Health Care 4Africa

Health Care 4Africa To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear. Dr. Samuel

UGONJWA WA KUOTA KINYAMA SEHEMU ZA SIRI NA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI (GE***AL WARTS SKIN)✳GE***AL WARTS ni ugonjwa wa k...
08/08/2022

UGONJWA WA KUOTA KINYAMA SEHEMU ZA SIRI NA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI (GE***AL WARTS SKIN)
✳GE***AL WARTS ni ugonjwa wa kuota vinyama laini vidogovidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando Laini unaozunguka maeneo ya sehemu za siri.Vinyama hivyo vinaweza kutokea kwenye uume,e uke, mrija wa mkojo (urethra), v***a, na shingo ya kizazi au maeneo yanayozunguka haja kubwa, ugonjwa huu huenezwa kwa njia ya kujamiiana (Sexual Transmitted Diseases (STDs)
CHANZO CHA TATIZO.
✳Ugonjwa wa Masundosundo husababishwa na virus waitwao Human Papilloma Virus(HPV) hata hivyo Kuna Aina 70 tofauti za virus wa HPV hivyo sio wote wanaosababisha tatizo hili kwani Kuna ambao wanasababisha Masundosundo katika mwili sehemu tofauti k**a vile mikono, miguu, mgongoni, pia wapo wanaosababisha saratani ya shingo ya kizazi (Carcinoma Of The Cervix),saratani ya uume na saratani ya njia ya haja kubwa -A**l Cancer... kwa jinsia zote mbili
✳°ugonjwa huu wa Masundosundo umejitokeza kwa kiasi kikubwa baada ya kuwepo kwa janga la UKIMWI hivyo waathirika wengi ni..
✅Wenye wapenzi wengi,
✅Wanaofanya mapenzi kwa njia ya haja kubwa,
✅Wajawazito,
Watumiaji wakubwa wa sigara na pombe,
✅Watu wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo Wana hatari ya kupata tatizo hili.
✳DALILI ZA MASUNDOSUNDO
✅Mgonjwa wa tatizo hili hutokewa na vinyama Laini vidogovidogo vinavyojitokeza juu ya ngozi katika maeneo tofauti ingawa wakati mwingine huwa ni vidogo kiasi cha kutoweza kuonekana kwa njia ya kawaida.
✅Mgonjwa kupata ganzi maeneo yaliyozungukwa na Masundosundo
✅kutokwa na uchafu sehem za siri na kuwashwa kupita maelezo
✅kutokwa damu ukeni mara baada ya kufanya tendo la ndoa
✳USHAURI NA MATIBABU
✅kwanza kabisa lazima mtu binafsi ajielewe yeye mwenyewe na kujikinga na vitendo vinavyo pelekea adha ii kutokea mfano. STDs,Ngono zembe,Mapenzi kinyume,sigara na vingine ii itasaidia sana.
✅K**a umeathiriwa na ugonjwa uu, ondoa shaka tuwasiliane uanze dose mapema, itakayo kupa nguvu ya mwili na seli na kupambana na HPV Virus.
Text/whatsapp 0710877640 au kwa 0789162838

08/07/2021

It is gratifying to see that we are making great strides in improving our infrastructure in improving our Services! This proves that everything is possible if we are committed to achieving our goals and our dreams!

Read Article 'Intestinal Metaplasia – Causes, Risk Factors, and Prevention.'Using app 'Diseases Treatments Dictionary'So...
05/06/2021

Read Article 'Intestinal Metaplasia – Causes, Risk Factors, and Prevention.'
Using app 'Diseases Treatments Dictionary'
Source :

Intestinal metaplasia is a condition in which epithelial cells (the cells that line the stomach and esophagus) become altered or replaced.

𝐖𝐡𝐚𝐭 𝐈𝐬 𝐚 𝐇𝐞𝐚𝐫𝐭 𝐀𝐭𝐭𝐚𝐜𝐤?A heart attack (or myocardial infarction) occurs when the blood supply is cut off from or severel...
05/06/2021

𝐖𝐡𝐚𝐭 𝐈𝐬 𝐚 𝐇𝐞𝐚𝐫𝐭 𝐀𝐭𝐭𝐚𝐜𝐤?

A heart attack (or myocardial infarction) occurs when the blood supply is cut off from or severely reduced to part of the heart. It is caused by a blockage in one of the coronary arteries. This blockage could be caused by a blood clot or by plaque, cholesterol, and fat buildup in the arteries (usually a combination of both). Heart cells starved of blood die rather quickly if blood flow is not restored. If too much heart tissue dies, heart function can be permanently altered or the person could die from the heart attack.

𝐓𝐚𝐭𝐢𝐳𝐨 𝐋𝐚 𝐊𝐮𝐧𝐞𝐧𝐞𝐩𝐚 𝐊𝐮𝐩𝐢𝐭𝐚 𝐊𝐢𝐚𝐬𝐢!“Tunakabili tatizo kubwa ambalo linaweza kuathiri sana afya ya watoto wetu. Hatua isipoc...
01/06/2021

𝐓𝐚𝐭𝐢𝐳𝐨 𝐋𝐚 𝐊𝐮𝐧𝐞𝐧𝐞𝐩𝐚 𝐊𝐮𝐩𝐢𝐭𝐚 𝐊𝐢𝐚𝐬𝐢!

“Tunakabili tatizo kubwa ambalo linaweza kuathiri sana afya ya watoto wetu. Hatua isipochukuliwa sasa ili kuzuia tatizo hilo, watu watazidi kunenepa kupita kiasi.”—William J. Klish, profesa wa magonjwa ya watoto.

WATU fulani wasio na tatizo la kunenepa huwachambua watu walionenepa kupita kiasi na kuwaona kuwa wavivu na goigoi. Lakini je, kweli tatizo hilo ni dogo hivyo? Je, kunenepa kupita kiasi ni tatizo la watu wavivu wasiopenda kufanya mazoezi? Au je, mara nyingi tatizo hilo husababishwa na mambo makubwa ambayo ni vigumu kuyazuia?

Je, Husababishwa na Urithi, Mazingira, au Yote Mawili?

Kwa muda mrefu watu wamejadili ikiwa kunenepa kupita kiasi husababishwa na urithi au mazingira.
Ni nini maana ya urithi katika habari hii? Wengine husema kwamba kwa kawaida mwili wa mwanadamu huhifadhi kalori za ziada kwa ajili ya mahitaji ya wakati ujao.
Kwa makumi ya miaka, uchunguzi umefanywa ili kugundua jinsi urithi unavyosababisha kunenepa kupita kiasi. . . . Utafiti mwingi umefanywa kuhusu chembe za urithi za wanadamu na kunenepa kupita kiasi. Mbinu za hali ya juu zinatumiwa kutambua chembe za urithi zinazowafanya watu wawe na uwezekano wa kunenepa na kupata magonjwa k**a vile kisukari. Kulingana na wanasayansi, yaelekea kwamba asilimia 25 hadi 40 ya uzito wa mwili hutegemea chembe za urithi.

Ijapokuwa watu wanene kupita kiasi hulaumiwa kwa kujisababishia hali hiyo, idadi hizo zinaonyesha wazi kwamba chembe za urithi zinahusika sana, ingawaje, inasemekana kwamba mazingira huhusika kwa asilimia 60 au zaidi katika kuamua uzito wa watu. Hilo linaonyesha kwamba mtindo wa maisha ya mtu ni kisababishi kikuu cha kunenepa kupita kiasi. Je, kila siku yeye hula vyakula vyenye kalori nyingi na kutumia kalori chache? Je, yeye hula vyakula visivyofaa? Je, yeye hutenga wakati kila siku ili kufanya mazoezi kwa kiasi?

Huenda chembe za urithi zikasababisha kunenepa kupita kiasi, lakini uzito wa mwili hutegemea hasa kile unachokula na mazoezi ya mwili.
Mwishowe, kula vyakula vyenye kalori nyingi kupita kiasi, kutofanya mazoezi, au yote mawili husababisha kunenepa kupita kiasi.

Haimaanishi kwamba ni lazima uwe mnene kwa sababu ya chembe za urithi. . . . Ingawa chembe zako za urithi zinahusika, uzito wa mwili hutegemea kile unachochagua kula na mazoezi unayofanya.

Mashirika ya kuwasaidia watu kupunguza uzito hupata mamilioni ya dola kwani watu wengi hutamani sana kurudia umbo lao la zamani. Hata hivyo, wataalamu husema nini kuhusu kupunguza uzito?

Ni vigumu sana kushughulikia tatizo la kunenepa kupita kiasi, na wengi wanaopunguza uzito huongeza uzito tena. Inakadiriwa kwamba ni asilimia 25 [robo moja] tu ya watu ambao hufaulu kupunguza uzito na kuudumisha, baada ya jitihada nyingi.

