08/05/2024
MAISHA NI WATU NA KUISHI NI KUHUSIANA NA KUCHANGAMANA NA WATU HAO
Licha ya kitabu cha "A Man of the People" kuchapishwa miaka mingi iliyopita kila kukicha kinazidi kujipatia umaarufu na kupendwa zaidi kwa sababu ya umahiri wa gwiji Chinua Achebe katika kueleza mambo yasiyopitwa na wakati.
Naomba nitoe mfano mmoja kutoka kwenye kitabu hicho kilichochapishwa na kampuni ya Heinemann mwaka 1966. Katika kitabu hicho kuna mhusika aitwaye Odili ambaye baada ya kuhitimu chuo alirudi kwao na kuanza kufundisha shule. Baadaye Odili anakutana na mheshimiwa mmoja aitwaye Chifu Nanga ambaye ni mbunge na waziri na kabla ya kuwa mbunge alikuwa mwalimu kwenye shule hiyohiyo Odili anayofundisha.
Baada ya wasomi hawa wawili wanaofahamiana na kutoka sehemu moja kukutana, Chifu Nanga anamsihi Odili akawe katibu ofisini kwake maana katibu wake ni wa kabila jingine. Mhe. Nanga anahitimisha kauli yake kwa kusema, "Nowadays, it doesn't matter what you know but who you know". Basi, k**a hali ilikuwa hivyo miaka ya 66 kitabu hiki kilipochapishwa je itakuwaje leo miaka zaidi ya 50 baadaye? Bila shaka itakuwa ni mbaya zaidi ya mara mia.
Kwanini nimeanza na mfano huu ama kueleza kuhusu kitabu hiki? Katika jamii yetu ya sasa kuna watu hawana habari na watu. Wao wanajidai kuwa wako bize na mambo yao wenyewe na wanajua kujifungia kwelikweli. Hata siku moja huwezi kuwaambia kuchangamana na watu wengine kwenye maeneo yanayokutanisha watu k**a michezo, sherehe mbalimbali n.k. Wakati mwingine hata wanapokuwa katika mikusanyiko ya watu wanabaki kuwa wao k**a wao hata huwezi kuwaambia kuchangamana ama kusemeshana na wenzao. Watu wa hivi hata akikukuta umekaa ama upo sehemu ambayo naye amekuja si ajabu hata akakuvungia hata kukusalimu tu.
K**a wewe ni mmoja wa watu wa aina hii napenda leo nikujulishe kuwa maisha ni watu na kuishi ni kuchangamana nao. Kwa kadiri unavyojifungia mwenyewe ndivyo unavyojikwamisha mwenyewe. Labda tu nikwambie kwamba unavyojifungia ndivyo unafungia michongo unayohitaji ili utoboe maisha.
Kwa taarifa yako unahitaji watu ili ufanikiwe. Katika dunia ya leo kila kitu unachohitaji kipo kwa watu na ili ukipate itategemea jinsi unavyohusiana na watu hao. Kazi ama fedha ama mwenza unayemhitaji leo ili ubutue maisha yupo kwa watu hao unaowachukulia poa. Siku hizi watu wengi wanasota kitaa kwa kukosa kazi na wengine wameshahaso kila kona kupata ajira imekuwa ngumu kwao wakati mwingine anapata kazi ya heshima na mshahara mnono bila hata ku-apply kwa sababu anajuana na mwajiri k**a Odili na Chifu Nanga.
Kuna mtu baada ya kuhitimu chuo amekaa mtaani miaka ya kutosha mpaka anazeekea nyumbani kwa kukosa "connection" wakati mwingine anamaliza mtihani leo kesho anaenda kuanza kazi. It's doesn't matter what you know but who you know - hivi ndivyo dunia inakwenda siku hizi ndugu yangu.
Mpendwa k**a kweli unataka kufanikiwa katika ndoto yako unahitaji watu kuliko kitu kingine chochote kile unachofikiria wewe. K**a bado upo chuo unasoma labda digrii ya kwanza na una ndoto za kusoma Master's na kuendelea nikukumbushe kuwa unahitaji kuwa na mtu atakaye-recommend application/scholarship yako.
K**a huna ndoto za kuendelea kuongeza kisomo na unafikiri wewe ukimaliza chuo utazama moja kwa moja kufanya kazi na kula mshahara. Basi ngoja nikukumbushe tu kuwa ndugu yangu unahitaji referee wa kuweka kwenye CV yako ili upate hiyo kazi unayoitaka. Soko la ajira siku hizi limechangamka mno, hata k**a una sifa zote ama hata za ziada anazohitaji mwajiri k**a huna referee wa kukunenea mema ajira hiyo uliyostahili utaikosa hivihivi huku ukiitazama kwa macho yako mawili (wakati mwingine na miwani juu).
Lakini huenda huwazi kuendelea na masomo ama kufanya kazi. Labda wewe unafikiria kufanya biashara na kupiga hela. Mwenzangu huku nako si salama. Ili ufanikiwe katika biashara yako unahitaji mtu atakayekupa machimbo/masoko ya bidhaa zako. Unahitaji mtu wa kukuletea wateja. Biashara yako itahitaji mtu atakayekusaidia katika masuala ya usajili, (hapa Bongo bila kuwa na mtu leseni ya biashara utaipata umepata taabu sana ama la ukubali kuzunguka mbuyu) kulipa ritani za TRA na k**a utahitaji mikopo ili kuipanua zaidi, utahitaji mtaalamu wa masuala ya fedha wa kukusaidia katika eneo hilo.
Aidha, k**a hufikirii kufanya lolote kati ya hayo niliyoyataja hapo juu lakini ungali kijana basi utahitaji watu kwa ajili ya send off/harusi yako. Hii ndiyo sehemu yenye utata sana hasa kwa vijana wengi - linapofika jambo lake ndiyo anakutafuta ili tu umchangie apate mume ama mke kwa sapoti ya jasho lako wakati hakuwa na muda nawe. Kwani wewe haijawahi kutokea unawasha data kwenye simu yako mara paaaap unajikuta kwenye group la michango ya sherehe ama harusi ya mtu ambaye hajawahi kukutafuta japo hata kwa kukutumia sms moja kwa zaidi ya miaka 5? Kwa sababu maji yanakuwa yamemfika shingoni ndio anakumbuka kulazimisha undugu hata kwa watu ambao hatukuwa na muda nao.
Kila mtu kwenye jamii anahitaji watu. Hawa watu sio lazima wawe ndugu, wala watu unaotoka nao sehemu moja huko kijijini. Si lazima wawe wa umri, elimu ama jinsi yako. Bali hawa ni watu wako wa nguvu, watu waliotayari kulichukulia jambo lako k**a jambo lao wenyewe. Ni watu ambao ukianguka wapo tayari kukuinua na ukiteleza watajitoa kukudaka ili k**a utaumia au kuanguka basi potelea mbali muumie ama kuanguka wote. Waingereza wana msemo wao usemao, "You will never walk alone" k**a wewe unafikiri unaweza kwenda peke yako basi endelea kujifungia nimekaa palee, mwisho wa siku tutaona. Ukitoboa kwa mtindo huo basi nasi tutafuata nyendo zako.
Ndugu yangu maisha ni watu. Husiana na watu, changamana na watu ishi na watu hayo ndiyo maisha. Kumjua mtu jina lake haitoshi katika zama za leo bali tafuta kila namna ya kutengeneza naye undugu. Nakuhakikishia k**a sio kesho basi keshokutwa huyo mtu atakufaa. Katika maisha ya sasa ni vema mtu kuwa na watu anaojuana nao katika nyanja zote za maisha. Tengeneza undugu na watu wa afya (madaktari, wauguzi n.k), tengeneza uhusiano mwema na watu wa ulinzi na usalama (wanajeshi, polisi, mgambo n.k), tengeneza ukaribu na watu wa masuala ya utawala (wanasiasa, mameneja, wakurugenzi n.k) tengeneza familia na watu wa rohoni kulingana na imani yako (wachungaji, manabii, wainjilisti, mapadri, masheshe, waganga wa kienyeji n.k) hao ndio watakaokuufaa kwa wakati usiotarajia.
Kwa leo naomba niishie hapa. Naamini umepata kitu cha kujifunza... Si mbaya ukiweka comment yako hapo chini ama kushea kwa wenzako ujumbe huu ili nao wapate cha kujifunza pia. Maisha ni watu na unavyowatumia andiko hili ndivyo unaiishi dhana hii.
Wasalaam;
Ayoub Butandu
ayoubbutandu@gmail.com