17/04/2024
PID(PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI)
UGONJWA WA PID NI NINI??
Ni ugonjwa wa maambukizi unaotokea katika via vya uzazi vya mwanamke ambapo huhusisha maambukizi katika shingo ya kizazi (CERVICITIS) , nyama katika mfuko wa uzazi (ENDOMETRITIS) na mirija ya uzazi (SALPINGITIS)
VYANZO NA VIHATARISHI VYA KUPATA UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)
Vimelea aina ya NEISSERIA GONORHOEAE pamoja na CHLAMYDIA TRACHOMATIS ndio chanzo cha
maambukizi ya ugonjwa wa PID ingawaje kuna aina kadhaa za vimelea vinahusishwa kusababisha ugonjwa wa PID hivyo nilivyotaja ndio vinaongoza Kwa umaarufu kusababisha ugonjwa wa PID.
Pamoja na vimelea hao kuwa chanzo kikuu cha
ugonjwa wa PID zipo njia KADHAA HATARISHI
KUSABABISHA MAAMBUKIZI HAYA NAZO NI;
*kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) k**a njia mojawapo ya uzazi wa mpango.
*Kufanya ngono isiyo salama
*Maambukizi ya njia za uzazi mara baada ya kujifungua au mimba kuharibika.
*Kuambukizwa kupitia damu yenye vimelea wa PID.
*Kupata maambukizi wakati wa kutoa mimba kwa njia isiyo salama.
DALILI/VIASHIRIA VYA UGONJWA WA PID
Kuna dalili mbalimbali zinazoweza kuashiria ugonjwa huu
wa PID miongoni mwa dalili hizo ni,
*Mwanamke kupata maumivu ya tumbo hasa maeneo ya
chini ya kitovu.
*Kupata maumivu wakati wa kukojoa.
*Kupata homa na kuhisi kichefuchefu.
*Kupata maumivu ya mgongo na kutapika
*Kutokwa na hedhi bila mpangilio
*kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
*Kutokwa na uchafu(utoko)mweupe ukeni unaotoa
harufu mbaya.
NAMNA YA KUJIEPUSHA NA UGONJWA WA PID
Pamoja na kuwepo kwa dawa za kutibu tatizo hili ni vyema ukajiepusha na vihatarishi vya kupata tatizo hili kwa kuzingatia yafuatayo,
*Epuka kufanya ngono isiyo salama.
*Jiwekee tabia ya kufanya vipimo mara kwa mara hasa
kizazi.
*Usifanye mapenzi mara baada ya kujifungua au mimba
kutoka mpaka utakapohakikisha shingo ya uzazi
imefunga vema.
*Kuwahi kuonana na daktari unapoona dalili za ugonjwa
*Kuwa msafi na kula lishe bora
Note:
Uonapo dalili za ugonjwa huu wahi kupata matibabu
kwani ugonjwa huu ni mkubwa huweza kusababisha
ugumba ikiwa hautapata tiba vizuri.
asante kwa kuwa nami kusoma ujumbe huu rafiki k**a una