Sadick_Tibalishe

Sadick_Tibalishe Kwa Tiba na Ushauri +255714695406

12/01/2023
FAIDA ZA MATANGO:Tango Ni moja kati ya matunda yenye virutuhisho vingi na muhimu sana kwa mwanadamu. Ulaji wa tango kwa ...
06/01/2023

FAIDA ZA MATANGO:

Tango Ni moja kati ya matunda yenye virutuhisho vingi na muhimu sana kwa mwanadamu. Ulaji wa tango kwa ukawaida humsaidia mtumiaji kujiepusha na maradhi mbali mbali. Baadhi ya maradhi ambayo tango huweza kutibu au kuzuia yasitokee ni k**a vile.
1. Vidonda vya tumbo
2. Magonjwa ya ngozi
3. Majipu
4. Kulainisha ngozi kwa kutakata tango kwenye vipande vidogo vidogo Kisha kusugua uso taratibu kwa kutumia vipande hivyo
5. Inasafisha utumbo mwembamba na kurahisisha mmeng'enyo wa chakula.
6. Inatibu figo na kuongeza uwezo wa figo kuchuja maji hivyo kumuepusha mtumiaji na matatizo ya kuvimba miguu uzeeni
7. Huweka mwili katika hali bora zaidi kiafya

+255 714 695 406

FAIDA 8 ZA MCHICHA MWILINI:Mchicha ni moja kati ya mboga maarufu sana kwa watu wengi. Huenda wengi wetu tunatumia mchich...
05/01/2023

FAIDA 8 ZA MCHICHA MWILINI:

Mchicha ni moja kati ya mboga maarufu sana kwa watu wengi. Huenda wengi wetu tunatumia mchicha pasi na kujua kuwa unafaida kiasi gani mwilini mwetu. Basi leo napenda kukwambia kuwa kamwe usiuchukulie poa mchicha na wala usiuone ni sawa na mboga zingine kwani mchicha una faida lukuki kiafya ikiwa ni pamoja na kukinga na kutibu maradhi mbalimbali. Baadhi ya maradhi ambayo unaweza kujikinga nayo kwa kula mchicha kwa ukawaida ni k**a vile
1. Maumivu ya mgongo
2. Kusafisha njia ya mkojo
3. Ugonjwa wa figo
4. Minyoo
5. Baridi yabisi (Pneumonia)
6. Mchafuko wa damu
7. Matezi
8. Homa

Hayo ni baadhi tuu maradhi ambayo yanaweza yakazuilika au kutibika kwa kutumia mchicha kwa ukawaida.

MATAYARISHO:
Baada ya kujua faida za mchicha mwilini mwetu basi ni vyema ukajua namna Bora ya kuuandaa mchicha ili uweze kuwa na faida tajwa hapo juu. Wengi wetu tumekuwa tukiupika mchicha kwa desturi k**a vile tunavyopika mboga zingine. Ili mchicha uweze kuwa na faida hizo unatakiwa kuuchukua mchicha, uuoshe vizuri kisha chemsha kwa dakika zisizozidi 10 pasipo kuweka nyanya na viungo vingine, sana sana weka tuu chumvi na mafuta kidogo. Kunywa supu hiyo walau bakuli moja kwa siku kwa siku saba.

+255 714 695 406

USIPUUZIE HII:Huenda katika pitapita zako umekwisha wahi kuona watu wakiongelea faida za kula karanga mbichi. Lakini wen...
03/01/2023

USIPUUZIE HII:

Huenda katika pitapita zako umekwisha wahi kuona watu wakiongelea faida za kula karanga mbichi. Lakini wengi tumekuwa tukichukulia kwa mazoea au masihara pasipokujua faida zake kiundani na uhusiano wake kisayansi na miili yetu. Karanga mbichi ni moja ya chakula muhimu sana kwa miili yetu, huenda wengi wetu tunajua tuu kuwa zinatumika sana na wanaume katika kuboresha huduma ya unyumba, kwanza hebu niweke sawa hapa ili uweze kujua kuwa inakuwaje karanga mbichi zikatumika katika kuongeza uwezo wa mwanaume. Endapo wewe ni mwanaume na kwa namna moja ama nyingine umekuwa ukishindwa kurudia tendo baada ya mzunguko wa kwanza basi naomba hapa usome kwa umakini. Mbegu za mwanaume hutengenezwa na vitu vitu 6 yaani maji, sukari, vitamin C, zinc, protein na prostaglandins. Sasa kazi kubwa ya Zinc kwenye mbegu ni kuzikomaza kusudi ziwe tayari kwa kutoka na kurutubisha. Karanga na korosho ni vyakula vyenye zinc kwa kiasi kikubwa sana hivyo kula karanga mbichi au korosho kunapelekea mwanaume kukomaza mbegu nyingi zaidi ndiyo maana mtu anaweza akala karanga leo, kufikia kesho akajikuta anahamu sana ya kushiriki tendo, kwasababu mbegu nyingi zinakuwa zimekomazwa na zinc iliyopatikana baada ya kula karanga. Siyo kwa wanaume tuu bali hata kwa wanawake karanga ni kitu muhimu sana, hasa wanawake wenye ujauzito kuanzia wiki 4 mpaka 6 wanashauriwa sana kutumia karanga mbichi kwasababu karanga zina kirutubisho kinachoitwa 'folate' ambacho ni muhimu sana kwaajili ya kukuza ubongo na uti wa mgongo kwa mtoto aliyepo tumboni.

Pamoja na faida hizo lakini pia karanga hutajwa kuwa na faida na matokeo bora zaidi kwa wale wanaotaka kupungua uzito kwa njia ya diet kwasababu karanga hupunguza kwa kiasi kikubwa appetite ya kula hivyo kumfanya mtu kuhisi ameshiba kwa muda mrefu na hatimaye mwili kupungua.

Hali kadhalika kwa wale wenye matatizo ya kukosa choo, au kupata choo kigumu basi ulaji wa karanga hufanya mtu aweze kupata choo kwa ukawaida.

Address

Ilala
Dar Es Salaam

Telephone

+255714695406

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sadick_Tibalishe posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram