Eimmer_medics

Eimmer_medics Ukurasa huu unahusika na kutoa elimu juu ya visababishi, vihatarishi dalili, madhara, njia za kujikinga pamoja na matibabu juu ya magonjwa mbalimbali.

Pia inahusika na utoaji ushauri juu ya masuala mbalimbali yahusuyo afya.

Siku kadhaa zilizopita watafiti katika mji wa Pittsburgh nchini marekani walilipoti mgonjwa wa kwanza kutengeneza pombe ...
12/05/2020

Siku kadhaa zilizopita watafiti katika mji wa Pittsburgh nchini marekani walilipoti mgonjwa wa kwanza kutengeneza pombe katika kibofu chake.

Mwanamke huyu ambae ana umri wa miaka 61 ambae alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ini na kisukari alienda katika hospitali iliopo katika mji huo kwa ajili ya kupata utaratibu wa kupandikizwa ini baada ya ini lake kuharibika sana kwa kile ambacho awali waliamini ni kutokana na matumizi ya pombe kwa muda mrefu.

Japo kuwa mwana mama huyo alikataa mara kadhaa kuwa hakuwa hakitumia pombe na hata hivyo hakuwa akionesha kabisa kuwa na dalili za ulevi.

Walipofanya vipimo vya mkojo na damu waligundua kuwa katika mkojo kuna kiwango kikubwa sana cha pombe na kiwango kikubwa cha sukari. Utafiti zaidi ulionesha kuwa fangasi "candida glabrata" ambae hupatikana katika sehemu mbalimbali mwilini ndie aliekuwa akibadilisha ile sukari katika mkojo na kuichachusha na kuwa pombe.

Jitihada zilifanyika na mwanamme huyo alipewa dawa za kutibu fangasi lakin haikuwa rahisi inawezekana ni kutokana na tatizo lake la kisukari.

Watafiti waliuita huu ugonjwa "bladder fermentation syndrome" walinukuliwa wakisema inawezekana wako wagonjwa wengi wenye tatizo hili ambao hawakugundulika.

Happy birthday daktari .czyaadfun
12/05/2020

Happy birthday daktari .czyaadfun

Heri ya siku ya kuzaliwa daktari
12/05/2020

Heri ya siku ya kuzaliwa daktari

Mama ni nguzo na mhimili imara, mama ni chachu ya tabia, mienendo, matendo na maisha katika kila mmoja wetu. Mama ni fum...
10/05/2020

Mama ni nguzo na mhimili imara, mama ni chachu ya tabia, mienendo, matendo na maisha katika kila mmoja wetu. Mama ni fumbo la upendo, mama ni maisha. Tunatambua mchango wenu katika kujenga jamii bora. Mungu awabariki sana. Heri ya sikukuu kina mama wote duniani.

Heroes are those who risk the lives every day to protect our world and make it a better place.
07/05/2020

Heroes are those who risk the lives every day to protect our world and make it a better place.

FAHAMU KUHUSIANA NA FISTULAFISTULA ni shimo/kitundu au uwazi usiosahihi unaounganisha sehemu mbili katika mwili. Zipo ai...
06/05/2020

FAHAMU KUHUSIANA NA FISTULA

FISTULA ni shimo/kitundu au uwazi usiosahihi unaounganisha sehemu mbili katika mwili. Zipo aina nyingi za fistula ila kwa leo nitazungumzia fistula inayotokea kati ya kibofu cha mkojo na sehemu ya siri ya mwanamke(uke) kitaalamu inaitwa (vesicovaginal fistula). Fistula imekuwa ni moja ya matatizo yanayowakumba kina mama na kumekuwa na ongezeko hivi karibuni hii ni kutokana na kuongezeka kwa mimba za utotoni, kuongezeka kwa upasuaji na sababu nyingine nyingi. Fistula husababisha athari nyingi katika jamii ikiwemo za kiuchumi, kijamii na hata kisaikolojia.

