10/10/2025
Kila tarehe 10 mwezi wa kumi dunia huadhimisha siku ya Afya ya Akili.
Kauli mbiu ya mwaka huu 2025 ni: “Upatikanaji wa Huduma za Afya ya Akili Wakati wa Majanga na Dharura.”
Kauli mbiu hii inasisitiza umuhimu wa kuhakikisha huduma za afya ya akili zinapatikana hata wakati wa majanga k**a vita, mafuriko, au magonjwa ya mlipuko. Inahimiza serikali na wadau kuingiza huduma za afya ya akili katika mipango ya dharura, kutoa msaada wa kisaikolojia, na kupunguza unyanyapaa.
Takribani watu bilioni 1 wanaishi na magonjwa ya akili duniani, mtu 1 kati ya watu 8 atapitia hali ngumu ya afya ya akili au kupata magonjwa ya akili katika maisha huku mahala pa kazi mtu 1 kati ya watu 7 huwa na matatizo ya afya ya akili.
Siku hii hutumika kuwakumbusha watu kuhusu umuhimu wa Afya ya Akili. Afya ya akili ni eneo lililosahaulika sana katika afya ya jamii.
Tunawashukuru wadau wanaoendelea kutoa elimu na huduma za afya ya akili
Kwa maulizo yoyote kuhusu afya ya akili wasiliana nasi: 0742 501 501