Salim Health Care

Salim Health Care Karibu katika page inayojihusisha na Afya pamoja na mfumo bora wa chakula kwa afya bora ya binadamu

Welcome to Salim healthcare that delivers relevant information in clear, free language that puts health into context in peoples' lives. Through medical content, insights from experts and real people, and breaking news, we answer: how it happened, what it feels like, what you can do about it, and why it matters.

𝕁𝕀ℕ𝕊𝕀 𝕐𝔸 𝕂𝕌ℙ𝕌ℕ𝔾𝕌ℤ𝔸 𝕌ℤ𝕀𝕋𝕆 𝕂𝕀𝕌𝕊𝔸ℍ𝕀ℍ𝕀 ( 𝕄𝕒𝕞𝕓𝕠 𝕪𝕒 𝕜𝕦𝕫𝕚𝕟𝕘𝕒𝕥𝕚𝕒 )SEHEMU YA  1Ni vema kupunguza uzito taratibu kadiri siku zinav...
04/10/2021

𝕁𝕀ℕ𝕊𝕀 𝕐𝔸 𝕂𝕌ℙ𝕌ℕ𝔾𝕌ℤ𝔸 𝕌ℤ𝕀𝕋𝕆 𝕂𝕀𝕌𝕊𝔸ℍ𝕀ℍ𝕀 ( 𝕄𝕒𝕞𝕓𝕠 𝕪𝕒 𝕜𝕦𝕫𝕚𝕟𝕘𝕒𝕥𝕚𝕒 )

SEHEMU YA 1

Ni vema kupunguza uzito taratibu kadiri siku zinavyoenda . Iko hivi unapopunguza uzito wako haraka sana utapoteza misuli (Nina maanaisha ubora , na wingi wa misuli), mifupa itapoteza ubora na utapoteza maji mengi pia badala ya mafuta ( The Academy of Nutrition and Dietetics )

🌏Fikiria kupunguza nusu kilo hadi kilo 1 kwa kila wiki , na usikimbilie kupunguza uzito kwa bidhaa au suppliments au vyakula ambavyo vina kupunguza kilo nyingi kwa haraka . Mwili wako unahitaji utaratibu , kila kitu kwenye mwili wako kinataka utaratibu , mwili unapopungua taratibu unabadili mifumo yake ya kihuduma kulingana na mahitaji ya mwili kwa wakati husika

🌏Nakushauri ukiamua kuanza zoezi hili , uwe na usimamizi wa daktari ili kuhakikisha unapungua katika utaratibu mzuri , na hukosi virutubisho muhimu kwa afya yako.

Sishauri kabisa na wala sio utaratibu mzuri kusema uache kula wanga , hapana , swala la msingi hapa ni kupunguza ratio (Kiasi) unachotumia na upate kiasi salama na kisichozidi mahitaji , mazoezi ufanye pia

🌳WEKA LENGO /MALENGO

Ule msemo kwamba ule tu chakula kingi na utafanya mazoezi , haisaidii kabisa wewe kupunguza uzito . Fanya utaratibu huu ufuatao endapo utataka upate kiwango cha kawaida cha calories kwa siku :

🍎Punguza mlo wako ( Ratio/kiasi)

Kwanza fikiria ni kiasi gani cha chakula huwa unakula katika mlo mmoja ( Ni calories ngapi unakula ) , kisha punguza kidogo . Mfano huwa unakula sahani nzima ya chakula , sasa waweza amua kwamba kuanzia sasa utakua unakula robo tatu ya sahani . Kisha kadiri siku zinavyoenda utazidi kupunguza , ila uhakikishe hautapunguza chini ya kiwango cha kawaida na cha chini sana mfano robo sahani.
Sasa hapo unakazia na maji ya kutosha ili ujihisi umeshiba

Kwa mlo wowote utakao kula hakikisha sahani yako inahusisha vyakula aina ya wanga ( Naweza ita nafaka) , protein , mbogamboga na matunda ili upate virutubisho vyote muhimu kwa afya yako

Inaendelea......

MADHARA YA KULALA MDOMO WAZI AU KUPUMUA KWA MDOMODr SALIM AMOUR💉UTANGULIZI📝Kwa kawaida binadamu huvuta hewa kwa kutumia ...
11/10/2018

MADHARA YA KULALA MDOMO WAZI AU KUPUMUA KWA MDOMO

Dr SALIM AMOUR

💉UTANGULIZI

📝Kwa kawaida binadamu huvuta hewa kwa kutumia pua na mara chache kwa kutumia mdomo,kuna wakati ambapo inakubidi kutumia mdomo kuvuta hewa mfano ukiwa na mafua makali,nyama za pua au magonjwa yeyote yanayosabbisha hewa ishindwe kupita vizuri puani.

💉faida ya kuvutia hewa puani:

kifiziolojia kuna faida nyingi kutumia pua kuvuta hewa kuliko mdomo,faida hizo ni k**a..

1.Pua ina vinyweleo ambavo vinaweza kuchuja uchafu k**a vumbi na kuzuia uchafu huo kuingia kwenye mfumo wa hewa.

2.Hewa inayopita puani hupata joto taratibu hivo inafika kwenye mapafu ikiwa inalingana na joto la mwili.

3.Hewa inayopita puani hupata unyevu ambao unazuia kusababisha mazingira ya ukavu kwenye mapafu na mfumo wa ndani wa upumuaji .

💉MADHARA

📝Baadhi ya watu wanatumia mdomo kupumua bila kuwa na matatizo tajwa hapo juu nah ii inaweza kusababisha matatizo mbalimbali k**a,

1. Kukaukiwa na mate kinywani (dry mouth) hiii ni kwa sababu hewa inaingia na kutoka kupitia mdomoni hivo inabeba unyevu wa kwenye mate na kuacha kinywa kikavu

2. Kutokwa na harufu mbaya mdomoni kwa kuwa kinywa ni kikavu

3. Magonjwa ya fizi,mate yana kemikali ambazo huua baadhi ya bakteria hivo hulinda kinywa na fizi, yanapokauka mdomoni inaruhusu bakteria kukua kwa wingi na kushambulia fizi kirahisi.

4. Kutoboka kwa meno.

5. Maambukizi kwenye maskio na koo.

6. Kwa watoto hupelekea uso kuwa mrefu kuliko kawaida ukubwani na kuharibu tabasamu kufanya fizi ziwe zinaonekana sana apotabasamu(gummy smile)

7. Kukoroma wakati wa kulala

8. Maambukizi kwenye maskio na koo.

📝Huwa siyo rahisi sana kwa mtu kugundua k**a ana tatizo la kupumulia mdomo mara nyingi tatizo hili linaweza kugundulika pale unapomtembelea daktari wa meno au wa pua,masikio na koo na kufanyiwa uchunguzi.Tiba sahihi huwa ni kuondoa kwanza kisababishi k**a vile vinyama vya puani(nasal polyps),kutibu maambukizi ya koo na masikio k**a kuvimba kwa matezi ya shingo(tonsillitis),kutibu magonjwa ambayo yanasababisha pua kuziba k**a maambukizi ya mfumo wa juu wa hewa,kwa wagonjwa wenye aleji ni kutibu dalili zote za aleji ambazo zinasababisha pua kuziba.

MWISHO NA ASANTENI 🙏

ACHENI KULALA MDOMO WAZI NA MSIPUMUE KWA MDOMO 😂😂😂😂😂

FAIDA ZA KULA PAPAIDr SALIM AMOUR📖UTANGULIZI NA FAIDAWatu  wengi  hulitumia  tunda  la papai  kwa  sababu  ya  utamu wak...
08/10/2018

FAIDA ZA KULA PAPAI

Dr SALIM AMOUR

📖UTANGULIZI NA FAIDA

Watu wengi hulitumia tunda la papai kwa sababu ya utamu wake.

Hata hivyo mbali na kuwa na ladha nzuri, tunda la papai lina faida lukuki kwa afya ya mwanadamu.

UTAJIRI WA VITAMINI

📖Tunda la papai lina vitamini A,B,C,D, na E jambo linalo liweka tunda hili katika kundi la matunda na vyakula vyenye utajiri mkubwa wa vitamin.

FAIDA ZA KIAFYA ZA TUNDA LA PAPAI

📖Tunda la papai lina faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuwa na uwezo wa :

📖Mbegu za Papai:

1. Kutibu tatizo la Shida ya kusaga chakula tumboni

2. Kutibu Udhaifu wa tumbo

3. Kutibu Kisukari na asthma au pumu.

4. Kutibu Kikohozi kitokacho mapafuni
Mizizi Ya Papai

5. Kutibu Kifua kikuu endapo itatumika kwa muda mrefu

6. Tunda hili huleta afya nzuri ukitumia kila siku

7. Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda

8. Vilevile yanasaidia kutibu sehemu palipoungua moto

9. K**a hiyo haitoshi, maziwa yanayotoka katika jani la mpapai yanatibu kiungulia na magonjwa ya colon (njia ya haja kubwa ndani)

📖Majani Ya Mpapai;

10. Pia yanasaidia kutofunga choo

11. Maganda ya tunda la papai yanasaidia kutibu tatizo la kuungua, vipele na saratani ya ngozi.

12. Mbegu zake zinatibu ugonjwa wa ini zikitafunwa 10 – 12 kwa siku 5.

13. Majani yake yakaushie ndani, yanatibu pumu. Inapoanza kubana yachome majani yaliyokaushwa kisha jifukize, kule kubanwa kutakisha.

14. Majani yake yanasaidia katika kutibu shinikizo la damu.

15. Papai likimenywa na kupondwa linafaa Sana katika masuala ya urembo kwani linaweza kutumika K**a vile unavyotumia lotion kulainisha uso.

16. Mbegu za papai zina uwezo wa kutibu homa. Meza mbegu za papai kiasi cha kijiko cha chakula mara 3 kwa ajili ya kutibu homa.

17. Mbegu za papai zilizokaushwa ndani kisha zikasagwa kuwa unga zinatibu malaria, tumia kijiko 1 cha chai changanya na uji, kunywa mara 3 kwa siku 5 Mgonjwa wa kifua kikuu akila matunda haya kwa muda mrefu atapona bila dawa nyingine.

18. Mizizi yake ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa, lita 2 na nusu kwa dakika 15, yanatibu matatizo mengi ya figo, bladder, yanazuia kutapika. Nusu kikombe cha chai kutwa mara 3 kwa siku 5.

*USHAURI :
[ TUMIA TUNDA HILI KWA AFYA YAKO, NA UNAPOKUA MGONJWA NASHAURI UENDE HOSPITALI ILI UFANYIWE VIPIMO NA UPEWE DAWA ZA KUTIBU TATIZO LAKO, HILO TUNDA LITUMIE TU K**A ZIADA, HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI NI ZA MUHIMU SANA]*

MATUMIZI SAHIHI YA PARACETAMOL (PANADOL)💊💊Dr SALIM AMOUR👂 SABABU YA KUIELEZEA DAWA HII, NI KUTOKA NA KWAMBA PARACETAMOL ...
06/10/2018

MATUMIZI SAHIHI YA PARACETAMOL (PANADOL)

💊💊

Dr SALIM AMOUR

👂 SABABU YA KUIELEZEA DAWA HII, NI KUTOKA NA KWAMBA PARACETAMOL INATUMIKA VIBAYA KATIKA JAMII NA KILA MMOJA HUICHUKULIA K**A DAWA YA KAWAIDA SANA, ISIYOHITAJI UANGALIZI AU UMAKINI WAKATI WAKUTUMIA 😭 KITU AMBACHO SIO SAHIHI,

PARACETAMOL ISIPOTUMIKA KIUMAKINI NI HATARI SANA HATA KULIKO DAWA ZINGINE 🙏

☁Dawa ya Paracetamol au acetaminophen ni dawa inayotumika kutuliza homa na maumivu mbalimbali ya mwili. Hujulikana sana k**a Panadol, majina mengine ya kibiashara ni Asmol, Sheladol, Tempra na Tylenol. Wakati mwingine huchanganywa na dawa k**a Aspirin na caffeine k**a kwenye tembe za Hedex.

Paracetamol hupatikana k**a vidonge vya kunywa, dawa ya maji (syrup), vidonge vya kuweka njia ya haja kubwa (suppository) na ya maji ya dripu (intravenous).

☁Paracetamol hutuliza maumivu ya kichwa au homa, lakini haitibu au kuondoa maumivu au homa.

Matumizi Ya Paracetamol

Paracetamol au panadol hutumika;

📖Kutuliza maumivu mbalimbali ya mwili yasiyo makali sana k**a kichwa, viungo na misuli.
Kutuliza homa, kupanda kwa joto la mwili kutokana na magonjwa mbalimbali.
Kunywa vidonge kwa maji yaliyopoa, nusu saa kabla au masaa 2 baada ya kula.

Kwa siku moja usitumie Paracetamol zaidi ya gramu 2.6 kwa mtoto chini ya miaka 12, gramu 3.75 kwa mtoto juu ya miaka 12 na gramu 4(gram 4 ni vidonge 8 vya paracetamol, sina maana kwamba waweza meza vyote kwa pamoja, ila nina maana ya 2×4, yaani viwili kila baada ya masaa 6, hayo ndio matumizi makubwa zaidi ya kutumia PCM kwa mtu mzima) kwa mtu mzima. Kuzidisha kiwango hiki cha dawa ya paracetamol kinaweza kusababisha madhara kwenye mwili hasa ufanyaji kazi wa ini.

Ikiwa homa ua maumivu yanaendelea zaidi ya siku 3 baada ya kutumia paracetamol nenda hospitali.

👂 MADHARA KATIKA MATUMIZI YA KAWAIDA NA HATA KWA ALIYEZIDISHA DOZI

Matumizi ya paracetamol katika dozi iliyoshaurishwa kwa kipindi kifupi yanaweza kuleta madhara kidogo au isilete madhara kabisa. Madhara yafuatayo yanaweza kutokea, hasa unapotumia kwa muda mrefu au yasitokee kabisa;

Kizunguzungu

Ngozi kuwasha

Manjano kutokea kwenye macho na mwili

Huathiri seli za ini

Kutokwa na damu kwenye njia ya chakula

☁Ukizidisha Dozi ya Paracetamol (Paracetamol overdose)⚠

Kutumia Paracetamol (panadol) zaidi ya kiwango kilichoshauriwa au kunywa paracetamol nyingi kwa makusudi huleta madhara kwenye ini lako, na inaweza kupelekea ini kushindwa kufanya kazi(liver failure). Wahi kwenye kituo cha afya k**a umekunywa paracetamol nyingi na unapata dalili k**a kutapika, kichefuchefu, tumbo kuuma, kutokwa na jasho, manjano na moyo kwenda mbio.

Pia Figo huathirika kiasi fulani, japo sio kwa kiwango kikubwa k**a ini.

Kuna Wakati pia husababisha ulcers (vidonda vya tumbo) maana hukwangua pia ukuta wa ndani wa tumbo, Usitumie k**a hujala chochote.

☁Tahadhari⚠

Haishauriwi kutumia paracetamol k**a;

Una ugonjwa wa ini ambao haujapona.

Mara chache sana, huweza kusababisha magonjwa ya ngozi k**a malengelenge, ngozi kuwa nyekundu na kuwasha. Usitumie paracetamol k**a hali hii imewahi kutokea.

▶Wakati wa Ujauzito na Kunyonyesha

Paracetamol inaweza kutumika katika kipindi chote cha ujauzito, kwa muda mfupi bila kuleta madhara yoyote.

Dawa hii ni salama kutumia wakati unanyonyesha mtoto.

NOTE : HAKIKISHA UNATUMIA VIZURI NA KWA USAHIHI PARACETAMOL, USIICHUKULIE K**A DAWA ISIYOKUA NA UZITO. NI HATARI SANA

MWISHO.... 🙏

Njia tano za kujichunguza k**a una saratani ya mat**i ( BREAST CANCER )Saratani ya mat**i imekua ikiwatesa wanawake weng...
03/05/2018

Njia tano za kujichunguza k**a una saratani ya mat**i ( BREAST CANCER )

Saratani ya mat**i imekua ikiwatesa wanawake wengi kutokana na dalili zake kutoonekana mapema.
Pia wanawake wengi hawana tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara na kupeleke kugundulika kuawana saratani ikiwa katika hali mbaya (late stage)

Kumbuka kujichunguza ndio njia bora ya kugundua saratani ikiwa bado ndogo, na una weza kujichunguza mara 2 au tatu kila mwezi.

Zifuatazo ni hatua tano muhimu katika kujichunguza k**a una satratani ya mat**i.

HATUA YA KWANZA
Simama mbele ya kioo mkono mmoja pembeni na angalia k**a kuna mabadiliko yeyote k**a vile uvimbe ,kovu,au matokwa yeyote kwenye chuchu.

HATUA YA PILI
Angalia k**a kuna mabadiliko yeyote kwenye mistari ya kontua ya mat**i.

HATUA YA TATU
Minya chuchu taratibu k**a kuna uchafu wowote unaotoka

HATUA YA NNE
Lala kitandani kwa mgongo, weka mkono mmoja nyuma ya kichwa, papasa kwa kutumia mkono mwingine. Anza na papasa kwa mizunguko midogo midogo na uhisi
k**a kuna uvimbe wowote ama maumivu.

HATUA YA TANO
Rudia hatua ya nne kwa upande mwingine wa t**i.
K**a utaona dalili zozote usizo zielewa ni vyema kumuona daktari kwa vipimo na ushauri zaidi.
kumbuka kua kujichunguza mwenyewe sio mbadala wala haku zuii wewe kumuona daktari kwa ushauri na uchunguzi zaidi.

by
Dr Salim
+255738252780
salimhealthcare@yahoo.com

Faida za kula chungwa kiafyaMachungwa ni miongoni mwa matunda ya msimu, ambapo kwa hapa Tanzania hupatikana kwa wingi ka...
30/04/2018

Faida za kula chungwa kiafya

Machungwa ni miongoni mwa matunda ya msimu, ambapo kwa hapa Tanzania hupatikana kwa wingi katika mkoa wa tanga. Tukiachana na hayo je wewe ni mtumiaji wa machungwa? K**a jibu ni ndio, basi nichukue fursa hii kikupongeza sana.

Na kwa wewe ambaye huna mazoea ya kutumia machungwa ni vyema ukaanza kutumia kuanzia leo kwani watalamu wanasema mtu anapotumia machingwa kuna uwezekano mkubwa kuweza kuzuia magonjwa yafuatayo.

1. Ukosefu wa choo.
Kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe (fibre), chungwa husaidia usagaji wa chakula tumbuni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo. Aidha, kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo chungwa ni zuri kwa wagonjwa wa kisukari.

2. Shinikizo la damu
Virutubisho vya Magnesi (Magnesium) na ‘hesperidin’ vilivyomo kwenye chungwa, husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu la juu (high blood pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa presha.

3. Ulaji wa chungwa hutibu maginjwa ya moyo.
Kiwango kikubwa cha Vitamin C na virutubisho vya ‘flavonoids’, ‘phytonutrients’ vilivyomo kwenye chungwa, huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo (Cardiovascular disease)!

4. Husaidia katika kuimarisha afya ya ngozi.
‘Anti oxidants’ iliyomo kwenye chungwa, hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa ya ngozi yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia huifanya ngozi ‘isizeeke’.

5. Huzaidia uzalishaji wa kinga mwilini.
Vitamin C iliyomo kwenye chungwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Unapokuwa na kinga imara, huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara, yakiwemo malaria.

by
Dr Salim
salimhealthcare@yahoo.com
+255738252780

29/04/2018

TIBA MBADALA YA MARADHI YA KWIKWI
( HICCUPS TREATMENT)

MARADHI YA KWIKWI (Hiccups)
Kwikwi hutokana na kushtuka na kusinyaa kwa ghafla kwa misuli mikuu ya upumuaji (diaphragm) ambako hujirudia rudia na kusababisha hewa kuingia kwa kasi kwenye mapafu.

Hii husababisha milango ya sauti katika koo (vocal cords or voice making cords) kufunga ghafla na kutoa sauti inayosikika wakati wa kwikwi.

Kwikwi sio ugonjwa; kwikwi ya muda mfupi ni kero ndogo tu ambayo inapita, lakini kwikwi isiyokatika inaweza kuwa dalili ya tatizo lingine ambalo huenda likahitaji uchunguzi wa kitaalamu.

💥Sababu zinazopelekea kupata kwikwi;

➖Kula haraka haraka au kula sana (kuvimbiwa)
➖Kula vyakula vyenye viungo sana (very spicy foods)
➖Kunywa vinywaji vyenye gesi(carbonated beverages) au vya baridi sana
➖Ulevi au kunywa pombe nyingi kwa mpigo
➖Upungufu wa maji na madini mwilini (dehydration)
➖Tumbo kujaa gesi, asidi (hyperacidity) au vidonda vya tumbo

Sababu hizi mara nyingi husababisha kwikwi ya muda mfupi ambayo huisha bila kuhitaji matibabu wala uchunguzi wa kitaalamu.

💥Sababu nyingine (Rare but serious) ni pamoja na;

➖Upungufu au kuvurigikwa kwa kiasi cha madini mwilini(electrolyte imbalances)
➖Kukusanyika kwa sumu mwilini k**a vile sumu ya figo (Uremia)
➖Magonjwa ya mapafu k**a vile vichomi(pneumonia), pumu(asthma), TB au maji kukusanyika nje ya mapafu(pleural effusion),
➖Saratani au uvimbe kwenye mapafu, ubongo, uti wa mgongo au tumboni.
➖Magonjwa ya moyo (heart attack, arrhythmias, infections to the heart)
➖Kidole tumbo(Apendix illness) na magonjwa ya kufanania nayo
➖Magonjwa ya Ini, kongosho au mfuko wa nyongo
➖Madawa au kunywa sumu aina fulani
➖Kuumia katika eneo la misuli ya upumuaji (diaphragm injuries).

Kwikwi itokanayo na matatizo haya huwa ya muda mrefu au inayojirudia rudia sana, na huisha tu k**a tatizo lililosababisha likigundulika na kutibiwa. Ukiona dalili ya kwikwi isiyoisha tafadhali muone daktari.

▶Sababu ya kisaikologia (psychological reason)– Hii huwapata watu wachache. Watu hawa hujidhania kuwa wana kwikwi isiyokatika, hivyo huendelea kutoa sauti k**a mtu mwenye kwikwi. Kwikwi ya aina hii haina mfumo maalum, na haitokani na kusinyaa kwa misuli ya upumuaji; kwa mtu mwenye tatizo hili ni muhimu kutafuta tatizo alilo nalo kisaikologia na kulitatua.

💥Namna ya Kuzuia Kwikwi

➖Kula taratibu – haraka haraka hujaza gesi tumboni na kusababisha kuvimbiwa
➖Kula kiasi kidogo kwa wakati – Inashauriwa kuongeza idadi ya milo kwa siku badala ya kiasi; milo mitano midogo midogo badala ya mitatu mikubwa kwa siku.
➖Punguza au ondoa kabisa vyakula vyenye viungo vingi/vikali.
➖Kunywa maji – Unywaji mzuri wa maji huzuia na kutibu kwikwi, pia hulinda mwili na maradhi k**a vile upungufu wa maji na madini(dehydration) na figo kutofanya kazi vizuri.
➖Fanya mazoezi - huboresha ufanyaji kazi wa mapafu na misuli ya upumuaji, pia husaidia kuongeza kinga mwilini na kuimarisha ufahamu (mind state)

Kuzuia kwikwi ni muhimu tu kwa wale wanaopata mara kwa mara.

💥Matibabu ya kienyeji: (Usifanye kwa mtoto)

➖Kumsh*tua mhusika, au kumzubaisha ili kuondoa mawazo yake kwenye kwikwi
➖Kunywa glasi ya maji iliyojaa bila kukata pumzi
➖Kubana pumzi na kuhesabu mpaka kumi
➖Kuweka sukari chini ya ulimi
➖Kulala. Usingizi ni dawa moja nzuri sana ya kwikwi
➖Kwa mtoto anayenyonya waweza kumnyonyesha, au kumuweka begani acheue.
➖KWIKWI-twanga hiliki changanya na maziwa kisha kunywa glasi moja.

💥Matibabu ya kitaalam
Muone daktari kwa matibabu k**a

➖Kwikwi haikatiki kwa muda mrefu (siku au zaidi),
➖Kwikwi inakusababisha kuchoka sana,
➖K**a mapigo ya moyo yanabadilika,
➖K**a unashindwa kulala kutokana na kwikwi
➖K**a inasababisha msongo mawazo kutokana na kujirudia mara kwa mara.

Kabla ya kuanzisha dawa ni muhimu kufanya vipimo ili kuhakikisha magonjwa yanayoweza kusababisha kwikwi yanapatiwa matibabu k**a yapo.

K**a chanzo cha kwikwi kimefahamika katika uchunguzi, tibu chanzo na kwikwi itaisha.

17/04/2018

Dawa ya jino ya asili

Maumivu ya jino ni moja ya maumivu mabaya sana kuyapata, maumivu mengine mabaya zaidi ni maumivu ya sikio. Jino linaweza kupatwa na maumivu ambayo yanaweza kupelekea jino kutoboka na hata kuong’olewa kabisa.

Maumivu haya yanaweza kuletwa na maambukizi ya bakteria kutokana na vyakula tunavyokula au kutokusafisha kinywa vizuri kila siku, jino kupata jeraha, magonjwa ya fizi, na udhaifu wa mifupa mwilini mwako kwa ujumla.

Maumivu mengi ya jino ni ishara kuwa huna chumvi ya kutosha mwilini, huna maji ya kutosha mwilini na hujishughulishi na mazoezi ya viungo kila mara.

Dawa zifuatazo zinaweza kutuliza maumivu ya jino na hata kuliziba kabisa iwapo tayari limeanza kutoboka.

1. Asali yenye mdalasini

dawa ya jino
Asali yenye mdalasini

Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha mdalasini ya unga na vijiko vikubwa viwili vya asali mbichi na upake kidogo kidogo juu ya jino linalouma mara kadhaa kwa siku mpaka maumivu yatakapopotea.

2. Aloe vera (mshubiri)

dawa ya jino
Aloe Vera (mshubiri)

Pata aloe vera fresh na uchane kupata maji maji yake (utomvu) na unyunyize juu ya hilo jino linalouma kidogo kidogo kutwa mara 2

3. Mafuta ya n**i na karafuu

Dawa ya Jino
Mafuta ya n**i

Chukua karafuu 3 zitwangwe kwenye kinu, changanya na mafuta ya asili ya n**i kijiko kidogo kimoja uliyotengeneza mwenyewe nyumbani. Pasha kwenye moto k**a dakika tatu, ipua na usubiri mchanganyiko wako upoe.

Paka mchanganyiko huu juu ya jino linalouma na uache kwa dakika 7 kisha jisukutue kinywa na maji.

Dawa ya Jino
Karafuu

4. Majani ya mpera

Dawa ya Jino
Majani ya Mpera

Majani freshi ya mti wa mpera yanatibu pia jino linalouma sababu ya sifa yake ya kutibu maambukizi na huua pia bakteria wabaya wanaoshambulia jino.

Tafuna tu jani au mawili ya mti huu mpaka mara mbili kwa siku kwa siku kadhaa na jino litaaacha kuuma.

Unaweza pia kuchemsha katika moto majani kadhaa ya mti huu kisha ipua chuja na uongeze chumvi kidogo ya mawe ya baharini na utumie kusafishia kinywa chako ukitumia mswaki mara 2 kwa siku kwa siku kadhaa.

5. Maji ya uvuguvugu na chumvi

Mchanganyiko rahisi wa maji ya uvuguvugu na chumvi unaweza kusaidia kutibu maumivu ya jino.

Changanya nusu kijiko cha chai cha chumvi ya mawe ya baharini na maji ya uvuvugu glasi moja na utumie kusafisha kinywa chako ukitumia mswaki mra 2 kwa siku kwa siku kadhaa.

Mchanganyiko huu husaidia kutibu bakteria, maambukizi na uvimbe katika fizi.

6. Kitunguu maji



Dawa ya Jino
Silesi za kitunguu maji

Kitunguu maji kina sifa ya kuzuia vijidudu nyemelezi ndani ya mwili na kinaweza kutumika pia kutibu maumivu ya jino kwa kuviua vijidudu vinavyosababisha kuoza kwa meno.

Tafuna silesi kadhaa cha kitunguu maji freshi ili kupunguza maumivu ya jino. Au k**a huwezi kukitafuna basi weka tu kipande cha silesi cha kitunguu maji juu ya jino linalouma kwa dakika 10 hivi mara kadhaa kwa siku ili kuondoa hayo maumivu.

7. Kitunguu swaumu

Dawa ya Jino
Kitunguu Swaumu

Kutumia kitunguu swaumu pia kunaweza kurahisha kwa haraka kuondoa maumivu ya jino. Kitunguu swaumu huua bakteria, huua virusi pia ni antibiotiki ya asili isiyo na madhara k**a antibiotiki za viwandani.

Tafuna punje 1 au 2 za kitunguu swaumu kila siku. Au katakata vipande vidogo vidogo vya punje 2 au 3 za kitunguu swaumu uchanganya na chumvi kidogo ya baharini kwa mbali na uweke mchanganyiko huo moja kwa moja juu ya jino linalouma na uache kwa dakika 5 au 7 hivi mara 2 kwa siku kwa siku kadhaa.

8. Pilipili na chumvi

Dawa ya Jino
Pilipili Manga

Pilipili na chumvi unaweza kuwa mchanganyiko mzuri sana wa dawa za asili kwa kutibu maumivu ya jino sababu vyote viwili chumvi na pilipili hudhibiti bakteria na maambukizi mbalimbali.

Pata pilipili manga nyeupe au nyeusi ya unga na uchanganye kiasi sawa cha pilipili na chumvi ya mawe ya baharini kisha ongeza kiasi kidogo cha maji kupata uji mzito kidogo na uuweke juu ya jino linalouma kwa dakika kadhaa kila siku kwa siku kadhaa.

Ni mhimu pia kuonana na daktari wa meno kwa uchunguzi zaidi kwani wakati mwingine dawa hizi zinaweza zisikuponye tatizo la jino kuuma au kutoboka k**a unavyotarajia.

Sehemu nyingi mijini zipo kliniki maalumu kwa ajili ya meno tu, waone madaktari hao kwa uchunguzi juu ya matatizo yako ya meno mara kwa mara.

Address

Mbezi Beach
Dar Es Salaam
2550

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Salim Health Care posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Salim Health Care:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram

Category