NINI HUSABABISHA FISTULA?
1. Uzazi pingamizi
Katika nchi zinazoendelea k**a Tanzania, fistula imekuwa ikisababishwa na uZazi pingamizi. Katika uzazi pingamizi mtoto hushindwa kushuka katika nyonga hali hii hupelekea kichwa cha mtoto kukandamiza viungo vilivyo kwenye nyonga ikiwemo kibofu cha mkojo. Mkandamizo huu huzuia damu kufika eneo hili na kupelekea seli kufa. Vijidudu huota pale na hivyo kusababisha kumeguka au kumomonyoka kwa vinyama sehemu ile na hivyo kutengeneza kitundu kinachounganisha sehemu hizo mbili yaani kibofu cha mkojo na uke. Mara nyingi fistula hutokea kati ya siku ya 3-5 baada ya kujifungua.

Sababu nyingine ni
2. Upasuaji wa uzazi au kuzalishwa kwa vifaa
3. Kutibiwa kwa kutumia dozi kubwa ya mionzi
4. Ajari- kuangukia kitu chenye ncha kali ambacho kinaweza toboa kibofu cha mkojo na sehemu mbalimbali za mfumo wa uzazi wa mwanamke
5. Saratani ambayo huweza shambulia sehemu mbalimbali za nyonga na hivyo kupelekea fistula
6. Maambukizi k**a TB katika uke, na kichocho.

Mara nyingi fistula huwapata wanawake wanaobeba mimba katika umri mdogo ambao pia wapo kwenye hatari ya kupata uzazi pingamizi.

DALILI ZA FISTULA,
1. Kutokwa na mkojo ukeni pasipo hiari/pasipo kujua
2. Kubabuka/kuungua kwa ngozi inayozunguka sehemu za siri.
3. Kutokuona siku zako za hedhi au hedhi kuvurugika mpangilio.
4. Kuchechemea kutokana na kuharibiwa kwa mishipa ya fahamu(nerves) wakati wa uzazi pingamizi.

MATIBABU YA FISTULA,
-upasuaji

KUJIKINGA,
1. Zuia mimba za utotoni
2. Maudhurio mazuri ya kliniki wakati wa ujauzito
3. Kuwekwa mpira wa mkojo kabla/baada ya kujifungua

By lwamayanga

FAHAMU KUHUSIANA NA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI (DYSMENORRHEA) haya ni maumivu ambayo huambatana na hedhi ambayo humfanya mw...
05/05/2020

FAHAMU KUHUSIANA NA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI (DYSMENORRHEA)

haya ni maumivu ambayo huambatana na hedhi ambayo humfanya mwanamke ashindwe kufanya kazi zake za kila siku.

Maumivu haya yamegawanywa katika makundi makuu mawili
A. Maumivu ambayo hutokea pasipokuwa na tatizo kwenye nyonga (via vya uzazi)

Maelezo,
Inakadiliwa maumivu makali sana huwapata asilimia 15-20. Matumizi ya vidonge vya majira na dawa za kutuliza maumivu zimepelekea kupungua kwa tatizo hili.

Sababu za maumivu
Namna ambayo maumivu hutokea haielezeki kwa urahisi lakin huonekana,
a) huonekana zaidi kwa vijana/mabinti
b) uhusiana na mzunguko wa hedhi
c) maumivu haya upona wakati wa mimba na kuzaa kwa njia ya kawaida
d) inasadikika maumivu haya yanatokana na kujikaza kwa mji wa mimba kusiko na mpangilio.

1. Uoga na wasiwasi kwa vijana huwafanya waweze kusikia hata maumivu hata k**a ni kidogo.
2. Kufanya kazi kulikopitiliza kwa kuta za mji wa mimba
3. Kuwiana kwa mifumo ya fahamu
4. Prostaglandin
Kuwako kwa kiwango kikubwa cho homoni ya Progesterone ktk sehemu ya pili ya mzunguko wa hedhi hupelekea kutengenezwa kwa wingi kwa prostaglandin ambazo hupelekea kukaza kwa misuli na hivyo maumivu.
5. Kuongezeka kwa vasopressin
6. Endothelins husababisha kujikaza kwa misuli hali inayopelekea kutokufika kwa oksijen na hivyo maumivu

Ni watu gan huwapata?
Huwapata zaidi mabinti hutokea miaka 2 baada ya kuvunja ungo. Mama na dada wa binti huyu huweza kuwa tatixo hili.

