23/06/2023
Je! unajua kuwa mwanaume utumia chini ya sekunde 30 wakati anapokojoa?
kwa mujibu wa tafiti bora kabisa zilizowai kufanywa na taasisi ya magonjwa ya mfumo wa mkojo zinasema kuwa mwanaume hutumia chini ya sekunde 30 anapokojoa k**a hana matatizo katika mfumo wake wa mkojo .
Na endapo mwanaume atatumia zaidi ya sekunde 30 kukojoa k**a hakunywa maji mengi sana ina maana tayari ameanza kupata matatizo katika mfumo wake wa mkojo.
Na tafiti zinaendele kusema wanaume wenye zaidi ya miaka 40 wako katika hatari kubwa ya kupata matatizo katika mfumo wao wa mkojo na katika mfumo wao wa uzazi , Na mara nyingi sana tatizo kubwa linalowakubwa wanaume wenye umri huu ni ''Tatizo la kuvimba kwa TEZI DUME''
Na hii hutokana na kuongezeka kwa vichocheo vya homoni katika mwili wa mwanaume hivyo kusababisha kuvimba kwa tezi hii na kuleta madhara katika mfumo wa mkojo.
Mpendwa msomaji wangu kabla ya kuendelea ningependa tupate kidogo kufahamu maana ya TEZI DUME.
TEZI DUME ni kiungo katika mfumo wa uzazi wa mwanaume na kiungo hiki kiko chini kidigo ya kibofu cha mkojo na kiungo hiki kinazu nguka mrija unaoleta mkojo nje.
Kiungo hiki hutumika kuzalisha ute telezi unaosaidia kupita vizuri mbegu za kiume zinapotoka nje.
Ni nini hasa hupelekea kiungo hiki kuvimba?
Yapo magonjwa ambayo yamedhibitishwa kusababisha kiungo hiki kuvimba nayo ni;
1: Uvamizi wa bakteria katika TEZI DUME{prostatitis}
2: Kansa ya TEZI DUME{prostate cancer}
3: Kukua na kuongezeka kwa TEZI DUME{benin prostate hypatrophy}
Utafiti unaendelea kusema kuwa aina hii ya tatu {3} ya tatizo linalosababisha kuvimba kwa TEZI DUME ndilo huwakumba wanaume wengi hasa wenye umri zaidi ya miaka 40.
Ni dalili gani utaziona baada ya TEZI DUME kuvimba?
Dalili zifuatazo huanza kuonekana baada ya tezi kuvimba.
1: kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
2: Maumivu wakati wa kukojoa,
3: Kutumia nguvu kusukuma mkojo wakati wa kukojoa ,
4: Mkojo kupungua nguvu na presha wakati unapotoka
5: Kushindwa kuuzuia mkojo kutoka