AFYA BORA KWA LISHE

AFYA BORA KWA LISHE habari wapendwa ukurasa huu kwaa ajili ya kujifunza afya zetu dhidi ya magonjwa

MAGONJWA YANAYOSABABISHA WANAWAKE KUWA WAGUMBAP.I.D(pelvic inflammatory disease) na FIBROIDS inavyotesa wanawake na kuwa...
22/08/2022

MAGONJWA YANAYOSABABISHA WANAWAKE KUWA WAGUMBA

P.I.D(pelvic inflammatory disease) na FIBROIDS inavyotesa wanawake na kuwasababishia ugumba.

P.I.D NI NINI??

P.I.D ni maambukizi kwenye via vya uzazi wa mwanamke. Ugonjwa huu unaweza kupelekea uharibifu mkubwa kwenye mayai,mfuko wa uzazi,mirija ya uzazi nk . Pia ugonjwa huu ni moja ya UGUMBA kwa mwanamke.Huu ni ugonjwa unaosababishwa na kutotibu magonjwa ya zinaa kwa ufasaha na kuacha wale bakteria kuendelea kusambaa kwenye via vya uzazi wa mwanamke.

Je utajuaje kwamba huenda umeathirika na ugonjwa huu wa P.I.D ????

DALILI ZA P.I.D
👉Maumivu ya tumbo sehemu ya chini au ya juu upande wa kulia
👉Kutokwa kwa uchafu ukeni usio wa kawaida na harufu mbaya(wengi hudhani ni fangas kumbe sio)
👉Maumivu makali na kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa
👉Maumivu wakati wa kukojoa
👉Kutapika na homa
👉Uchovu
👉Kutokwa kwa damu nyingi isiyokuwa na mpangilio wakati wa hedhi au wakati sio wa hedhi( hii dalili kubwa na huwa inafanana sana na fibroids)
👉Ugumba( unatafuta mtoto kwa muda mrefu na hupati)
👉Kukojoa mara kwa mara

FIBROIDS NI NINI??

FIBROIDS ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambapo uvimbe huu unaweza kuwa ndani ya kizazi(ukutani mwa kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi au nje kwenye ukuta wa kizazi

Je utajuaje k**a una fibroids?? Hebu angalia dalili zake

DALILI ZA FIBROIDS
👉Kutokwa damu nyingi kwenye via vya uzazi katikati ya mwezi au wakati wa hedhi
👉Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya(wengi wenu huwa mnakimbilia kwamba mna fangas)
👉Maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi ambayo husababishwa na kizazi kujaribu kusukuma huo uvimbe
👉Tumbo kuuma sana chini ya kitovu
👉Hedhi zisizikua na mpangilio na damu hutoka nyingi mpk kupelekea wengine kupungukiwa damu na kutakiwa kuongezewa damu
👉Maumivu wakati wa tendi la ndoa(hii hupelekea achukie tendo la ndoa)
👉Kukosa kwa choo kikubwa au choo kuwa kigumu(constipation)
👉Maumivu wakati wa kukojoa
👉Kukojoa mara kwa mara
👉Ugumba(kuchelewa au kutokupata mtoto)
👉Mimba kutoka mara kwa mara

KWANINI NIMEAMUA KUELEZEA KUHUSU P.I.D NA FIBROIDS????

JIBU:
👉Ni kwa sababu wanawake wengi wakiona dalili k**a kutokwa uchafu wanahisi ni FANGAS tu
👉 Wakiona mimba zinatoka mara kwa mara wengi hukimbilia kusema ni ushirikina au muhusika alikua anatoa mimba sana siku za nyuma wakati labda sio hivyo
👉Kingine mwanaume akiona mkewe hataki tendo la ndoa anahisi mkewe anamsaliti kumbe mwenzie anaumwa
👉 Lakini kubwa zaidi nimeeleza haya yote sababu dalili za magonjwa haya mawili yanafanana kwa ukaribu sana sana.

Tahadhari ukiona dalili yeyote iliyotofauti unapaswa kuwai hospital au kumuona mtaalamu wa afya ili kujua shida ni nini
Kuliko kusubiri mpka matatizo yakawa makubwa zaidi

🩺INAWEZEKANA UKAWA UNA CHANGAMOTO YEYOTE YA UZAZI au YA KIAFYA KWA UJUMLA.
Wasiliana Nasi Dr agustino afya line 1https://chat.whatsapp.com/GRCnRBZJ66aG3TTTqZRBrR

WhatsApp Group Invite

MAGONJWA YANAYOSABABISHA WANAWAKE KUWA WAGUMBAP.I.D(pelvic inflammatory disease) na FIBROIDS inavyotesa wanawake na kuwa...
22/08/2022

MAGONJWA YANAYOSABABISHA WANAWAKE KUWA WAGUMBA

P.I.D(pelvic inflammatory disease) na FIBROIDS inavyotesa wanawake na kuwasababishia ugumba.

P.I.D NI NINI??

P.I.D ni maambukizi kwenye via vya uzazi wa mwanamke. Ugonjwa huu unaweza kupelekea uharibifu mkubwa kwenye mayai,mfuko wa uzazi,mirija ya uzazi nk . Pia ugonjwa huu ni moja ya UGUMBA kwa mwanamke.Huu ni ugonjwa unaosababishwa na kutotibu magonjwa ya zinaa kwa ufasaha na kuacha wale bakteria kuendelea kusambaa kwenye via vya uzazi wa mwanamke.

Je utajuaje kwamba huenda umeathirika na ugonjwa huu wa P.I.D ????

DALILI ZA P.I.D
👉Maumivu ya tumbo sehemu ya chini au ya juu upande wa kulia
👉Kutokwa kwa uchafu ukeni usio wa kawaida na harufu mbaya(wengi hudhani ni fangas kumbe sio)
👉Maumivu makali na kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa
👉Maumivu wakati wa kukojoa
👉Kutapika na homa
👉Uchovu
👉Kutokwa kwa damu nyingi isiyokuwa na mpangilio wakati wa hedhi au wakati sio wa hedhi( hii dalili kubwa na huwa inafanana sana na fibroids)
👉Ugumba( unatafuta mtoto kwa muda mrefu na hupati)
👉Kukojoa mara kwa mara

FIBROIDS NI NINI??

FIBROIDS ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambapo uvimbe huu unaweza kuwa ndani ya kizazi(ukutani mwa kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi au nje kwenye ukuta wa kizazi

Je utajuaje k**a una fibroids?? Hebu angalia dalili zake

DALILI ZA FIBROIDS
👉Kutokwa damu nyingi kwenye via vya uzazi katikati ya mwezi au wakati wa hedhi
👉Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya(wengi wenu huwa mnakimbilia kwamba mna fangas)
👉Maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi ambayo husababishwa na kizazi kujaribu kusukuma huo uvimbe
👉Tumbo kuuma sana chini ya kitovu
👉Hedhi zisizikua na mpangilio na damu hutoka nyingi mpk kupelekea wengine kupungukiwa damu na kutakiwa kuongezewa damu
👉Maumivu wakati wa tendi la ndoa(hii hupelekea achukie tendo la ndoa)
👉Kukosa kwa choo kikubwa au choo kuwa kigumu(constipation)
👉Maumivu wakati wa kukojoa
👉Kukojoa mara kwa mara
👉Ugumba(kuchelewa au kutokupata mtoto)
👉Mimba kutoka mara kwa mara

KWANINI NIMEAMUA KUELEZEA KUHUSU P.I.D NA FIBROIDS????

JIBU:
👉Ni kwa sababu wanawake wengi wakiona dalili k**a kutokwa uchafu wanahisi ni FANGAS tu
👉 Wakiona mimba zinatoka mara kwa mara wengi hukimbilia kusema ni ushirikina au muhusika alikua anatoa mimba sana siku za nyuma wakati labda sio hivyo
👉Kingine mwanaume akiona mkewe hataki tendo la ndoa anahisi mkewe anamsaliti kumbe mwenzie anaumwa
👉 Lakini kubwa zaidi nimeeleza haya yote sababu dalili za magonjwa haya mawili yanafanana kwa ukaribu sana sana.

Tahadhari ukiona dalili yeyote iliyotofauti unapaswa kuwai hospital au kumuona mtaalamu wa afya ili kujua shida ni nini
Kuliko kusubiri mpka matatizo yakawa makubwa zaidi

🩺INAWEZEKANA UKAWA UNA CHANGAMOTO YEYOTE YA UZAZI au YA KIAFYA KWA UJUMLA.
Wasiliana Nasi Dr agustino afya line 1https://chat.whatsapp.com/GRCnRBZJ66aG3TTTqZRBrR

Complete ndio suluhu ya matatizo ya uzazi
16/08/2022

Complete ndio suluhu ya matatizo ya uzazi

14/08/2022

*🌹Utajuaje Una Uvimbe Kwenye Kizazi...?*
Kutambua una uvimbe kwenye kizazi utaona dalili hizi hapa 👇
●Kubleed mabonge
●Kubleed kiasi cha kuishiwa damu
●Tumbo Kuwa kubwa
●Tumbo kujaa gesi
●Kupata maumivu makali sana wakati wa period
●Kupata maumivu makali wakati wa ovulation
●Kutokwa na uchafu ingawa sio kwa wote
●Kutokwa damu baada ya tendo
●Mimba kutunga nje ya kizazi
●Kuvimba miguu
●Kupata ganzi
●Kupata pressure
Dalili hizi zinakuonyesha kuwa una uvimbe
*Kumbuka ni wakati wako wa kupona kabisaa uvimbe*

Ni kipi unahitajii nikusaidie fungukaa dr wako niko apaa leo nataka niwasaidie wanawake wengi katika research yangu nime...
11/08/2022

Ni kipi unahitajii nikusaidie fungukaa dr wako niko apaa leo nataka niwasaidie wanawake wengi katika research yangu nimeona mkiteseka na bila mafanikio mazuri

Ukweli ni kwamba uke ni makazi ya mabilioni ya bakteria wazuri na wale wabaya pia. Na harufu ya uke huwa inabadilika kil...
11/08/2022

Ukweli ni kwamba uke ni makazi ya mabilioni ya bakteria wazuri na wale wabaya pia. Na harufu ya uke huwa inabadilika kila siku wakati mwingine kila saa harufu hubadilika. Mabadiliko haya ni kawaida kabisa kutokana na mabadiliko ya mzunguko, afya yako pamoja na usafi kwa ujumla.
Zifuatazo ni aina za harufu ukeni na majibu kwa maswali yako je harufu husika ni mbaya au nzuri

1.Harufu ya Kuchacha(fermented)

Ni jambo la kawaida kabisa uke kuzalisha harufu ya kuchacha/sour aroma. harufu hii yaweza kufanana na harufu ya kuchacha kwa chakula. Ukweli ni kwamba baadhi ya vyakula na vinywaji kaama mtindi, bia na mkate vina bakteria wale wale ambao wapo kwenye uke wako.

Bakteria hawa wanaosababisha uchachu wanaitwa Lactobacilli. Lactobacilli wanafanya uke kuwa na tindikali nyingi, tindikali hii inalinda uke dhidi ya vimelea wabaya.

2.Harufu ya Kutu ama madini ya copper

Wanawake wengi huripoti kupata harufu k**a ya kutu ukeni. Hii ni kawaida kabisa wala usiwe na hofu kwamba kuna tatizo. Kinachosababisha harufu hii ni

Damu: Damu ina madini chuma , wakati wa hedhi damu iliyozalishwa baada ya ukuta wa kizazi kumeguka husafiri na kutolewa nje kwa njia ya uke.

Tendo la ndoa:Bleed kidogo baada ya tendo la ndoa ni jambo inalotokea sana kwa wanawake wengi hawa wale wakavu ukeni au k**a tendo lilifanyika kwa nguvu sana. Kuzuia hali hii jaribu kutumia vilainishi salama.
K**a haupo kwenye hedhi na wala hujakutana na mwanaume na unahisi harufu hii basi panaweza kuwa na shida. Nenda hospitali mapema k**a itatokea hivo.

3.Harufu nzuri

K**a harufu ya ukeni ni nzuri k**a kitu chene sukari basi usishtuke sana ni mabadiliko tu ya bakteria na ni jambo la kawaida.

4.Harufu ya kemikali k**a chumba kipya.

Kuna sababu mbili kubwa zinazopelekea upate harufu hii k**a
Mkojo: Mkojo una kemikali za ammonia. Unapovaa chupi kwa muda mrefu matone ya mkojo hujikusanya na kuzalisha harufu. K**a mkojo wako una harufu kali basi hakikisha unakunywa maji ya kutosha maana ni kiashiria kwamba umeishiwa maji.

Maambukizi ya bakteria: Sababu ya pili ni kwamba kuna shida ya maambukizi na unahitaji vipimo na tiba ya mapema. Endapo unapata dalili zingine k**a muwasho ukeni, maumivu wakati wa kukojoa, harufu mbaya inayonuka na uchafu wa kijivu au kijani basi ujue una maambukizi ya bakteria.

5.Harufu ya majani yaliyochomwa mfano wa bangi

Sababu kubwa ni stress ama msongo wa mawazo. Mwili una tezi mbili za jasho apocrine eccrine. Wakati wa joto sana tezi ya eccrine huzalisha zaidi jasho ili kupooza mwili na nyakati huku tezi ya apocrine ikifanya kazi kudhibiti athari ya msongo wa mawazo.

Ukiwa na mawazo apocrine huzalisha majimaji mepesi k**a maziwa yanatolewa kwenye kwamba na maeneo ya ukeni. Majimaji haya yakikutana na bakteria wa ukeni ndipo harufu kali huzalishwa.

6.Harufu ya shombo la samaki wabichi

Bilashaka umeshapatwa na hali hii ama kusikia kwa rafiri yako akipata harufu ya shombo la samaki. Sababu kubwa ni
Maambukizi ya akteria na ugonjwa wa trichomonisis. Magonjwa haya yote yanatibika, hakikisha unawahi hospitali haraka ukiona dalili hizo

7.Harufu mbaya K**a kitu kilichooza

Harufu mbaya inayokufanya hata wewe ubane pua ujue siyo ya kawaida kabisa. Ukiona harufu hii ujue kuna shida mahali na unahitaji kurekebisha haraka ili usiabike hata kwa mpenzi wako. Sababu kubwa ni maambukizi ama kutofanya usafi vizuri ukeni.

Lini Unapaswa Kumwona Daktari

Muone daktari mapema endapo harufu unayopata ukeni inaambatana na

muwasho au kuchoma ukeni
maumivu ya uke na maumivu kwenye tendo la ndoa
kutokwa uchafu mzito mweupe
kupata bleed wakati haupo kwenye hedhi
Vidonge Asili vya C P E Vinasafisha uke na kurejesha harufu nzuri ukeni.

**Je, Ni Vyakula Gani Vya Kawaida* *Vinavyosababisha Gesi?* * Vyakula mbalimbali vyenye wingi wa fiber vinaweza kusababi...
29/10/2021

**Je, Ni Vyakula Gani Vya Kawaida* *Vinavyosababisha Gesi?*
*
Vyakula mbalimbali vyenye wingi wa fiber vinaweza kusababisha gesi, navyo ni;

• Maharage na kunde
• Matunda
• Mbogamnboga
• Vyakula vya nafaka *NUKUU* : Ikiwa vyakula vyenye wingi wa fiber huongeza uzarishaji wa gesi, lakini fiber inafaa katika kuuweka mfuko wa umeng’enyaji katika utaratibu mzuri wa utendaji kazi na kurekebisha sukari kwenye damu pamoja na kiwango cha lehemu.

Je, Sababu Zingine Zinakuwaje?
Sababu zingine za lishe ambazo zinaweza kuchangia kuongezeka kwa gesi kwenye mfumo wa umeng’enyaji ni hizi zifuatazo;

• Vinywaji vyenye wingi wa Carbon, k**a vile soda na bia

• Tabia ya ulaji k**a vile, kula haraka haraka, kunywa harakaharaka, utafunaji, akuongea wakati unapotafuana ambako husababisha kuvuta hewa nyingi.

*Je, Nini Husababisha Tumbo Kujaa Gesi?* Gesi kujaa tumboni kwanza kabisa husababishwa na kumeza hewa wakati unapokula a...
29/10/2021

*Je, Nini Husababisha Tumbo Kujaa Gesi?*

Gesi kujaa tumboni kwanza kabisa husababishwa na kumeza hewa wakati unapokula au kunywa kinywaji. Gesi nyingi hupungua pale unapojamba. *NUKUU* : _Gesi hujengeka kwenye utumbo mkubwa wakati bakteria wanapotengeneza wanga, fiber, na baadhi ya sukari ambavyo havimeng’enywi kwenye utumbo wako mdogo. Bakteria pia huharibu baadhi ya gesi, lakini inayobaki hutolewa nje kwa kujamba_ .

**Je, Ni Kipindi Gani Unatakiwa Kufika Hospitali* ?* Fika hospitali ikiwa k**a tumbo lina gesi au maumivu ya gesi ni end...
29/10/2021

**Je, Ni Kipindi Gani Unatakiwa Kufika Hospitali* ?
*
Fika hospitali ikiwa k**a tumbo lina gesi au maumivu ya gesi ni endelevu au makali kiasi kwamba yanakufanya usijikie amani na furaha hata katika kufanya kazi zako za kila siku nyumbani au ofisini. Gesi au maumivu ya gesi yanayoambatana na dalili zingine yanaweza kuonyesha matatizo makubwa.
Fika hospitali haraka ikiwa k**a utaona dalili zozote kati ya hizi zifuatazo;

• Choo chenye damu
• Mabadiriko katika choo kinachotoka mara kwa mara
• Kupungua uzito
• Kukosa choo au kuharisha
• Kuhisi kichefuchefu au kutapika
Fanya juu chini uweze kupata matibabu haraka ikiwa k**a;
• Tumbo la chini litaendelea kuuma sana

• Kifua kuuma

*Je, Dalili Zake Zinakuwaje* ** ?Kwa kawaida huwa zipo aina mbalimbali za dalili za tumbo kujaa gesi au maumivu ya gesi ...
29/10/2021

*Je, Dalili Zake Zinakuwaje* ** ?

Kwa kawaida huwa zipo aina mbalimbali za dalili za tumbo kujaa gesi au maumivu ya gesi tumboni, nayo ni ni k**a ifuatavyo;

• Kujamba
• Kucheua
• Tumbo la chini kuunguruma, vichomi au kuuma
• Tumbo kujaa au kuunguruma
• Tumbo kuonekana kuwa kubwa

29/10/2021

*NUKUU* : _Kuongezeka kwa gesi au maumivu ya gesi yanaweza kutokana na ulaji wa vyakula ambavyo vinaweza kuzarisha gesi tumboni. Mara nyingi, mabadiriko katika tabia za ulaji yanaweza kupunguza masumbufu ya gesi._

_Matatizo mbalimbali katika mfumo wa umeng’enyaji, k**a vile kutoa choo hewa au chenye mak**asi k**asi, au tumbo kuvurugika, inaweza kusababisha dalili zingine kuongeza gesi na maumivu tumboni._

*ZIJUE SABABU ZA TUMBO KUJAA GESI NA KUUMA* Gesi katika mfumo wa umeng’enyaji ni sehemu kawaida ya njia ya umeng’enyaji....
29/10/2021

*ZIJUE SABABU ZA TUMBO KUJAA GESI NA KUUMA*

Gesi katika mfumo wa umeng’enyaji ni sehemu kawaida ya njia ya umeng’enyaji. Ili kuepukana na ongezeko la gesi, iwe ni kwa kujamba au kucheua, pia ni kawaida. Maumivu ya gesi yanaweza kutokea ikiwa k**a gesi haiendi vizuri kwenye mfumo wako wa umeng’enyaji.

*JE SABABU GANI HUPELEKEA TATIZO LA DAWASIL??.* 💫💫💫💫zipo sabau nyingi zinazopelekea tatizo hili.baadhi ya sababu hizo Ni...
06/08/2021

*JE SABABU GANI HUPELEKEA TATIZO LA DAWASIL??.* 💫💫💫💫

zipo sabau nyingi zinazopelekea tatizo hili.baadhi ya sababu hizo Ni

*Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu* 💫💫💫hii ndiyo sababu kubwa

Ujauzito; wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa.

Kushiriki mapenzi kinyume na maumbil

Sababu za kurithi; baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni kwa asilimia ndogo.
Kuharisha kwa muda mrefu.

Kutumia vyoo vya kukaa.

Kunyanyua vyuma vizito.

Ukihitaji maelezo ya kina juu ya sababu yoyote hapo niulize.

UFAHAMU UGONJWA WA PUMU/ASTHMA Leo Nina habari njema Kwa wale wote wanaosumbuliwa na pumu kwani suluhusho la matatizo ya...
06/08/2021

UFAHAMU UGONJWA WA PUMU/ASTHMA

Leo Nina habari njema Kwa wale wote wanaosumbuliwa na pumu kwani suluhusho la matatizo yao limepatikana, hata hivyo napenda tufahamu huu ugonjwa ili tuweze kujikinga na kuwashauri ndugu zetu wenye matatizo haya wapate dawa hiyo.
PUMU AU ASTHMA NI NINI???
-Pumu au asthma ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia ya hewa ambayo huingiza na kutoa hewa katika mapafu
-Ugonjwa huu wa pumu hufanya kuta za ndani ya njia ya hewa kuvimba na hivyo hupunguza kiasi cha hewa kinachoingia na kutoka katika mapafu
- Hali hii husababisha mgonjwa kutoa mlio k**a wa filimbi au mluzi wakati wa kupumua pia kubanwa na kifua, kushindwa kupumua vizuri na kukohoa sana
-Watu wenye pumu Mara nyingi hupata Dalili hizo wakati wa usiku na asubuhi sana
-Ugonjwa huu huwaathiri watu wa rika zote ingawaje Mara nyingi huanza utotoni hivyo huwaathiri zaidi watoto
-Ugonjwa huu wa pumu ni mpana sana kwasababu Kuna aina nyingi za pumu kutokana na visababishi vyake

AINA ZA PUMU
1.PUMU YA UTOTONI (CHILD-ONSET ASTHMA)
-Hii ni aina ya pumu inayotokea baada ya mtoto kuwa Kwenye Vizio k**a vile VUMBI LA WADUDU K**A MENDE, MANYOYA YA WANYAMA K**A PAKA, MBWA PIA KUTUMIA BABY WIPES ZENYE HARUFU (PERFUME)
Pumu hii hutokea kwa kuwa mwili wa mtoto hutengeneza Kinga ya mwili (ANTIBODIES) za IgE zinazosababisha pumu.
Ugonjwa wa pumu ni sugu sana kwa watoto wanaozaliwa na uzito mdogo wenye asili ya kiafrika pia pumu ya utotoni huwaathiri zaidi watoto wa kiume
2.PUMU YA UKUBWANI (ADULT-ONSET ASTHMA)
-Pumu hii huanza baada ya kufika miaka 20, pumu hii huwaathiri sana wanawake kuliko wanaume na pia haitokei sana k**a pumu ya utotoni, Vizio k**a vile perfume /cream zenye harufu kali /sabuni nk ndio husababisha pumu hii kwa asilmia kubwa
3.PUMU ITOKANAYO NA MAZOEZI (EXERCISE INDUCED ASTHMA)
-Pumu hii huwatokea Zaidi wanaofanya mazoezi, ikiwa utakohoa na kukosa pumzi wakati wa mazoezi au baada ya mazoezi kuna uwezekano wa wewe kuwa na pumu ambayo inasababishwa na mazoezi pia hata k**a sio mwana mazoezi kukimbia kwa kasi angalau dk 10 Kunaweza kusababisha kukosa pumzi kwa muda mrefu na kuonyesha kwamba una pumu
4.PUMU ITOKANAYO NA KUKOHOA SANA (COUGH INDUCED ASTHMA)
-Hii ni aina ya pumu ambayo ni ngumu sana na kuumiza vichwa vya madaktari kuigundua kwasababu katika pumu hii inawezekana isitokee hata Dalili zingine zaidi ya kukohoa kitu ambacho madaktari tunalazimika kuchunguza sababu nyingine za kukohoa sana na kuhakiksha sio zinasababishwa na kukohoa huko
6.PUMU YA USIKU (NOCTURNAL ASTHMA)
-Pumu hii hutokea Kati ya saa Sita usiku na saa mbili asubuhi, pumu hii huamshwa na vumbi la wadudu, rangi ya nyumba, na harufu ya gesi pia Mara nyingi wagonjwa wa pumu hii hushtuka usingizini wakati wa usiku wa manane baada ya kukosa pumzi
7.PUMU KALI ISIYOKUBALI DAWA (SEVERE ASTHMA)
-Wakati wagonjwa wengi wanapata unafuu baada ya kupata steroid wachache hawapati unafuu na hivyo kuhitaji matibabu makubwa Zaidi
8.PUMU YA NGOZI (ECZEMA /ATOPIC DERMATITIS)
-Huenda utashangaa kwamba kuna pumu ya ngozi na ipoje sasa maswali yako yote yamepata majibu, naomba ufahamu kwamba neno ECZEMA ambalo ni neno la kigiriki na linamaanisha KUTUTUMUKA SEHEMU YA NJE YA NGOZI hali ambayo huonekana pale mtu anapopata maradhi haya
-Ugonjwa huu huchangia asilimia 40 ya maradhi yote ya ngozi kwa ufupi huu ugonjwa huwapata Zaidi watoto na tatizo hili limekua likiumiza vichwa vya madaktari na wanasayansi wengi kutokana na kwamba haijajulikana sababu maalum. Ugonjwa huu ni wa muda mrefu nikimaanisha kwamba mtu huweza kukaa na ugonjwa huu kwa muda mrefu ingawa si muda wote mwili huonyesha dalil za ugonjwa huu

CHANZO CHA UGONJWA WA PUMU
-Visababishi vya pumu havijulikani wazwazi ila vitu vinavyochangia pumu ni VIZIO mfano MOSHI WA SIGARA, BANGI, GESI, PERFUME, KUWA NA MSONGO WA MAWAZO, KUOGEA MAJI YA MOTO KILA WAKATI, KUTOKUPAKA MAFUTA, KUKAA KWENYE VUMBI, KUVAA MAVAZI YASIYO YA PAMBA NA KURITHI
DALILI ZA PUMU
-NOTED :Sio watu wote wenye Dalili hizi wana pumu na sio wote wenye pumu Wana Dalili HIZI
��KUKOHOA Kikohozi huwa kikali wakati wa usiku na asubuhi
��KUTOA SAUTI K**A MLUZI WAKATI WA KUPUMUA
��KUBANWA NA KIFUA HASA NYAKATI ZA JIONI NA ASUBUHI SANA
��KUPUNGUKIWA PUMZI
��SEHEMU YA NGOZI ILIYOATHIRIWA HUWA INATUTUMKA
��MAENEO YENYE ATHARI KUBWA YANAVIMBA NA KUWA NA JOTO
��MUWASHO WA NGOZI HUWA MKALI WAKATI WA JIONI NA USKU

MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU
Matibabu ya ugonjwa kwa hospitali yapo ya aina mbili moja ni Ile ya dharura ili kutoa tu msaada, dawa hii ni zile zinazosaidia kutanua njia ya hewa ambazo zimesinyaa (Bronchopdilators) pia husaidia kulainisha misuli ya njia za hewa iliyosinyaa, aina ya pili ya matibabu ni kutumia dawa za steroid za kuvuta (inhaled corticosteroids) ila kwa kawaida matibabu haya poa huwa chanzo cha matatizo mengine kutokana na kwamba dawa hizo ni za kemikali hivyo huwa si nzuri kwani hazimalizi tatizo Zinampa mtu unafuu tu, pamoja na hayo ugonjwa huu unaweza kuuepuka kwa kuepuka kutumia vitu vyenye mzio ambavyo ni PERFUME, SABUNI ZENYE HARUFU KALI, RANGI ZA NYUMBA, KUACHA KUVUTA SIGARA NA BANGI, ACHA KUNYWA POMBE, EPUKA KUVUTA VUMBI LA WANYAMA, NA EPUKA KUKAA MAZINGIRA YENYE UNYEVU

JIFUNZE KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO NA SULUHISHO LAKE KUTOKA U.S.A..💧CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBOVidonda vya tumbo vina vya...
01/08/2021

JIFUNZE KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO NA SULUHISHO LAKE KUTOKA U.S.A..

💧CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO

Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;
▪️Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)
▪️Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu k**a asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)
▪️Kuwa na mawazo mengi
▪️Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
▪️Kunywa pombe na vinywaji vikali
▪️Uvutaji wa sigara
▪️Kuto kula mlo kwa mpangilio

💧DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na endelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vinadalili k**a;

▪️Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa k**a ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula
▪️Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo
▪️Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa
▪️Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu
▪️Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu
▪️Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
▪️Kushindwa kupumua vizuri

💧JINSI YA KUEPUKANA NA VIDONDA VYA TUMBO
▪️Kunywa maji mengi
▪️Punguza mawazo, fanya mazoezi yatakupunguza na mawazo
▪️Punguza (balansi) kiwango cha halemu (choresterol)
▪️Usivute sigara
▪️Punguza au acha kunywa pombe
▪️Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
▪️Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9

💧TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO.
Tatizo la Vidonda vya tumbo linatibika kufuatana na mda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakizalau dalili za vidonda vya tumbo na kudhani kuwa hakuna madhara makubwa.

💧DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO
Tuna dawa ya kutibu Vidonda vya tumbo ambayo ni ya asili isiyo na kemikali ambayo hufanya mtu kupona na kuimarika kabisa. Dawa hiyo hutibu kwa mda kulingana na mda wa tatizo, tatizo halirudi tena maana huondoa chanzo pamoja na ugonjwa sio kituliza maumivu, ukianza kutumia baada ya wiki moja mgonjwa huanza kupona na huonesha mabadiliko, pia mgonjwa anapewa mfumo wa maisha ambao inatakiwa autumie kwasababu kuna mtindo wa maisha unaendelea kuongeza tatizo pia kuna mtindo unapunguza hatari ya ugonjwa.

*JE UNATAKA KUPONA U.T.I SUGU KWA MDA WA SIKU SABA NA USIJIRUDIE TENA?*  *LIFAHAMU  TATIZO LA U.T.I DALILI ZAKE NA JINSI...
01/08/2021

*JE UNATAKA KUPONA U.T.I SUGU KWA MDA WA SIKU SABA NA USIJIRUDIE TENA?*

*LIFAHAMU TATIZO LA U.T.I DALILI ZAKE NA JINSI YA U.T.I SUGU*

U.T.I. (yaani Urinary Tract Infection kwa kirefu) ni ugonjwa unaotokana na
wa maambukizi (infection) katika mfumo wa mkojo (urinary tract). Maambukizi haya yanasababishwa na
viumbe k**a bakteria, fangasi na virus. bacteria.

Mara nyingi bakteria wanaoingia kwenye mfumo wa mkojo hutolewa na
mwili wenyewe. Lakini wakati mwingine bakteria wanaweza kuzidi kinga ya mwili na kusababisha maambukizi hayo.

U.T.I. inaweza kuathiri vitu vifuatavyo: ureta, urethra, kibofu cha
mkojo na hata figo.

TUANGALIE KIDOGO MFUMO WA MKOJO:

Mfumo wa mkojo ni mfumo wa mwili
unaotumika kuondoa uchafu na maJi ya ziada kupitia njia ya mkojo. Mfumo huu unaundwa na vitu vifuatavyo: figo, ureta, kibofu na urethra.
(Kwa sasa sitachambaua kwa undani hizi sehemu ili kutorefusha sana mada. Ila ukitazama picha hapo chini utaona jinsi hivi vitu vilivyo na namna vilivyo connected.)

KISABABISHI CHA U.T.I.

Mara U.T.I. inasababishwa na
bakteria aitwaye Escherichia coli (E. coli). Yaani 65% ya maambukizi yote ya U.T.I. hutokana na huyu bakteria. U.T.I. nyingine zinaweza kusababishwa na Chlamydia na Mycoplasma na U.T.I. hizi zinaathiri hadi mfumo wa uzazi na hapo wanandoa hupaswa kupata tiba kwa pamoja.

KWANINI WANAWAKE NDO WAHANGA
WAKUBWA?

Wanawake ni wahanga wakubwa sana wa ugonjwa huu kulingana na maumbile yao ya nje.

1.Urethra (mrija wa mkojo kutoka kwenye kibofu) kwa wanawake ni mfupi sana ukilinganisha na kwa wanaume. Hivyo ni rahisi kwa urethra ya mwanamke kuruhusu bakteria kufika kwa haraka hata kwenye kibofu.

2. Pia mrija huo unafungukia sehemu
ambazo zinaweza kuwa ni vyanzo bakteria ambayo ni sehemu ya uke na pili ni re**um.
Kwa wanaume ni vigumu sana kupata U.T.I. ila wakipata tatizo linaweza kuwa zito kutibu tofauti na kwa wanawake.

WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA U.T.I.

# Watu wasiojua au wasiozingatia namna sahihi na bora ya kujisafisha mfano kwa kutumia toilet paper. Unapaswa kujisafisha kutoka mbele kurudi nyuma na siyo kutoka nyuma kwenda mbele. Hasa wanawake.
# Mtu yeyote mwenye tatizo katika
mfumo wa mkojo
# Tendo la ndoa linaweza likahamisha
bakteria kutoka kwenye uke kwenda
kwenye urethra. Lakini pia tendo la ndoa kinyume na maumbile linaweza kuhamisha bakteria kirahisi zaidi na kuwafikisha kwenye urethra.
# Baadhi ya njia za uzazi wa mpango k**a kutumia diaphragm, spermicides, kondomu za k**e, nk.

KURUDIARUDIA KWA U.T.I. (yaani U.T.I. SUGU)

Mara nyingi wanawake wakipata U.T.I.
inaweza ikawa inajirudia mara kwa mara kulingana na sababu zifuatazo:

1. Uwezo wa bakteria kujishika kwenye
njia ya mkojo hivyo kutotibika na kurudia tena. Ni muhimu ukajifunza kwa nini hili linaweza kuwa ndo sababu kwako

2. Sababu nyingine ni wanawake kuwa non sector yani kuwa na damu grupu A, B na AB ambao hawawezi kuzalisha kinga nzuri dhidi ya hao bakteria. Au mfumo mzima wa kinga ya mhusika kuwa uko chini mno. Hili ni somo pana ila ukilielewa itakusaidia sana.

3. Lakini pia kushindwa kuzingatia usafi kamili na hivyo kujiambukiza U.T.I. wenyewe kila wakati. Wengi wanadhani wanajua kuzingatia usafi kumbe hawajajua vizuri na hawataki kujifunza. Matokeo yake U.T.I. inazidi kuwatesa kila wakati. U.T.I inaua usiifanyie mchezo U.T.I. siyo kitu cha kuchezea.

DALILI ZA U.T.I.

1. Kukojoa mara kwa mara na maumivu
wakati wa kukojoa. Wengi wanajisikia hivyo lakini wanapotezea tu.

2. Kuhisi kuunguzwa na mkojo kwenye
kibofu au mrija wa mkojo. Wengi Hapa ndo wanaanza kujiuliza kuna nini.

3. Maumivu ya misuli na tumbo. Wengi hapa ndo wanakodi bajaji kwenda hospitali.

4. Mkojo kuwa na harufu mbaya na pia
kubadilika kuwa au rangi ya nk. Wengi hii hawajali. Ndo maana vyoo vya umma vina harufu mbaya mbaya.

5. Kwa mtu aliyeathiriwa figo anaweza
kuwa na maumivu mgongoni au kwenye mbavu (hasa upande mmoja) pia kichefuchefu na kutapika. Wengi hapa wanajua malaria, au typhoid, nk.

6. Kushikwa na hamu ya kukojoa ila mkojo unatoka kidogo. Wengi hii pia huwapa hofu kidogo.

(Ukiona dalili hizo wahi hospitali kwanza au kituo cha afya ukapime. Ukichelewa inaweza kuwa too late)

JINSI YA KUZUIA U.T.I. SUGU

1.Kunywa maji mengi kunasaidia kusafisha bakteria kwenye mfumo

2. Mtu anatakiwa akojoe mara kwa mara kila anapojiskia kukojoa. Kubana mkojo ni chanzo kimojawapo cha kujiambukiza U.T.I. Mkojo ukikaa sana kwenye kibofu unaweza kuzalisha bakteria.

3. Na baada ya kukojoa wanawake
wanatakiwa kujisafisha kuanzia mbele
kurudi nyuma ili kulinda urethra

4. Vaa nguo za ndani za na ambazo hazibani sana kuruhusu hewa kupita vizuri. Epuka jinsi (jeans) zinazobana sana ambazo zinaweza kukusanya na kuleta tatizo.

5. Kwa wanawake tumia pedi zilizotengenezwa kwa pamba
na pedi zenye uwezo wa kuzuia kupata U.T.I. na pia zinaruhusu hewa kupita
vizuri.

Kwa msaada zaidi kuhusu tatizo hili la U.T.I. na matatizo mengineyo au k**a umetumia dawa nyingi lakini hazikusaidii wasiliana nasi kwa:
kupata suluhisho la kudumu

28/07/2021

*Je Umekuwa UKifanya kosa moja kati ya Makosa haya 5❓

1. *Unahisi miwasho ukeni lakini unapuuzia.*
2. *Ukivua chupi jioni unakuta imechafuka lakini unaona kawaida.*
3. *Uchafu unatoka k**a maziwa, na mda mwingine unarangi zingine lakini unaombatana na harufu mbaya lakini bado unachukulia poa.*
4. *U.T.I inakurudia mara kwa mara kwa mara ila unaona sawa tu.*
5. *Ukijaamiana unapata maumivu unatoka mpaka damu, hauna hisia na wala huchukui hatua yeyote.*

⚠️ *Inatosha Usiendelee kufanya makosa hayo*

Tafiti zinaonyesha kati ya wanawake 10 waliofanya kosa moja wapo kati ya hayo, 8 wamekumbwa na madhara yafuatayo ...
i) *kupata kansa ya kizazi hapo baadae*
ii) *kushindwa kushika ujauzito na kupata ugumba au kutoka kwa mimba mara kwa mara*
iii) *kushindwa kufurahia tendo la ndo na kuvuruga mahusiano*
iv) *Msongo wa mawazo ambao hupelekea kuvuruga homon na kusababisha kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi kunakoambatana na maumivu.*
v) *Tatizo la harufu mbaya na ukavu uliopitiliza ukeni*

Usiendelee Kupuuzia, karibu tuzungumze🏃🏻‍♀️🏃🏻‍♂️

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AFYA BORA KWA LISHE posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to AFYA BORA KWA LISHE:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram

Category