Medical Stores Department (MSD)

Medical Stores Department (MSD) MSD is annually audited by CAG and has fully-fledged competent internal audit Unit that oversees internal controls effectiveness.

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by the public health services as the Ministry of Health may from time to time approve. Board of Trustees is the highest decision-making body that governs and set the directions of MSD on behalf of the Minister for Health, The Board composed of nine(9) members appointed every three years. The Chairman appointed by the President of the United Republic of Tanzania, eight (8) members are appointed by the Minister responsible for health.The Board is comprising of a multidisciplinary team including eminent public servants, scientists, practicing medical doctors, lawyers, accountants, professors and renowned economists. To implement its responsibilities the Board operates through three committees namely; Audit and Risk Management Committee that provides the management with accurate information on the effectiveness of risk management and internal controls including regulatory compliance by the Department; Technical Services Committee that handles all matters related to quality of medicines and medical supplies together with management expired medicines. Finance and Administration Committee tha is mandated in handling all matters related to MSD Financial Management, Human Resources Management and Administrative functions of the Department. The Board delegates the day to day management of the department operations to Director General who is appointed by the President of the United Republic of Tanzania. The administrative functions and operations of Department are carried by and through the Executive Management Team (EMT).The EMT is constituted by the Director General, Director of Human Resources and Administration, Director of Finance and Planning, Director of Logistics, Director of Procurement, Director of Information and Communication Technology, Director of Customer Service and Zonal Operations as well as Chief Legal Counsel. The departnment operates through eight zonal stores in Dar-es-salaam, Mwanza, Iringa,Moshi,Mbeya,Tabora, Dodoma and Mtwara suppoted by two Sales Points in Tanga and Muleba.

Baada ya mafunzo kutamatika, watumishi  wa MSD Tanga walipata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ambapo wali...
16/02/2026

Baada ya mafunzo kutamatika, watumishi wa MSD Tanga walipata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ambapo walijionea wanyama mbalimbali na vivutio vya asili vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo, hatua iliyochangia kuongeza ari na kuimarisha mshik**ano miongoni mwao.

*MSD KANDA YA TANGA YAFANYA RETREAT ILIYOCHAGIZWA KWA KUTEMBELEA HIFADHI YA MIKUMI*Watumishi wa MSD Kanda ya Tanga wamef...
15/02/2026

*MSD KANDA YA TANGA YAFANYA RETREAT ILIYOCHAGIZWA KWA KUTEMBELEA HIFADHI YA MIKUMI*

Watumishi wa MSD Kanda ya Tanga wamefanya retreat mkoani Morogoro kwa lengo la kujitathmini, kuimarisha mshik**ano na kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha huduma kwa wateja wa kanda hiyo.

Retreat hiyo ilifanyika tarehe 14 hadi 15 Februari, 2026 ikihusisha mafunzo maalum yaliyotolewa na mshauri mwelekezi wa masuala ya rasilimali watu, Mosses Raymond.

Katika mafunzo yake, Raymond alisisitiza umuhimu wa ubunifu, ushirikiano kazini, uvumilivu na kuacha alama chanya katika kila jukumu la kazi. Alieleza kuwa misingi hiyo ni muhimu katika kuongeza ufanisi na tija kwa taasisi, sambamba na kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja.

Mbali na mafunzo, watumishi walipata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ambapo walijionea wanyama mbalimbali na vivutio vya asili vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo, hatua iliyochangia kuongeza ari na kuimarisha mshik**ano miongoni mwa watumishi.

Kwa mujibu wa baadhi ya watumishi, retreat hiyo imekuwa chachu ya kuimarisha mbinu za utendaji kazi kupitia maarifa mapya waliyoyapata. Aidha, wameishukuru Menejimenti ya MSD kwa kuridhia kufanyika kwa retreat, wakieleza kuwa imewasaidia kujitathmini, kupanga mikakati na kuongeza ubunifu katika kuhudumia wateja wa Kanda ya Tanga.

