Maarifa ya Kuikomboa Afya yako.

Maarifa ya Kuikomboa Afya yako. Maarifa ya kuyashinda magonjwa yanayo uwa wengi kwa sasa. Rejesha ndoto na furaha yako na uwapendao.

UKWELI JUU YA MAGONJWA YANAYO TESA WATU WENGI KWA SASA;1... K**a mwili wako unaweza kubadilika kutoka uzima wa afya Hadi...
24/03/2023

UKWELI JUU YA MAGONJWA YANAYO TESA WATU WENGI KWA SASA;

1... K**a mwili wako unaweza kubadilika kutoka uzima wa afya Hadi ugonjwa
Basi hii inamanisha ugonjwa unao kusumbua unaweza kupona kwa mwili wako kufanya mabadiliko ya kutoka ugonjwa kwenda afya

📍Mwili umeumbwa kwa namna ya kubadilika kulingana na Nini unakula, Nini kinabakia ndani ya mwili na Nini kinatoka nje ya mwili.

2..K**a Kuna chanzo Cha ugonjwa au tatizo la kiafya
Basi pia ipo namna ya kulishinda au kupona ugonjwa huo au tatizo hilo la kiafya

3...Ugonjwa unaweza kumpata mtu yoyote sababu UKWELI ni kuwa kila mtu anakutana na mabadiliko ya maisha ya kijamii, kiuchumi , kihisia na kimazingira hivyo basi kila mtu yupo kwenye hatari ya kupata ugonjwa wowote kulingana na mapokeo ya mabadiliko hayo na namna ya kuyaishi.
Hivyo usijione mwenye hatia sana juu ya tatizo lako la kiafya... Kwani wewe ni nani usikutane na mabafiliko ya kimaisha.

5...UHALISIA ni kwamba Kuna ugonjwa moja tu ambao ni upungufu au ukosekanaji wa mahitaji muhimu ya seli za mwili na ndio maana karibia magonjwa yote yanafanana dalili zake au dalili zake kuingiliana.

Hii Ina maana majina ya magonjwa hutokana na upungufu huo upo sehemu gani ya mwili na umeathiri ufanyaji kazi wa mfumo gani wa mwili.
Hii inamanisha nafasi ya kushinda magonjwa upo kwenye kuupa mwili unachohitaji kuwa sawa.

6... Kila mwili wa mtu una lugha ya kutoa taarifa kwamba una ugonjwa au tatizo la kiafya au upo hatarini kupata tatizo la kiafya au ugonjwa au pia HAUPO sawa kiafya
Je wewe unajua lugha ya mwili wako?
Ni muhimu kujua mwili wako unakuambia nini juu ya afya yako ili kujiazari au kuchukua hatua ya kutatua tatizo la kiafya mapema K**a unalo kabla halijawa kubwa.

7... Ni muhimu kujua kuwa sio kila ugonjwa au tatizo la kiafya unalipata ili likuangamize. Mengine yanakuja kukuamsha au kukupa taarifa ya mabadiliko unayo takiwa kufanya kwenye maisha yako ili Kujenga au kurejesha afya yako bora

Kumbuka Kila unacho kiamini na kukizingatia zaidi katika afya yako ndio kinacho kuangamiza au kukuponesha na sio ugonjwa au tatizo lenyewe la kiafya.

Je umejifunza kitu kwenye hili?

Share kwenye comment 👇

By. GGL

SIRI 2 ZA KUONDOKANA NA TATIZO LA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU NA KUREJESHA AFYA YAKO.Moja ya jambo linalo watesa watu wengi...
04/03/2023

SIRI 2 ZA KUONDOKANA NA TATIZO LA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU NA KUREJESHA AFYA YAKO.

Moja ya jambo linalo watesa watu wengi wakati huu ni magonjwa,

Na kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) magonjwa yanayo ongoza kwa kusababisha vifo vya watu wengi zaidi duniani ni Magonjwa ya moyo, na la kusikitisha zaidi ugonjwa wa Shinikizo la juu la damu ni moja katika Kundi la Magonjwa hayo ya moyo na pia ni kichochezi Cha magonjwa mengine ya moyo.

Kuwa na ugonjwa wa Shinikizo la juu la damu ni hatari zaidi maana mara nyingi halionyeshi dalili yoyote na hivyo husababisha kifo cha ghafla tu kwa mtu na kwasababu hiyo limepewa jina la "silent killer" yaani kuua kimyakinywa.

Pia Shinikizo la juu la damu huchangia uzalishaji wa magonjwa mengine ya moyo K**a Kupooza, mshtuko wa moyo, moyo kushindwa kufanya kazi, moyo kutanuka, pia huzalisha magonjwa na matatizo mengine ya kiafya k**a kisukari, matatizo ya uzazi, Presha ya macho K**a shinikizo hilo la juu la damu lisipo tatuliwa mapema.

