16/01/2025
Insulin resistance ni neno la kitabibu liki maanisha kuwa ni kitendo kinachotokea pale chembe chembe hai (Cells) za Misuli (muscle) Mafuta na Ini kushindwa kupokea sukari kwa msaada wa Hormone ya Insulin.
Cells za Misuli, Mafuta (Adipose tissue), na Ini hupokea na kuhifadhi kiwango cha Sukari kinacho zidi kwenye mzunguko wa damu.
Kazi kubwa ya Hormone hii iitwayo Insulin ni kuhakikisha kiwango Cha (glucose) sukari kwenye mzunguko wa damu kinabaki katika Kiwango sahihi, na chenye afya.
Hivyo Insulin resistance inapotokea huchochea kuongeza kwa mlundikano wa sukari (glucose) kwenye mzunguko wa damu, hivyo na kupelekea kuongeza nafasi kubwa ya kuwa hatari kuugua ugonjwa wa Kisukari.
Hali hii huchochewa na Unene uliokithiri (Obesity) , Magonjwa ya Moyo, Wanawake Wenye Changamoto ya Vimbe kwenye Mayai, Watu wenye viwango kikubwa cha mafuta kwenye Ini na baadhi ya matumizi ya dawa, mfano , ARVS , Prednisone.
Kwa tafiti za kina za kisayansi zinaonyesha insulin resistance husababishwa na kiwango cha mafuta Tumboni,
Kuto kuushughulisha mwili (sedentary lifestyle).
Ukiwa unapitia changamoto hii , Tezi inayo tengeneza Hormone hii huongeza kiwango cha uzalishaji ili kuweza kukabiliana na ongezeko la glucose kwenye mzunguko wa damu.
Kitendo hiki kikifanyika kwa muda mrefu hupelekea cell kupoteza uwezo wa kuzalisha Insulin ya kutosha hivyo hupelekea kuongezeka kwa glucose.
Hivyo mtu anaefikia hatua hii hupata dalili hizi
*Kupoteza uzito usioelezeka
*Uchovu uliokithiri
*Kiu iliyo kithiri
*Kukojoa mara kwa mara.
*Njaa iliyo kithiri
*Uono hafifu.
Jinsi ya kuzuia hali hii isikutokee ni
Mazoezi ,( mazoezi hurahisisha misuli kupokea kirahisi glucose)
Kuepuka mtindo wa hovyo wa Ulaji chakula
Kwa maelezo ya kina wasiliana nasi kwa namba
0783905545
0712808001.