Mira Wellness Tz

Mira Wellness Tz Karibu upate ushauri wa kiafya na tiba ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kwa mifumo yote ya mwili.

27/03/2026
27/03/2026

Umewahi kujiuliza kisukari kinaathiri vipi mwili wako? Na tofauti kati ya kisukari Type1 na 2 ni ipi?
Kisukari ni hali ambapo mwili unashindwa kudhibiti sukari kwenye damu. Kwa kawaida, kongosho huzalisha homoni inayoitwa insulin ambayo husaidia sukari kuingia kwenye seli ili kutoa nguvu.
Lakini kwa mtu mwenye kisukari, mfumo huvurugika.
Kisukari aina ya kwanza, ni ugonjwa wa kinga mwili ambapo mwili hushambulia kongosho, hivyo huzalisha insulin kidogo au hakuna kabisa. Mgonjwa hulazimika kutumia sindano za insulin maisha yote, na mara nyingi huanza utotoni au ujana.
Kisukari aina ya pili, mwili huzalisha insulin lakini haitumiki vizuri.
Mara nyingi huhusishwa na mtindo wa maisha na hali ya kurithi
Sukari ikibaki juu kwa muda mrefu inaweza kusababisha: Uchovu , Macho kufifia, Vidonda visivyopona, Magonjwa ya moyo na uharibifu wa mishipa
Njia ya kujilinda ni kula lishe bora, kufanya mazoezi, na kufanya vipimo mara kwa mara
Kwa ushauri na matibabu wasiliana nasi kwa namba 0713 622 699

26/03/2026

IMARISHA KINGA YA MWILI KWA NJIA RAHISI:
Unajua unaweza kuongeza kinga ya mwili wako kwa vyakula vya kawaida tu?
Anza na machungwa – yana vitamin C kwa wingi kusaidia mwili kupambana na maambukizi.
Kisha garlic (kitunguu swaumu) – ina nguvu ya kupambana na bacteria na virusi mwilini.
Usisahau ginger (tangawizi) – husaidia kupunguza uchochezi na kuimarisha kinga yako.
Pia kula spinach (mchicha) – una virutubisho muhimu k**a iron na vitamin A zinazolinda mwili.
Mwisho kabisa, yogurt – ina probiotics zinazojenga afya ya utumbo, ambayo ni msingi wa kinga imara.
Linda afya yako leo… kinga yako inaanza na unachokula! 💪✨
Kwa ushauri na matibabu wasikiana na Mira Wellness Tz kwa namba 0713 622 699 tutakuhudumia

24/03/2026

⚠️ MATUNDA HATARI KWA MGONJWA WA FIGO (USIYATUMIE HOLELA!)
K**a una matatizo ya figo, tahadhari na matunda haya:
🍌 Ndizi – Zina potassium nyingi sana, inaweza kuongeza mzigo kwa figo na kuathiri mapigo ya moyo.
🍊 Machungwa – Pia yana potassium na asidi nyingi, yanaweza kuchochea matatizo kwa figo dhaifu.
🥑 Parachichi – Licha ya kuwa na afya kwa watu wengine, kwa mgonjwa wa figo ni hatari kutokana na kiwango kikubwa cha potassium.
🌴 Tende – Zina sukari na potassium nyingi, zinaweza kuleta madhara zaidi kwa figo zisizofanya kazi vizuri.
⭐ Star fruit (Karambola / Tunda la Nyota) – HILI NI HATARI ZAIDI! Lina sumu inayoweza kuathiri ubongo kwa wagonjwa wa figo na kusababisha madhara makubwa.
👉 Kumbuka: Figo zikishindwa kuchuja vizuri, madini k**a potassium hukusanyika mwilini na kuwa hatari.
📌 Usikose episode inayofuata – nitakuletea matunda salama yanayofaa kwa mgonjwa wa figo!
Wasiliana basi kwa namba 0713 622 699 kwa msaada zaidi

13/03/2026

FREQUENT INFECTIONS (Maambukizi Yanayojirudia Mara kwa Mara)
Je, unapata maambukizi mara kwa mara k**a fangasi, maambukizi ya njia ya mkojo, maambukizi ya ngozi au ya mdomo?
Hii inaweza kuwa ishara kwamba kinga ya mwili wako imeanza kudhoofika au kuna tatizo la kiafya k**a kisukari.
Watu wengi hupata:
• Fangasi sehemu za siri wanaorudia mara kwa mara
• Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) yanayorudia
• Maambukizi ya ngozi k**a vipele au majipu
• Vidonda au maambukizi ya mdomoni
Tatizo hili hutokea mara nyingi kwa sababu mwili unapokuwa na sukari nyingi kwenye damu au kinga inaposhuka, bakteria na fangasi hupata mazingira rahisi ya kuzaliana.
Ndiyo maana baadhi ya watu hupata maambukizi kila mara hata baada ya kutumia dawa.
⚠️ Usipuuze hali hii. Maambukizi yanayojirudia yanaweza kuwa dalili ya tatizo kubwa zaidi ndani ya mwili.
Pata ushauri na msaada wa kitaalamu leo.
📍 Mira Wellness Tz tunakujali na unaweza kutupigia kwa namba unayoiona hapa chini tukusaidie
Call/Whatapp 0713 622 699

13/03/2026

ERECTILE DYSFUNCTION (KUKOSA NGUVU ZA KIUME)
Wanaume wengi hukumbwa na changamoto ya Erectile Dysfunction (ED) bila hata kujua chanzo chake.
Hali hii hutokea pale mwanaume anaposhindwa kupata au kudumisha uume kusimama vizuri wakati wa tendo la ndoa.
Tatizo hili linaweza kuathiri ndoa, kujiamini na hata afya ya akili.
Sababu zinazoweza kusababisha Erectile Dysfunction ni pamoja na:
• Kisukari (huathiri mishipa na neva za uume)
• Shinikizo la damu
• Kuziba au kudhoofika kwa mishipa ya damu
• Kuvuta sigara na matumizi ya pombe kupita kiasi
• Msongo wa mawazo (stress)
• Matatizo ya homoni za kiume (testosterone)
• Matatizo ya tezi dume
Dalili za Erectile Dysfunction:
• Uume kushindwa kusimama kabisa
• Uume kusimama lakini kushindwa kudumu muda wa kutosha
• Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa
• Kushindwa kuridhisha mwenza wako
Habari njema ni kwamba tatizo hili linaweza kudhibitiwa na kutibiwa mapema endapo utapata ushauri sahihi wa kitaalamu na tiba stahiki.
Usikubali kuishi na tatizo kimya kimya. Chukua hatua mapema kulinda afya yako na mahusiano yako.
📍 Mira Wellness Tz
📞 0713 622 699

Address

Kimara Dar-es-Salaam
Dar Es Salaam
±255713622699

Telephone

+255622622699

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mira Wellness Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Mira Wellness Tz:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram