07/11/2025
Uvimbe kwenye kizazi, unaojulikana pia k**a fibroids au myomas, ni ukuaji wa nyama laini ndani au juu ya ukuta wa mji wa mimba (uterus). Mara nyingi, uvimbe huu si wa saratani na hauwezi kusambaa kwa sehemu nyingine za mwili.
❓Aina za Uvimbe Kwenye Kizazi
Intramural Fibroids: Hukua ndani ya misuli ya ukuta wa kizazi.
Subserosal Fibroids: Hukua nje ya kizazi na inaweza kusababisha maumivu mgongoni au presha tumboni.
Submucosal Fibroids: Hukua ndani ya ukuta wa kizazi na inaweza kusababisha hedhi nzito na matatizo ya uzazi.
Pedunculated Fibroids: Hushikiliwa na shina dogo na inaweza kuzunguka na kusababisha maumivu makali.
Dalili za Uvimbe Kwenye Kizazi
1.Hedhi nzito na yenye mabonge ya damu
2.Maumivu ya nyonga na mgongo
3.Tumbo kujaa au kuonekana kubwa
4.Maumivu wakati wa tendo la ndoa
5.Kukojoa mara kwa mara
6.Ugumba au matatizo ya kushika mimba
❓Sababu za Uvimbe Kwenye Kizazi
1.Mabadiliko ya homoni: Homoni za estrogen na progesterone huchochea ukuaji wa fibroids.
2.Mambo ya kijenetiki : Historia ya familia inaweza kuongeza hatari ya kupata uvimbe huu.
3.Mtindo wa maisha: Uzito mkubwa, lishe isiyo na virutubisho muhimu, na msongo wa mawazo vinaweza kuongeza hatari.
❓Kabla ya Kufanyiwa Upasuaji
Kabla ya kufikiria upasuaji, ni muhimu kuzingatia njia mbadala za matibabu k**a:
✅ Matibabu ya lishe na virutubisho – Kula vyakula vyenye antioxidants, iron, na fiber inaweza kusaidia kupunguza uvimbe.
✅ Tiba ya homoni – Dawa za kurekebisha homoni zinaweza kusaidia kudhibiti ukuaji wa uvimbe.
✅ Upasuaji mdogo (Myomectomy) – Unaondoa uvimbe bila kuathiri mfuko wa uzazi.
✅ Embolization – Njia ya kufunga mishipa inayosambaza damu kwa uvimbe ili kuukausha.
Madhara ya Kufanyiwa Upasuaji wa Uvimbe Kwenye Kizazi
Uwezekano wa kuathiri uzazi – Ikiwa kizazi kitaondolewa (hysterectomy), hautaweza kushika mimba tena.
Maumivu na muda mrefu wa kupona – Baadhi ya upasuaji huchukua muda mrefu kupona.
Hatari za kuvuja damu nyingi – Hasa ikiwa uvimbe ni mkubwa.
Kurejea kwa uvimbe – Ikiwa siyo hysterectomy, kuna uwezekano wa uvimbe kurudi
Kwa Hudumaa ya Ushauri na Matibabu Zaidi Wasiliana Na Dr Baraka 📞 0752927862