Ujumbe wa wataalamu wa afya kutoka Madagascar umeipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika u...
14/02/2026

Ujumbe wa wataalamu wa afya kutoka Madagascar umeipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika ujenzi wa ghala la kisasa la kuhifadhia bidhaa za afya lililopo Dodoma.

Ujumbe huo ulitoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea ghala jipya la MSD Dodoma, ambapo walipata fursa ya kujionea miundombinu ya kisasa inayokidhi viwango vya kimataifa katika uhifadhi na usambazaji wa dawa na vifaa tiba.

Akizungumza kwaniaba ya ujumbe huo Mfamasia Mkuu wa Bohari ya Dawa ya Madagascar Bi. Soafara Andriamiadamanana alisema wamevutiwa na kiwango cha uwekezaji na teknolojia iliyowekwa katika ghala hilo, akieleza kuwa ni la hadhi ya kimataifa na linaendana na mifumo bora ya kisasa ya usimamizi wa mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.

“Tumeshuhudia miundombinu ya kisasa yenye mifumo madhubuti ya udhibiti wa halijoto, usimamizi kwa njia ya kidijitali na usalama wa bidhaa. Hii ni hatua kubwa sana kwa MSD na kwa sekta ya afya kwa ujumla,” alisema. Bi. Andriamiadamanana

Kwa upande wake, uongozi wa MSD kupitia Meneja wa ghala la Kati Bw. Robert Lugembe alieleza kuwa ujenzi wa ghala hilo ni sehemu ya mkakati mpana wa kuboresha miundombinu ya MSD na kuimarisha mfumo wa ugavi wa bidhaa za afya nchini, ili kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Ziara hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya ushirikiano na kubadilishana uzoefu kati ya nchi hizo mbili katika kuimarisha mifumo ya afya, huku MSD ikitajwa kuwa mfano wa kuigwa katika ukanda wa Afrika kwa usimamizi bora wa bidhaa za afya, hivyo kuvutia mataifa mengi kuja kujifunza Tanzania.

Bohari ya Dawa (MSD) imetwaa tuzo ya Huduma kwa Wateja sekta ya Dawa na Vifaa Tiba, iliyoandaliwa na taasisi ya kimataif...
14/02/2026

Bohari ya Dawa (MSD) imetwaa tuzo ya Huduma kwa Wateja sekta ya Dawa na Vifaa Tiba, iliyoandaliwa na taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na kutoa mafunzo, vyeti, na viwango vya taaluma ya huduma kwa wateja (customer service) na vituo vya kupokea simu (call centers) Chartered Institute of Customer Management (CICM) Tanzania.

Tuzo hii inaonesha namna MSD ilivyofanya maboresho ya huduma zake kwa wateja na wananchi kwa ujumla katika eneo la mawasiliano ya pande mbili na kwenye upatikanaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Hadi sasa MSD inahudumia vituo vya kutolea huduma za afya 8,893 nchi nzima, huku vituo vyote vikipelekewa bidhaa hizo hadi mlangoni mara sita kwa mwaka.

Wataalamu wa Afya kutoka Madagascar wakiwa wametembelea MSD Kanda ya Dodoma kujifunza kuhusu uhifadhi na usambazaji wa b...
13/02/2026

Wataalamu wa Afya kutoka Madagascar wakiwa wametembelea MSD Kanda ya Dodoma kujifunza kuhusu uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya, pamoja na mifumo madhubuti ya mnyororo wa ugavi.

  building activities.
11/02/2026

building activities.

Watumishi wa MSD Mwanza, wakishiriki kwa mafunzo maalum kwa vitendo, (team building activities), ikiwa ni moja ya mbinu ...
11/02/2026

Watumishi wa MSD Mwanza, wakishiriki kwa mafunzo maalum kwa vitendo, (team building activities), ikiwa ni moja ya mbinu za kuimarisha ushirikiano, utatuzi wa changamoto k**a timu, sambamba na kuimarisha umoja na mshik**ano baina ya watumishi, ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa wakati na kwa weledi k**a timu moja.

Watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Mwanza wakipatiwa mafunzo maalum, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa MSD wa kuimar...
11/02/2026

Watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Mwanza wakipatiwa mafunzo maalum, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa MSD wa kuimarisha uwajibikaji, kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja na wadau wake.

Kupitia mafunzo hayo, watumishi hao wamejengewa uwezo katika maeneo mbalimbali muhimu kwa maendeleo ya taasisi na ustawi wa rasilimali watu, k**a vile maadili na miongozo ya Utumishi wa Umma, usawa wa maisha na kazi (work-life balance) kwa kuzingatia masuala ya udhibiti wa msongo wa mawazo (stress management) na afya ya akili (mental health).

Kupitia mafunzo hayo, MSD Kanda ya Mwanza imeonesha dhamira yake ya kuwekeza katika maendeleo ya rasilimali watu k**a nyenzo muhimu ya kuboresha utoaji wa huduma bora, salama na kwa wakati kwa wateja wake. Mafunzo haya yanatarajiwa kuongeza ari ya kazi, kuimarisha mshik**ano miongoni mwa watumishi na kuchochea uwajibikaji wa hali ya juu katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

MSD inaendelea kutumia mbinu mbalimbali za kujenga uwezo wa watumishi wake ili kuhakikisha taasisi inatimiza wajibu wake wa msingi wa kusambaza bidhaa za afya kwa ufanisi, kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na viwango vya juu vya utendaji.

Ujumbe kutoka Bohari ya Dawa ya Madagascar (SALAMA) Ukiwa umetembelea moja ya mghala ya kisasa ya MSD, kujifunza namna b...
11/02/2026

Ujumbe kutoka Bohari ya Dawa ya Madagascar (SALAMA) Ukiwa umetembelea moja ya mghala ya kisasa ya MSD, kujifunza namna bidhaa za afya zinavyo hifadhiwa na jinsi ubora na usalama wa bidhaa hizo unazingatiwa.

Ziara hii inaakisi Dira ya MSD, Kituo cha Umahiri katika Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi wa Bidhaa za Afya barani Afrika.” (To be A Center of Exellence for Health Commodities Supply Chain in Africa)

*BOHARI YA DAWA YA MADAGASCAR, KUPATA UZOEFU MSD*Dar es Salaam, Feb 9—10, 2026 Bohari ya Dawa (MSD) imeupokea ujumbe wa ...
10/02/2026

*BOHARI YA DAWA YA MADAGASCAR, KUPATA UZOEFU MSD*

Dar es Salaam, Feb 9—10, 2026

Bohari ya Dawa (MSD) imeupokea ujumbe wa wataalam kutoka Bohari ya Dawa ya Madagascar (SALAMA) kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya, hususan mifumo na mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai, alisema kuwa ujio huo ni hatua muhimu ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika sekta ya afya, kwani mbali na kujifunza pande hizo mbili zitaingia makubaliano ushirikiano.

“Tunafurahi kupokea ugeni kutoka Salama Central Medical Stores ya Madagascar. Ziara hii ni fursa muhimu ya kubadilishana uzoefu na kujifunza kutoka pande zote mbili. MSD itaendelea kushirikiana na taasisi nyingine za afya ili kuimarisha mifumo ya ugavi wa dawa na kuhakikisha wananchi wanapata dawa salama, bora na kwa wakati,” alisema Tukai.

Tukai amebaisha kwamba MSD itasaini hati ya Makubaliano (MoU) na Bohari ya Dawa ya Madagascar kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kitaalamu na kiufundi kati ya pande hizo mbili. Makubaliano hayo yanalenga kuwezesha kubadilishana uzoefu, maarifa ya kitaalamu na teknolojia ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya taasisi husika.

Aliongeza kuwa kupitia hatua hiyo, MSD na Madagascar zitashirikiana katika masuala ya ununuzi, kubadilishana taarifa na kuimarisha mifumo ya mawasiliano. Ushirikiano huu unatarajiwa kuchangia kuboresha mipango ya pamoja na kuimarisha mahusiano ya muda mrefu kati ya pande hizo mbili.

Naye mwakilishi wa ujumbe huo kutoka Madagascar, ambaye ni Mfamasia Mkuu wa Bohari ya Dawa ya Madagascar (SALAMA), Bi. Soafara Andriamiadamanana, alieleza kuvutiwa na mifumo ya uendeshaji ya MSD, hususan katika maeneo ya maghala ya kisasa na mtandao wa usambazaji wa dawa nchini.

“Tumefurahishwa sana na mifumo ya MSD, hasa usimamizi wa maghala na usambazaji wa dawa. Tumejifunza mbinu muhimu zitakazotusaidia kuboresha utoaji wa huduma za dawa nchini Madagascar,” alisema Andriamiadamanana

Vilevile, ujumbe huo umepata fursa ya kujionea na kujifunza kwa vitendo namna MSD inavyotekeleza majukumu yake manne makuu ambayo ni ununuzi, uhifadhi, uzalishaji na usambazaji wa bidhaa za afya.

Tazama picha sanifu za muonekano wa Ghala letu jipya la MSD Chato, lilipo kwenye hatua za ujenzi, pindi litakapo kamilik...
09/02/2026

Tazama picha sanifu za muonekano wa Ghala letu jipya la MSD Chato, lilipo kwenye hatua za ujenzi, pindi litakapo kamilika

*WATUMISHI WA MSD KANDA ZA DAR ES SALAAM NA DODOMA WASHIRIKI MICHEZO KUIMARISHA USHIRIKIANO*Watumishi wa Bohari ya Dawa ...
08/02/2026

*WATUMISHI WA MSD KANDA ZA DAR ES SALAAM NA DODOMA WASHIRIKI MICHEZO KUIMARISHA USHIRIKIANO*

Watumishi wa Bohari ya Dawa (MSD) kutoka Kanda za Dar es Salaam na Dodoma wameshiriki michezo ya kirafiki iliyofanyika jijini Dodoma, yenye lengo la kuimarisha mshik**ano, kukuza mahusiano ya kikazi na kujenga afya bora miongoni mwa watumishi.

Michezo hiyo ilitoa fursa kwa watumishi kubadilishana uzoefu, kujifunza kutoka kwa wenzao pamoja na kuonesha umuhimu wa wafanyakazi kujenga mahusiano chanya yanayochochea ari ya kazi na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa michezo hiyo, Meneja wa MSD Kanda ya Dodoma, Bi. Mwanashehe Jumaa, alisema michezo ni nyenzo muhimu katika kuimarisha mshik**ano, kujenga malengo ya pamoja na kuimarisha uhusiano mzuri baina ya Kanda. Aliongeza kuwa michezo hiyo imekuwa jukwaa la kipekee kwa watumishi kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano wa kikazi.

Kwa upande wake, Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Bi. Betia Kaema, alisema tukio hilo linaonesha dhamira ya MSD katika kuimarisha umoja wa watumishi na kujenga familia moja yenye maono na malengo ya pamoja.

“Kupitia michezo hii tunajenga urafiki, kuaminiana na mshik**ano, ambao ni msingi muhimu katika utoaji wa huduma bora na endelevu kwa wananchi,” alisema Bi. Kaema.

Mbali na kushiriki michezo, watumishi hao walipata fursa ya kutembelea ghala jipya la MSD Dodoma, ambapo walijionea miundombinu ya kisasa, mifumo ya uhifadhi wa bidhaa za afya pamoja na taratibu za usimamizi wa ghala zinazolenga kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi.

Address

Off, Nyerere Road, Keko Mwanga
Dar Es Salaam
9081

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Medical Stores Department (MSD) posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram