30/09/2025
K U J I K U B A L I (ACCEPTANCE):
Wiz Khalifa, amethibitisha rasmi kuacha kunywa pombe kabisa. Kupitia ujumbe wake, rapa huyo alisema:
โNilikwisha kuacha kunywa pombe kabla na sasa naweza kusema tena kwamba hakuna pombe yoyote itakayoweza kuingia mwilini mwangu kamwe.โ
Wiz Khalifa ameeleza kuwa hata alipobakiza kunywa kinywaji kimoja tu kwa wiki, mwili wake haukushindwa kuhimili. Alisema:
โNimepunguza hadi kinywaji kimoja kwa wiki lakini mwili wangu hauwezi hata kushughulikia hicho tena. Hangovers zinahisi k**a milango ya mbinguni inafunguka na hiyo haifai kwa starehe ya muda mfupi.โ
Aidha, rapa huyo aliongeza kuwa kunywa pombe hakukuleta furaha ya kweli:
โZaidi ya yote, si starehe hata kidogo. Yote ninayofanya ni kusema maneno yasiyo na maana na kulala kwenye kochi nikiwa nimevaa nguo zote. Niko sawa. Imatosha.โ
Kwa mujbu wa maneno yake, sasa Wiz Khalifa anafurahia afya yake akiwa mbali na pombe.