05/12/2025
WAFANYAKAZI MUHIMBILI -MLOGANZILA WASHAURIWA KUTAMBUA UMUHIMU WA KUJIUNGA NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI.
Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili -Mloganzila wameshauriwa kutambua umuhimu wa kujiunga na vyama vya wafanyakazi kulingana na taaluma au kada zao ili vyama hivyo kuwa daraja zuri baina ya mwajiri na mwajiriwa ambapo itarahisisha mawasiliano na kuongeza utendaji mzuri wa kazi.
Akizungumza katika kikao cha mwaka cha Chama cha Madaktari na Wafamasia, Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu na Utawala, Bw. Abdallah Kiwanga ametaja faida mbalimbali za kuwa mwanachama wa chama cha wafanyakazi kuwa ni pamoja na kulinda usalama kwa mfanyakazi, kupata jukwaa la kusemea kero za mfanyakazi, kuboresha mahusiano, ushirikishwaji katika mambo mbalimbali na kumsaidia mwajiri kutochukua maamuzi akiwa peke yake.
Ameongeza kuwa kila mwanachama wa chama cha wafanyakazi anatakawi kutambua wajibu wake k**a kuzingatia sheria na katiba, kushiriki katika shughuli za chama, kusemea, kutetea na kutangaza chama, kuhamisha wafanyakazi kutoa michango na kuhamasisha wafanyakazi kujiunga na chama.
Kikao hicho kimeambatana na uchaguzi ili kupata viongozi wapya wa muhula ujao ili kuendelea kutimiza majukumu ya chama chao.