YOUR Health Matters Coaching

YOUR Health Matters Coaching "Tunakusaidia kupata elimu ya afya, pia utatuzi wa matatizo ya Uzazi na magonjwa Sugu kupitia Tiba l

Je,
Ulishawahi kuugua au kujisikia vibaya katika afya yako na hujui nini sababu? Uko mbali na unatamani angalau uweze kuongea na daktari aweze kukusaidia ushauri wa kitabibu na hujui wapi pa kumpata? Unayo simu na unatamani uwe na rafiki daktari ili aweze kukupatia ushauri wa kitabibu wakati unapohitaji? Usihangaike YOUR HEALTH MATTERS COACHING inakuwezesha kuongea na daktari kupitia simu yako ya mkononi. Unachohitaji ni wewe kutuma ujumbe wa SMS/ WhatsApp kupitia namba zetu +255789699225 Dr Sam na kuzungumza na daktari kila mara, na pindi unapohitaji msaada wa haraka zaidi.

21/02/2023
29/04/2022

Hii ndio maana ya Big Baby

Mtoto anapozaliwa na u*ito wa zaidi ya kilo nne (4kg) inasemwa kwamba huyo mtoto ni mkubwa. Hata hivyo hatari huongezeka zaidi mtoto anapozaliwa na zaidi ya kilo nne na nusu(4.5kg), wataalam wenyewe wanaita Macrosomia.

Sababu kubwa zinazosababisha mtoto kuzaliwa mkubwa ni
1.Sababu za kurithi. Mama anapoongezeka u*ito mkubwa wakati wa ujau*ito inawezekana akajifungua mtoto mwenye u*ito mkubwa
2.Ugonjwa wa Kisukari. Ugonjwa wa Kisukari ndio sababu kubwa ya mama kuzaa mtoto mkubwa
3. Mara chache mtoto anakuwa na ugonjwa ambao unamfanya awe mkubwa akiwa tumboni

Kinyume na watu wengi wanavyofikiria kuzaa mtoto mkubwa ni sifa, kitaalam sio salama. Mtoto mkubwa anafanya mama kuwa katika hatari kubwa ya kujifungua kwa njia ya upasuaji. Pia inaongeza hatari ya mtoto kuumia wakati wa kuzaliwa. Madhara mengine ni pamoja na mama kuvuja damu nyingi au mfuko wa uzazi kupasuka
-
Wewe ulipojifungua mwanao alikuwa na kilo ngapi..!? Tushare experience kwa pamoja kwa Mama wanaokuja 🤰🏽🤱

Faida za kutumia mayai kwenye kifungua kinywa.1. Huongeza Shibe,  protein iliyopo katika mayai humfanya mtu kukaa muda m...
25/04/2022

Faida za kutumia mayai kwenye kifungua kinywa.

1. Huongeza Shibe, protein iliyopo katika mayai humfanya mtu kukaa muda mrefu Bila kusikia njaa tofauti na vyakula vyengine k**a bidhaa za ngano

2. Chanzo kikubwa Cha protein.,
Mayai Yana kiasi kikubwa Cha Amino Acid, ambazo huupa mwili kiasi kikubwa Cha protein.

3. Hulinda macho., Kemikali Aina ya Leutin, na zeaxanthin zinaaminika kulinda macho dhidi ya mionzi mikali . Pia husaidia kuepuka tatizo la mtoto wa jicho kwa wazee

4. Huimarisha afya ya ubongo, kurutubisho Aina ya "Choline" ambacho hupatkan katika ubongo husaidia kuimarisha ubongo na kuweka kumbukumbu sawa.

👉🏽 Ovulation test kit.Hizi anaweza kutumia mwanamke yeyote anaehitaji kushika mimba lakini huwafaa zaidi wanawake ambao ...
24/04/2022

👉🏽 Ovulation test kit.
Hizi anaweza kutumia mwanamke yeyote anaehitaji kushika mimba lakini huwafaa zaidi wanawake ambao wanataka kupata mimba ambao;

● Mizunguko yao haieleweki yaani sio rahisi kupiga hesabu na kujua siku zao za hatari ni zipi.

● Umetafuta mimba muda mrefu hupati na hata ukipimwa unaambiwa huna shida yeyote.

● Uko bize sana na kazi kiasi kwamba huwez kutulia na kufuatilia siku zako.

● Mme wako au mpenzi wako muda mwingi hauko naye hivyo sio rahisi kulala naye mara kwa mara

● Unataka mtoto haraka.

Ni rahisi sana kukitumia na kujipima mwenye.
Ukimaliza kuona siku zako za hedhi, chukua kipimo kimoja kila siku kisha kikojolee au chukua mkojo kwenye chupa ndogo kisha tumbukiza k**a vile unavyopima mimba kisha angalia majibu,

Endelea kupima kila siku mpaka uone hedhi nyingine, k**a siku zako za hatari zifika kipimo kitaonyesha mistari miwili k**a siku zako hazijafika kipimo kitaonyesha mstari mmoja,

kutokana na matatizo mbalimbali ya uzazi unaweza usione siku zako za hatari mwezi huo hivyo unaweza kuendelea kujaribu miezi mingine lakini asilimia kubwa siku zako hu*iona baada ya kutumia kwa mzunguko mmoja tu.

Kumbuka, kipimo hichi kinatakiwa kisomwe ndani ya dakika kumi, na muda wa kupima ni saa nne asubuhi mpaka saa mbili usiku, usipime haraka baada ya kuamka kwani homoni hizi huchelewa kuongezeka mwilini baada ya kuamka, usinywe maji mengi sana kabla ya kipimo kwani mkojo utakua mwepesisana na kushindwa kusoma majibu.

Vipimo Vinapatikana Kwetu Kwa Bei Nafuu Sana, Kwa Elfu 20 tu!


*ito

MAMA MJAMZITO FANYA HAYA KILA SIKU1: Kunywa maji mengi 2. kula matunda na mboga za majani kwa Wingi3. Pata Muda wa kupum...
23/04/2022

MAMA MJAMZITO FANYA HAYA KILA SIKU

1: Kunywa maji mengi
2. kula matunda na mboga za majani kwa Wingi
3. Pata Muda wa kupumzika
4. Relax, usiwe mtu wa kuwa na stress,hasira kutukana..Mwanao anasikia😁 na unamfundisha tabia mbaya

5. kula vitu vyenye faida KIAFYA,vinampa mtu madini,ma Omega 3 k**a yote uzae mtoto mwenye Akili(samaki,vitutubisho vyenye Haya madini),vyakula vya Calcium k**a Samaki,dagaa na Virutubishi Mfano Pregnacare,prenatal etc mtoto anakuwa na mifupa ina nguvu imara...usile kujifurahisha tu,kula vitu vitamjenga mtoto afya
Vyakula vya protein vinamfanya mwanao apate pate misuli azaliwe ana Afya

6. Fanya mazoezi mepesi Mepesi,kuweka nyonga yako Sawa,kukufanya uwe Fit,maana kuwa na mimba Sio Ugonjwa(labda k**a mimba Inasumbua na umekatwa na dr kufanya chochote).

7. Fanya tendo landoa,haikatazwi labda k**a unaumwa na haitakiw kwa usalama wa mimba
8. Tumia FOLIC ACID au SUPPLIMENTS ulizopewa na dr Wako.
9. Anza Clinic Mapema na hudhuria clinic Zako zote na kufuata Unayoambiwa.
10. Fanya maandalizi ya Nguo za kumpokelea mtoto,vitu vinavyotakiwa kwenda navyo hospitali.

Wangapi tumeelewana?? SHOW LOVE ❤️, MTAG Rafiki yako au Mama K kumsaidia kupata Elimu hii🤝😍.

Mtoto anaweza kuanza kugeuka kuanzia wiki ya 32 mpaka wiki 36 Endapo hajageuka kuanzia wiki 35 kurudi chini hiyo inaweze...
22/04/2022

Mtoto anaweza kuanza kugeuka kuanzia wiki ya 32 mpaka wiki 36

Endapo hajageuka kuanzia wiki 35 kurudi chini hiyo inawezekana isiwe shida kwa sababu anaweza kugeuka mpaka wiki ya 36 ila endapo hajageuka mpaka wiki ya 36 hiyo ndio tunaita “BREECH PRESENTATION”.

Kuna aina 3 za Breech presentation.

1. Kutanguliza miguu na matako kwa pamoja huitwa COMPLETE BREECH

2. Kutanguliza Matako na kukunjua miguu sehemu ya goti huitwa FRANK BREECH.

3. Kutanguliza mguu mmoja au miwili huitwa FOOTLING BREECH

Je naweza kujifungua kwa njia ya kawaida K**a mtoto Yuko BREECH?

Hutegemeana mama moja na mwingine na mtoa huduma njia atakayo chagua lakini kwa siku hizi Madaktari wengi hupendelea kufanya operation (Cesarian section) ili kuepuka shida mbalimbali.

Lakini Kuna njia ambayo Daktari anaweza fanya maneuver kwenye tumbo la Mjamzito njia hiyo huitwa _EXTERNAL CEPHALIC VERSION_ ambayo hufanyika Kati ya wiki 36 na 38 za Ujau*ito.
-
_EXTERNAL CEPHALIC VERSION_ huu ni utaratibu unaotumika kugeuza kijusi kutoka nafasi ya breech au nafasi ya kulala-upande (transverse) kuwa nafasi ya kichwa-chini (vertex) kabla ya leba kuanza. Ukifanikiwa, hufanya iwe rahisi kwa mama kujifungua Kwa njia ya kawaida!

MWISHO;
Unaweza kuwa mwalimu kwa wengine kwa KUS-hare makala hii zaidi na zaidi ili wengi wapate Elimu hii uliyoipata wewe.

- Pia kupata masomo mengine k**a fanya kulike ukurasa wetu 🤝

BADO SIKU MOJA TU😲🏃🏽‍♀️Za KUJISAJILI NA MAMA K WATSUP GROUP.Ni group linalojumuisha Wamama wajawazito TU, Tanzania 🇹🇿 na...
19/12/2021

BADO SIKU MOJA TU😲🏃🏽‍♀️

Za KUJISAJILI NA MAMA K WATSUP GROUP.
Ni group linalojumuisha Wamama wajawazito TU, Tanzania 🇹🇿 na nchi za jiran, mpaka sasa Mama K wapo 115 ❤❤🥰 (japo kuna wengine Wameishajifungua karibun waliingia Na mimba zao kwa group).

Huku utakutana na mama wajawazito wenzako,mtashauriana juu ya mambo mbali mbali, lakin Pia tupo Doctor Mle, tunashauri kitaalamu kabisa.
Lakin pia, utajifunza Lolote unalotamani kujifunza🔥🔥.

UMUHIMU WA HILI GROUP👇🏾

1. Ushauri wa Kitaalamu wa Dr na ma nurse UNAUPATA unapohitaji masaa 24

2. Uta share safari yako na Mama K wenzako,aisee wana enjoy sana hawa Mama K,yaan hupati upweke hata kidogo.

3. kuna vitu vidogo vidogo mama k wenzako watakushaur la kufanya ili upate unafuu...

Kuna MAMA K mliniomba niwaunge, Naomba NICHEK Tena Niwaunge, Na kwa ambao mlinitafuta week hii kesho ndio Group letu la tatu linaanza rasmi 😍💃....

Lakin pia mama k wote mnaotamanI, Nafasi zipo na IMEBAKI SIKU MOJA TU YA KUJISAJILI😲🏃🏽‍♀️, wahi

DM/ inbox nikupe Utaratibu.....

Hautajuta hata kidogoooo.

Hili group wananifanya na mimi nataman ningekuwa mama K aiseee, full ku enjoy maisha yao humo ndani ya Group.

Mambo 5 Ya Ajabu Usiyoyafahamu Kuhusu Uke Wako1⃣ Uke una mfumo unaojisafisha wenyewe kwa ndani na ni sehemu moja ya mwil...
06/12/2021

Mambo 5 Ya Ajabu Usiyoyafahamu Kuhusu Uke Wako

1⃣ Uke una mfumo unaojisafisha wenyewe kwa ndani na ni sehemu moja ya mwili wako ambayo ni safi kuliko maelezo, safi kuliko hata midomo yetu.

2⃣ Uke una Mfumo unaosafisha damu ya hedhi na shahawa wenyewe, hauhijaji
msaada wa aina yeyote

3⃣ Uke wenye afya una bacteria, lactobacilli, ambao ni kawaida kuwepo humo. Hawa hupambana na vijidudu visivyopaswa kuwepo huko kulinda uke
na mfumo wa uzazi kwa ujumla.

4⃣ Uke wenye afya sio mkavu, muda wote una ute usiokua na rangi (k**a maji), mwepesi na unaonata. Uzito, wingi na mnato wa ute huu hutegemea na mabadiliko ya mwili wa mwanamke. (Jifunze kutofautisha ili ujue muda inapaswa kumuona daktari)

5⃣ Uke wenye afya una harufu, ambayo ni nzuri, murua na isiyokera
K**a harufu itakua kali na inayokera (k**a yai bovu) basi uke wako
hauko katika afya njema na unahitaji kumuona daktari.

*Tunza Uke wako Ukutunze*

kwa kufuatilia ukurasa wetu wa Afya, share ujumbe huu uwafikie watu wengi.

Imeandaliwa na Dr.Sam

(+255) 0657251686 (whatsapp) for Dr Sam 🤳

“JIFUNZE na Chukua Hatua Juu Ya Afya Yako”.

NJIA SABA ZA KUTUMIA ILI MKE APATE MIMBA KIRAHISI. 1.Kufanya tendo la ndoa katika mtindo (style) ambayo itafanya mbegu z...
16/10/2021

NJIA SABA ZA KUTUMIA ILI MKE APATE MIMBA KIRAHISI.

1.Kufanya tendo la ndoa katika mtindo (style) ambayo itafanya mbegu za kiume zikae kwa muda mrefu ukeni na hivyo nyingi kupanda kuingia kwenye kizazi na kwenda kurutubisha yai.

'missionary position' ni nzuri zaidi, ambapo mwanaume anakuwa juu, epuka positions za mwanamke kuwa juu kwani hufanya mbegu zimwagike kwa gravity. Jaribu pia kuweka mto chini ya kiuno ili kukiinua na kufanya mbegu ziingie ndani kwa urahisi zaidi.

2. Tumia ovulation prediction kit, hiki ni kifaa ambacho kitakusaidia kujua wakati hasa mwanamke ameengua yai na ndio kipindi ambacho mwanamke ana uwezo wa kushika mimba akikutana na mumewe. Ni rahisi kutumia.

3. Fanya tendo la ndoa kabla ya kuengua yai (kabla ya ovulation), huongeza uwezekano wa kushika mimba kuliko kusubiria ovulation au kufanya baada ya ovulation.

Kutaneni siku mbili au tatu kabla ya ovulation. Ukitumia ovulation test kit, mkutane kuanzia siku itakapokuwa positive kwani huwa inapredict ovulation kutokea 48 hrs after it tests positive.

4. Usitegemee njia ya kalenda kutabiri uenguaji yai, njia hii kwa kiasi fulani huweza kuwasaidia wale wenye mzunguko wa siku 28, lakini pia haina uhakika wa 100%, wengi wa wanawake hawaengui yai siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, kwa hiyo kutegemea kalenda kutakuchelewesha kupata ujau*ito.

5. unapotaka kushika mimba, acha au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya.

