Janeth Kalinga

Janeth Kalinga Tunatoa ushauri kuhusu elimu kwa wanafamilia wakiwemo wazazi na wasichana wa kazi kwani hawa ni waal

02/10/2022
Namshangaa Mungu kila wakatiMimi ni nani niwe hivi nilivyo?Wewe ni nani uwe hivyo ulivyo?Ndio, hivyo ulivyo kimuonekano,...
12/10/2021

Namshangaa Mungu kila wakati
Mimi ni nani niwe hivi nilivyo?
Wewe ni nani uwe hivyo ulivyo?
Ndio, hivyo ulivyo kimuonekano, kiimani, kiafya, akili, uwezo, elimu, familia, marafiki, ndugu, nk. Naaanisha hivyo hivyo ulivyo
Ninamshangaa Mungu kwa jinsi alivyoniumba kwa jinsi ya ajabu, kwa jinsi alivyonikuza kufikia hapa nilipo, kwa jinsi anavyonipambania na kunishindia
Asante Mungu kwa neema na baraka zangu nyingi kwangu na kwa msomaji wa ujumbe huu
Kipo chakumshukuru Mungu kwacho. Mwambie Mungu asante kwa hivyo ulivyo
Count your blessings one by one, utaona sababu ya kumshukuru Mungu
Yes, mshukuru Mungu

TV, GAMES NA VIFAA VINGINE K**A TABLETS NK.Wataalamu wanashauri mtoto wa miaka 2-5 asikae kwenye screen ya simu au compu...
11/10/2021

TV, GAMES NA VIFAA VINGINE K**A TABLETS NK.
Wataalamu wanashauri mtoto wa miaka 2-5 asikae kwenye screen ya simu au computer au kifaa kingine k**a ipads and gadgets zingine kwa muda mrefu
Kwanini? Watoto wa umri hiu wanatakiwa kuchangamsha viungo vya mwili. Mwili mzima uwe unashughulishwa kwa njia ya kukimbia, kupanda na kushuka, kuruka, kubembea, kutengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia mikono yao ili kuufikirisha ubongo hivyo kuongeza ubunifu
Sasa utakuta tunawawashia TV kianzia asubuhi mpaka wajikuta wanalala hapohapo
Hii sio sawa, ina madhara kwa afya ya mwili na ubongo wa mtoto












UNAONA NINI?Mungu ametupa macho ili tuweze kuona vitu mbalimbali, na wale wenye ulemavu wa macho Mungu amewapa namna ful...
29/09/2021

UNAONA NINI?
Mungu ametupa macho ili tuweze kuona vitu mbalimbali, na wale wenye ulemavu wa macho Mungu amewapa namna fulani ya kuhisi uwepo wa vitu mbele yao
Baada ya kuona kinachofwata ni tafsiri.
Na hii hutegemea na namna mtu anavyofikiri
Nimeamua kuwa na mtizamo chanya kwa kila jambo ninaloliona (positive thinking)
Haimaanishi kutochukua tahadhari, la hasha, nitachukua tahadhari zote lakini sitaruhusu mitizamo potofu initawale
Unaweza kugeuza kile unachokiona hata k**a sio kizuri, kwa mtizamo wako chanya utaanza kutafuta uzuri kabla ya kutafuta ubaya.
Na hii ni namna nzuri ya kuishi katika ulimwengu huu uliojawa na changamoto nyingi
Mtizamo wako unaweza kukupelekea kuona fursa zaidi kuliko kuona changamoto, kuona uzuri wa mtu zaidi kuliko kuona ubaya wake, kuona uwezo wa mtu zaidi kuliko kuona udhaifu wake, KUONA UKUU WA MUNGU ZAIDI KULIKO KUONA UKUBWA WA JARIBU

Aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo.
UNAONA NINI KWA MWENZI WAKO?
















TUSIPENDE KUWA NA MAWAZO FINYUUkubwa wa jambo hutuongezea uwezo wa kufikiri na kutendaUwezo ulio ndani mwetu ni mkubwa m...
28/09/2021

TUSIPENDE KUWA NA MAWAZO FINYU
Ukubwa wa jambo hutuongezea uwezo wa kufikiri na kutenda
Uwezo ulio ndani mwetu ni mkubwa mno, na hakuna mwanadamu ameweza kuutumia uwezo wote aliopewa na Mungu
Usiogope kuweka mipango mikubwa maana utaweza kutekeleza yale tu uliyaiambia akili yako ifanye
Usione changamoto unayopitia kuwa ni kubwa kuliko nguvu iliyo ndani mwako. Ukubwa wa changamoto unatufanya tufikiri kwa mapana namna ya kutatua
USIZIMIE MOYO, INUKA, PAMBANA, UNAWEZA KWA SABABU IPO NGUVU ISIYO YA KAWAIDA NDANI MWAKO
NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU















#


SO NATURAL Maisha yana mambo mengi. Kuna wakati wa kutulia na kufurahi kwingiKuna wakati wa maumivu na changamoto, mawim...
28/09/2021

SO NATURAL
Maisha yana mambo mengi. Kuna wakati wa kutulia na kufurahi kwingi
Kuna wakati wa maumivu na changamoto, mawimbini mengi kutoka pande zote
Yote hayo yanatuhusu sisi binadamu
BE YOU, KUWA WEWE MAANA WEWE UNA NGUVU YA AJABU NDANI MWAKO YA KUWEZA KUKABOLIANA NA HALI ZOTE
K**a ni gumu, na sio la kiwango chako basi utapewa mlango wa kutokea.
I love you good people
NAYAWEZA MAMBO YOTE KTK YEYE ANITIAYE NGUVU




NDOA YAKO INAWEZA KUPITA KWENYE VIPINDI MBALIMBALISio wakati wote bahari inakuwa kwenye hali ya utulivuKuna wakati kunak...
28/09/2021

NDOA YAKO INAWEZA KUPITA KWENYE VIPINDI MBALIMBALI
Sio wakati wote bahari inakuwa kwenye hali ya utulivu
Kuna wakati kunakuwa na nawimbi madogo madogo ambayo kimsingi hayana athari kubwa kwa watumiami wa bahari
Kuna wakati mawimbi yanaongezeka kiasi cha kuhatarisha maisha ya watumiaji wa bahari. Mitumwi inaweza kupinduka hata kusababisha chombo kuzama
Kuna wakati bahari inakuwa na utulivu, ukiwa unasafiri unakuwa huna wasiwasi, unarelax na kufurahia uumbali
Maisha ya ndoa yana nyakati tofauti tofauti hivyo jipange kushinda na sio kushindwa
Kukaa na mtu aliyezaliwa kwingine na kulelewa huko kwa malezi tofautitofauti inahitaji ukomavu wa akili na nguvu za rohoni ili uweze kujua ufanye nini katika majira gani.
Nakuombea kwa Mungu ktk kipindi ulichopo bado uwe na ujasiri wa kuendelea kusimamia kiapo chako na ukiona mawimbi yanapindua chombo kutaka kuleta kifo basi Roho Mtakatifu akufundishe cha kufanya usije kufa bureeee.
Kumbuka tunayaweza mambo yote katika yeye atutiaye nguvu.












UNGEPENDA KUWA NA MAFANIKIOKila mtu anapenda kuwa katika hali bora. Mafanikio ya kiuchumi na nyanja nyingineWala Mungu h...
23/09/2021

UNGEPENDA KUWA NA MAFANIKIO
Kila mtu anapenda kuwa katika hali bora. Mafanikio ya kiuchumi na nyanja nyingine
Wala Mungu hachukizwi na mafanikio yetu, tena anapenda tufanikiwe
Cha kujua ni kuwa mafanikio yetu yako katika Mungu. Mungu anataka tutumie neno lake k**a msingi wa mafanikio yetu
Amini neno la Mungu na kuwa ndio msingi wa baraka zako
We are blessed to be a blessing (Mwanzo 12:1-3)
Nawaombea wale wote wanaotamani kutoka, tuweke msingi wetu kwa Mungu kwanza, kumjua yeye na nguvu zake, tuchape kazi, tuzishuhudie baraka zake maishani mwetu














MIAKA 20 YA NDOANi katika kipindi hiki Mungu ametupa zawadi ya watoto wazuri 3Wamefanyika baraka katika nyumba yetu. Tun...
22/09/2021

MIAKA 20 YA NDOA
Ni katika kipindi hiki Mungu ametupa zawadi ya watoto wazuri 3
Wamefanyika baraka katika nyumba yetu. Tunawaombea Mungu awakuze hata kufikia kusudi la wao kuwepo duniani
Nawaombea wanandoa wote wanaohitaji baraka hii ya watoto Mungu awasikie
















18/09/2021

MIAKA 20 YA NDOA
Jambo la 4 ninaloweza kusema kuhusu hii miaka 20 ya ndoa ni kuwa na DHAMIRA YA DHATI YA KUKAA PAMOJA
Maana halisi ya ndoa ni kuwaweka watu pamoja wakati wote hasa wakati wa changamoto
Cha kushangaza ni kwamba, watu wengi tunatengana wakati wa changamoto badala ya kukaa pamoja
Mmojawapo wa wanandoa anapopata changamoto k**a ya kuumwa, kupata ulemavu wa kudumu, kuachishwa kazi, kufilisika nk ndio wakati anamhitaji mwenzi wake zaidi ili kumfariji na kumtia moyo.
Sio wakati wa kumsema na kumkimbia. Ni wakati wa wewe kuchukua nafasi ya kusaidia kwa uwezo wako wote tena bila masumango, manung'uniko wala majivuno
Ndio maana tunaweka viapo vya ndoa kuwa tutaishi pamoja katika RAHA NA SHIDA. Ila hutakiwa kusababisha maumivu
Nilimsikia binti mmoja akimwambia mwenzake "ananioa lakini akinizingua mamwacha". Huyu anaingia kwenye ndoa na mtizamo potofu. K**a huu ndio mtizamo wako huna haja ya kula kiapo cha ndoa maana huna dhamira ya ndani ya kuishi kwenye ndoa
Mwanaume anaoa huku amejiwekea kichwani kuwa hasumbuliwi na mwanamke. Akimsumbua atamwacha. Kwa msingi huu hakuna ndoa itakayodumu maana changamoto ni sehemu ya maisha. Na changamoto hazikimbiwi ila tunapambana nazo
Je! Una dhamira ya dhati ya kuishi ndani ya ndoa? K**a ndio, fahamu kuwa sisi ni wanadamu na tunaishi kwenye ulimwengu wenye fursa na changamoto mbalimbali. Vyote ni vyetu na vinapokuja tuvipokee pamoja na kuona namna ya kuvuka pamoja
Sisi tumepita na tunapita kwenye changamoto, lakini zinatufanya kuwa pamoja zaidi maana ndio maana halisi ya ndoa, kuwa na mtu wa karibu wa kukusaidia wakati wa shida lakini pia wa kufurahi naye unapobarikiwa
Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza ndugu kukaa pamoja kwa umoja.
Nawaombea wanandoa wote umoja hasa mnapopita katika changamoto mbalimbali za maisha.




















MIAKA 20 YA NDOAJambo la 3 ninaloweza kusema limetusaidia kufika hapa tulipo ni KUSIKILIZANA na KUELEWANAKuwa tayari kus...
17/09/2021

MIAKA 20 YA NDOA
Jambo la 3 ninaloweza kusema limetusaidia kufika hapa tulipo ni KUSIKILIZANA na KUELEWANA
Kuwa tayari kusikiliza mawazo ya kila mmoja wetu hata k**a wakati mwingine unaona kuwa unafahamu zaidi
Kusikilizana kunasaidia kusonga mbele pamoja na kutekeleza majukumu mbalimbali kwa pamoja
Kusikilizana kunamjengea kila mmoja ujasiri na kujiona kuwa anathaminiwa hivyo kuwa na nguvu ya kujituma na kufanya zaidi
Kusikilizana kunaimarisha mawasiliano kati ya wanandoa hivyo kuimarisha umoja na upendo
Hakuna mwenye jambo la peke yake. Tulivyo navyo ni vyetu na k**a hatuna wote tunajua hatuna. Shida yangu ni yake na shida yake ni yangu
Kusikilizana kunatusaidia kupanga kwa pamoja na kutekeleza kwa pamoja.
Nawatakia wanandoa wote masikilizano kwani huimarisha upendo, furaha na amani ndani ya nyumba
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu
















Jambo la pili lililotusaidia kufika hapa tulipofika ni UPENDOSikulazimishwa kuolewa na wala hakuna aliyenichagulia. Nili...
16/09/2021

Jambo la pili lililotusaidia kufika hapa tulipofika ni UPENDO
Sikulazimishwa kuolewa na wala hakuna aliyenichagulia. Nilimpenda mwenyewe k**a alivyo na wala sikupenda mali, elimu wala uchungaji wake.
Nilijua hivi vinaweza kupita wakati wowote na akabaki yeye k**a yeye. Hivyo nilimpenda yeye
Hii imetusaidia kutembea pamoja licha ya madhaifu tuliyo nayo.
Kuishi na mtu aliyelelewa sehemu tofauti, kabila tofauti, sio jambo jepesi. Inahitaji kuchukuliana kwa upendo na kuvumiliana, kutohesabu makosa ya mwingine tukijua kuwa sisi ni binadamu ambao ni wadhaifu, wakosa hivyo kusameheana
Upendo wa kweli ndani ya kila mmoja umetufanya kukaa pamoja kwa furaha pamoja na madhaifu ya kila mmoja wetu. Udhaifu wangu ni mtaji kwake na udhaifu wake ni mtaji kwangu
Namaanisha nini hapa, udhaifu wake kwangu ni project ya kuifanyika kazi, kutafuta namna ya kumsaidia kuondokana nao k**a ni udhaifu unaoweza kuondoka, kutafuta sababu au chanzo cha tatizo kwa lengo la kutafuta tiba au kutengeneza, kufanya kwa niaba yake pale anaposhindwa kufanya, na yeye kufanya vivyo hivyo.
Upendo haukosi kuwa na adabu. Tunaheshimiana, wakati wote kuhakikisha kuwa simuumizi kwa maneno au matendo yangu naye hufanya hivyo.
Zaidi ya yote ni pendo la Kristo lililondani mwetu hutuwezesha.
Sijidhanii kwamba nimefika..., nakaza mwendo...
Nawatakia wanandoa wote baraka, amani nafuraha













Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Janeth Kalinga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Janeth Kalinga:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram