Afya Plus+ Na Dk Devich

Afya Plus+ Na Dk Devich Page inahusiana na mambo ya afya ya mwili na magonjwa yanayo wasumbua wengi na matibabu yake

Tangawizi (ginger) ni zao la asili lenye faida nyingi kwa mwili wa binadamu, ndani na nje. Hapa kuna baadhi ya faida zak...
17/04/2025

Tangawizi (ginger) ni zao la asili lenye faida nyingi kwa mwili wa binadamu, ndani na nje. Hapa kuna baadhi ya faida zake:

# # # **Faida za Ndani ya Mwili:**
1. **Kupunguza Uchochoro na Mafua**
- Tangawizi ina antiviral na anti-inflammatory properties zinazosaidia kupunguza dalili za mafua, kikohozi, na maumivu ya koo.

2. **Kusaidia Kuhara na Kupunguza Tumbo Kuvimba**
- Inaweza kusaidia kusimamisha kichefuchefu, kutapika, na kuharakisha utoaji wa chakula kwenye mfumo wa utumbo.

3. **Kupunguza Maumivu ya Miguu na Viungo**
- Ina uwezo wa kupunguza inflammation, hasa kwa wenye arthritis au maumivu ya misuli.

4. **Kusaidia Kudhibiti Sukari ya Damu**
- Tangawizi inaweza kusaidia kudhibiti mazingira ya sukari kwa wenye ugonjwa wa kisukari (diabetes).

5. **Kupunguza Maumivu ya Menstruation**
- Watu wanaouma wakati wa hedhi wanaweza kunywa chai ya tangawizi kupunguza maumivu.

6. **Kusaidia Kupunguza Mafuta ya Mwili**
- Inaweza kusaidia kuchoma mafuta na kuongeza kiwango cha metabolism, hivyo kusaidia kupunguza uzito.

7. **Kuongeza Kinga ya Mwili**
- Ina antioxidants nyingi zinazosaidia kuimarisha mfumo wa kinga na kupambana na magonjwa.

# # # **Faida za Nje ya Mwili:**
1. **Kusaidia Kupunguza Madoa na Kuongeza Nuru ya Ngozi**
- Tangawizi inaweza kutumika kwenye ngozi kwa kupunguza madoa na kuifanya iwe na nuru zaidi.

2. **Kupunguza Uvimbe na Kuvu Kwenye Ngozi**
- Ina antifungal na antibacterial properties zinazoweza kusaidia kukabiliana na mwasho wa ngozi na uvimbe.

3. **Kusaidia Kuzuia Kuiva kwa Nywele**
- Inaweza kutumika kwenye nywele kuziweka laini na kuzuia ukatakavu.

4. **Kupunguza Kuvimba kwa Chuchu (Pimples)**
- Inaweza kusaidia kupunguza uchafu na bacteria zinazosababisha chunusi.

# # # **Matumizi ya Kawaida:**
- Kunywa chai ya tangawizi
- Kutumia k**a kiungo katika vyakula
- Kutumia mchanganyiko wake kwenye ngozi kwa mask
- Kuvuta k**a dawa ya asili (supplements)

Tangawizi ni dawa nzuri ya asili, lakini kwa watu wenye shida za tumbo au wenye allergies, ni vizuri kushauriana na daktari kabla ya kuitumia kwa kiasi kikubwa.

23/11/2022
DAWA ZA ASILI  ZINAZOTIBU CHUNUSIChunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza k**a viuvimbe au vipele vidogo vidogo hasa...
20/09/2017

DAWA ZA ASILI ZINAZOTIBU CHUNUSI

Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza k**a viuvimbe au vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso, kifuani na hata mgongoni.

Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani bakteria.

Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris. Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni 17.

Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe (adolescents).

DAWA ZA ASILI 20 ZINAZOTIBU CHUNUSI

1. Barafu

Dawa ya kwanza katika orodha hii ni barafu. Barafu inaweza kuzipunguza chunusi zionekane ni ndogo na kupunguza madhara yatokanayo na chunusi.

Namna ya kutumia barafu kutibu chunusi ni rahisi na haraka zaidi. Chukua kipande cha barafu na ukipitishe sehemu zilipo chunusi mara kadhaa kwa dakika 3 hadi 5 hivi.

Kumbuka kusafisha vizuri uso wako kabla ya kuanza kupitisha hii barafu kwenye uso wako.

2. Kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu hujulikana k**a kitu cha kushangaza katika tiba huko mashariki ya mbali, Kitunguu swaumu ni maajabu ya Mungu mwenyewe.

Kina nguvu za kuua bakteria mbalimbali na kuzuia magonjwa ikiwemo kutibu chunusi. Kuna namna 2 za kutumia kitunguu swaumu kutibu chunusi; namna ya kwanza ni kukitumia kitunguu swaumu kwenye vyakula vyako unavyopika kila siku, namna ya pili ni kukitwangwa kitunguu swaumu na kukipaka moja kwa moja katika sehemu yenye chunusi.

Ukiacha harufu yake isiopendwa na wengi, kitunguu swaumu kinaweza kukupa afya na urembo unaouhitaji.

Kitunguu swaumu husaidia kupunguza ukubwa wa chunusi. Hata hivyo uwe makini kwani kitunguu swaumu kinaweza kuunguza ngozi yako usipokuwa makini na ili kuepuka hili jaribu kuchanganya kidogo na maji baada ya kukitwanga ili kupunguza makali yake.

3. Limau

Dawa nyingine nzuri kwa ajili ya chunusi usoni na mwilini ni limau. Limau linajitokeza kwenye vyakula vingi tunavyokula kila siku mathalani limau halikosekani pakiwepo supu au mapishi yoyote ya samaki.

Limau lina kiasi kingi cha vitamini C ambayo inaweza kutumika k**a antibiotiki inayozuia kuongezeka na kukua kwa bakteria wanaosababisha chunusi.

Limau pia ina tindikali maalumu inayohamasisha chunusi kutoka katika ngozi.

Unachotakiwa kufanya ni kukata limau pande mbili au nne na upake majimaji yake moja kwa moja kwenye chunusi pole pole kwa dakika 10 hivi kasha jisafishe na maji safi.

Tindikali katika limau inaweza kuzidhuru seli zilizopo juu ya ngozi yako hivyo tumia dawa hii mara 1 au 2 tu kwa wiki na siyo kila siku.

Vitamini C iliyomo kwenye limau husaidia kukinga mwili dhidi ya magonjwa mengi sababu ndiyo vitamini inayosaidia kuongeza kinga ya mwili.

Kinga ni bora kuliko tiba!

Hivyo tumia vitamini C mara kwa mara au kunywa juisi ya limau kila siku ili kuweka mwili wako katika afya bora zaidi muda wote.

4. Mshubiri (Aloe Vera)

Mshubiri au Aloe Vera k**a ilivyozoeleka na namna nzuri kwa wale wote wanaotaka kubaki na ngozi nyoro na ya kupendeza kila siku.

Chukua kipande cha mshubiri freshi na ukikate kasha chukua maji maji yake (jeli) na upake moja kwa moja kwenye uso wako na ujisuguwesuguwe kwa dakika 15 hadi 20 hivi pole pole kasha jisafishe na maji safi.

Tumia dawa hii mara 2 au 3 kwa wiki. Hii ndiyo njia rahisi ya kutibu chunusi bila kukuacha na madhara mengine mabaya.

5. Dawa ya mswaki

Dawa ya mswaki au dawa ya meno ni dawa nyingine ya asili unayoweza kutumia kujitibu chunusi. Hii inatumia usiku tu.

Pakaa kiasi fulani cha dawa hii kwenye chunusi zako na uende ulale kasha asubuhi jisafishe na maji safi. Fanya zoezi hili kila baada ya siku 1 mpaka umepona.

6. Tango

Tango ni tunda na ni mboga pia na ni chanzo kizuri cha potasiamu na vitamini nyingi ambazo zina kazi mhimu katika ngozi yako na huifanya ngozi ngozi ionekane laini na yenye kupendeza.

Tango ni moja kati ya dawa kamili za kutibu chunusi. Ni rahisi kulitumia tango kutibu chunusi.

Kata tango katika silesi ndogo ndogo na uvibandike juu ya ngozi yenye chunusi. Kumbuka kusafisha kwanza ngozi yako kabla ya kubandika hizi silesi za tango.

Namna nyingine na kusaga tango upate juisi yake na uchanganye na sukari kasha jisuguwe kwenye ngozi yenye chunusi kwa dakika 2 au 3 kisha jisafishe na maji safi.

7. Asali

Asali hasa asali mbichi ya asili ni dawa nzuri sana ya kutibu chunusi. Asali ni antibiotiki ya asili ambayo husaidia kupunguza ukubwa wa chunusi na maumivu ya chunusi.

Asali inaweza pia kuzuia ngozi yako isipatwe na maambukizi mengine ambayo yangeweza kusababisha matatizo kwenye ngozi au makovu.

Hivyo asali inachukuliwa k**a moja ya dawa za asili nzuri za kutibu chunusi unazotakiwa kuzijaribu.

Kwanza safisha ngozi yako vizuri na maji ya uvuguvugu kasha jipake asali moja kwa moja sehemu yenye chunusi. Iache kwenye ngozi kwa dakika 30 kisha jisafishe na maji safi ya uvuguvugu.

Tumia dawa hii mara 2 au 3 kwa wiki na uniletee majibu.

8. Baking Soda

Moja ya sababu za kutokea chunusi katika ngozi yako ni kuwepo kwa takataka au uchafu juu ya ngozi yako na njia rahisi ya kusafisha taka hizo ni kwa kutumia baking soda hivyo kuifanya ngozi ipumuwe vizuri.

Kwahiyo ukiwa na chunusi hebu fikiri kuhusu baking soda. Baking Soda husaidia kubandua seli za ngozi zilizokufa na kufanya mafuta yaliyozidi kuondoka.

Ni rahisi zaidi kutumia baking soda kutibu chunusi. Chukua baking soda na uchanganye kidogo na vijiko vinne vidogo vya maji au vya maji maji ya limau na upake uji huo moja kwa moja kwenye chunusi. Subiri kwa dakika 10 na ujisafishe na maji ya moto.

9. Mvuke

Mvuke husaidia kusafisha ngozi. Ni rahisi sana kutumia mvuke kutibu chunusi.

Chemsha maji kwenye sufuria jikoni funika na uache nafasi kidgo ya mvuke uwe unatoka, kisha chukua taulo na ujifunike usoni huku ukisogelea karibu na mvuke unapokea na uruhusu mvuke huo ukupate kwa mbali.

Baki hapo kwa dakika 5 mpaka 10 hivi huku ukiwa umetulia (relaxed). Huu mvuke utakusaidia pia kujis**ia mtulivu na kukuondolea mfadhaiko wa akili.

Mwishoni mwa zoezi jisafishe uso wako na maji ya baridi.

Endelea kusoma makala hii kujifunza zaidi dawa nyingine za asili za kutibu chunusi.

10. Papai

Dawa nyingine madhubuti ya chunusi ni papai. Tunda hili ni moja ya matunda yanayotumika kwa ajili ya urembo hasa kwa wanawake.

Chukua papai na uchanganye na asali kidogo, likoroge kidogo na ujipake sehemu yenye chunusi moja kwa moja kwa dakika 15 hivi hivi kisha jioshe uso wako na maji ya moto kisha malizia na kujisafisha na maji baridi mra baada ya kutumia maji ya moto.

Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa wiki.

11. Aspirin

Aspirin inaweza kuwa ni moja ya dawa nzuri za chunusi. Chukua vidonge viwili au vitatu vya aspirin na utwange upate unga wake kisha ongeza maji kidogo upate uji mzito hivi.

Kisha pakaa mchanganyiko huo moja kwa moja sehemu yenye chunusi kwa 10 hivi kisha jisafishe na maji safi.

Fanya zoezi hili mara 1 tu kwa wiki.

12. Ute mweupe wa yai

Hii inaweza kuchukuliwa k**a njia rahisi na isiyo na gharma katika kutibu chunusi. Kwa mjibu wa wanasayansi kutumia mchanganyiko wa ute mweupe wa yai na maji maji ya limau ni namna nzuri ya kutibu chunusi.

Changanya ute mweupe wa mayai matatu na kijiko kidogo kimoja cha maji maji ya limau na ukoroge vizuri. Pakaa mchanganyiko huu usoni na uache kwa dakika 15 hivi kisha jisafishe na maji moto.

Fanya zoezi hili mara 1 au 2 tu kwa wiki.

13. S**i ya tufaa

S**i ya tufaa (Apple cider vinegar) ni moja kati ya dawa zinazojulikana katika kutibu chunusi ahsante kwa uwezo wake wa kurudishia tindikali katika ngozi. Bakteria wabaya, mafuta na uchafu mwingine wowote utaondoka juu ya ngozi yako bila kupenda ukitumia dawa hii.

Tafuta tu s**i ya tufaa ya asili kabisa bila kuongezwa vingine ndani yake. Changanya s**i hii na maji kidogo na umwagie ndani ya kitambaa kisafi kizito na upitishe hiki kitambaa sehemu yenye chunusi mara kadhaa kwa dakika 10 kisha jisafishe uso wako na maji ya baridi.

14. Chumvi na mafuta ya zeituni

Mchanganyiko wa chumvi na mafuta ya zeituni (olive oil) ni dawa nyingine inayotibu chunusi. Mafuta ya zeituni yandhibiti bakteria na huondoa sumu vitu ambavyo vinafanya kuwa dawa nzuri kutibu chunusi na matokeo ya chunusi.

Changanya nusu kijiko kidogo cha chai cha mafuta ya zeituni na kiasi kidogo cha chumvi katika chombo kisafi. Safisha vizuri uso wako. Kisha jipake mchanganyiko huu kwenye uso wako na uache kwa dakika 10 hivi.

Mwisho jisafishe vizuri na maji ya uvuguvugu.

15. Mdalasini na asali

Mchanganyiko wa mdalasini na asali ni dawa nzuri ya kutibu chunusi.

Changanya asali vijiko vikubwa viwili na mdalasini ya unga kijiko kikubwa kimoja. Safisha vizuri uso wako.

Kisha pakaa mchanganyiko huo kwenye uso wako usiku na asubuhi ujisafishe vizuri uso wako.

16. Binzari, maziwa na asali

Unahitaji vitu vifuatavyo:

a)Binzari ya unga b)Maziwa fresh c)Asali d)Bakuli e)Kijiko cha chai

Hatua kwa hatua namna ya kutumia:

a)Weka kijiko kidogo kimoja cha binzari ya unga ndani ya bakuli b)Ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali ndani yake c)Ongeza tena kijiko kidogo kimoja au viwili vya maziwa fresh d)Changanya vizuri mchanganyiko huu upate uji mzito e)Pakaa pole pole sehemu yenye chunusi mchanganyiko huu f)Baada ya dakika 5 au 7 hivi jisafishe uso wako g)Fanya zoezi hili mara 2 au 3 tu kwa wiki

17. Uwatu (Fenugreek)

Uwatu ni dawa nyingine ya asili inayotumika kutibu chunusi. Uwatu unaondoa sumu na maambukizi mbalimbali.

Hizi ni hatua chache cha kutibu chunusi kwa kutumia uwatu::

a)Chukua kijiko kidogo cha unga wa mbegu za uwatu b)Ongeza maji kidogo kupata uji mzito (paste) c)Pakaa mchanganyiko huu sehemu yenye chunusi d)Acha kwa dakika 20 au kwa usiku mzima e)Kisha jisafishe a maji safi f)Fanya zoezi hili mara 2 au 3 kwa wiki

18. Tumia maganda ya ndizi

Maganda ya ndizi ni dawa nyingine nzuri ya kuondoa chunusi. Unachohitaji ni kuwa tu na maganda ya ndizi kwa ajili hii.

Hatua kwa hatua namna ya kutumia dawa hii:

a)Menya ndizi na ule b)Chukua ganda la ndizi uliyokula na ukandamizekandamize sehemu ya ndani ya ganda hilo sehemu yenye chunusi c)Subiri kwa dakika 30 kisha jisafishe na maji safi

19. Parachichi na asali

Unahitaji:

a)Kijiko kimoja cha asali b)Parachichi 1

Hatua kwa hatua namna ya kufanya tiba hii:

a)Safisha vizuri uso wako b)Kausha na taulo uso wako c)Chukua nyama ya ndani ya parachichi d)Ongeza asali kijiko kimoja ndani ya parachichi e)Changanya vizuri vitu hivyo viwili upate uji mzito. f)Pakaa mchanganyiko huo kwenye sehemu yenye chunusi g)Acha kwa dakika 15 mpaka 20 hivi h)Mwisho jisafishe na maji ya uvuguvugu na ujifute vizuri

20. Mtindi na asali

Kutumia mtindi na asali ni moja ya dawa rahisi zaidi za kutibu chunusi.

Unahitaji:

a)Kijiko kimoja cha asali b)Kijiko kimoja cha mtindi

Hatua kwa hatua namna ya kutumia:

a)Changanya hayo mahitaji yako mawili vizuri b)Pakaa ple pole mchanganyiko huu kwenye uso wako c)Ikikauka unapaka tena, hivyo hivyo mpaka umepaka mchanganyiko wote d)Acha dakika 10 mpaka 15 hivi e)Mwishoni jisafishe na maji ya uvuguvugu

Mambo mhimu ya kuzingatia

1. Fanya mazoezi ya viungo kwa saa moja kila siku 2. Kunywa maji mengi kila siku 3. Ondoa mfadhaiko (stress) 4. Weka homoni sawa k**a hazipo sawa 5. Kuwa msafi wa mwili wote kila mara 6. Usiziguse chunusi au kuzitoboa na mikono yako au na chochote kuepuka makovu yasiyo ya lazima 7. Epuka vyakula vifuatavyo k**a unasumbuliwa na chunusi kila mara, navyo ni pamoja na:

a)Vyakula vyenye mafuta sana

b)Vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi

c)Kahawa

d)Chai ya rangie)

e)Pombe na vilevi vingine

f)Chokoleti

g)Popcorn

h)Maziwa

i)Mapera

j)Vyakula vya kwenye makopo

FAIDA YA TANGO KATIKA MWILI WA BINADAMU # #MATANGO si matunda mageni katika jamii ya Watanzania kwani hulimwa katika mik...
20/09/2017

FAIDA YA TANGO KATIKA MWILI WA BINADAMU # #
MATANGO si matunda mageni katika jamii ya Watanzania kwani hulimwa katika mikoa mbalimbali na mengine kuagizwa kutoka nchi za nje, hivyo kufanya upatikanaji wake uwe mzuri katika masoko ya ndani.Kihistoria,asili ya matango ni

bara la Asia, hasa nchini India. Na matango yalianza kulimwa huko Asia zaidi ya miaka 3000 na baadae zao hilo kusambaa na kupokowa vizuri na nchi za magharibi hasa Ufaransa katika karne ya tisa. Baadae Uingereza na Marekani walianza kulima zao hilo katika karne ya 14 na 16.

Matango yana uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali na kwa njia rahisi isiyokuwa na madhara kwa mtumiaji, pia matibabu yake ni rahisi yenye kumuwezesha kila mwanajamii kumudu gharama, kwani yamekuwa yakiuzwa kwa kwa bei nafuu sana.

Baadhi ya madini yanayopatikana katika matango ni Calcium, Phosphorus, Potassium, Zink, Vitamin B, C na E. Madini haya ni muhimu sana katika mwili wa binadamu na yanapopungua au kukosekana mwilini husababisha magonjwa mbalimbali k**a magonjwa ya moyo na saratani.

Faida za tango mwilini

Madini ya Potassium yanayopatikana katika matango ndicho chakula cha moyo kwa sababu huwezesha moyo kupiga mapigo katika hali ya kawaida.

Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha potassium k**a tango ni muhimu sana hasa kwa mtu mwenye tatizo la moyo, shinikizo la chini la damu. Pia tango linaaminika kupunguza kiwango cha rehemu, mafuta

yenye madhara mwilini, huimarisha misuli na pia husaidia usagaji wa chakula tumboni hivyo kuondoa tatizo la ukosefu wa choo.

Virutubisho vilivyopo katika tango hutoa nafuu kawa mtu mwenye matatizo ya ini, kongosho, figo na matatizo katika kibofu cha mkojo.

Watalamu wetu wanatueleza kuwa tango lina kirutubisho kinachojulikana k**a �erepsin� ambacho husaidia uzalishaji wa �amino acids� ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa protini mwilini. Vile vile tango lina kiwango kikubwa cha vitamin C hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo yatokanayo na ukosefu wa vitamin hiyo, k**a vile fizi kuvuja damu, upunguvu wa damu kwa watoto wachanga na kuota meno na mifupa vibaya.

Kinga ya Saratani Pengine faida kubwa kuliko zote unazoweza kuzipata kwa kula tango au juisi yake mara kwa mara ni kinga dhidi ya saratani za aina mbalimbali. Jambo hili linalotokana na ukweli kuwa tango lina kiwango kikubwa cha uchachu �alkaline�, na kufanya seli za saratani kuwa katika mazingira magumu ya kusambaa mwilini, kwani kwa kawaida seli za saratani

haziwezi kuishi kwenye mazingira zenye uchachu. Hivyo ni vyema kujijengea mazoea ya k

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255654347988

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya Plus+ Na Dk Devich posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram