18/12/2024
Tupo katika kipindi kigumu hasa Wakazi wa Maeneo ya Pwani ya Afrika mashariki. Ni kipindi cha Joto Kali na Watuu wengi wanapata tabu.
kutokana na halii hii ya joto Mwili wa mwanaadamu unapoteza maji kwa wingi na wakati mwengine bila hata kujijua.
Matokeo yake Unaweza kuugua Kichwa, kizunguzungu, mwili kuishiwa nguvu hata kupoteza hamu ya kula.
Jitahidi sana Kunywa Maji kadri uwezavyo ili kusaidia kurudisha maji mwilini, Epuka kufanya Mazoezi wakati wa Jua Kali na Pata Muda wa kupumzika Kivulini kila unapopata nafasi..