24/10/2025
*HATARI YA KUPUNGUZA UZITO HARAKA KUPITA KIASI.*
Katika dunia ya leo yenye presha ya "mwili model", watu wengi wamekumbatia mbinu za kupunguza uzito haraka k**a suluhisho la maumivu yao ya kisaikolojia, kujithamini au hata kujiamini. Lakini je, unajua kuwa kupungua uzito mwingi ndani ya muda mfupi si mafanikio, bali inaweza kuwa mwaliko wa magonjwa?
Leo nataka nikuambie ukweli ambao wengi hawausikii vizuri, kupunguza uzito haraka sana ni hatari kwa afya yako. Ndiyo, unaweza kuonekana umekonda, lakini ndani ya mwili wako kuna sehemu inalia kimya kimya.
1. Unapoteza Misuli, Si Mafuta Pekee.
Uzito unaposhuka kwa kasi, mwili huanza kutumia misuli k**a chanzo cha nishati badala ya mafuta. Mwisho wa siku unakuwa dhaifu zaidi.
2. Mapigo ya Moyo Yanaweza Kuvurugika.
Lishe duni ya haraka sana, hasa zile zenye nishati kidogo kupita kiasi, huathiri kazi ya moyo. Hali hii inaweza kupelekea mapigo yasiyo ya kawaida na hiyo ni hatari ya kimya inayonyemelea maisha yako.
3. Matatizo ya Homoni na Hedhi Kuvurugika.
Kwa wanawake, kupungua uzito kwa kasi kunaweza kuathiri mzunguko wa hedhi. Homoni huingia kwenye taharuki, na unaweza kupoteza mzunguko wako kwa miezi au zaidi.
4. Ngozi Kudondoka na Kukunjamana.
Uzito unapopungua ghafla, ngozi haina muda wa kujibana taratibu. Matokeo yake ni ngozi kuachia na kuonekana “legelege”.
5. Kupungua kwa Kinga ya Mwili
Mwili unaponyimwa virutubisho vya msingi kutokana na lishe ya haraka, kinga ya mwili hushuka. Magonjwa madogo yanakuwa makubwa, na maambukizi yanakuwa ya kawaida k**a salamu za asubuhi.
6. Kurudi kwa Uzito Kwa Kasi (Yo-yo Effect).
Mwili una kumbukumbu. Unapounyima chakula sana, unahifadhi mafuta kwa woga wa njaa nyingine. Na ukirejea kula kawaida, unanenepa tena kwa kasi kuliko ulivyopungua.
Ushauri 1.🩷💯
TUMIA DAWA HII YA MANEMANE IWEZE kukupunguza tumbo, uzito,kitambi mafuta machafu na wakati huo ukitoa sumu za MAGONJWA nyemelezi bila kuleta athari hizo hapo juu.
Ushauri.2♨️
K**a kweli unataka kupunguza uzito, fanya hivyo taratibu. Punguza kilo 0.5 – 1 tu kwa wiki. Chagua kula vizuri, fanya mazoezi mara kwa mara, na upe mwili wako muda wa kubadilika. Mwili si nguo ya kubadilisha wikiendi, ni makazi yako ya maisha.
Mwisho wa siku, uzuri ni afya. Usiuuze afya yako kwa muonekano wa haraka.
Safiri na mwili wako kwa subira, na utakufikisha kule unapotaka ukiwa salama.
Mimi PrayGod
Mr MANEMANE. Smart MAASAI
Maswali,maoni, ushauri na huduma ya tiba ya Kimaasai na lishe.
0764628888
0655181127
0683181127
Jiunge na group la Tiba asilia ya Kimaasai ili ujifunze mambo mbalimbali kuhusu afya yako kwa kubonyeza Link hapo chini