28/02/2026
Munyonyo - Kampala, Uganda.
Katika mkutano wa 5 wa Kansa na Tiba Shufaa (Palliative Care).
Shule kidogo!
Kansa sio ugonjwa mmoja, ni kundi la maradhi mengi yanayoweza kufikia hata 100 au zaidi.
Karibu kila kiungo mwilini kinaweza kuathiriwa na kansa. Moyo pekee ndio ogani ambayo ni vigumu sana kupata kansa inayochipukia kwenyw moyo wenyewe, isipokuwa unaweza kuathiriwa na kansa kutoka kwenye ogani nyingine.
Kuna kansa ya Ubongo, kansa ya koo, kansa ya tumbo, kansa za utumbo mdogo, utumbo mkubwa, kansa ya kibofu, kansa ya uume, kansa kinywa, kansa ya jicho, kansa ya ulimi, kansa ya koromeo, kansa ya umio, kansa ya tezi mbalimbali (thyroid, adrenal nk), kansa za ngozi, kansa za mifupa, kansa za damu, kansa ya kongosho, kansa ya figo, kansa ya ini, kansa ya matiti, kansa ya shingo ya kizazi. Kansa ni nyingi sana. Binadamu ana ogani zinazokadiriwa kuwa 78 na karibu zote zinaweza kupata kansa.
Bado haitoshi, kuna aina za kansa kwa kutegemea aina ya seli au tissue zilizoathiriwa. Mfano, ngozi ya mwanadamu inaundwa na aina nyingi za seli. Kwa hiyo ukisema kansa ya ngozi bado haitoshi, inabidi ijulikane ni aina gani ya seli za ngozi zilizoathiriwa. Kwahiyo ngozi au ogani nyingine zinaweza kupata kansa za aina tofauti. Kuna Carcinomas, Sarcomas, Lymphomas, Leukemias nk. Na hizo aina pia zina aina zake tofautitofauti.
Bado!
Kuna kansa ambazo zina mahusiano na maambukizi ya aina fulani ya vimelea vya magonjwa, ingawa kansa nyingi haziambukizwi.
Sasa, kwanini nimeandika hivi?
Bila shaka umewahi kusikia huko mitaani habari za "DAWA YA KANSA" au Chanjo ya Kansa.
Sasa kwa elimu hiyo ndogo hapo juu, unadhani kuna dawa moja inaweza kutibu kansa zote hizo kwa pamoja?
Unaweza kuwa na funguo ya kuendesha magari yote ya Toyota na yote ya Nissan na yote ya Ford na yote ya Tesla na yote duniani?
Mganga wako wa kienyeji alikwambiwa anatibu kansa, ulimuuliza Kansa ipi?
Ulikuwa unajua Kansa sio ugonjwa mmoja?
Karibuni msosi.
Pombe Kistaarabu!
Sigara Acha!
Nawasilisha.
Dr. Chris Cyrilo.