21/11/2025
Unapokosa ajira mara nyingi, ni rahisi kuhisi kukata tamaa. Gloria Bulondo ( ), Mhasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Ignite Youth Future, anaeleza katika video hii jinsi alivyokabiliana na changamoto za afya ya akili baada ya kuapply kazi 250 na kukosa zote. Hofu, wasiwasi, na huzuni mara nyingine huchukua nafasi kubwa kimya kimya, lakini Gloria anatufundisha jambo muhimu: kamwe usikate tamaa. Kila changamoto ni fursa ya kujifunza. Tafuta msaada unapohitaji, jenga mtazamo chanya, na chukua hatua ndogo kila siku kuelekea ndoto zako.