15/10/2025
JE UMEHANGAIKA KUPATA UJAUZITO BILA MAFANIKIO NA UNAHISI KUKATA TAMAA??
Suala la kupata ujauzito limekuwa changamoto kubwa sana kwa miaka ya hivi karibuni na kadri siku zinavyoenda ndivyo jinsi ambavyo tatizo hili linazidi kukithiri,Ushawahi kujiuliza ni kwanini??zifuatazo ni baadhi ya sababu:
๐ SABABU ZA KIBIOLOJIA NA UMRI
Kuchelewesha kupata watoto: Wanawake wengi leo wanaamua kuzaa watoto wakiwa na umri mkubwa kutokana na kazi, masomo, au sababu binafsi. Uwezekano wa kupata mimba unashuka kadri umri unavyoongezeka, hasa baada ya miaka 35, kwa sababu
Idadi na ubora wa mayai hupungua.
Hali za kiafya k**a PCOS na Endometriosis,PID,Hormone imbalance(Kuvurugika kwa vichocheo),Kuziba kwa mirija ya uzazi Hali hizi nimezizungumzia zaidi kwenye post zangu zilizopita
๐ SABABU ZA MTINDO WA MAISHA
Uzito mkubwa au lishe duni: Uzito kupita kiasi unaweza kuathiri homoni na ovulation. Vilevile, uzito mdogo sana pia unaweza kuathiri uzazi.
Kutofanya mazoezi: Kutokuwa na mwendo wa kutosha kunaweza kusababisha usawa wa homoni kuharibika.
Msongo wa mawazo: Msongo sugu unathiri homoni za uzazi na mzunguko wa hedhi.
Kunywa pombe, kuvuta sigara, na dawa za kulevya: Hizi zinaweza kupunguza uzazi kwa kuharibu mayai, mbegu za kiume, au mfumo wa uzazi.
๐ SABABU ZA MAZINGIRA
Kemikali zinazoharibu homoni: Kemikali zilizoko kwenye plastiki (k**a BPA), viuatilifu, na vipodozi zinaweza kuingilia homoni.
Uchafuzi wa hewa: Uchafuzi wa hewa umehusishwa na kupungua kwa uzazi na ongezeko la hatari ya kutolewa mimba.
๐ฅChangamoto za kushika ujauzito k**a nilivyosema awali ni changamoto inayokithiri sana,na huwafanya wanawake kukosa amani na furaha katika ndoa zao jambo ambalo hupelekea mpaka msongo wa mawazo.
๐ฟWanawake wengi wamejaribu tiba mbali mbali bila mafanikio na kuishia kukata tamaa,na kutotaka kabisa kuendelea kutafuta suluhisho ya changamoto hii,Habari njema ni kuwa tiba kwa ajili ya changamoto hii ipo
Unaweza kuwasiliana nasi kwa ajili ya ushauri,na elimu juu ya masuala ya afya pamoja na tiba
Huduma ya ushauri au maswali yoyote kuhusu afya ni bure kabisa
WhatsApp/Calls:0753843505
Tuma sms What'sApp/Dm muda wowote ule 24/7