DALILI
maumivu huanza masaa machache kabla au huanza wakati hedhi inaanza. Maumivu haya hudumu kwa masaa kadhaa, kwa baadhi hufika masaa 24 na nadra hufika masaa 48. Maumivu haya huja ghafla hupatikana chini ya kitovu huweza kusambaa kuelekea mgongon na kwenye mapaja, huambatana na kichefuchefu, kutapika uchovu, kuharisha, maumivu ya kichwa na mapigo ya moyo kwenda kasi. Mara chache husababisha mtu kupoteza fahamu.

MATIBABU
Iwapo maumivu si makali mtu anahitaji ushauri tu lakin iwapo maumivu ni makali matibabu uhusisha
1. Dawa
2. Upasuaji

B. Maumivu ambayo hutokea ikiwa kuta tatizo kwenye nyonga.
Itaendelea.....

Kwa maswali tuwasiliane kupitia namba 0764723526 asanteni
By Emmanuel Lwamayanga

FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU, DALILI, NA MATIBABU YA MANJANO KWA WATOTO WACHANGA (NEONATAL JAUNDICE) Umanjano ni hali ya n...
04/05/2020

FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU, DALILI, NA MATIBABU YA MANJANO KWA WATOTO WACHANGA (NEONATAL JAUNDICE)

Umanjano ni hali ya ngozi, macho, mikono na unyayo wa miguu kuwa na rangi ya njano. Hali hii ni tofauti na homa ya manjano naomba tusichanganye.

65% ya watoto wanaozaliwa hupata tatizo hili ikiwa kiwango cha bilirubin kwenye damu ni zaid ya 6mg/dl ndan ya sku 7 za kwanza za maisha yao. 8-10% ya watoto wanaozaliwa wanapata kiwango kikubwa cha bilirubin kwenye damu, na asilimia chache hupata kiwango kikubwa sana ambacho huathiri ubongo. Bilirubin hutokana na heme.

AINA ZA MANJANO
A. Manjano ya kifisiolojia
Sifa
1. Hutokea masaa 24 baada ya mtoto kuzaliwa
2. Kiwango cha kuongezeka kwa bilirubin kwenye damu ni

FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU ZA KUSHINDWA KUSIMAMISHA AU KUDUMISHA USIMAMAJI WA UUME ( ERECTILE DYSFUNCTION) Ili mwanaume ...
02/05/2020

FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU ZA KUSHINDWA KUSIMAMISHA AU KUDUMISHA USIMAMAJI WA UUME ( ERECTILE DYSFUNCTION)

Ili mwanaume aweze kushiriki tendo la ndoa anahitaji hamu ya tendo, uwezo wa kusimamisha uume, na uwezo wa kutengeneza na kutoa mbegu. Hamu ya tendo kwa mwanaume hutokana na kuona, kusikia, kunusa, kugusa, kufikiri na michocheo ya homoni. Homoni ya testosterone uongeza hamu.

Kusimama kwa uume hutegemea ongezeko la damu ktk mtandao wa mishipa na uwazi ktk uume ikiambatana na kulegea kwa kuta za mishipa ya ateri na misuli. Mfumo wa fahamu pia unamchango mkubwa juu ya hili. Nitric oxide ambayo huzalishwa mwilini inachochea usimamaji wa uume.

TATIZO la kushindwa kusimamisha uume linapatikana zaidi kwa wanaume wenye matatizo k**a kisukari, uzito uliopitiliza, matibabu ya saratani ya tezi dume kwa mionzi na upasuaji, magonjwa ya moyo, kupungua kwa cholesterol nzur mwilini, uvutaji wa sigara na matatizo ya ugwe mgongo.
Kisukari, matatizo ya mishipa ya damu na madhara ya dawa kwa pamoja ufanya 80% ya tatizo hili.

NAMNA INAVYOTOKEA
tatizo hili huweza kutokana na
1. Kushindwa kuanzisha usimamaji (mfumo wa fahamu (kisaikolojia) na Homoni)
2. Kushindwa kujaza mishipa ya damu
3. Kushindwa kuhifadhi damu kwenye uume
Makundi haya matatu hutegemeana

1. Mishipa ya damu
Miongoni mwa sababu kubwa ni tatizo la damu kufika au kutoka kwenye uume. Matatizo ya mishipa k**a kutuama kwa mafuta kwenye kuta zake hupelekea kupunguza kiwango cha damu kinachofikia uume na hivyo kushusha uimara lakin pia kutoka kwa damu ktk uume kurudi ktk mfumo wa mzunguko wa damu husababisha tatizo hili. Mabadiliko ya kimaumbile ndan ya uume ni sababu pia

2. Mfumo wa fahamu
Ajari ktk ungwe mgongo na matatizo ktk mfumo wa fahamu

3. Homoni
Kuongezeka kwa homoni ya prolactin na kupungua kwa homoni ya testosterone husababisha tatizo hili

4. Kisukari
Madhara ya kisukari ktk mishipa ya damu na mishipa ya fahamu lakini pia kiwango kidogo cha nitric oxide kwa wagonjwa hawa husababisha tatizo hili

5. Matatizo ya kisaikolojia
Uoga wa kushindwa kumlizisha mwenza, sonono, ugomvi/kutokuelewana, uoga aa mimba na magonjwa ya zinaa nk.

6. Dawa
Baadhi ya dawa za presha
Na dawa za kulevya

By Emmanuel Lwamayanga

Heri ya sikukuu ya wafanya kazi
01/05/2020

Heri ya sikukuu ya wafanya kazi

Hongera sana daktari   kwa kufunga pingu za maisha.  Mwenyezi Mungu akawe kiongozi katika ndoa yenu na muishi katika mis...
30/04/2020

Hongera sana daktari kwa kufunga pingu za maisha. Mwenyezi Mungu akawe kiongozi katika ndoa yenu na muishi katika misingi impendezayo yeye.

Ningetoa ushauri wa ndoa 😊😊😁😁😁 ila doctor .255 aliniambia sina ndoa hivyo sijui maisha ya ndoa. Ila Mwenyezi Mungu awe na nyie sasa na hata siku zote

FAHAMU KUHUSIANA NA ATHARI ZA POMBE NA ULEVI ULIOPINDUKIA. pombe iingiapo mwilini husambaa ktk mwili mzima na huathiri k...
29/04/2020

FAHAMU KUHUSIANA NA ATHARI ZA POMBE NA ULEVI ULIOPINDUKIA.

pombe iingiapo mwilini husambaa ktk mwili mzima na huathiri kila mfumo mwilini, huzidisha makali ya magonjwa na huathiri utendaji kazi wa dawa mbalimbali.

Uwezekano wa kupata madhara yatokanayo na pombe ni 20% kwa mwanaume na 10% kwa mwanamke ktk maisha yake yote. Madhara haya upunguza mpaka miaka 10 ya kuishi kwake duniani.

Pombe hufyonzwa/hunyonywa ktk kiwango kidogo mdomoni na koo la chakula, kiwango cha kati katika tumbo na utumbo mpana na kwa kiwango kikubwa katika sehemu ya juu ya utumbo mwembamba. Asilimia kadhaa hutolewa kwa njia ya mapafu, mkojo na jasho na inayobaki hubadilishwa kuwa acetyladehyde ambayo huaribiwa haraka na kemikali za mwili.

Pombe huathiri visafirishi (neurotransmitters) k**a GABA, NMDA, dopamine na serotonin na hivyo kupelekea athari kisaikolojia, kifisiolojia na kitabia.

Mabadiliko ktk utambuzi na tabia hutokea ikiwa kiwango cha pombe ktk damu ni kati ya 0.02-0.04g/dl na kifo hutokea iwapo imefikia 0.30-0.40g/dl

FAIDA ZA POMBE
Pombe ktk kiwango kidogo,
1. kinaongeza kiwango cha cholesterol nzuri mwilini
2. Kupunguza mkusanyiko wa visahani vya damu na hivyo kupunguza uwezekano wa matatizo ya moyo

ATHARI ZA POMBE
a) mfumo wa fahamu
1. Kupoteza kumbukumbu za kile kilichotokea baada ya kunywa
2. Kukosa usingizi
3. Kukoroma
4. Ndoto mbaya usingizini
5. Kutokuwa na maamuzi sahihi na kukosa ushirikiano ktk sehemu za mwili
6. Miguu kufa ganzi
7. Matatizo ktk mfumo tambuzi
8. Maumivu ya kichwa, kiu, kichefuchefu, na kuchoka siku inayofuata baada ya kunywa (hangover)

B) matatizo ya akili
Pombe huweza kuchochea au kuhamsha magonjwa ya akili

C) mfumo wa mmeng'enyo wa chakula
1. Kutokwa na damu
2. Kushuka kwa kiwango cha sukari mwilini
3. Matatizo ktk ini

D) saratani

E) mfumo wa mzunguko wa damu
1. Matatizo ya moyo
2. Shinikizo la damu
3. Kupungua kwa utengenezwaji wa sele nyeupe za damu, inapunguza uwezo wa udundaji wa moyo

F) mfumo wa uzazi

a) mwanaume
1. Kupungua kwa uwezo wa kusimamisha uume
2. Kusinya/kukonda kwa korodani
3. Kupungua kwa mbegu za kiume
b) mwanamke
1. kutokuingia hedhi
2. Kuharibika mimba
3. Ugumba

By Emmanuel Lwamayanga.

Karibu nikuhudumie..
28/04/2020

Karibu nikuhudumie..

FAHAMU KUHUSIANA NA TETENASI/PEPOPUNDA. TETENASI ni maambukizi ya papo hapo/ghafla yenye sifa bainifu ya mvutano/kukak**...
28/04/2020

FAHAMU KUHUSIANA NA TETENASI/PEPOPUNDA.

TETENASI ni maambukizi ya papo hapo/ghafla yenye sifa bainifu ya mvutano/kukak**aa kwa misuli pamoja na shida ktk mfumo wa fahamu.

SABABU
tatizo hili husababishwa na sumu kali itengenezwayo na bakteria wafahamikao k**a clostridium tetani. Bakteria hawa wanapatikana pahali kote duniani na hupatikana kwenye vumbi udongo nk. Bakteria hawa hutengeneza mbelewele/mbegu (spores) ambazo zinauwezo wa kudumu kwa muda mrefu ktk mazingira na pia haziharibiwi kwa kemikali nyingi au kuchemshwa. Pia mbegu hizi hupatikana kwenye utumbo wa wanyama wengi na hivyo kufanya kinyesi kuwa moja ya njia ya kusambaa kwake. Mbelewele/mbegu hizi huingia mwilini kupitia jeraha litokanalo na mkwaruzo, mchubuko au donda. Kwa watoto wachanga huweza pitia kwenye kitovu hasa kwa zile jamii zenye desturi za kuweka kinyesi cha wanyama kwenye vitovu vya watoto wachanga.
Iwapo matibabu hayatopatikana mapema matokeo ya ugonjwa huu ni makubwa na hata kifo.

DALILI
1. maumivu makali ya misuli na kukak**aa
2. Maumivu ya mgongo
3. Shida katika kumeza
4. Kushindwa kunyonywa(mtoto mchanga)
5. Joto kali
6. Mvutano wa misuli
7. Shinikizo la damu
8. Mapigo ya moyo kwenda mbio
9. Kukosa choo
10. Kuongezeka makohozi
11. Figo kushindwa kufanya kazi ghafla.
12. Kushindwa kupumua na kupaliwa.

MATIBABU

TAFADHARI UONAPO DALILI AMA UPATAPO KIDONDA AU JERAHA KATIKA MAZINGIRA HATARISHI FIKA HOSPITALI MAPEMA, KUCHELEWA KUPATA HUDUMA HUPELEKEA KIFO.

NJIA ZA KUJIKINGA
1. Usafi na utunzaji bora wa majeraha/vidonda
2. Kupata chanjo sahihi na kumaliza dozi ya chanjo sitahiki. Mama mjamzito hakikisha unapata chanjo, hakikisha mwanao anapata chanjo nawe mtu mzima iwapo umepata tatizo/ajari/jeraha fika kituo kitoacho huduma mapema na k**a utastahiri chanjo hakikisha unamaliza dozi.

DALILI ZINAZOONESHA UWENDA MATOKEO YAKAWA MABAYA

1. Umri zaidi ya miaka 70
2. Shinikizo la juu la damu
3. Joto zaidi ya 38.5
4. Dalili kuonekana chini ya siku 7 toka kupatikana kwa jeraha.
5. Dalili kuongezeka kwa kasi kubwa
6. Mapigo ya moyo zaid ya 140/m

Kwa maswali tuwasiliane DM au kupitia namba 0764723526

Afya ni kitu bora zaidi
By Emmanuel Lwamayanga.

FAHAMU KUHUSIANA NA UZAZI PINGAMIZIUZAZI PINGAMIZI NI NINI?Huu  ni uzazi ambao licha ya kuwepo kwa uchungu wa kutosha mt...
28/04/2020

FAHAMU KUHUSIANA NA UZAZI PINGAMIZI

UZAZI PINGAMIZI NI NINI?
Huu ni uzazi ambao licha ya kuwepo kwa uchungu wa kutosha mtoto anashindwa kushuka/kupita kwenye njia ya uzazi. Yaani inakuwa ni ngumu kuzaa kupitia njia ya kawaida.
Hali hii inawezasababishwa na matatizo kwenye njia ya uzazi au mtoto mwenyewe.

Uzazi pingamizi ni miongoni mwa sababu kubwa zinazosababisha vifo vya kinamama hasa katika nchi zinazoendelea.

Kutokana na ongezeko la mimba za utotoni, uzazi pingamizi umekuwa ukiongezeka katika nchi zinazoendelea.

SABABU ZINAZOPELEKEA UZAZI PINGAMIZI
Matatizo katika njia ya uzazi,
1. Kutokuwiana kwa nyonga na mtoto au kuwa na nyonga yenye shida
2. Uvimbe katika shingo ya kizazi au katika ligamenti
3. Makovu kwenye njia ya uzazi yatokanayo na upasuaji

Matatizo kwa mtoto
1. Mlalo mbaya tumboni
2. Kutanguliza uso wakati wa kuzaliwa
3. Mtoto kuwa mkubwa (big baby)
4. Mtoto kutanguliza kichwa na kiungo kingine k**a mkono wakati wa kuzaliwa
5. Mapacha walioungana

DALILI ZA UZAZI PINGAMIZI
Kwa mtu wa kawaida inawezekana asizigundue dalili hizi hivyo kina mama wote wanashauriwa kujifungulia hospitali ili kuondokana na madhara yatokanayo na uzazi pingamizi.
1. Kutengenezeka kwa mkanda unaotenganisha sehemu ya juu na ya chini ya mji wa mimba(retraction or bandl’s ring)
2. Kukojoa mkojo wenye damu
3. Kuvimba sana kwa sehemu ya nje ya uke

MADHARA YA UZAZI PINGAMIZI

KWA MAMA
1. Kuchoka kutokana na kusukuma pasipo mafanikio
2. Kupungua kwa kiwango cha maji mwilini
3. Kuongezeka kwa kiwango cha asidi mwilini
4. Maambukizi katika njia/mfumo wa uzazi wa mwanamke
5. KUPASUKA KWA MJI WA MIMBA
6. Kutokwa na damu nyingi mara baada ya kujifungua
7. KUPATA FISTULA

MADHARA YA MIMBA PINGAMIZI KWA MTOTO
1. Mtoto kukosa okisijeni ya kutosha halii hii inaweza pelekea shida katika maendeleo ya ukuaji katika mfumo wa fahamu na mifumo mingine katika mwili
2. Kuvujia kwa damu kichwani
3. Maambukizi
4. Kifo

JINSI YA KUJIKINGA NA UZAZI PINGAMIZI
1. Zuia mimba za utotoni
2. Wanawake wote wajawazito wawe na maudhulio mazuri kliniki ili kugundua k**a wapo katika hatari ya kupata uzazi pingamizi na hivyo kufanya maandalizi kwa ajili ya kujifungua.
3.Lishe wakati wa utotoni
By lwamayang

FAHAMU FAIDA ZA MAZIWA NA VYAKULA VIONGEZAVYO UTENGENEZAJI WA MAZIWA.Maziwa ya mama kwa mtoto yanafaida nyingi sana ikiw...
20/04/2020

FAHAMU FAIDA ZA MAZIWA NA VYAKULA VIONGEZAVYO UTENGENEZAJI WA MAZIWA.

Maziwa ya mama kwa mtoto yanafaida nyingi sana ikiwemo kinga na virutubisho vinavyomsaidia mtoto kukua. Kitaalamu inashauriwa mtoto anyonye pasipo kuchanganyiwa kitu kingine kwa muda usiopungua miezi sita na baada ya miezi sita mama anaruhusiwa kuongeza vyakula laini na huku akiendelea kumnyonyesha. Maziwa ya mama yanakila kitu ambacho mtoto anatakiwa kupata ndani ya miezi sita ya mwanzo ikiwemo maji, protini, vitamin, madini mafuta na kinga za mwili. Hivi vyote uchangia katika ukuaji wa mtoto.
FAIDA ZA MAZIWA YA MAMA KWA MTOTO.
1. Zinachangia ukuaji na kumkinga mtoto na magonjwa
2. Yanasaidia mahusiano mazuri ya mama na mtoto pamoja na kumkinga na baadhi ya allergy.
3. Maziwa ya mama yanameng’enywa kwa urahisi ukilinganisha na maziwa au vyanzo vingine vya chakula.
FAIDA ZA KUNYONYESHA KWA MAMA
1. Inapunguza hatari ya kupata saratani ya ovari na matiti.
2. Inasaidia nyumba ya uzazi kurudi haraka katika hali yake ya kawaida
3. Inapunguza hatari ya kupoteza damu nyingi baada ya kujifungua lakini pia inamsaidia mama kupunguza uzito ambao huongezeka wakati wa mimba
3. Hayana gharama ukilinganisha na vyanzo vingine vya maziwa au chakula.

VYAKULA VINAVYOONGEZA UTENGENEZWAJI WA MAZIWA.
Wanawake wengi wanekuwa wakulalamika au kukubwa na tatizo la kutokutengeneza maziwa ya kutosha na hivyo kupelekea ukuaji hafifu wa watoto wao. Vifuatavyo ni vyakula na matunda yaongezayo utengenezaji wa maziwa.
1. Mboga za majani k**a spinachi na matembele
2. Vitunguu swaumu na tangawizi. Mbali na kuongeza radha ya chakula viungo hivi vinaaminika kwa kuongeza utengenezaji wa mazima.
3. Siagi ya karanga
4. Viazi vikuu, viazi vitamu, karoti na mapapai
5. Maziwa ya ng’ombe, maji mengi na juisi ya kutengeneza
6. Mbegu za mikunde kunde (zina protini nyingi)
7. Mayai na nyama( k**a supu ya kuku)
8. Parachichi (avocado)
9. Mafuta ya samaki
10. Nafaka na vyakula vya wanga k**a mkate, mtama, mahindi na vyakula vya ngano.

SABABU ZINAZOPELEKEA UPUNGUFU WA MAZIWA.
1. Kutokunyonyesha mara kwa mara hasa hasa wakati wa usiku.
2. Kuchelewa kuanzisha unyonyeshaji wa mtoto.
3. Uwekaji mbaya wa mtoto katika ziwa
4. Matumizi ya chupa

By Emmanuel Lwamayanga

FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU,  DALILI NA MATIBABU YA KUTANUKA/KUKUA/ KUONGEZEKA KWA UKUBWA WA TEZI DUME. Kutanuka kwa tezi...
19/04/2020

FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU, DALILI NA MATIBABU YA KUTANUKA/KUKUA/ KUONGEZEKA KWA UKUBWA WA TEZI DUME.

Kutanuka kwa tezi dume imekuwa ni tatizo linalokua sana kwasasa kutokana na ukweli kwamba muda/umri wa kuishi wa binadamu umeongezeka. Tezi dume kitaalamu prostate gland hupatikana kwa wanaume na kila mwanaume yupo katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili. Ukubwa wa tezi kati ya miaka 20-55 inaaminika kuwa ni gramu 20.

Kutanuka kwa tezi dume kunawapata hasa watu wazima kuanzia miaka 50 na kuendelea.
Tezi dume imegawanyika katika matabaka/ kanda kuu tatu, kanda ya pembeni ambayo mara nyingi saratani ya tezi dume hutokea, kanda ya kati na kanda mpito ambayo huzunguka mrija wa mkojo. Kanda hii ndio chanzo kikubwa cha tatizo la ukuaji au kutanuka kwa tezi dume.

KWANINI TEZI INAKUA/INATANUKA.

Ukuaji wa tezi dume unaendeshwa na visababishi vingi, kisababishi kikuu ikiwa ni homoni iitwayo testosterone. Homoni hii hubadilishwa na kuwa homoni ambayo kitaalamu inaitwa DHT ambayo hupatikana kwa wingi katika tezi hii.
Katika hali ya kawaida kiwango cha testosterone hupungua mwilini kadri umri unavyoongezeka lakini kiwango cha oestrogenic steroids hakipungui kwa uwiano sawa na ule wa testisterone. Hivyo inasadikika kuwa kutanuka kwa tezi dume kunachangikiwa na ongezeko la madhara ya oestrogen.
Kutanuka kwa tezi dume hupelekea kuongezeka kwa urefu wa mrija wa mkojo.

DALILI ZA KUTANUKA KWA TEZI DUME

1. mtiririko dhaifu wa mkojo
2. Kukojoa kwa shida, mkojo kushindwa kutoka hata wakati mtu anapohisi kukojoa
3. Mkojo kuendelea kutoka kidogo kidogo/ matone kwa muda mrefu baada ya kumaliza kukojoa
4. Shida katika kuanza kukojoa au kuubana mkojo
5. Hali ya kujisikia kukojoa mara kwa mara au ghafla
6. Kuhisi kibofu kutokuisha mkojo
7. Kuamka mara nyingi zaidi usiku kwa ajili ya kukojoa
8. Kutumia nguvu kuanzisha mkojo hata pale mgonjwa anapohisi kibofu kimejaa pamoja na maumivu.

MADHARA

1. Mkojo kushindwa kutoka kabisa
2. Ukuta na misuli ya kibofu kutanuka na hivyo kupoteza uwezo wa kuzuia mkojo
3. Kuharibika kwa figo
4. Maambukizi ktk njia ya mkojo
5. Mawe katika mfumo wa mkojo.

MATIBABU
1. dawa
2. Upasuaji
Bila kusahau kubadili mfumo wa maisha.

By Emmanuel Lwamayanga

Address

Gongo La Mboto
Dar Es Salaam

Telephone

+255764723526

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Eimmer_medics posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram

Category