25/10/2025
Kuchelewa au kukosa hedhi kwa muda wa miezi 3–4 (ambayo kitaalamu huitwa amenorrhea) kuna sababu mbali mbali zinazo pelekea zinazohusiana na homoni, afya ya uzazi, au hata maisha ya kila siku.
Sababu zinazoweza kusababisha kutokupata hedhi kwa muda mrefu:
1. Maradhi ya PID..haya ni maambukizi ya kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke yani kizazi (uterus),mirija ya uzazi(fallopian tubes) na ovary.
PID huleta adhari za kama
● Uharibifu wa mirija na kizazi
Maambukizi ya muda mrefu huleta makovu (scarring) na kuziba kwa mirija ya uzazi.
Hii inaharibu usawa wa homoni na mzunguko wa kawaida wa hedhi.
●Kuzorotesha kazi ya ovari
PID ikifika kwenye ovari, huleta uvimbe na kovu linalozuia kutolewa kwa mayai (ovulation).
Bila ovulation, hedhi inaweza kusimama au kupungua sana.
2. Mabadiliko ya homoni – mfano PCOS (Polycystic Ovary Syndrome), matatizo ya tezi (thyroid), au homoni za uzazi kutozunguka vizuri.
3. Msongo wa mawazo au kupungua/kuzidi uzito – stress, kula isivyo sahihi, au kufanya mazoezi kupita kiasi.
4. Matatizo ya mfumo wa uzazi – kama kuziba mirija ya uzazi, shida ya mfuko wa uzazi, au kovu kwenye uterasi.
5. Matumizi ya dawa fulani – mfano vidonge vya homoni, au dawa zinazobadilisha usawa wa homoni.
6. Magonjwa sugu – mfano kisukari, upungufu mkubwa wa damu, au matatizo ya ini/figo.
WASILIANA NASI KWA
WHAT'SAPP/PIGA
0769287659