16/03/2023
MVURUGIKO WA HOMONI HORMONE IMBALANCE
#0756601653
Mvurugiko wa homoni za mwanamke ni kitendo cha kuongezeka au kupungua kwa vichochezi katika mwili wa mwanamke pale anapo pata hedhi, hivyo kufanya mwili kubadilika. Mvurugiko huo huathiri kila mwanamke kwa zaidi ya 80%.
VYANZO/SABABU ZA MVURUGIKO WA HOMONI
Mvurugiko wa homoni ni tatizo linalowakumba wanawake wengi kwa sasa, hii ni kutokana na maisha wanayoishi, elimu finyu waliyonayo juu ya afya zao na kutokula kulingana na makundi ya damu. Vyanzo vya kuvurugika kwa homoni ni:
-Uwepo wa sumu mwilini
-Unbalanced Lifestyle (mfumo mbovu wa maisha)
-Umri ukienda sana
-Kukoma kwa hedhi
-Kutofanya mazoezi, na kutokulala masaa anayostahili kwa siku
-Uzito mkubwa
-Mabadiliko ya mazingira au hali ya hewa
-Msongo wa mawazo
-Upungufu wa lishe mwilini
-Matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango
-Utoaji wa mimba
-Family History (Upungufu au ongezeko ya homoni ya progesterone na Estrogen)
- Wanawake wa Afrika wengi wana hili tatizo la ongezeko ya Homoni ya Estrogen, ndiyo maana wana maumbile makubwa"
DALILI ZA MVURUGIKO WA HOMONI
Mfumo wa homoni ni muhimu sana kwa afya ya ubongo na mili yetu. Husaidia kuzuia magonjwa yasiyo ambukizi kadri umri unavyo songa mbele. Baadhi ya dalili zinazoweza kuonekana kwa mtu mwenye changamoto ya mvurugiko wa homoni ni k**a vile:
- Ukavu ukeni
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Kutoa jasho usiku
- Maumivu chini ya kitovu wakati wa hedhi
- Upungufu wa hamu ya tendo la ndoa
- Mabadiliko ya siku za hedhi na kupata hedhi kwa muda mrefu unaozidi siku 7.
- Kukosa hedhi kwa muda mrefu, na kutoa damu yenye mabonge mabonge wakati wa hedhi
- Uchovu wa mara kwa mara
- Homa za usiku na Kizunguzungu cha mara kwa mara
- Kuharibika kwa ngozi (chunusi, vipele… n.k)
- Maumivu ya viungo
- Kusahau sana (kukosa kumbukumbu)
- Kupata hedhi wakati wa ujauzito (progesterone ikiwa imezidi)
- Kutokupata hedhi (balehe) adi umri wa miaka 20 na kuendelea
MADHARA YA MVURUGIKO WA HOMONI
Pamoja na dalili nyingi tulizoziona tungependa wanawake waelewe vitu vifuatavyo hutokea iwapo atatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango. Njia hizo husababisha saratani ya kizazi, CD4 kushuka, sehemu ya uke kuwa baridi, huchangia kwa 50% kufanyiwa upasuwaji (operation) wakati wa kujifungua, huathiri mtoto atakayezaliwa, huathri ubongo (inapunguza uwezo wa kufikiria), kutokwa na majimaji yenye harufu mbaya ukeni na magonjwa ya mara kwa mara.
Ukiendelea kubaki na dalili tajwa hapo awali kwa muda mrefu, kinga ya mwili itashuka kwa kiasi kikubwa na kusababisha madhara mengi k**a yafuatayo:
-Kutoshika ujauzito kwa muda mrefu
-Mimba kuharibika mara kwa mara;
-Kukosa mtoto au Ugumba
-Maumivu wakati wa tendo la ndoa
-Kuwa na tabia na maumbile ya kiume
-UTI (Urinary Tract Infection) ya mara kwa mara
-Maambukizi kwenye njia ya uzazi (PID)