04/01/2026
๐คฐ๐ฝ โDAKTARI, MIMI NINA UJAUZITO WA WIKI NGAPI?โ
Hili ni moja ya mfano wa maswali maarufu sana kwenye machapisho yetu hapa Afya Room ๐๐ฝ
โDaktari, mara ya mwisho niliona hedhi tarehe 26/05/2025, je nina ujauzito wa wiki ngapi na nitajifungua lini?
Leo nikueleze kwa lugha rahisi kabisa ๐๐ฝ
Madaktari huhesabu ujauzito kuanzia siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho, si siku ya kushika mimba.
๐ Tarehe hii ndiyo msingi wa:
Umri wa ujauzito (Gestational Age โ GA) na Tarehe ya makadirio ya kujifungua (Estimated Due Date โ EDD)
JINSI YA KUJUA UMRI WA UJAUZITO (GA) NA TAREHE YA MAKADIRIO (EDD)
Leo nikufundishe mwenyewe ujihesabie, hatua kwa hatua ๐ก
๐ HATUA YA 1: JUA TAREHE YA MWISHO YA HEDHI (LMP)
Hakikisha unajua siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho.
๐ Mfano wetu: 26/05/2025
Hii ndiyo tarehe muhimu zaidi katika kuhesabu ujauzito.
๐ HATUA YA 2: FUNGUA UpToDate Pregnancy Calculator
Kwenye simu au kompyuta:
Fungua Google
Andika: โUpToDate pregnancy due date calculatorโ
Fungua ukurasa wa calculator ya ujauzito ya UpToDate
(Usihofu, ni rahisi kutumia hata k**a si daktari ๐)
๐ HATUA YA 3: INGIZA TAREHE YA MWISHO YA HEDHI
Ndani ya calculator:
โ
Weka tarehe ya mwisho ya hedhi
โก๏ธ Chagua 26 / 05 / 2025
MM, ni mwezi, DD ni siku , YYYY ni mwaka.
๐ HATUA YA 4:
Baada ya kujaza hiyo tarehe, mfumo utakupa majibu haya ๐๐ฝ
๐น Gestational Age (GA)
โ Wiki na siku ulizonazo kulingana na tarehe ya leo
๐น Estimated Due Date (EDD)
โ Tarehe ya makadirio ya kujifungua (takribani miezi 9 + wiki 1 kutoka LMP)
โ ๏ธ MAMBO MUHIMU YA KUFAHAMU
EDD ni makadirio, si lazima ujifungue siku hiyo
Kujifungua kati ya wiki 37โ42 ni kawaida
Ultrasound ya mapema (wiki 6โ12) ni sahihi zaidi kuthibitisha GA
๐ก USHAURI WANGU , DAKTARI WAKO WA AFYA ROOM
Kujua GA na EDD:
โ
Hukusaidia kufuatilia ukuaji wa mtoto
โ
Husaidia kupanga kliniki na vipimo
โ
Hupunguza hofu kwa mama mjamzito
๐ Swali la leo:
Je, tayari umeshawahi kujaribu kuhesabu ujauzito wako mwenyewe? Ilikuwaje? Tuambie kwenye comments ๐๐ฝ
Asante sana kwa kuendelea kujifunza nasi ๐ค
Usisahau kufollow AFYA ROOM kwa elimu sahihi ya ujauzito na uzazi.