Wengi hugundua Wana Shinikizo la juu la damu wanapo jisikia kuumwa na kwenda hospitali kupata matibabu ndipo huambiwa wakapime na kugundulika kuwa na tatizo hilo, ila Kwa wale ambao wanapata dalili K**a hizi ni muhimu kwenda kupima maana ndio huashiria unauwezekano wa kuwa na tatizo la shinikizo la juu la damu 1. Maumivu ya kichwa yasio koma 2. Kukosa usingizi 3.kupumua kwa shida 4.makelele maskioni 5. Kuona mawinguwingu 6.kutokwa damu puani na kwenye macho 7. Kizunguzungu 8. Kuvimba uso, miguu na mikono, 9. Kuzimia 10. Kuwa na hasira na mgomvi .
Ni muhimu kutopuuzia dalili hizi maana unaweza ukawa unapuuzia tatizo hili maana vyanzo vya tatizo la shinikizo la juu la damu ni kutoka kwenye mitindo ya maisha yetu tunayo ishi kila siku K**a 1. Kula vyakula vya wanga kwa wingi, vyenye chumvi nyingi na vya Mafuta mengi 2. Kuto kufanya mazoezi 3. Kutokunywa maji ya kutosha 4. Uzito mkubwa 5.msongo wa mawazo 6. Matumizi ya sigara na tumbaku na pombe 7.Matumizi ya kahawa sana na vinywaji vya kuongeze nguvu (enegy drinks) 8. magonjwa K**a ya figo au kisukari
Hivyo ni muhimu ukapate vipimo ukiona dalili hizo maana huwezi jua mtindo gani wa maisha umeathiri afya yako katika hili.

Hivyo basi kwa kudokezea Siri hizi mbili za kutatua tatizo hili la shinikizo la juu la damu. ni hizi 1. Kuondoa sumu na mafuta mwilini pamoja na mafuta mabaya ya lehemu ili kusafisha mishipa yako ya damu ili damu iweze kusafiri vyema na hivyo kuondoa msukumo au mgandamizo unao leta shinikizo la damu la juu au pandisha presha
2. Kuupa mwili virutubisho vyote muhimu. Hii husaidia kuboresha ufanyaji kazi wako wa kila mfumo wa mwili sawasawa na hivyo hukukinga na kukusaidia kupona magonjwa hatarishi ya sasa. Pia husaidia kudhibiti afya yako isirudi kwenye tatizo la mwanzo.

Mambo matatu ya kuzingatia katika kutumia Siri hizi mbili ni 1. Kuna vitu na mambo ya kuacha kwenye maisha 2 . Kuna Mambo na vitu vya kubadilisha kwenye maisha na 3. Kuna Mambo na vitu vya kudhibiti kwenye maisha
Ili mwili wako uweze kufanya matendo makuu 2 ya lazima ili kurejesha afya yako
Matendo hayo ni haya
1.. mwili lazima utoe visivyohitajika mwilini
2.. Lazima uingize vinavyohitajika mwilini

Hivyo basi Kupata elimu na maelezo zaidi kutumia Siri hizi 2 na kujua nini kitoke na Nini kiingizwe mwilini ili kukabiliana na tatizo lako la kiafya
ungana na darasa letu kupitia linki

WhatsApp Group Invite

VITU 7 MWILI WAKO UNAHITAJI ILI KUWA NA AFYA 1... Hewa ya oksijeni ya kutosha Hii hupatikana kwa kufanya mazoezi hasa ya...
30/01/2023

VITU 7 MWILI WAKO UNAHITAJI ILI KUWA NA AFYA

1... Hewa ya oksijeni ya kutosha
Hii hupatikana kwa kufanya mazoezi hasa ya kukibia kuruka kamba nk

2... Kunywa maji mengi ya kutosha
Kazi zote za mwili zinategemea maji hivyo asilimia 75% ya mwili ni maji ndio maana mwili unahitaji maji ya kutosha.

3.. Virutubisho vitano muhimu kwa afya ya seli .
Seli zenye afya ndio hujenga mwili wenye afya
Hivyo kuwa na seli zenye afya unatakiwa kuzipa seli zako aina 5 ya virutubisho wanga, rotini, madini, mfuta na vitamini.

4... Kulala na kupunzika kwa muda wa kutosha
Hii huupa mwili wako na mifumo ya mwili kupunzika ili kufanya kazi zake vyema kwa ufanisi.
Pia huondoa sumu mwilini

5...Kuondoa sumu mwilini
Ni muhimu kusafisha mwili kwa kuondoa sumu mwilini na taka mwili maana zikibaki ndani ya mwili nduio huzalisha magonjwa yasio ya kuambukiza pamoja na unene ulio pitiliza.

