02/12/2022
Katiika Ukurasa wako, unazungumza na wateja sahihi wa Bidhaa zako?
Au Umechagua tu kufanya hiyo Biashara kwa sababu watu wengi wanafanya, Uliambiwa kuna Hela, au una jaribu tu?
Labda Pengine, unafanya Kwa sababu unapenda, hata k**a hakuna faida yoyote unayoipata?
Watu wengi sana, wengine ni wanafunzi wangu hapa, wanafanya sana hili kosa.
"Kufanya Biashara Kwa sababu watu wengi wanaifanya na kudhani watapata Pesa za Haraka Haraka."
Acha KABISA Kufanya Hivyo, Utakata Tamaa mapema mno!
Acha kudhani kwamba, kwa sababu watu wengi wanafanya Biashara flani, basi na wewe unaweza kuifanya.
Au Kwa sababu unaweza kufanya Biashara flani, basi automatically tu utaanza kupata wateja.
Aina ya Biashara unayoichagua, pamoja na uhitaji wa Biashara yako sokoni, ndio vitaamua k**a utapata wateja au lah (Hasa huku Mtandaoni).
Kazi kubwa unayopaswa kufanya ni kufanya utafiti mdogo kwanza, kabla ya kuchagua aina ya Biashara na Bidhaa unayotaka kuileta Sokoni.
Hili unapaswa kulifanya Kabla hata hujaanza kufungua Ukurasa wako wa Biashara.
You see, inawezekana unapata changamoto kwa sababu, chimbuko la Biashara na bidhaa zako, halitokani na kuangalia uhitaji wa soko.
Umeanzisha Biashara yako kwa sababu Rafiki zao wanafanya.
K**a wewe mwenyewe hupendi kubeba Mikoba, hupendi kufanya Makeup, ni ngumu sana kuongea lugha moja na wateja wako.
Je, hii ina maanisha uache sasa kufanya Biashara yako au Kuuza Bidhaa zako?
Majibu utayapata kwa kujiuliza Maswali haya;
▶ Je, wateja wanaweza kununua Bidhaa zako Mara kwa mara?
▶Je, wateja wanaweza kununua Bidhaa hizo Online?
▶Je, Wateja wako tayari kutumia Pesa zao ili kupata Bidhaa zako?
▶Kuna Changamoto gani sokoni, kuhusu Bidhaa zako?
Majibu ya Maswali haya, yatakuongoza kutambua k**a unastahili kuendelea kutumia pesa na muda wako katika Bidhaa au Biashara unayoifanya.
Muhimu ninachoweza kukuambia ni kwamba, sio KOSA kabisa kubadili bidhaa au aina ya Biashara unayoifanya.
Kwa sababu ulianza na aina flani ya Bidhaa, basi haimaanishi huwezi kubadilika.
Hata makampuni makubwa duniani, yamewahi kufanya mabadiliko kutokana na uhitaji wa soko.
Umenielewa vizuri?
Anza Kufanyia kazi👏