28/04/2024
33. JE! TANZANIA KUNA WATAFITI/WANASAYANSI KWELI?.
(SOMA MAKALA HII MWANZO HADI MWISHO TAFADHALI). NUKUU KUTOKA KITABU CHA KUWA NA UWEZO MKUBWA KIAKILI 2018. Kuna mambo yamekuwa sababu ya mimi kujiuliza maswali haya. Ili kujiridhisha na hata kujua au kupata jawabu na kisha kutoa ushauri wangu kwa mustkabali wa taifa langu Tanzania.
Moja ya sababu zilizonifanya nijiulize maswali haya ni.
1. Daraja la Jagwani/ Kituo au ofisi kuu ya mabasi yaendayo
kasi UDART Jangwani.
Hii imetokana na baada ya mvua nyingi kutokea mwaka 2018 za masika, daraja lilifunikwa na maji, na ukizingatia barabara husika ni mpya kabisa na imejengwa kwa gharama kubwa. Na isitoshe ofisi za mwendokasi kufurika maji hata kupelekea ofisi hizo kufungwa kwa muda ili kupisha maji yatoke.
Maswali ya kujiuliza.
Utafiti gani uliofanyika hata ukaona ujenzi wa barabara k**a ile ndio inafaa kwa eneo lile? Ni mtafiti gani aliyeona kuwa ofisi ya mwendo kasi ikijengwa pale jangwani na kwa mtindo ule hakutakuwa na madhara? Hivi huwezi kukubaliana nami kuwa, hata wewe ambaye haujasoma au si mtaalam wa mambo ya ujenzi utabaini kuwa haikupaswa kujengwa daraja k**a lile pale jangwani? Au haikupaswa kujengwa ofisi za UDART Kwa aina k**a ile? Aidha ilipaswa kuwa juu zaidi kutoka usawa wa ardhi ya kawaida?
Kutokana na asili ya eneo la jangwani na kukaribiana na bahari ya hindi kutoka darajani wastani wa kilomita moja kasoro makutano ya mto msimbazi na bahari ya hindi (Sarenda brige). Historia ya mto msimbazi, na uwingi wa maji yanayosafirishwa na mto huo. Inaaminika kuwa karibu maji yote ya jiji la Da es salaam yanasafirishwa kupitia mto huo. Mto Msimbazi umetokea nje ya jiji la Dar es salaam meneo ya Pugu, ukaingia Gongolamboto, ukapitia Vingunguti, Kisha Buguruni, na maeneo ya Buguruni chini maeneo Kigogo kuna makutano ya mito kadhaa ya jiji la Dar es salaam inakutana kwa pamoja na kuunda mto mmoja mkubwa maeneo ya Jangwani huitwa Jagwani, lakini Jangwani ni makutano ya mito yote, na mto huo sana unaelekea kufika maeneo ya makutano ya bahari ya Hindi (Sarenda brige).
Kwa wastani mto huu umepita katika Wilaya ya Ilala yote, ikiwa na maana karibu maji yote ya Wilaya ya Ilala na ikijumuishwa na maji yatokayo katika majengo ya katikati ya jiji hasa Kariakoo yote yanaingia katika mto huo.
Pia asilimia ya mito mingi ya Wilaya ya Kiondoni iliyopita maeneo ya Kigogo, Magomeni, Mkwajuni nk, yote inaingia katika Mto wa Msimbazi. Hii bila ya kujumuisha tani za taka ngumu au shehena za taka ngumu zinazoingia katika mito hii.
Tabia ya makutano ya bahari na mito.
Kwa kawaida maji yanayoingia bahari yanaingia taratibu ili kuchanganyika na maji ya bahari, pia wakati fulani bahari inakuwa kupwa na kujaa. Kwa hiyo ikiwa ndio wakati wa kujaa na mvutano wa mawimbi makubwa, bila ya shaka maji ya mto yataingia lakini kasi yake haitakuwa kubwa k**a wakati bahari imekuwa kupwa (Maji yamepungua). Bila shaka uwezekano wa kuwepo mafuriko ni mkubwa sana, katika eneo hili la Jangwani kipindi ambacho maji mengi ya mvua za masika yakitaka kuingia kwa wingi na kwa wakati mmoja.
2. Barabara ya mwengo kasi Kariakoo mtaa wa/barabara ya
Msimbazi,
Maeneo ya mataa Uhuru na Msimbazi, na karibu na kituo cha DDC. Kituo cha mwendokasi DDC Kariakoo, Kabla ya kujengwa barabara mpya ya mwendokasi, palikuwa na utiririshaji majitaka kutoka katika mifereji ya barabara kwa miaka mingi. Lakini cha kusikitisha, hata baada ya kujengwa barabara mpya na ya kisasa zaidi na mifereji kujengwa upya, lakini bado tatizo la mifereji ya maji taka inaenedelea kububujisha au kutiririsha maji taka ndani ya barabara hadi kuleta tishio la kiafya kwa wakaazi wake. (Hii ni hadi kufikia mwaka 2018)
Swali la kujiuliza.
Ni utafiti gani uliofanyika na kujiridhisha kuwa, iwapo barabara ikijengwa kwa aina k**a ile na mifereji k**a ile utaondoa tatizo la utiririsha wa maji taka barabarani k**a hapo kwanza? Kwa nini wakandarasi wetu na wataalamu wetu, kwa mfano wataalamu wa mazingira wasiwe na majibu sahihi ya matatizo ya mazingira yetu? Au kazi yao ni nini k**a sio kuchunguza
nini kinahitajika katika mazingira yetu ili kuondoa tatizo? Leo tunapoona matatizo k**a haya yakijirudia huwa tunapata shaka na wataalamu wetu, au tunajaribu kuhisi k**a hatuna wataalamu au watafiti?
3. Madaraja mapya kusombwa na maji au maji kuacha daraja na kupasua sehemu nyingine.(Hii ni kwa mjibu wa utafiti wangu hadi kufikia mwaka 2018.)
Ndugu msomaji, kuna mambo huwa yanatia aibu kubwa taaluma za watu, au pia yanaitia aibu nchi yetu kwa kiasi kikubwa. Hivi unajiuliza iwapo daraja likisombwa na maji au maji kuacha kupitia darajani na kuvunja sehemu nyingine na kutoroka, je utafiti ulifanyika kikamilifu?
Ni wazi kabisa iwapo madaraja yakikatika au maji kupasua sehemu nyingine na kumomonyoa udongo na kuikata barabara, hii inaonyesha wazi wajenzi hawakuchunguza eneo hilo vya kutosha. Au hatuna tafiti zinazo saidia kujua tabia za asili za maeneo yanayotaka kujengwa madaraja au mifereji. Mjenzi anatakiwa awe na majibu ya matatizo kabla hayaja tokea. Ikiwa na maana aione hatari ya eneo husika analofikiria kulijenga na kujenga kulinga na mahitaji ya eneo. Nadhani kipimo cha mkandarasi mzuri ni pale majanga k**a haya yakitokea na kisha kazi yake ikibaki salama huyo ndio mjenzi bora. K**a umejenga kwa udanganyifu mvua zikija kazi yako itapimwa na kuonekana ni kazi mbovu.
4. Ujenzi wa shule.
Kwa mujibu uchunguzi wangu hadi kufikia mwaka 2018. Kumekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi haswa kwa shule za serikali hata kufikia madarasa hayatoshi kuchukua idadi kubwa k**a hiyo. Na majengo kila kukicha yanajengwa na hata maeneo ya kujenga yanakosekana.
Ujenzi wa nyumba za chini.
Kosa kubwa linalofanyika ni ujenzi ya nyumba za chini ambazo si ghorofa. Kwa kawaida nyumba za paa (Ambazo sio ghorofa) Zinachukua Idadi ndogo ya watu na pia zinatumia eneo kubwa la ardhi. Katika kitabu changu kiitwacho UCHUMI HURU USIOKUWA NA MAJUTO, Nimeandika umuhimu wa matumizi bora ya ardhi.
Na katika mada hiyo, nimeelezea umuhimu wa kutumia eneo dogo la ardhi kwa manufaa makubwa. Ukubwa wa ardhi wenye urefu wa mita 20x20. Unaweza kujenga nyumba zaidi ya moja kuwenda juu, ikiwa na maana unaweza kujenga nyumba moja ya ghorofa yenye ghorafa 5 au 10, au 20. Sawa na nyumba moja kwa 5 au moja kwa 10 au moja kwa 20. Ambapo k**a nyumba tano za chini zingechukua eneo la ukubwa wa mita 100 sasa unatumia mita 20 kwa nyumba tano na zaidi katika eneo moja tu.
Swali langu la msingi ni.
Tumekosa wataalamu waliogundua kuwa serika inatumia vibaya ardhi na kuingia gharama za kujenga kila kukicha na kuishauri serika kwa sasa waanze kujenga nyumba za juu?
5. Wamachinga.
Sijaelewa k**a ni utafiti gani umefanyika na kubaini kuwa kuwa na umachinga holela itasaidia kitu fulani katika taifa letu? Nani aliyefanya utafiti ili kujua kuwa kuna faida kadhaa na madhara kadhaa?
6. Tatizo ni idadi ya watumishi au udhaifu wa watumishi?
Kwa nini serikali zetu za Africa huona kuwa jibu la utendaji
bora ni kuwa na watumishi wengi au Wizara nyingi?
Hali ya kuwa utitiri wa watumishi hao wanafanya kazi chini ya kiwango? Gharama za uendeshaji serikali zinakuwa kubwa kutokana na kuwa na serikali yenye watumishi wengi. Kwa nchi za Afrika hazinabudi kupunguza idadi ya watumishi wake, na kuzingatia usimamizi mzuri wa watumishi wachache watakao kuwanao ili wafanye kazi kwa ufanisi mkubwa, na huku wakiwalipa malipo mazuri.
NUKUU KUTOKA KITABU CHA KUWA NA UWEZO MKUBWA KIAKILI 2018.
BEI YA KITABU NI TSH 20,000 MAWASILIANO 0717528272 / 0788170367 /0755528965