6... Kudhibiti msongo wa mawazo
Maisha ya sasa hivi watu hawawezi epuka msongo wa mawazo Bali KUJIFUNZA namna ya kukabiliana nao.

7... Kuepuka Matumizi ya vitu hatarishi kwa afya k**a uvutaji, ulezi, matumizi ya madawa ya kulevya,

Kukupatia mwili hivi vyote kikamilifu ndio hujenga mwili wenye afya njema.

SIRI YA KUONDOKANA NA TATIZO LA PRESHA AU SHINIKIZO LA JUU LA DAMU ILI UFURAHIE MAISHA Moja ya jambo linalo umiza na kus...
28/01/2023

SIRI YA KUONDOKANA NA TATIZO LA PRESHA AU SHINIKIZO LA JUU LA DAMU ILI UFURAHIE MAISHA

Moja ya jambo linalo umiza na kusikitisha ni jinsi gani ugonjwa wa presha au shinikizo la juu la damu linavyo watesa wengi na kusabisha kuzalishwa kwa magonjwa mengine tishio kadiri unavyozidi kukaa nao kwa mda mrefu bila kupona husababisha magonjwa au matatizo mengine ya kiafya k**a magonjwa ya kisukari, kupooza, mshtuko wa moyo, presha ya macho na matatizo ya macho, matatizo ya uzazi kwa wanaume na wanawake, matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume pamoja na kutanuka kwa moyo ambayo ndio huhatatisha maisha ya wengi na kusababisha vifo vya wengi duniani.

Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu au presha ni ugonjwa mmoja wapo katika lile kundi la magonjwa ya moyo ambalo kutokana na takwimu ya shirika la afya duniani (WHO) ni magonjwa yanayo ongoza kwa kuuwa watu wengi sana duniani kuliko magonjwa mengine yote, na ugonjwa huu wa shinikizo la juu la damu kuna wakati hauna dalili yoyote na hivyo unaweza kumuua mtu ghafla tu na ndio maana umepewa jina la “silent killer” yaani linauwa kimya kimya, pia ni muhimu kufahamu kuwa unapo kuwa na shinikizo la juu la damu au presha kwa mda mrefu unakuwa hatarini kupata na magonjwa mengine ya moyo maana yote yanatokana na ufanyaji kazi wa moyo ambapo ukiwa na shinikizo la juu la damu tayari ufanyaji kazi wa moyo unakuwa umeathirika.
Na dalili ya shinikizo la juu la damu au magonjwa ya moyo ni 1. Kusikia uchovu sana usio fafanulika, 2. Kupumua kwa shida, 3. Maumivu katika kifua, 4. Kusikia kizunguzungu na kuona giza, 5. Kuumwa na kichwa sana, 6. Kuvimba mikono na miguu, 7. Mapigo ya moyo kuto kwenda kawaida, 8. Kikohozi kisicho endelea
Kutokana na hali hii watu wengi wamekuwa na mahangaiko ya kutafuta dawa ya kuwasaidia wapone kabisa na kuondokana na tatizo hilo bila mafanikia hata baada ya kutumia dawa nyingi na mbalimbali, habari njema ni kuwa ipo njia sahihi ya kiafya ambayo imewasaidia wengi ambayo unaweza itumia na kukusaidia wewe pia kuondokana na tatizo hilo k**a utakuwa tayari kujifunza na kuchukua hatua muhimu na kuzingatia unayopaswa kufanya ili kurejesha afya njema na furaha ya maisha yako na uwapendao.

Kwa kupata elimu hiyo bonjyeza liki apo chini kujiunga na darasa letu.

https://chat.whatsapp.com/JkYhhXi6sMUCLehdYkfHB6

MAMBO 7 YA KUZINGATIA ILI USIPOTEZE AFYA YAKO 1. KUFANYA MAZOEZI Husaidia mwili kupata oksijeni ya kutosha na kufanya ka...
15/01/2023

MAMBO 7 YA KUZINGATIA ILI USIPOTEZE AFYA YAKO

1. KUFANYA MAZOEZI

Husaidia mwili kupata oksijeni ya kutosha na kufanya kazi za mwili kufanyika vizuri.

2. KUNYWA MAJI YA KUTOSHA
kila kg 20 za mwili wako zinahitaji Lita moja ya maji kila siku.
Maji ndio husababisha kazi za mwili kufanyika kila siku.

3. KULA MLO KAMILI WA KIAFYA
Hakikisha mwili unaupatia mlo kamili kwaajili ya kuupa virutubisho vyote muhimu

4. KULALA USINGIZA WA KUTOSHA.kulala usingizi mzito usiku masaa yasio pungua 7-8 (tengeneza utaratibu wa maisha yako)

5.. DHIBITI MSONGO WA MAWAZO
huu Huleta magonjwa na kuua wengi kwa ghafla K**a haudhibitiwi mapema

6... ONDOA NA EPUKA SUMU MWILINI
Sumu ni sababu ya magonjwa yote yaletwayo bila Maambukizi na kushindwa kufanya kazi kwa ogani za mwili na mifumo ya mwili. Sumu za mwili huua mwili wako taratibu ukiwa bado unaishi.

7.. EPUKA MATUMIZI NA TABIA ZINAZO ANGAMIZA AFYA YAKO.
K**a uvutaji sigara, matumiziya pombe, madawa ya hospitali kiholela.

Sijui nimekusaidia au unahitaji darasa zaidi?

" Afya zetu ni za THAMANI "

ISHI SASA Huu mwaka 2023 Hakikisha jambo moja la muhimu katika maisha yako linafanyika nalo ni Kuishi. ISHI Kuishi ni se...
10/01/2023

ISHI SASA

Huu mwaka 2023
Hakikisha jambo moja la muhimu katika maisha yako linafanyika nalo ni
Kuishi.

ISHI
Kuishi ni sehemu ya afya Bora na ni moja ya namna ya kuhakikisha watu huweza kujirejeshea afya zao.

ISHI
Yaani chochote ufanyacho au utiacho Hakikisha unaijali afya yako kabla ya kutumia au kufanya kitu chochote.

ISHI
Ishi uokoe afya yako
Ishi uboreshe afya yako
Ishi ubaki na afya yako Bora siku zote

"Hakuna jambo LOLOTE ambalo ni sehemu ya maisha , Bali kila jambo ni maisha halisi"

Ishi kila wakati kulingana na haja ya wakati huo.

Unaweza ukawa wakati wa kuipigania KUIKOMBOA AFYA yako , wakati wa kuiboresha afya yako au wakati wa kudhibiti afya Bora uliyo ipata kuendelea kudumu.
Ishi kulingana na kipindi unacho pitia kiafya hasa kwenye vitu vya kuacha, kuepuka au kubadilisha kufanya au kutumia.

ISHI ...ISHI ...ISHI SASA pamoja na mambo yote yanayoendelea duniani.

GG

04/01/2023

SABABU 3 ZA MWILI WAKO KUTEGEMEA MOYO WAKO KUWA NA AFYA.

1... Mzunguko wa damu unafanywa na moyo na bila mzunguko wa damu hamna maisha

2... Moyo wako unapo pata tatizo la kiafya kimwili huathiri mwili wako moja kwa moja

3... Moyo wako unahisisha mwili wako kiimani yaani usipo kuwa na Amani moyoni basi mwili wako pia huathirika

Moyo wako ni kitu muhimu katika maisha na kina nafasi kubwa ya kuweka sawa maisha yako kimwili,kiakili na kihisia . Kamwe usiipuuze afya yake.

01/01/2023

AFYA YA MOYO WAKO NI MUHIMU KWA MWILI WAKO NA AKILI YAKO,

JALI AFYA YA MOYO WAKO.

27/12/2022

NAMNA YA KUONDOKANA NA MAGONJWA NA KUJIKINGA NAYO.

UGONJWA NI NINI?

Huwa tunasema naumwa hili au lile, au Fulani anaumwa.
Sasa hebu tujifinze Kuumwa ugonjwa wowote ule ni Nini maana yake hasa.

👇✍️

Mwandishi RYMOND FRANCIS wa kitabu Cha "NEVER BE SICK AGAIN"

Yeye kwenye kitabu chake aliansika Ugonjwa au Magonjwa ni kushindwa kufanya kazi kwa seli za mwili ipaswavyo.

Na kushindwa kufanya kazi huko kwa seli za mwili Kuna sababishwa na sababu 2 tu ambazo ni;
1... Seli kukosa virutubisho na vitu muhimu kuweza kujitegema katika UTENDAJI kazi wake

2... Mwili kuwa au kulindika sumu nyingi mwilini zinazo sababisha madhara kwenye seli za mwili.

Hivyo basi
Mtu anapokuwa anaumwa hasa magonjwa makubwa yasio ya kuambukiza, ni Ishara asilimia kubwa ya seli zake za mwili hazina Tena uwezo wa kufanya kazi zake ipaswavyo, na njia pekee itakayo msaidia mtu kupona kutoka magonjwa hayo hatarishi K**a kisukari, presha nk ni kwa kuzipa seli za mwili vitu muhimu vinavyo hitajika .

Mwandishi MATT TRAVERSO wa kitabu Cha "REVERSE DIBETES "

Yeye anasema Ugonjwa au Magonjwa ni Ishara ya mwili kukosa virutubisho na mahitaji muhimu ili kuweza kujitibu wenyewe, kujikinga wenyewe na kujitenga kiafya na pia ni Ishara ya mwili kuonyesha umeshindwa kutoa sumu angamizi mwilini ipaswavyo na madhara ya sumu hizo zinaonekana kwa njiaa ya ugonjwa .
Anasema "WATU HULA NA KUSHIBA CHAKULA , LAKINI WANA NJAA YA VIRUTUBISHO MUHIMU MWILINI"

Hivyo basi ili kuweza kuondokana na magonjwa ni kuupa mwili vitu vyote muhimu unavyo hitaji.

NA

Kutokana na makala ilio andikwa na. "THE. CALIFORNIA SOCIETY FOR BIOMEDICAL RESEARCH" walio andika kuhusu HOW HUMAN BODY WORKS
Wao walielezea ugonjwa au Magonjwa ni Hali ya mwili kuonyesha umeathiriwa na sumu ambazo zimeingia mwilini na unajaribu kupambana kuzitoa ili kuweza kurejesha mwili katika Hali ya kawaida na inapokuwa hivyo ndipo UNAPATA maumivu K**a ya kichwa, tumbo, maumivu ya mwili na kushindwa kufanya kazi kwa baadhi ya ogani za mwili, na pia mwili kukosa vitu muhimu seli za mwili zinazohitaji ili kujenga mwili wenye afya.

Hivyo basi mwisho wa siku ... Swala la watu kupona magonjwa lipo kwenye kuupa mwili vitu muhimu vinavyo hitajika na kutusaidia kuondoa sumu mwilini ili zisiasthiri seli za mwili.

Habari njema ukiweza kuupa seli za mwili Nini zinataka, unakuwa pia umeusaidia mwili kuondoa sumu pia. Hivyo unaua ndege wawili kwa jiwe moja.

MUHIMU

Ukweli ni kwamba magonjwa yote kujionyesha kwake huanza na DALILI mbalimbali ambazo mtu huanza zisikia kidogo kidogo na pale zinapokuwa zinaleta madhara makubwa ndipo unaenda fanya uchnguzi Nini kinaleta shida.

Na ukitaka kujua kuwa seli za mwili zinapo pata shida ndo mtu UNAPATA Hali inayokufanya ujihisi yeye ni mgonjwa na ndio maana magonjwa yote DALILI ZAKE hufanana na ndio maana vipimo ndio vinakwambia kwa uhakika una umwa Nini.,

Seli za mwili zinapo pata shida au kushindwa fanya kazi yake unaanza Kujisikia uchovu, viungo au mwili kuuma, joto Kali la mwili, kutapika, kuharisha, maumivu mbalimbali, kuvimba au vimbe, vidonda, matatizo ya ngozi nk
Sasa kulingana na dalili ulizo nazo ndo daktari anasema upime Nini ili ujue tatizo na ndio maana mara nyingi huambiwi upime kipimo kimoja Bali zaidi ya kimoja.

HIVYO BASI
Haijalishi unaumwa na ugonjwa gani sasa, unasumbuliwa na ugonjwa gani mara kwa mara na umekutesa aumekaa nao mda mrefu kiasi gani ...kupona kunawezekana K**a utaweza kuupa mwili (seli za mwili) vitu vyote muhimu zinahitaji kwa adamu na kwa kudhamiria. Utasahau kabisa swala la wewe kuugua kila kukicha au hata kukosa usingizi kwa Kuumwa.

Anza kubadili ufahamu juu ya afya ...kulinda afya yako

AFYA YAKO NI JUKUMU LAKO .. CHUKUA HATUA SASA.

KIla la kheri.

GG

JINSI YA KUZUIA  SHINIKIZO LA DAMU* Chanzo kikubwa Cha shinikizo la juu la damu ni mtindo wa maisha, upungufu wa vitamin...
15/12/2022

JINSI YA KUZUIA SHINIKIZO LA DAMU*

Chanzo kikubwa Cha shinikizo la juu la damu ni mtindo wa maisha, upungufu wa vitamini na madini na mafuta na sumu nyingi mwilini

Hivyo basi kuweza kurejesha afya yako kutoka kwenye tatizo la Presha ni kubadili mtindo wa maisha, kuondoa sumu na mafuta mabaya na kupata madini na vitamini vinavyotakiwa.

Nini Cha kufanya, kubadilisha na kuupa mwili wako ili kudhibiti shinikizo la juu la damu
👇👇

1. Fanya Mazoezi mara kwa mara- angalau dakika 30-45 mara mbili kwa siku. Na mara 4-5 kwa wiki

2. Kwa wavutaji sigara kuacha kuvuta sigara kabisa na matumizi ya tumbaku

3. Kuacha matumizi ya pombe kabisa

4. Punguza utumiaji wa chumvi hasa ya kuongeza mezani (usitumie zaidi ya gramu 1.5)

5. Dhibiti msongo mawazo au epuka msongo wa mawazo pale unapo weza.

6. Kupunguza uzito au unene ,Hakikisha unakuwa kwenye uzito wa afya, k**a uko kwenye uzito wa hatarishi kwa afya yako anza mpango wa kupunguza uzito.

7. Tumia omega 3 au omega 6 .
hii huipata kwa kula samaki wa kina kirefu wa baharini ni ndio yana mchango mkubwa sana wa kuondoa Presha kabisa.

8. Punguza au acha kabisa matumizi ya sukari, kahawa, chai nueusi , cola na enegy drinks

9. Punguza kula mafuta mengi
Hasa vyakula vyenye niongeza ya mafuna na lehemu nyingi K**a Mayai, siagi, Maziwa, ice cream,
Biskuti, chokoleti, keki na vyakula vya kukaanga.

10. Upe Mwili vitamini na madini ya calcium, potassium na magnesium …. Huwa yanashusha presha (unaweza kuvipata kwenye limao, ndizi, viazi, peasi, broccoli, tomato, caulflouwer , sprouts and oranges

11. Upe Mwili Vitamin C, vitamin B 3(niacin) and vitamin E. ….. vizuri kwa kushusha presha kwakuondoa sumu mwilini

12. Kula vyakula vya nyuzinyuzi kwa wingi (high fiber intake) ; chakula k**a nyanya, ndizi, viazi chungwa, apple, maharage (green beans), Kabichi ili kusaidia mwili wako kutoa taka mwili ambazo hupunguza sumu mwilini.

13. Tumia vhakula muhimu kwa kushusha presha k**a vitunguu saumu, asali, juisi ya limao na vitunguu maji … vinahusika katika kusaidia kuopunguza presha.

14. Mapunziko yanayo punguza msongo wa mawazo na utulivu wa akili. k**a massage, music, meditation, hummer/laughter , lying or walk in a fresh air in garden.

15. Kunywa maji mengi , hasa wakati wa asubuhi ukiwa hujala chochote ….. hii husaidia kuifanya damu yako kuwa nyepesi na kupunguza tabia ya kuganda .

16. Badili mtazamo wako juu ya maisha ….. kuwa chanya kwenye mambo ya maisha kupunguza msongo wa mawazo.

17.. lala kwa masaa yanayotakiwa kiafya 7-8 ili kusaidia mwili wako kupunzika na kutoa sumu.

18. Kula mlo kamili kila siku.

Tunza afya yako ikutunze.

SHINIKIZO LA JUU LA DAMU  *UGUNDUAJI, AINA, DALILI NA MADHARA* *UGUNDUAJI* : Mara nyingi wagonjwa wa shinikizo la juu la...
13/12/2022

SHINIKIZO LA JUU LA DAMU
*UGUNDUAJI, AINA, DALILI NA MADHARA*

*UGUNDUAJI* :

Mara nyingi wagonjwa wa shinikizo la juu la damu hawana dalili zinazoashiria kuwa Wana tatizo hili. Na kwa kawaida wengi hugundulika kuwa na tatizo la Shinikizo la juu la damu katika uchunguzi wa kawaida tu wa magonjwa mengine wawapo hospitalini. Mara chache baadhi ya watu huja tayari wakiwa na madhara ya shinikizo la juu la damu

*AINA YA SHINIKIZO LA DAMU*
Kuna makundi mawili ya aina ya shinikizo la damu kutegemeana na chanzo chake ;

*Aina ya kwanza*
Asilimia 90-95 sababu huwa hazijulikani na kitaalamu huitwa primary or essential hypertension. Ingawa vitu vifuatavyo vimehusishwa kupelekea kupata aina hii ya shinikizo la damu.
Navyo ni:
• Uvutaji sigara

• Unene (visceral obesity)

• Unywaji wa pombe

• Upungufu wa madini ya potassium

• Upungufu wa vitamin D

• Kurithi
• Umri mkubwa

• Chumvi na madini ya sodium kwa ujumla

• Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)

• Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin

*Aina ya Pili*
Asilimia 5 huwa na sababu dhahiri zinazopelekea kupata aina hii ya shinikizo la damu na huitwa kitaalamu secondary hypertension.
Na sababu hizi ni:
• Hali ya kukosa hewa usingizini (sleep Apnea)
• Kasoro ya kuzaliwa nayo katika mshipa mkubwa wa damu (Coarctation of Aorta)
• Saratani za figo (wilm’s tumor, renal cell carcinoma)
• Saratani ya tezi iliyo juu ya figo (pheochromocytoma)
• Ujauzito – wapo wakina mama wajawazito ambao hupata shinikizo la damu na huwa hatarini kupata kifafa cha mimba (eclampsia)
• Magonjwa ya figo (renal artery stenosis, glomerulonephritis)

*DALILI ZAKE*
Mara nyingi huwa hamna dalili zozote, na k**a zikiwepo mgonjwa huwa na dalili zifuatazo;
• Uchovu

• Maumivu ya kichwa (hasa yanayo sababishwa na hasira na kufanya kazi kwa msukumo sana “under pressure”

• Kuhisi mapigo ya moyo kwenda haraka

• Kichefuchefu

• Kutapika

• Damu kutoka puani

• Kutoweza kuona vizuri (blurred vision)

• Kusikia kelele masikioni

• Na mara chache kuchanganyikiwa

• Kukosa usingizi

• Kizunguzungu

• Uso ulio jaa (Flushed face on exertion)

• Kuongeza kwa ukali, hasira na ugonvi.

• Kuwa na haraka na kutokuwa mvumilivu. Siku zote anakimbizana na muda.

*Vipimo na uchunguzi**
👇
Huitajika kupima angalau mara tatu kwa wiki moja tofauti ilikuweza kusema mgonjwa ana shinikizo la damu kwa kutumia kifaa kinachoitwa kitaalamu Sphygmomanometer.

Vipimo vingine ni:

• Damu kuchunguza wingi wa lijamu/lehemu mwilini (cholesterol), na pia vitu k**a (BUN, na electrolytes)

• Kipimo cha mkojo (Urinalysis)

• Electrocardiogram (ECG)

• Echocardiography

• Ultrasound ya figo

*MADHARA YA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU*
1. mwili kupooza, kiharusi (stroke), kuvuka damu kwenye ubongo…(bleeding in the brain)

2. shambulio la moyo
(Heart attack),
Mishipa ya ateri kuwa miembamba au kuziba kabisa ndio husababisha shambulio la moyo.

3. moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure), kwasababu moyo unafanya kazi sana zaidi ya inavyotakiwa na kuanza kutanuka na baada ya mda unachoka na kushindwa kufanya kazi yake Tena.

4. kufanya moyo kuwa mkubwa,
Sababu ya nguvu inayotumia kusukuma damu kwa mda mrefu

5. ugonjwa wa figo … ( when BP rise figo haiwezi fanya kazi yake ya kuchuja damu inavyoakiwa , na chunvi na sumu zinazo jikusanya mwilini. Kila gm ya chumvi inayojikusanya mwilini ina uwezo wa kushikilia gm 70 ya maji yasitolewe nje, uhifadhi huo wa maji unaweza leta heart failure , na pia hu destroy cell na kufaile kwa figo inatambulika kwa kupoteza virutubisho vya matumizi kupitia mkojo.

6. kupunguza nguvu za kiume
Mfumo wa uzazi wa mwanaume unategemea sana mfumo wa mzunguko wa damu kufanya kazi yake

7. Kifafa cha mimba kwa mama wajawazito

8. Kisukari
Kwa madhara ya uzalishaji wa insulini mwilini

9. Presha ya macho au kuto kuona vizuri
(Kushindwa kuona)

10..Madhara katika mshipa mkubwa wa damu ambapo ukuta wa ndani huchanika na damu hukusanyika katika ukuta wa mshipa huo(aortic dissection)

11. Magonjwa ya mishipa ya damu

12.. Athari katika ubongo

Afya yako ni jukumu lako .

Jiandae kwa SoMo la utatuzi wake.

GG

VYANZO (Visababishi) VYA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU. Kulingana na Uchunguzi wa Wana sayansi wengi hakuna chanzo ambazo ni ...
12/12/2022

VYANZO (Visababishi) VYA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU.

Kulingana na Uchunguzi wa Wana sayansi wengi hakuna chanzo ambazo ni maalumu Cha shinikizo la damu .. Ila shinikizo la juu la damu linahusishwa na mtindo wa maisha unao husika sana na mambo haya yafuatayo

👇👇👇👇

1. Historia ya ugonjwa katika familia yao (kurithishwa)

2. Uzito mkubwa kupindukia,

3. Matumizi ya chumvi nyingi kwa mda mrefu, hasa ya kuongezea moja kwa moja kwenye chakula

4. Kuto kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi katika maisha ya mtu

5. Uvutaji wa sigara na matumizi ya tumbaku.

6. Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi K**a vya kukaanga na vya kusindikwa.

7. Ulaji wa vyakula kwa kiwango cha juu k**a wanga nyingi na protini nyingi tofauti na mwili wako unavyohitaji, pamoja na vyakula vya kusindikwa na vyakula vya kisasa

8. Mwili kuto kutoa taka mwili na sumu zinazo ingia mwilini (K**a kuwa unapata matatizo ya kupata choo kikubwa constipation kwa mda mrefu)

9. Umri mkubwa

10. Msongo wa mawazo hasa uletwao na woga, wasiwasi na sintofahamu

11. Kukaa mda mrefu au kuto ufanyisha kazi mwili

12. Matumizi ya pombe kwa wingi

13. Matumizi ya uzazi wa mpango,

14. Kuwa na ugonjwa wa kisukari

15. Matumizi ya kahawa na vinywaji vyenye kofeini (K**a enegy drinks)

16. Matatizo ya magonjwa ya figo

17. Uja uzito hasa kipindi cha miezi mitatu ya mwisho.

Vyanzo vingi hapa husababisha wembamba na ugumu wa arteries (atherosclerosis) sababu ya kujiwekeza kwa lehemu mbaya (cholrsterol) kwenye kuta hizo za ateri (arteries) na kuzifanya ziwe dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kutanuka na kusinyaa na hivyo damu inalazimishwa kusukumwa kwanguvu na muyo ambapo ndipo shinikizo la juu la damu linapo anzia. Ndio maana umri pia unaonekana kuwa ni chanzo hasa kwa watu wa umri mkubwa kuathirika zaidi ya vijana.

Zamani ilionekana wazee wengi ndio wanakuwa na tatizo hili zaidi ya vijana lakini sasa hali imebadlika sababu mpaka kufika kwa vijana na watoto kutokana na hao wazee kuwarithisha watoto na vizazi vyao ambao wakipata kwa kurithi ukichanganya na mabadiliko ya mfumo wa maisha kwa sasa ndio hufanya ugonjwa huu kuathiri watu wa rika lote na kusababisha vifo vingi zaidi.

Tunza sana afya ya moyo wako

GG

AFYA YA MOYO HUTABIRI AFYA YA MWILI WAKO MZIMA USIPUUZIE AFYA YAKO. *Afya yako ni chanzo Cha  furaha yako na mafanikio y...
08/12/2022

AFYA YA MOYO HUTABIRI AFYA YA MWILI WAKO MZIMA

USIPUUZIE AFYA YAKO.

*Afya yako ni chanzo Cha furaha yako na mafanikio yako ..KIUCHUMI na kimahusiano *

Afya ni furaha na furaha ndio hujenga afya Bora.

SIRI YA KUPONA UGONJWA WA PRESHA ( SHINIKIZO LA JUU LA DAMU)Watu wengi wamekuwa wakihangaika na huu ugonjwa na wengine k...
06/12/2022

SIRI YA KUPONA UGONJWA WA PRESHA ( SHINIKIZO LA JUU LA DAMU)

Watu wengi wamekuwa wakihangaika na huu ugonjwa na wengine kufikia hatua ya kuukubali kuwa ni Ugonjwa wa maisha usio pona ambao unakuhitaji unywe dawa maisha yako yote.

Lakini ipo Siri ilio jificha kwenye kutatua tatizo hili ambalo ukiishi nalo kwa mda mrefu linazalishwa matatizo mengine ya kiafya K**a
KISUKARI, FIGO, MACHO, KUPOOZA, MSHTUKO WA MOYO, MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI, UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KURITHISHWA KWA WATOTO WAKO NA KIZAZI CHAKO.

SIRI ipo kwenye kuondoa na kukabiliana na vyanzo vya shinikizo la DAMU ili kuondoa mzizi wa tatizo na ndio maana mtu anaweza tumia dawa miaka na asipate nafuu ..hi ni kwasababu dawa HUSAIDIA kuondoa dalili za tatizo na sio tatizo na ndio maana. Baada ya nguvu ya dawa hiyo kuisha tatizo linajirudia na kuwa baya ambalo linakufanya uwe tegemezi kwa dawa hizo.
Vyanzo vya shinikizo la damu la juu mi kuziba na kuwa mwembamba kwa mishipa ya damu na kusababisha damu kulazimisha kupita ... Hivyo Siri ipo kwenye kusafisha mishipa ya damu ili kuondoa vikwazo hivyo vilivyo ziba mishipa na kusaidia mishipa kurudi katika Hali yake ya kawaida.

Kwa maelezo zaidi tumia liki 👇

https://www.whatsapp.com/business/

Afya yako ni jukumu lako

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maarifa ya Kuikomboa Afya yako. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram