 ya walio na virusi hivyo hupata nafuu bila kuhitaji msaada wa matibabu.

Makundi yaliyo kwenye hatari zaidi ni yapi?

WHO inasema wazee na watu wenye magonjwa ya kudumu k**a Shinikizo la Damu, Kisukari, Matatizo ya Figo ndiyo walio kwenye hatari zaidi ya kuathika pindi wanapopatwa na virusi vya Corona. Watu wa umri wa wastani na wenye afya imara wanaweza kupata virusi vya Corona na kupona bila kuhitaji matibabu.

Virusi vya Corona vinasambaa vipi?

Watu wanaweza kupata Virusi vya Corona kutoka kwa watu walioambukizwa. Virusi vinaweza kusambaa kupitia maji maji kutoka kwenye pua au mdomo wa aliyeathirika. Iwapo mtu anagusa maji maji k**a mafua, mate na makohozi ya mtu aliye na virusi na kisha kujigusa mdomo, macho na pua anaweza kupata virusi vya Corona.

Ninaweza kujikinga vipi na Virusi vya Corona?

Nawa vizuri na kila wakati mikono yako kwa maji ya vuguvugu, sabuni au dawa za kuua vijijidudu kwa angalau sekunde 20.
Kaa umbali wa angalau hatua mbili (2) kutoka mtu anayepiga chafya au kukohoa.
Epuka kushika macho, pua na mdomo kwa mikono isiyo safi kwa sababu mikono hushika sehemu nyingi na ni rahisi kubeba vimelea vya maradhi.
Hakikisha wewe, na walio karibu yako wanazingatia ustaarabu wa kuzuia pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya.
Baki nyumbani ikiwa hujisikii vizuri. Iwapo una mafua makali, homa, kikohozi na kushindwa kuhema nenda hospitali kwa sababu huko wataalamu watakupatia msaada muhimu
Epuka kuwa sehemu yenye msongamano, k**a vyombo vya usafiri, maduka na maeneo yenye yenye mgandamizo wa hewa.
Fuatilia taarifa za afya na matangazo yake kuhusu virusi vya Corona.

Kwanini watu wanawekwa karantini?

Kwa ufupi neno Karantini linamaanisha kuwa chini ya uangalizi. Watu wenye dalili au wanaotokea maeneo yenye maambukizi makubwa ya virusi vya Corona hulazimikwa kuwekwa karantini (kutengwa na watu wengine) ili kufuatilia afya yao kwa karibu na kuzuia kueneza virusi. Ukiambiwa unapaswa kuwekwa Karantini, usiogope. Ni kwa ajili ya afya yako na wengine.

Virusi vya Corona vina tiba?

Hadi sasa hakuna tiba au chanjo dhidi ya virusi vya Corona lakini kwa sababu virusi hivyo vinaleta dalili mfano wa zile za mafua makali, mchanganyiko wa tiba unatumika kupunguza athari za virusi vya Corona.

Ninapaswa kuwa na hofu?

Hapana. Hupaswi kuogopa wala kuwa na hofu. Bali unapaswa kuchukua tahadhari. Kila mtu duniani yuko kwenye uwezekano wa kupata virusi vya Corona lakini k**a tulivyokufahamisha, athari zake bado hazitishi.

Ni kweli watu weusi hawawezi kupata Corona?

Hapana, k**a ilivyo kwa watu wa rangi na jamii zote sisi watu weusi pia tunaweza kuambukizwa virusi vya Corona. Mfano ni mgonjwa aliyegundulika Kenya.

Zingatia haya
17/03/2020

Zingatia haya

Usifwate Mkumbo
17/03/2020

Usifwate Mkumbo

☆KISUKARI Fika kituo cha afya kilicho karibu na wewe k**a unapata dalili hizi zifuatazoDALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI.🍁 K...
13/03/2020

☆KISUKARI
Fika kituo cha afya kilicho karibu na wewe k**a unapata dalili hizi zifuatazo

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI.

🍁 Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.

🍁 Kwenda haja ndogo mara kwa mara. Watoto kukojoa kitandani.

🍁 Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.

🍁 Kupungua uzito au kukonda licha ya kula vizuri.

🍁 Kusikia njaa kila wakati na kula sana.

🍁 Wanawake kuwashwa ukeni.

🍁 Kutoona vizuri.

🍁 Kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake.

🍁 Ganzi, kuchomwa chomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole.

🍁 Miguu kuoza na hata kupata gangrini

🍁 Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ganzi katika miguu.

🍁 Vidonda au majeraha kutopona haraka sehemu yoyote mwilini.

🍁 Majipu mwilini.

Wenye dalili hizi wanashauriwa kupima sukari ili kubaini k**a wana kisukari.

U.T.IFika kituo cha afya kilicho karibu na wewe mara uonapo dalili hizi za UTIDalili za UTI huwa k**a ifuatavyo:1. Kusik...
10/03/2020

U.T.I
Fika kituo cha afya kilicho karibu na wewe mara uonapo dalili hizi za UTI

Dalili za UTI huwa k**a ifuatavyo:
1. Kusikia maumivu wakati wa kukojoa.
2. Kuhisi homa
3. Kuhisi uhitaji wa kukojoa mara Kwa mara na pia mkojo kuwa na hali ya kuunguza wakati wa kukojoa
4. Kuhisi maumivu ya tumbo chini ya kitovu au mgongo.
5. Mkojo kuonekana kuwa wenye rangi ya damu au usaha.
6. Kutokwa na uchafu wenye harufu sehemu za siri, hasa tatizo hili linapokuwa la muda mrefu.

MAABARA YA AFYA:-TUPO :- SANAWARI SOKONI/ SOKO LA JUU Kwa vipimo vya uhakika, ubora na Gharama  nafuu
09/03/2020

MAABARA YA AFYA:-
TUPO :- SANAWARI SOKONI/ SOKO LA JUU
Kwa vipimo vya uhakika, ubora na Gharama nafuu

Maabara ya AfyaTupo:- Sanawari sokoni juuKaribu tukuhudumie
08/03/2020

Maabara ya Afya
Tupo:- Sanawari sokoni juu

Karibu tukuhudumie

Ofa bado inaendelea kwa waliopo Arusha
25/06/2019

Ofa bado inaendelea kwa waliopo Arusha

Karibu tukuhudumie, usipitwe na hili kwa wewe uliopo Arusha
24/06/2019

Karibu tukuhudumie, usipitwe na hili kwa wewe uliopo Arusha

Address

Sanawari Sokoni Juuu, Karibu Na Ofisi Ya Mtendaji
Arusha

Opening Hours

Monday 08:00 - 20:00
Tuesday 08:00 - 20:00
Wednesday 08:00 - 20:00
Thursday 08:00 - 20:00
Friday 08:00 - 20:00
Saturday 08:00 - 20:00
Sunday 11:00 - 17:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tras Medical Laboratories Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram