19/09/2022
Dr.BILL
0745831146
Baridi yabisi ni moja ya magonjwa kwenye kundi la (autoimmune diseases) magonjwa yanayotokana na kinga ya mwili kushambulia tishu za mwili na kupekelea tishu hizi kututumka na kuvimba.Tatizo hili huathiri maeneo ya maungo na kuletekeza maumivu makali yasiyokwisha, kuvimba kwa joint na kusababisha ugumu kukunja viungo. Changamoto inaweza kuwa kubwa pale mpambano kwenye joint (inflammation) unapokuwa mkubwa na baadae maumivu hupungua.
Kwa mgonjwa mwenye baridi yabisi ni muhimu kurekebisha lishe na mtindo wa maisha k**a ambavyo nitaelekeza hapa chini ili kupunguza makali ya ugonjwa. Ugonjwa wa baridi yabisi k**a usipochukuliwa hatua za haraka kuudhibiti unaweza kusababisha matatizo makubwa k**a kuharibika kwa maungio, neva na athari kwenye mishipa ya damu.
Baridi yabisi husababishwa na muunganiko wa sababu ikiwemo lishe, vinasaba, mtindo wa maisha, vichocheo pamoja na kinga ya mwili.Tafiti zinasema kwamba kwa mgonjwa anayeanza tiba mapema hupata nafuu zaidi na kuepuka madhara ya baridi yabisi. Pamoja na dawa za hospitali wataalamu wa tiba asili tunashauri mgonjwa azingatie zaidi lishe na mazoezi ili kupunguza maumivu.
Dalili za Mgonjwa Mwenye Baridi Yabisi.
Dalili za baridi yabisi hutokana na kupotea kwa utando mweupe uliopo mwishoni mwa mfupa (cartilage). Utando ambao hupunguza msuguano kati ya mfupa na mfupa. Kuvimba kwa tishu zinazozunguka jointi na kukaza kwa joint. Kwa mgonjwa mwenye baridi yabisi ute uliopo kati ya mfupa na mfupa hupungua na kufanya mifupa kusagana. Dalili kuu za mgonjwa mwenye baridi yabisi ni
Maumivu ya joint-Kuvimba kwa tishu zinazozunguka maungio ya mifupa husababisha maumivu makali kwa mgonjwa. Jointi zinazoathirika zaidi ni kwenye mikono, enka, vidole vya miguuni na kwenye magoti.
Ngozi ya joints kuwa nyekundu,laini na inayochoma k**a vile imeungua moto.
Maumivu na kushindwa kusonga mbele baada ya kuamka asubuhi, hali hii huchukua dakika 30 na baaade mgonjwa anaweza kuendelea kutembea.
Mwili kufa ganzi na maumivu ya misuli
Kupata ugumu kwenye kutembea, kushika kitu, kufanya mazoezi na kupanda ngazi.
Kwa baadhi ya wagonjwa hupoteza hamu ya kula na kupata homa za muda mfupi.
Madhara gani ya Muda Mrefu Anaweza Kupata Mtu Mwenye Baridi Yabisi.
Kwa baadhi ya wagonjwa wenye baridi yabisi hupata madhara ya kiafya ya muda mrefu mwilini. Tafiti zimebaini matatizo haya huzaliwa na uwepo wa arthritis.
Kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi.
Maumivu ya kifua, pumzi kukata na kushindwa kupumua kutokana na athari kwenye mapafu.
Maumivu ya kichwa yasiyoisha.
Matatizo ya figo na kujikusanya kwa maji mwilini
Maumivu na kudhoofika kwa mifupa
Kuishiwa damu na kupata ganzi
Kuota vinyama vidogo vidogo kuzunguka eneo la maungio ambavyo huongeza ukali wa maumivu
Nini Kinasababisha Uugue Baridi Yabisi
K**a nilivoeleza mwanzo ugonjwa huu ni moja ya kundi la magonjwa ya autoimmune. Kumanisha kwamba ugonjwa unaletekezwa na mazingira ambayo husababisha kinga yako ya mwili ishambulie kimakosa tishu zinazozunguka maungio ya mifupa.
Swali la msingi ni kwanini kinga ya mwili ishambulie tishu kimakosa? Mpambano kwenye tishu inaweza kuletekezwa na vihatarishi vifuatavyo
Kuzorota kwa afya ya mfumo wa chakula
Lishe mbaya na vyakula vinavyoleta alegi (vyakula vinavyoletekeza mpambano k**a vyakula vilivyosndikwa, sukari na vyakula vilivyokaushwa kwa mafuta)
Uzito mkubwa na kitambi hasa kwa watu chini ya umri wa miaka 55
Mazingira yenye sumu ambayo yanaathiri mwili na kuvuruga mpangilio wa homoni, ndomana tunashauri utumie Detox Care Package yetu kutoa sumu kwanza kabla hujaanza tina nyingine.
Kushuka kwa utendaji wa kinga ya mwili kutokana na athari za kiafya na
Uvutaji wa sigara