Familia Katika Uislamu

Familia Katika Uislamu Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Familia Katika Uislamu, Psychologist, Dar es Salaam.

27/10/2025

💍Kumbuka kwamba Harusi ni siku moja, lakini ndoa ni safari ya maisha. Usitumie nguvu zote kwa siku moja ukasahau safari yote.

23/10/2025

🌷Mke mwenye Hekima hampi mume wake maneno mengi, bali utulivu unaotuliza roho yake. Wakati ulimwengu unamchosha kwa mapambano ya kila siku, ni upendo wa mke wake unaomrudishia nguvu na maana ya kuendelea kuishi. Upendo wa kweli si makelele, ni utulivu unaoongea kwa ukimya.


21/10/2025

Maneno ya mzazi ni kama mbegu — yakipandwa kwa upendo, huzaa ujasiri; yakipandwa kwa hasira, huota
Kila neno tunalosema kwa mtoto lina nguvu ya kumwinua kutoka sifuri hadi mia au kumuangusha kutoka mia hadi sifuri.
Watoto ni vioo vya maneno yetu — wanajiona jinsi tunavyowaona.
Tuseme vizuri. Tufanye kila neno letu liwe daraja, si kizuizi. ❤️

14/10/2025

📌 Fundisha mtoto wako kusema hapana nyumbani.
Maana kama hajajifunza kusema hapana kwa wazazi, kaka, dada au marafiki wa karibu, atashindwa kusema hapana kwa dunia.
Dunia ambayo itampimia upendo kwa masharti, itamtaka akubali kila kitu ili apendwe, ili asichekewe, ili asiachwe.

Mtoto anayejua kusema hapana kwa utulivu, anajua thamani yake.
Anaelewa kuwa heshima si utii wa kila kitu, bali ni kujua mipaka ya nafsi yake.

Anza leo! Jenga mtoto anayeweza kusema hapana bila woga, kwa sababu hiyo ndiyo ngao yake atakapoanza kukutana na ulimwengu usio na huruma

11/10/2025

Kumbuka, maisha ya mtoto ni kucheza. Ndiyo lugha yake ya kwanza ya kujifunza dunia, kujua watu, na kuelewa hisia. Kila mchezo anaocheza ni somo jipya katika safari yake ya ukuaji .

Usimdhibiti sana kwa kucheza, maana humo ndimo anajifunza kujiamini, kushirikiana, na kufurahia maisha. Ukimnyima muda wa kucheza, ni kama unamnyima nafasi ya kuwa yeye mwenyewe .

Mtazame akicheka, akikimbia, akibuni vitu visivyo na mpangilio — hapo ndipo utamu wa utoto ulipo. Mtoto anapocheza, dunia yake inakuwa salama, huru, na yenye matumaini .

09/10/2025

Mfundishe mtoto wako jinsi ya kuishi na wengine akiwa bado mdogo, kwa sababu usipomfundisha akiwa mdogo, atakapokua itakuwa vigumu kwake kuishi katika jamii na watu wengine.


06/10/2025
25/09/2025
14/09/2025

Jaribu kuongea na mtoto wako mara nyingi ...

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Familia Katika Uislamu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram

Category