Hatari za Kunenepa Kupita Kiasi

Kunenepa kupita kiasi kunaweza kusababisha matatizo makubwa ya afya. Dakt. Scott Loren-Selco, mtaalamu wa mfumo wa neva katika Kituo cha Tiba cha Chuo Kikuu cha Southern California, anaonya kwamba hata vijana walionenepa kupita kiasi wanakabili hatari ya kupata Aina ya 2 ya ugonjwa wa kisukari.

Anasema hivi:
Tunaona wengi wakiugua ugonjwa huo siku hizi, na inaogopesha sana. Mimi huwaambia [watu walionenepa kupita kiasi] kwamba ninaweza kuwapeleka kwenye chumba cha wagonjwa wa kisukari ili niwaonyeshe madhara wanayoweza kupata: hiyo inatia ndani vipofu, watu waliokatwa miguu, na watu wengi sana ambao wamelemazwa kabisa na aina ya 2 [ya kisukari]—kwa sababu ya kunenepa kupita kiasi.” Ni nini husababisha hali hiyo? Loren-Selco anasema hivi: “Kwa sababu wana pesa, wao hununua mikate mikubwa iliyotiwa nyama katikati na chipsi. Hakuna anayewaonya kwamba kula vyakula vingi vya aina hiyo kutawafanya wanenepe kupita kiasi, iwe ni wenye biashara hizo za chakula, au madaktari ambao hawajafundishwa kuhusu lishe.”

Dakt. Edward Taub, mwandishi maarufu kuhusu lishe, anasema: “Hivi karibuni, watu wameamini kwamba kunenepa sana ni jambo la kawaida na linalokubalika maishani. Wazo hilo la ajabu linaendelezwa na wenye biashara za chakula ambao hupata faida kwa kutunenepesha.”

Wataalamu wanasema kwamba watu walio na mafuta mengi mapajani huenda wakawa na afya nzuri kuliko wale walio na mafuta mengi tumboni (hasa ikiwa kiuno chao kinazidi sentimeta 90 hadi 100). Kwa nini? Kitabu Mayo Clinic on Healthy Weight kinasema kwamba “kuwa na mafuta tumboni huongeza uwezekano wa kupanda kwa shinikizo la damu, kupata ugonjwa wa moyo, kisukari, kiharusi, na aina fulani za kansa. Ikiwa una nyonga kubwa, mapaja manene, na matako makubwa, basi hukabili hatari kubwa sana ya afya.”

Hivyo, mamilioni ya watu wazima na watoto ulimwenguni pote ambao wamenenepa kupita kiasi na wanakabili uwezekano wa kupata magonjwa hatari wanaweza kufanya nini? Je, kuna matibabu yanayofaa?

𝐁𝐌𝐈 Ni Nini? Inaonyesha Nini?

BMI (body mass index) ni kipimo cha kulinganisha kimo na uzito ili kutambua ikiwa mtu ni mnene au mnene kupita kiasi. Kulingana na Kliniki ya Mayo, BMI ya 18.5 hadi 24.9 inaonyesha kwamba mtu ana afya bora. Ikiwa BMI yako ni kati ya 25 na 29.9, basi wewe ni mnene. Ikiwa imepita 30, basi wewe ni mnene kupita kiasi. Unaweza kutumiaje chati ya BMI? Je, unahitaji mashauri ya daktari ili upate madokezo au ujue hali yako?

Ili ujue BMI yako, gawa uzito wako katika kilo kwa kimo chako katika meta, kisha ugawe tena matokeo kwa kimo chako katika meta. Kwa mfano, ikiwa una kilo 90 na kimo cha meta 1.8, BMI yako ni 28 (90 ÷ 1.8 ÷ 1.8 = 28).

𝐊𝐚𝐥𝐨𝐫𝐢 ni nini?

Kalori ni nini? Ni kipimo cha nishati ya joto. Hivyo, unapotokwa na jasho unatumia kalori, au nishati ya joto. “Kalori ni kiasi cha joto kinachohitajiwa kuongeza halijoto ya kilo moja ya maji kwa sentigredi moja.” (Balance Your Body, Balance Your Life) Kila mtu huhitaji viwango tofauti-tofauti vya kalori au nishati kila siku, ikitegemea kimo, uzito, umri, na shughuli anazofanya.

Unahitaji kufanya mazoezi ikiwa

▪ Unatumia wakati mwingi kila siku ukiwa umeketi, iwe ni kutazama televisheni, kufanya kazi ofisini, au kusafiri ndani ya gari

▪ Mara nyingi hutembei kwa zaidi ya meta 100

▪ Unafanya kazi ambayo haikuwezeshi kufanya mazoezi

▪ Hutumii dakika 20 hadi 30 kufanya mazoezi angalau mara moja kila juma

Je, Wewe hufanya Mazoezi mara Ngapi kwa Juma?

29/05/2021

How to help someone who is fainting:
Do It Quickly!

15/05/2021

How We Can Solve Internal Hemorrhoids! In the best way and in Modern Technology Surgery!

𝐌𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐌𝐮𝐡𝐢𝐦𝐮 𝐲𝐚 𝐊𝐮𝐡𝐚𝐤𝐢𝐤𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐂𝐡𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐧𝐢 𝐒𝐚𝐥𝐚𝐦𝐚 𝐧𝐚 𝐂𝐡𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐋𝐢𝐬𝐡𝐞 𝐁𝐨𝐫𝐚!~Kwa nini ni muhimu kuhangaikia unachokulaIli uwe na ...
11/05/2021

𝐌𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐌𝐮𝐡𝐢𝐦𝐮 𝐲𝐚 𝐊𝐮𝐡𝐚𝐤𝐢𝐤𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐂𝐡𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐧𝐢 𝐒𝐚𝐥𝐚𝐦𝐚 𝐧𝐚 𝐂𝐡𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐋𝐢𝐬𝐡𝐞 𝐁𝐨𝐫𝐚!

~Kwa nini ni muhimu kuhangaikia unachokula
Ili uwe na afya nzuri?
Sehemu fulani inategemea unakula nini.

Ukihakikisha chakula chako ni salama na unakula chakula chenye lishe, unaweza kuboresha afya yako. Tofauti na hilo, usipohangaikia usalama wa chakula chako na ukila chakula kisicho na lishe, unaweza kujisababishia matatizo makubwa ya afya, k**a vile mafuta yasiyofaa yanavyoweza kulisababishia gari matatizo.
Huenda matatizo hayo yasionekane mara moja!

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linasema kwamba “kila nchi ulimwenguni huathiriwa na aina moja au zaidi za utapiamlo-'' ``Utapiamlo ni neno linalotumiwa kuonyesha si ukosefu wa chakula chenye lishe tu bali pia hali k**a vile kuwa mnene kupita kiasi.

Kutumia mara nyingi vyakula na vinywaji visivyo na lishe huongeza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo, kiharusi, kisukari, na kansa. Kulingana na uchunguzi mmoja, kula chakula kisicho na lishe kulisababisha vifo milioni 11 katika mwaka.

WHO inakadiria kwamba chakula chenye sumu hutokeza vifo vya zaidi ya watu elfu moja kila siku na kuwasababishia mamia ya mamilioni ya watu matatizo ya afya.

Uhai ni zawadi Takatifu tuliyopewa na Mungu, na tunaonyesha uthamini kwa kutunza afya yetu na ya familia zetu.
Hvyo tunao wajibu wa kufikiria jinsi tunavyoweza kuhakikisha Usalama wetu, na usalama wa Familia zetu.

~𝐌𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐦𝐚𝐧𝐧𝐞 𝐲𝐚 𝐊𝐮𝐡𝐚𝐤𝐢𝐤𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐂𝐡𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐧𝐢 𝐒𝐚𝐥𝐚𝐦𝐚~

🅐. 𝐓𝐚𝐲𝐚𝐫𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐂𝐡𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐧𝐣𝐢𝐚 𝐒𝐚𝐥𝐚𝐦𝐚 𝐧𝐚 𝐔𝐬𝐚𝐟𝐢

Kwa nini?
Ni kwa sababu Viini hatari vilivyo katika chakula na maji yaliyochafuliwa vinaweza kuingia mwilini mwako na kukufanya kuwa mgonjwa.

Wataalamu wa afya wanapendekeza:

❶. Kabla ya kutayarisha chakula, nawa mikono ukitumia maji na sabuni. * Sugua mikono yako kwa angalau sekunde 20. Sugua upande wa nyuma wa mikono na pia katikati ya vidole vyako na chini ya kucha. Suuza na ukaushe mikono vizuri.

❷. Tumia maji na sabuni kuosha mbao unazotumia kukatia vyakula, vyombo, na chochote kingine kinachogusa chakula.

❸. Epuka kutumia ubao uleule kukatia chakula kitakachopikwa na ambacho hakitapikwa.

❹. Osha matunda yote na mboga, pia ni muhimu kutumia dawa ya kuua viini ikiwa unaishi katika eneo ambalo mimea inaweza kuwa imenyunyiziwa maji yaliyochafuliwa na kinyesi.

🅑 𝐔𝐬𝐢𝐰𝐞𝐤𝐞 𝐩𝐚𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐯𝐲𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐯𝐢𝐥𝐢𝐯𝐲𝐨𝐩𝐢𝐤𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐚𝐦𝐛𝐚𝐯𝐲𝐨 𝐡𝐚𝐯𝐢𝐣𝐚𝐩𝐢𝐤𝐰𝐚

Kwa nini?
Kwa sababu viini kutoka kwenye vyakula ambavyo havijapikwa k**a vile nyama na umajimaji yake vinaweza kuchafua vyakula vingine.

~Kiafya indanidekezwa:

❺. Tenganisha vyakula ambavyo havijapikwa—hasa nyama—na vyakula vilivyo tayari kuliwa unapovibeba kutoka sokoni na unapovihifadhi.

❻. Baada ya kukata nyama mbichi, nawa mikono yako kabisa, safisha kisu na ubao uliotumia kukatia kabla ya kukata chakula kingine chochote.

🅒. 𝐇𝐚𝐤𝐢𝐤𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐤𝐰𝐚𝐦𝐛𝐚 𝐂𝐡𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐤𝐢𝐧𝐚𝐜𝐡𝐨𝐡𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐤𝐮𝐩𝐢𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐢𝐧𝐚𝐢𝐯𝐚 𝐕𝐢𝐳𝐮𝐫𝐢.

Kwa nini?
Kwa sababu viini hatari huuawa wakati tu chakula kinafikia kiwango kinachofaa cha joto.

~Kiafya inapendekezwa:

❼. Pika chakula hadi kinapokuwa moto sana. Kwa angalau sekunde 30, chakula, na K**a ni nyama, basi sehemu za ndani kabisa za nyama, zinapaswa kupigwa na joto la digrii 70 Selsiasi.

❽. Hakikisha supu na michuzi inachemka.

❾. Unapotaka kula masalio (kiporo), hakikisha unayapasha hadi yanapokuwa moto kabisa na kutokeza mvuke.

🅓. 𝐇𝐢𝐟𝐚𝐝𝐡𝐢 𝐂𝐡𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐤𝐢𝐰𝐚𝐧𝐠𝐨 𝐂𝐡𝐚 𝐣𝐨𝐭𝐨 𝐊𝐢𝐧𝐚𝐜𝐡𝐨𝐟𝐚𝐚.

Kwa nini?

Ni kwa sababu chakula kinapohifadhiwa katika hali-joto ya kati ya digrii 5 na 60 Selsiasi kwa dakika 20 tu, idadi ya bakteria inaweza kuongezeka mara mbili. Mbali na hilo, nyama mbichi isipohifadhiwa katika viwango vya joto vinavyofaa, bakteria fulani wanaweza kutokeza sumu ambazo haziwezi kuangamizwa kwa kupika.

~Kiafya inapendekezwa:

𝟏𝟎. Dumisha chakula kikiwa moto au baridi, si kikiwa vuguvugu, ili kupunguza au kuzuia viini visiongezeke.

𝟏𝟏. Usiache chakula nje kwa zaidi ya saa mbili. Ikiwa chumba kina joto la zaidi ya digrii 32 Selsiasi, usiache chakula nje kwa zaidi ya saa moja.

𝟏𝟐. Baada ya kupika, dumisha joto la chakula hadi kabla tu ya kukiandaa mezani.

𝐌𝐀𝐃𝐎𝐊𝐄𝐙𝐎 𝐊𝐔𝐇𝐔𝐒𝐔 𝐌𝐋𝐎 𝐊𝐀𝐌𝐈𝐋𝐈

~Mambo matatu muhimu ya kula chakula chenye afya~

𝟏. Kula aina mbalimbali za matunda na mboga kila siku.

𝐅𝐚𝐢𝐝𝐚 𝐲𝐚 𝐌𝐚𝐭𝐮𝐧𝐝𝐚 𝐧𝐚 𝐌𝐛𝐨𝐠𝐚.

Matunda na mboga ni chanzo muhimu cha vitamini, madini, na vitu vingine ambavyo ni muhimu ili kuwa na afya nzuri.
WHO inasema kwamba mwili wako unahitaji angalau sehemu tano ya matunda na mboga kila siku. Visehemu hivyo havipaswi kuwa na mizizi yenye wanga, k**a vile viazi au viazi vitamu.

𝟐. Kula kiasi kidogo tu cha mafuta.

Vyakula vilivyokaangwa na kushughulikiwa kiwandani.

WHO inapendekeza ule kiasi kidogo sana cha vyakula vilivyokaangwa na vyakula vilivyowekwa kemikali ya kuzihifadhi au vilivyookwa ambavyo mara nyingi vina mafuta hatari kwa afya. Inapowezekana, tumia mafuta yasiyoganda ya nafaka na mboga unapopika.
Mafuta hayo ni mazuri zaidi kuliko yale yanayoganda!

𝟑. Dhibiti kiasi cha chumvi na sukari unachokula.

Mapendekezo katika matumizi ya sukari na chumvi.

WHO inapendekeza kwamba watu wazima wasitumie chumvi inayozidi kijiko kidogo cha chai kwa siku. Pia, WHO inapendekeza kiasi cha sukari kisizidi milimeta 60 (vijiko 12 vya kawaida) kwa siku. * Sukari ndicho kiungo kikuu katika vyakula na vinywaji vingi vilivyotayarishwa viwandani. Kwa mfano, kinywaji k**a vile soda ya milimeta 355 inaweza kuwa na milimeta 50 (vijiko 10 vidogo) vya sukari. Licha ya kwamba vinjwaji k**a hivyo huwa na kalori nyingi sana, havisaidii mwili kupata lishe kwa njia yoyote.

Biblia inasema: “Mtu mwerevu huona hatari na kujificha, Lakini wajinga husonga mbele na kupata madhara.” (Methali 22:3) Ukitenda kwa werevu kuhusiana na mazoea yako ya kula na kufanya mabadiliko yanayohitajika, utamwonyesha Mungu kwamba unathamini uhai na afya yako.

𝐌𝐚𝐨𝐧𝐢 𝐲𝐚𝐬𝐢𝐲𝐨 𝐒𝐚𝐡𝐢𝐡𝐢:

𝐍𝐢 𝐔𝐨𝐧𝐠𝐨 𝐤𝐮𝐬𝐞𝐦𝐚: ~Chakula ni salama ikiwa mwonekano, harufu, na ladha yake iko sawa.

𝐍𝐢 𝐔𝐤𝐰𝐞𝐥𝐢: ~Bakteria bilioni 10 wanapojikusanya ndipo maji ya lita moja yanaweza kutokeza rangi nzito, lakini bakteria 15 hadi 20 tu ni hatari kiasi cha kukufanya kuwa mgonjwa. Ili kuhakikisha kwamba chakula na vinywaji vyako ni salama, fuata maagizo ya kiwango cha joto na muda ulioonyeshwa wa kuandaa, kula, na kuhifadhi.

𝐍𝐢 𝐔𝐨𝐧𝐠𝐨 𝐊𝐮𝐬𝐞𝐦𝐚: ~ Nzi hawachafui chakula.

𝐍𝐢 𝐔𝐤𝐰𝐞𝐥𝐢: ~Nzi hula na kuzaliana katika uchafu k**a vile kinyesi, kwa hiyo, mara nyingi miguu yao hubeba mamilioni ya viini vinavyoweza kusababisha magonjwa. Ili kulinda chakula kilichotayarishwa kisichafuliwe na nzi, kifunike kabisa.

𝐍𝐢 𝐔𝐨𝐧𝐠𝐨 𝐊𝐮𝐬𝐞𝐦𝐚: ~ “Nimekuwa nikila chakula kisicho na lishe kwa muda mrefu hivi kwamba hakuna faida hata nikibadili mazoea yangu ya kula.”

𝐍𝐢 𝐔𝐤𝐰𝐞𝐥𝐢: ~Wataalamu wamegundua kwamba kula chakula chenye lishe sasa kutapunguza uwezekano wa kufa mapema na kwamba utapata manufaa mengi kadiri unavyoendelea kula chakula chenye lishe.
Ingawa uhai wetu hautegemei tu jitahada zetu bali na Matakwa ya Mungu, lakini kufanya hivyo kunafaa Katika kuboresha afya zetu!

𝑳𝒊𝒏𝒅𝒂 𝑨𝒇𝒚𝒂 𝒀𝒂𝒌𝒐, 𝑭𝒖𝒓𝒂𝒉𝒊𝒂 𝑼𝒉𝒂𝒊 𝒘𝒂𝒌𝒐!

08/05/2021

Nasotracheal Suctioning - 3D training animation

Address

Dar Es Salaam
128546618

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Health Care 4Africa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram