23/02/2017
Mume kutoa affection kwa mke ni lazima.
Tuendelee na mada yetu ya mume kutoa affection kwa mke. Kwa posts za huko nyuma, imeshajadiliwa kuwa affection ni nini na inakuwaje. Ni ukweli ulio wazi, kuwa mume ameamua kuoa, basi affection ni lazima ni wajibu wake wa msingi k**a ilivyo kwenye kutoa mahitaji na tendo la ndoa. Ila ni ukweli usiopingika kuwa kuna wanaume wengi wamefanikiwa katika meeengi na wakafeli kwenye hili, wakiwemo waliokoka, watumishi na majina yao makubwa makubwa kabisa, na maafisa na vyeo vyao vikubwa vikubwa kabisa.
Kwa post iliyopita ilijadiliwa baadhi ya sababu zinazowafanya wanaume walio wengi kufeli kwenye affection.Je mke ufanyaje?
1. Ni busara, na hekima na muhimu kumjua mumeo. Ni vizuri kumjua kuwa kwenye maisha ya kawaida anaweza nini zaidi, anashindwa nini zaidi, anapenda nini zaidi na anachukia nini zaidi, ( Irene Mbowe anasemaga kutoa alama sijui) na kwa uhalisia jizoeshe kuishi na kufurahia yale anayoweza zaidi, na potezea yale asiyoweza.
2. Jifunze kutafsiri lugha yake ya affection. Hili ,linaweza lisiwe zoezi jepesi, maana hata yeye anaweza asiseme au asijue. Ila kila mwanaume anapooa anakuwa na ndoto zake kichwani, kuwa yeye kumpenda mke ni kufanyaje na kumuonyesha anampenda ni kufanyaje. Badala ya kulazimisha afanye k**a wale wa kwenye movie, soma lugha yake. Kuna mwingine anasimulia zaidi nje, kuliko kukwambia wewe, kuna mwingine akiandika message atasema nakupenda, ila kusema na mdomo anapata ganzi, kuna mwingine akihudumia familia ndio anaona amekuwa affectionate, huwezi kulazimisha awe asivyo, au afanye asivyoweza au asivyotaka, kwa muda huo shukuru na uendelee kuridhika.
3. Fanya sehemu yako bila kujalisha yeye anafanya au hafanyi. Huko duniani, kuna wanawake wengi utasikia, asipoleta mboga, namuwekea ugali na chumvi, wazungu wanakwambia ''two wrongs do not make one correct thing". Kosa lako haliwi halali kwasababu wa kwanza kakukosea. Wewe tenda wema, jifunze kwa Paulo aliyemquote Yesu, ''ni heri kutoa kuliko kupokea''.
4. Usipimie thamani yako kwa jinsi mume anavyokutendea. Hutakaa uwe na furaha, na Kibo na Mawenzi utavisikia kwa watalii. Amini kuwa thamani yako haiongezeki kwa jinsi watu wanavyokutendea, bali inabaki vile unavyoitengeneza wewe kwa msaada wa Mungu. Ukitupa elf kumi chini na kuikanyaga, thamani yake inabaki kuwa elf kumi. Hivyo na wewe, upate affection usipate, upate kwa uchache au kwa wingi, unabaki kuwa ni wewe, na furaha haiongezeki au kupungua k**a wewe mwenyewe usipoiruhusu.
Happiness is a choice