26/07/2023
CHANZO HALISI CHA KUVIMBA TEZI DUME.
Chanzo halisi cha KUVIMBA TEZI DUME au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa KUVIMBA TEZI DUME hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa KUVIMBA TEZI DUME haitokei kwa wanaume ambao wamewahi kufanyiwa operesheni ya kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa KUVIMBA TEZI DUME ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani.
Dhana (theories) kadhaa Zinazoelezea chanzo cha KUVIMBA TEZI DUME. Dhana hizo ni pamoja na
Uhusiano kati ya KUVIMBA TEZI DUME na homoni ya estrogen: Wanaume huzalisha testosterone, homoni ya muhimu sana katika mwili wa mwanaume. Hali kadhalika huzalisha pia estrogen ambayo ni homoni ya k**e kwa kiwango kidogo sana. Kadiri jinsi mtu anavyozeeka, ndivyo uzalishaji wa testosterone unavyokuwa mdogo na kufanya kiwango chake katika damu kupungua kulinganisha na kiwango cha estrogen ambacho huongezeka kwa kiasi fulani. Pamoja na kazi nyingine, estrogen pia huchochea ukuaji wa chembe hai za mwili. Tafiti zilizofanywa kwa wanyama zimeonesha kuwa hutokea kwa sababu kiwango kikubwa cha estrogen katika damu huchochea ukuaji wa seli za tezi dume na hivyo kufanya tezi dume kuvimba.
Uhusiano kati ya KUVIMBA TEZI DUME na Dihydrotestosterone (DHT): DHT ni kiasili kinachozalishwa kutokana na testosterone kwenye tezi dume, ambacho husaidia kuthibiti ukuaji wa tezi dume. Ingawa wanyama wengi hupoteza uwezo wa kuzalisha DHT wanapofikia umri wa uzee, baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa, kwa binadamu, hata k**a kiwango cha testosterone kitapungua sana katika damu, wanaume watu wazima bado wana uwezo wa kuzalisha kiasili hiki cha DHT katika tezi dume zao. Uzalishaji huu wa DHT huchochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa seli za tezi dume na kusababisha KUVIMBA TEZI DUME. Wanasayansi wamegundua kuwa wanaume watu wazima wenye kiwango kidogo cha DHT hawapati KUVIMBA TEZI DUME
Uhusiano kati ya KUVIMBA TEZI DUME na maelekezo ya seli. Dhana nyingine inasema kwamba baadhi ya seli kutoka katika sehemu fulani ya matezi yanayohusika na ukuaji mwilini hupewa maelekezo wakati mtu anapokuwa bado mdogo. Seli hizi hutunza maelekezo hayo na baada ya miaka kadhaa maelekezo haya huanzwa kutekelezwa na seli za matezi mengine. Mojawapo ya melekezo hayo ni kuchochea ukuaji wa tezi dume na kusababisha KUVIMBA TEZI DUME.
DALILI ZA KUVIMBA KWA TEZI DUME
Kukojoa mara kwa mara
Kubakiza mkojo kwenye kibofu
Kukujoa sana usiku
Maumivu wakati wa kukojoa
Kupungukiwa nguvu za kiume
UTI ya mara kwa mara
Mawe kwenye kibofu kutokana na mrundikano wa mkojo.
Figo kujaa maji. Hii sababu mkojo huo unarudi nyuma kuelekea figo (hydronephrosis)
Kupoteza fahamu(uremia)
Madhara ya Kuvimba Tezi Dume
BPH k**a ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na:-
Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)
Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo
Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
Madhara katika figo au kibofu
Shinikizo la damu
Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ej*******on)
Nimonia (Pneumonia)
Damu kuganda
KWA USHAURI ZAIDI WASILIANA NAMI 0712685645 AU 0624603899