04/12/2025
MWANAMKE RUDISHA UPENDO MWANAUME AKUGANDE
JE! UNA MASIKIO YANAYOSIKIA
Dada zangu katika ndoa huwezi kupata kila kitu, angalia cha muhimu kwako na ridhika nacho.
(1) Kuna ambao wanalia na kuteseka ili tu wapate wanaume wanaohudumia angalau watoto wale ingawa kitandani wanaridhishwa.
(2) Kuna ambao wanahudumiwa kila kitu wamepewa kila kitu lakini kitandani hakuna kitu wanachotaka ni mwanaume wakuwaridhisha tu kitandani.
(3) Kuna ambao wanaume ni walevi, wanawapiga, kuwanyanyasa na kuwafanyia kila aina ya madudu lakini wanavumilia kwakua angalau wanahudumiwa.
(4) Kuna ambao hawapati chochote kabisa, yaani hakuna cha tendo la ndoa, hakuna cha kuhudumiwa, kipigo wanakula na kila aina ya manyanyaso.
(5) Kuna ambao wamebahatisha na kupata vyote; hawa ni wachaache tena sana lakini mara nyingi nao hawaridhiki wanakua na visirani kwakua tu mwanaume kasahau siku ya kuzaliwa!.
Hivyo dada zangu kabla ya kumuonyesha kiburi mwanaume, kutaka kumuacha hembu pima hicho unachokipata kuona k**a kinathamani ya kile unachokikosa.
Maana ni ngumu kupata kila kitu.
Mtumishi wa Mungu wa huduma ya Agape na Mwalimu 0621001042