05/03/2025
Vyakula vinavyoweza kudhuru figo zako:-
1. Vyakula Vyenye Sodiamu Nyingi.
E.g matumizi ya chumvi nyingi k**a ulaji wa fast foods ambazo Mara nyingi huwa na chumvi nyingi.
2. Vyakula Vyenye Phosphorus Nyingi :
Phosphorus nyingi inaweza kujikusanya kwenye damu hasa endapo figo zako hazifanyi kazi vizuri, na kusababisha mifupa dhaifu na magonjwa ya moyo. E.g Vinywaji vya Cola na Soft Drinks zenye asidi ya phosphoric & Baadhi ya bidhaa za maziwa k**a yogurt.
3. Vyakula Vyenye Potasiamu Nyingi:
K**a figo zako zimeathirika tayari punguza vyakula hivi. E.g nyanya, viazi vitamu, na ndizi
4. Vyakula Vyenye Sukari Nyingi:
e.g Sodas, energy drinks, na chai zenye sukari, Keki, biskuti, na p**i.
5. Ulaji wa nyama nyekundu kupindukia
Ulaji mkubwa wa nyama au vyakula vyenye protini kwa wingi unaweza kuweka mzigo kwa figo zako, hasa ikiwa zimeathirika tayari. Vyakula vilivyochakatwa pia vina chumvi nyingi na kemikali. E.g sausages, Steak na nyama nyekundu:
6. Pombe:
Pombe husababisha upungufu wa maji mwilini na kuongeza hatari ya shinikizo la damu, ambalo ni chanzo kikubwa cha uharibifu wa figo.
7. Vichocheo vya utamu vya Bandia (Sweeteners):
Utafiti mwingine unaonyesha kuwa matumizi ya vichocheo vya bandia yanaweza kuathiri kazi za figo. E.g soda, soft drink
Endapo umebainika kiwa na tatizo la figo, Zungumza na daktari wako juu ya vyakula unavyopaswa kutumia au kuepuka.
Mtag ndugu, rafiki au jamaa anaepaswa kujifunza hili!