10/02/2022
Kaka yetu, k**anda mwenzetu na kiongozi wetu mpendwa, Mheshimiwa Joseph Haule (Prof Jay) ni mgonjwa yapata wiki 3 sasa, akiendelea na matibabu hospitali ya taifa ya Muhimbili chini ya uangalizi maalum wa kitabibu.
Ni jambo la kutia moyo kwamba anaendelea vizuri ingawa kwa kasi ya taratibu hivyo tuendelee kumuombea aweze kupona kabisa. Kwa kuheshimu misingi ya "right to privacy" kwa sasa imeshauriwa na familia kutoweka hadharani tatizo linalomsumbua. Muda ukifika na familia ikawa tayari basi mtajulishwa anasumbuliwa na nini.
Pamoja na kwamba familia haijaomba msaada katika kumhudumia Jay, lakini sisi k**a jamii tuna wajibu wa kufanya. Jay ni kaka kwa baadhi yetu, ni baba wa familia, ni rafiki, ni kiongozi na ni mwanamuziki ambaye sauti yake imetuburudisha na kukonga nyoyo zetu kwa zaidi ya miongo miwili sasa.
Kwa kuzingatia hayo yote, tuna wajibu wa kufanya kwake. Tusisubiri hadi familia iombe msaada, tutimize wajibu wetu kumuonesha kwamba tupo pamoja nae katika kipindi hiki kigumu.
Pia kwa ndugu yetu Jay tushik**ane na familia kuonesha upendo wetu kwake katika wakati huu wanapomuuguza mwenzao. Taarifa zinaonesha Jay anatumia zaidi ya 4M kwa wiki hospitalini. Pamoja na kwamba familia inapambana kumudu gharama hizo lakini si vibaya na sisi kumshika mkono.
Tunaweza kuweka malengo ya kumsupport matibabu yake kwa mwezi mmoja ujao wakati tukiendelea kumuombea na tathmini za kitabibu zikiendelea kupima unafuu na utoshelevu wa huduma za ndani au hitaji la matibabu ya ziada nje ya nchi.
Tujipe challenge ya masaa 72 (siku 3 kuanzia leo hadi jumamosi jioni kumshika mkono mwenzetu.
Michango yote itapokelewa na familia kwa niaba yake kupitia;
MPESA: 0757919192 Joseph Haule,
TiGOPesa: 0715919192 Joseph Haule,
CRDB account no: 0112044845200 Joseph Leonard Haule.
Mungu akubariki ukafanye jambo kwa ajili ya uhai na uzima wa mpiganaji mwenzetu huyu. Amen!
PLZ SHARE.❗