12/09/2021
*BAWASIRI/MGOLO*
β
Bawasiri ni ugonjwa unaotokea katika njia ya haja kubwa, hujitokeza k**a uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje.
β
Kwa kiingereza hujuliakana k**a piles.
β
Na kitaalam hujulikana k**a hemorrhoids
πAINA ZA BAWASIRIπ
1. BAWASIRI YA NJE
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina hii ya bawasiri kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
2.BAWASIRI YA NDANI
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu.
β
Aina hii imeainishwa katika mainisho ya madaraja manne yafuatayo:
β
Daraja la 1 - Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
β
Daraja la 2 - Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya haja.
β
Daraja la 3 - Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya haja.
β
Daraja la 4 - Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya haja.
*DALILI ZA BAWASIRI*
β
Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
β
Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia
β
Muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa
β
Uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa
β
Haja kubwa yaweza kujitokea tu muda wowote