6. unapotaka kupata mimba, tendo la ndoa liwe kitu 'enjoyable' na sio tendo 'mechanical' kwa ajili ya kutafuta mtoto. Plan a romantic evening or try something different to spice things up.

How you are feeling sexually may increase your chances of getting pregnancy. For women a better or**sm may help pull the s***ms into the uterus and for men a better or**sm may increase their s***m count.

7Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, angalau siku tatu kwa wiki, ikiwezekana on alternate days.

Kumbuka kuna asilimia 10 - 25 ya couples ambazo zina matatizo ya infertility lakini vipimo havionyeshi tatizo, inaweza kuwa namna ya kufanya mapenzi ndio ikawa shida, jaribu njia hizo 7 juu.

K**a hizi njia hazijakusaidia basi utakuwa na matatizo na unaweza kumuona daktari kwa msaada wa vipimo na matibabu. Natumaini u*i huu unaweza kuwa msaada kwa watafutao watoto...

Ndugu kwa kufatilia Makala zetu za Afya za Kila siku .K**A BADO HUJALIKE USISAHAU KULIKE NA KUSHARE UKURASA

“JIFUNZE na Chukua Hatua Juu Ya Afya Yako”.

Kwa kawaida mtoto huanza kucheza kwa mara ya kwanza, kuanzia wiki ya 16 hadi wiki ya 25 katika kipindi cha ujau*ito,K**a...
31/05/2021

Kwa kawaida mtoto huanza kucheza kwa mara ya kwanza, kuanzia wiki ya 16 hadi wiki ya 25 katika kipindi cha ujau*ito,K**a ni ujau*ito wa kwanza inawezekana usimsikie hadi ikikaribia wiki ya 25.Ujau*ito wa pili ,mama huanza kumsikia mtoto akicheza mapema kuanzia wiki ya wiki 13.

Mtoto anatakiwa kucheza mara ,6-10 ndani ya saa moja. Ile miezi 6 ya mwanzo kucheza kwa mtoto hua sio sana.Kipindi cha usiku ndio muda wa mtoto kupigapiga tumbo la mamaye kuliko mchana.

MTOTO ANAWEZA KUCHEZA MIEZI MITATU YA MWANZO?

Mtoto hua mdogo sana miezi mitatu ya mwanzo.Hua na urefu wa 7.6-10 cm (3-4 inches) na u*ito wa gramm 28g (1 ounce) ,katika kipindi hiki viungo vya mtoto hua ni vilaini na vinakua havijakomaa hivo kusababisha mtoto kutokusikika akiwa anacheza.Mtoto hua mkubwa na kuongeza mwishoni mwa mwezi wa nne (second trisemister).

SABABU ZINAZOMPELEKEA MTOTO KUTOCHEZA AKIWA TUMBONI.
1. Kukosa nguvu za kutosha kutokana na lishe duni ya mama yake.
2. Mama anapotembea sana au kusimama kwa muda mrefu ,kuna mfanya mtoto achoke hivo kumpelekea kulala na kumfanya asicheze.
3. Mama anapokua na maradhi au matatizo ya kiafya,hudhoofisha afya ya mtoto ,hivo hupelekea mtoto kukosa nguvu na kushindwa kucheza.
4. Mtoto kuwa mdogo sana na u*ito mdogo pia humfanya ushindwe kucheza.
5. Mama anapokuwa amechoka kutokana na kazi nzito,mtoto nae huchoka na huhitaji kupumzika na huwa kimya sana.
6. Kupoteza uhai kwa mtoto (kufa)

SABABU ZINAZOWEZA KUMFANYA MTOTO ACHEZE AKIWA TUMBONI.
1. Kunywa maji ya baridi.
2. Fanya kitu cha kustusha kwa sababu maalumu.
3. Kula vyakula vya sukari.
3. Kula vyakula vya pilipili.
2. Ongea na mtoto

USHAURI:
Mama mjamzito,usimposikia mtoto akicheza katika muda ambao anatakiwa acheze ni vema ukafika katika kituo cha afya na kukutana na waatalamu,kwa ajir ya uchungu*i wa hali ya mtoto.

ZINGATIA:
Matumizi ya pombe na sigara ni hatari kwa afya ya mama na mtoto.
-
MWISHO
Prepared by Dr Sam CEO/ founder of Sam Nutritional Clinic
For more help Contact with us :-
(+255) 0789699225 (Watsup/call/sms) Dr Sam 🤳👨🏻‍⚕️

Ukiwa umependa makala hii na ungepanda kupata elimu sahihi ya afya kila siku, usihaau kuliki ukurasa Wetu ili kutopitwa na makala zetu pendwa za afya.

Pia Unaweza kuwa mwalimu kwa wengine kwa KUS-hare makala hii zaidi na zaidi ili wengi wapate Elimu hii uliyoipata wewe.

26/04/2021

VITU VITATU VINAVYOPUNGUZA KIUNGULIA KWA MAMA MJAMZITO.

1. Kula kiasi kidogo cha chakula na usile ukashiba sana. Kwa kuwa mama mjamzito huwa anasikia njaa mara kwa mara na anahitajia kula vyema ili aujenge vizuri mwili wake na watoto,
basi ni bora chakula chake ukigawe katika sehemu kadhaa ndogo, na ale mara kadhaa, badala ya kula sana wakati mmoja.

Suala hilo litafanya tumbo lake lisijae na kusaidia kuzuia asidi isipande juu ya tumbo na kusababisha kiungulia na gesi.

2. Jitahidi usinywe maji mengi sana baada ya chakula au wakati wa kula,

3. Jitahidi usilale tu mara baada ya kula, subiri k**a nusu saa hivi ipite ndio ulale.
Unapolala usilaze kichwa moja kwa moja bila mto, bali tumia mito kuegemeza kichwa ili kuzuia asidi isirejee juu ya tumbo na kusababisha kiungulia.
Unapohisi kiungulia kunywa glasi ya maziwa au kula mtindi.
Na k**a hali hiyo haijatoweka kunywa maji ya moto glasi moja yaliyowekwa kijiko kimoja cha asali.
-

MWISHO
Prepared by Dr Sam CEO/ founder of Sam Nutritional Clinic
For more help Contact with us :-
(+255) 0789699225 (Watsup/call/sms) Dr Sam 🤳👨🏻‍⚕️

Ukiwa umependa makala hii na ungepanda kupata elimu sahihi ya afya kila siku, usihaau kuliki ukurasa Wetu ili kutopitwa na makala zetu pendwa za afya.

Pia Unaweza kuwa mwalimu kwa wengine kwa KUS-hare makala hii zaidi na zaidi ili wengi wapate Elimu hii uliyoipata wewe.

20/04/2021

FAIDA ZA PARACHICHI KATIKA NYWELE

✅Moisturisers hair (unyevu katika nywele)
✅Faster growth of hair (hukuza nywele haraka)
✅Protect against dandruff (kuzuia/kuondoa mmba
✅Rejuvenates hair(hufufua nywele)

Namna ya kutengeneza mchanganyiko wa parachichi

Parachichi moja+Nazi changanya, paka kwenye nywele kaa dakika 10 na zaidi, osha nywele zako. Kumbuka usichane nywele zikiwa mbichi kwa sababu nywele zikiwa mbichi huwa dhaifu.

⚠️Tumia Natural Feminine Wash isiyokuwa na kemikali Kuoshea uso, kuzuia Nywele kukatika, kung'arisha Nywele na kutoa mba na vidonda kichwani. Tuwasiliane kwa kupiga simu au WhatsApp 0789699225, Dr Sam.
-
Upendo ni kujifunza kwa pamoja, kuonyesha Upendo unaweza kushare kwa marafiki zako pia.

Address

Dar Es Salaam
9225

Telephone

+255789699225

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when YOUR Health Matters Coaching posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to YOUR Health Matters Coaching:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram