IJUE AFYA YAKO

IJUE AFYA YAKO Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from IJUE AFYA YAKO, Health & Wellness Website, buguruni rozana, Dar es Salaam.

**🌿 Huduma ya Afya Yenye Kugusa Maisha!
🩺 Kipimo cha mwili mzima kwa TSH 30,000 tu
✅ Tiba & ushauri: Uzazi, PID, Moyo, Saratani,
Vidonda vya tumbo, Kisukari, Pressure & Mifupa
📞 0625 257 681 | 📍Buguruni

15/06/2024

Ngiri ni nini?
Ngiri ya kinena hufahamika kwa Kiingereza k**a Inguinal Hernia. Ngiri katika eneo la kinena hutokea pale utumbo hujitokeza kwenye uwazi katika ukuta wa tumbo kwenye kinena. Ngiri kwenye kinena hutokea mara nyingi na huwaathiri zaidi wanaume.

Dalili kuu ni uvimbe kwenye kinena, ambao ukisukumizwa ndani unapotea kwa muda.
Dalili nyingine pia ni maumivu ya upande mmoja wa korodani, pia wakati maumivu yakianza kujitokeza korodani moja upanda na maumivu huwa makali. Utambuzi hufanywa na daktari kuchunguza uvimbe kwa kutumia kipimo cha ultrasound. Hali hii isipotibiwa inaweza kusababisha utumbo kunaswa na hivyo kushindwa kupatiwa damu na hatimaye kuoza. Hali hii hurekebishwa kwa upasuaji. Ngiri iliyonaswa ni hali ya dharura na inahitaji matibabu ya dharura kwa njia ya upasuaji.
Zaidi zipo tiba mbali mbali za asili ambazo zinaweza kumaliza tatizo hili jumla bila upasuaji.

KWA WEWE MWENYE HILI TATIZO USISITE WASILIANA NASI.
0625257681.

DALILI ZA HATARI KWA MJAMZITO KTK KIPINDI CHA UJAUZITO, WAKATI WA KUJIFUNGUA NA BAADA YA KUJIFUNGUA.Dalili hizo ni k**a ...
15/06/2024

DALILI ZA HATARI KWA MJAMZITO KTK KIPINDI CHA UJAUZITO, WAKATI WA KUJIFUNGUA NA BAADA YA KUJIFUNGUA.

Dalili hizo ni k**a ifuatavyo;

1. Kutokwa Damu Ukeni kwa Mjamzito Mimba ya Wiki 28 au zaidi.

2. Mimba kuharibika au kutishia kuharibika.

3. Mimba kutunga nje ya Mji wa Uzazi.

4. Presha ktk Ujauzito au Mimba.

5. Chupa kupasuka na kutokwa maji ukeni kabla ya Mimba komaa kati wiki 28 hadi wiki 36 na siku 6.

6. Udhaifu wa Mlango wa Uzazi.

7. Mtoto kupunguza kucheza kuanzia Mimba ya wiki 28 kwenda juu.

8. Kupasuka kwa Mji wa Uzazi kabla au wakati wa Kujifungua.

9. Uchungu Pingamizi wakati wa Kujifungua.

10. Uchungu wa muda mrefu wakati wa Kujifungua.

11. Mrija kujitokeza au kutangulia wakati wa Kujifungua kabla Mtoto kuzaliwa.

12. Kutokwa Damu Ukeni baada ya kujifungua.

13. Kutokwa na Uchafu wenye harufu kali Ukeni baada ya kujifungua au ndani ya siku 42 tokea kujifungua.

14. Homa au kuchemka sana mwili ndani ya siku 42 tokea kujifungua.

KUMBUKA:
Mama Mjamzito au Mama unayenyonyesha unapoona dalili hizo wahi hospitali bila kujiuliza maswali, nenda hospitali hata k**a ni usiku wa manane ili kupewa msaada na huduma za DHARULA.

Wakati wa Kujifungua Madaktari huweza kufanya huduma ya dharula mfano; Kufanyiwa upasuaji wa dharula endapo Mrija umetangulia kabla ya mtoto na umebanwa kwa sababu ni hatari kwa afya ya Mtoto wako aliyeko Tumboni mwa Mjamzito.

MIMBA KUHARIBIKA (Miscarriage) CHANZO NA SABABU, DALILI NA NINI UFANYE ILI KUZUIA ISITOKEE TENA0625257681.Somo hili ni r...
15/06/2024

MIMBA KUHARIBIKA (Miscarriage)

CHANZO NA SABABU, DALILI NA NINI UFANYE ILI KUZUIA ISITOKEE TENA
0625257681.

Somo hili ni refu na kwa hiyo limegawanyika sehemu kuu tatu
1- Dalili za mimba kuelekea kuharibikiwa
2- Chanzo na sababu za mimba kuharibika
3- Nini cha kufanya ikiwa huwa unapatwa na hali hiyo mara kwa mara.

SEHEMU YA KWANZA

Ni kawaida sana mimba kutoka au kuharibika bila kukusudia au bila wewe kujua k**a imetoka au inakaribia kutoka. Wakati mwingine hutoka tu bila sababu yeyote na hata k**a utapimwa na vifaa vya kisasa kabisa bado sababu za mimba kuharibika hazitajulikana. Ikiwa utajua ya kwamba mimba imetoka

CHAKWANZA ni vizuri kujua sababu ya mimba hiyo kutoka, hasa k**a imeharibika kwa mara ya pili na zaidi. Sababu zinaweza kuwa nyingi k**a vile utakavyo ona katika aya zifuatazo

CHA PILI kupambana na icho kisababishi, baada ya kupima na kupata ushauri basi itakufaa sasa upate dawa au kufuata ushauri uliopewa, ukimaliza dozi rudi hospitalini ili uweze kujua k**a umepona kabisa au la.

Kunayo tabia ya watu wengi tu askisha maliza dozi ndio inakuwa basi anaendelea na Maisha yake, hapo unakuwa unakosea. Jitahidi kurudi hospital na kupima tena upate uhakika wa tatizo k**a limeisha au la. K**a halijaisha inakuwa rahisi kwa daktari kuchukua vipimo vingine au kukupa dawa ingine.

CHA MWISHO ni kujaribu tena kubeba mimba, baada ya kuona mambo yote yako sawa, au sasa unaamini uko vizuri basi unajaribu tena kupata mimba. Zingatia siku zako za uzazi, na zingatia kupika vyakula vizuri ili mume wako apate nguvu ya kutoa mbegu nyingi na zenye afya njema.

Usafi pia wa mwili na kitanda ni muhimu. Usinuke na kutoa harufu mbaya.
Mara nyingi swala la kwanza na pili watu huruka na kuendelea nakutafuta mimba.

Zamani wakati vifaa na wataalamu walikuwa hakuna hiyo ilikuwa sawa lakini Siku hizi kuna vifaa ujitahidi kutafuta sababu.

Hii ni Kwa sababu pia uwezo wa wanawake kuzaa umepungua sana. Wanawake wachache wanazaa watoto zaid ya 6 hata wakitaka kuzaa wanajikuta hawawezi. Wengine wanachelewa kuolewa, kwa mana hiyo wanaanza kutafuta watoto wakati Mayai bora mengi yameishaisha. mawasiliano*
0625257681.

Suala la kupata mtoto katika familia  haliegemei upande wa kina mama tu.Mimba kutunga ni matokeo yanayotegemea upande wa...
15/06/2024

Suala la kupata mtoto katika familia haliegemei upande wa kina mama tu.

Mimba kutunga ni matokeo yanayotegemea upande wa k**e na wa kiume japokuwa kwa jamii zetu tumezoea kuwa familia ikikosa mtoto basi lawama huenda moja kwa moja kwa mwanamke kuwa yeye ndiye chanzo cha tatizo jambo ambalo huwa sio la kweli mpaka wote kwanza mfanye vipimo kubaini nani haswa ni chanzo.

Mwanaume unaweza kujiona upo vizuri kitandani na show unaiweza haswaa ila kumbe ukawa na tatizo k**a

1. Oligospermia-hii ni hali ya kupungua kwa mbegu za kiume

2. Aspermia =hii ni hali ya kutokuwa na majimaji yaani (semen) ambayo husaidia kusafirisha mbegu za kiume

3. Azoospermia-ukosefu wa mbegu za kiume

4.Teratospermia- hii ni hali ya kuongezeka kwa mbegu za kiume ambazo hazijakamilika yaani hazina aidha kichwa au mikia

5. Asthenozoospermia - hii ni hali ya mbegu za kiume kushindwa kujongea (kuogelea au kusafiri) kuelekea ndani ya via vya uzazi wa mwanamke ili kuweza kurutubisha

Zingatia haya

Jipe ulaji wa vyakula visivyokobolewa k**a ugali dona, mihogo, viazi n.k huku mboga na matunda ikiwa ni samaki wabichi, bamia, ndizi mbivu, karanga, tikiti, mbegu za maboga, mayai ya kienyeji, komamanga, parachichi, asali mbichi na mboga za majani. K**a mwanaume atapata walau viwili hadi vitatu kwenye hiyo orodha kwa wingi wa kutosha .

Contact/watsup 0625257681.

Je, Unapatwa na Changamoto za Nguvu za kiume K**a Hizi?* Uume Kusinyaa na Kuwa Mdogo K**a wa Mtoto?* Kukosa Hamu ya Tend...
15/06/2024

Je, Unapatwa na Changamoto za Nguvu za kiume K**a Hizi?

* Uume Kusinyaa na Kuwa Mdogo K**a wa Mtoto?

* Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa?

* Kuchelewa Kurudia Bao la Pili?

Ikiwa unakumbana na changamoto hizi za kawaida za nguvu za kiume, usijali! Hauko peke yako.

Wanaume wengi duniani kote hupitia matatizo haya, na kuna suluhisho.

Wasiliana nasi 0625257681.

GOUT NI NINI HASA? 👇👇👇👇👇👇👇👇👉 Gout ni namna moja ya Arthritis, ugonjwa ambao hushambulia joints (sehemu za maungio ya mif...
15/06/2024

GOUT NI NINI HASA?

👇👇👇👇👇👇👇👇

👉 Gout ni namna moja ya Arthritis, ugonjwa ambao hushambulia joints (sehemu za maungio ya mifupa).

👉 Huu ndiyo ugonjwa wa joints ambao huwashambulia sana na kuwapa maumivu makali wanaume.

👉Wanawake pia huweza kuathirika na ugonjwa huu hasa baada ya kukoma hedhi. Ugonjwa huu huleta maumivu makali ya ghafla, hasa kwenye sehemu linapoanzia dole gumba la mguu.

👉Dalili za ugonjwa huanza kuonekana pale uric acid, tindikali ambayo huzalishwa na mwili katika ufanyaji kazi wake (ambayo haina manufaa kwa mwili) inapobakia katika viungo vya mwili na katika majimaji ya mwili.

👉 Uric acid iliyoganda (tophi) huweza kujikusanya na kubaki chini ya ngozi inayozunguka joints, huweza pia kujikusanya ndani ya figo na kusababisha kidney stones (namna ya kokoto ndogo ndani ya figo).

👉 Gout ni ni ugonjwa wa maungio ya mifupa unaoambatana na maumivu makali sana.

👉 Ugojwa huu unasababishwa na mkusanyiko wa uric acid kupita kiasi kwenye joint zako.

👉 Mkusanyiko huu hupelekea kufanyika kwa vijimawe vidogo mithili ya sindano-crystals ambavyo ndo vinakuchoma na kuleta maumivu makali.

👉 kidole kilichovimba kwa gout
Uric acid ni zao linapatikana baada ya mwili kuvunjavunja purine inayopatikana kwa wingi zaidi kwenye vyakula k**a nyama, samaki, mazao ya vyakula vyenye nundu (legumes) k**a maharage, karanga, pombe, na sukari ya fructose inayopatikana kwenye matunda.
Wasiliana nasi 0625257681.

*UGONJWA WA KISUKARI*👉Ugonjwa wa kisukari (diabete mellitus)  ni tatizo linalosababishwa na Upungufu wa  *insulin* ambay...
15/06/2024

*UGONJWA WA KISUKARI*

👉Ugonjwa wa kisukari (diabete mellitus) ni tatizo linalosababishwa na Upungufu wa *insulin* ambayo huzalishwa na kongosho. Ogani ya KONGOSHO huzalisha homoni aina mbili
1: GLUCAGON
Kazi yake ni kupandisha kiwango Cha sukari mwilini.
2: INSULIN
Kushusha kiwango Cha sukari mwilini.
Kongosho inaposhindwa kuzalisha kiwango sahihi Cha INSULINI ambayo kazi yake kubwa ni kubalance KIWANGO Cha sukari mwilini inayozalishwa na Homoni ya GLUCAGON.. Basi ndipo mtu anapata TATIZO LA KISUKARI.

*Aina za sukari*
▶️Kisukari type 1
▶️Kisukari type 2
▶️ Kisukari type 3
*KISUKARI TYPE 1*
☑️Hii ni aina ya sukari ambayo kitaalamu huitwa *JUVENILE DIABETES* ambayo huwapata watoto na mara nyingi huwaga ni ya kurithi.

*DIABETES TYPE 2*
Aina hii ya sukari huwapata watu wazima umri kuanzia miaka 45.
*DIABETES TYPE 3*
Huwapata mama wajawazito kipindi Cha ujauzito wakati wa kujifungua

*SABABU ZA AINA HII YA SUKARI*
☑️Ulevi hasa wa pombe kali
☑️Uvutaji wa sigara
☑️Matumizi ya madawa makali hasa antibiotic
☑️Ulaji mbovu hasa mafuta mengi na vyakula vya kiwandani vyenye kemikali
☑️Magonjwa mengine, k**a vile
👉🏾Moyo
👉🏾Kiharusi
👉🏾Mishipa ya fahamu kushindwa kufanya kazi vzr
👉🏾Figo kufeli n.k.

*DALILI ZA KISUKARI*
☑️Kuhisi kiu sana
☑️Mdomo kuwa mkavu sana
☑️Matatizo ya ngozi na njia za mkojo
☑️Kiungulia na kichefu chefu kikali
☑️Kukojoa mara kwa mara
☑️Kuhisi njaa kila wakati
☑️Mwili kukosa nguvu
☑️Kushindwa kuona vizuri
☑️Uchovu mara kwa mara
☑️Ganzi na miguu kuwaka moto

*MADHARA YA SUKARI*
☑️Vidonda visivyopona
☑️Kukatwa baadhi ya viungo vilivyoathiriwa sana
☑️Mfadhaiko
☑️ Presha ya juu
☑️Anaemia n.k
☑️ Ugumba
☑️Kansa
☑️Utasa
☑️Upofu
☑️ Stroke/Kiharusi

huduma, ushauri, msaada, elimu na tiba zaidi ya kisukari kwa kutumia virutubisho lishe kwa namba 0625257681.

UGOVYA WA FIGO NI HATARI UKIPATA NAFASI YA KUSAFISHA MWILI NA KUUFANYIA DETOXING UNAKUWA UMEOKOA FIGO YAKOKati ya magonj...
15/06/2024

UGOVYA WA FIGO NI HATARI

UKIPATA NAFASI YA KUSAFISHA MWILI NA KUUFANYIA DETOXING UNAKUWA UMEOKOA FIGO YAKO

Kati ya magonjwa tofauti ya figo, ugonjwa huu wa figo huogopwa sana kwani sayansi ya matibabu haina tiba yake.

Magonjwa ya kudhoofisha figo yanaongezeka kwa haraka sana duniani kote.

Mtu mmoja kwa kila watu kumi ana aina fulani ya ugonjwa wa figo usiopona.

Kuongezeka kwa kisukari, matatizo ya shinikizo la damu,unene zaidi,uvutaji wa tumbaku na mafuta mengi mwilini(cholesterol) ndizo sababu kuu za ongezeko la ugonjwa huu usiopona wa figo.

UGONJWA SUGU WA FIGO NI UPI?

Figo kudhoofika kwa muda mrefu wa miezi hata miaka,na kushindwa kufanya kazi zake.

Hali hii ndio ugonjwa sugu usiopona wa figo.
Ishara kuu za ugonjwa huu ni ongezeko la umajimaji wa kreatinini katika damu na figo kupungua kwa ukubwa /kusinyaa.

Kwa wagonjwa wengine huwa hazishindwi kufanya kazi yake kabisa, bali uwezo wake hupungua kiasi.

Kwa hivyo kufeli haina maana ya kushindwa kabisa na kazi zake.

KIPINDI CHA MWISHO CHA UGONJWA WA FIGO NI KIPI?

Kipindi hiki cha tano cha ugonjwa wa figo ndio husemekana kuwa figo zimefeli.

Kazi yake hupungua sana, karibu kukoma kabisa.
Ugonjwa huu unapozidi, kazi za figo hupungua hadi asili mia kumi (10%) ya zile za kawaida.

Figo zinapofikisha kiasi hiki, huwa haziponi kwa kutumia matibabu yake ya msingi na huhitaji dayalisisi au kupatiwa figo ili kuendelea na uhai /maisha
Wasiliana nasi 0625257681.

KISUKARI NI NINI HASWA?Sukari mwilini hutokana na vyakula pamoja na vinywaji tunavyotumia kila siku na hutumika kuupa mw...
15/06/2024

KISUKARI NI NINI HASWA?

Sukari mwilini hutokana na vyakula pamoja na vinywaji tunavyotumia kila siku na hutumika kuupa mwili nguvu. Glukosi ni aina ya sukari ambayo huzipa chembe za mwili nishati. Hata hivyo ili glukosi iingie ndani ya chembe hizo inahitaji insulini. Insulini ni kemikali (Homoni) ambayo hutokezwa na kongosho (Pancrease).

Kisukari ni ugonjwa unaotokana na mtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati.

NI NANI ANAWEZA KUWA NA UGONJWA WA KISUKARI?

Watu walio katika makundi yafuatayo wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kisukari:-

– Wenye uzito uliozidi,

– Wenye historia ya kuwa na wagonjwa wa kisukari katika familia zao,

– Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,

– Watu wasiojishughirisha au wasiofanya mazoezi,

– Wenye shinikizo la damu,

– Wenye msongo wa mawazo na

– Wenye matumizi makubwa ya pombe na sigara.

Watu hawa wanashauriwa kupima sukari yao kila mwaka wakiwa na umri wa miaka 45 na kuendelea.

Kuna hatari kubwa ya kuugua ugonjwa huo ikiwa mtu ana mafuta mengi katika tumbo na kiuno chake kuliko katika mapaja yake. Mafuta katika kongosho na ini huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu.

Wavutaji wa sigara wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi kwani zoea hilo hudhuru moyo na mfumo wa mzunguko wa damu na kubana mishipa ya damu. Kitabu kimoja kinasema kwamba asilimia 95 ya watu wanaougua kisukari ambao hulazimika kukatwa viungo ni wavutaji wa sigara.

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

~ Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.
~ Kwenda haja ndogo mara kwa mara. Watoto kukojoa kitandani.
~ Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.
~ Kupungua uzito au kukonda licha ya kula vizuri.
~ Kusikia njaa kila wakati na kula sana.
~ Wanawake kuwashwa ukeni.
~ Kutoona vizuri.
~ Kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake.
~ Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole.
~ Miguu kuoza na hata kupata gangrini.
~ Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ngazi katika miguu.
~ Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.
~ Majipu mwilini.

Wenye dalili hizi wanashauriwa kupima sukari ili kubaini k**a wana kisukari.
Wasiliana nasi 0625257681.

HAUTAAMINI JINSI TATIZO LAKO LA MOYO AU PRESHA YA KUPANDA LINAVYOWEZA KUMALIZIKA KWA KUFUATA USHAURI HUU________________...
15/06/2024

HAUTAAMINI JINSI TATIZO LAKO LA MOYO AU PRESHA YA KUPANDA LINAVYOWEZA KUMALIZIKA KWA KUFUATA USHAURI HUU
___________________________
0625257681.

Umekuwa Ukisumbuliwa na Aina Mbali mbali ya Matatizo ya Moyo au Presha ya Kupanda...
..Na Mpaka sasa haujua ni Mambo gani au Njia zipi Ufanye Ili Kumaliza Shida Hizo Sii Ndio.!?

Basi naomba unisikilize hapa Kidogo.!

Hauwezi kuondokana na Matatizo hayo k**a bado haujajua Aina ya Matatizo ya Moyo au Presha ya Kupanda Husababishwa na Nini...
..Mambo gani unayopaswa kufanya au usiyopaswa kufanya na ni Aina gani ya Matibabu Sahihi unayopaswa kutumia.

Hivyo hauwezi kuondokana na matatizo hayo kamwe ikiwa bado haujapata Majibu Sahihi ya Maswali hayo.

Lakini Kwa kukusaidia tu ni kwamba ninaweza kukuandalia Darasa Maalumu kwaajili yako...
..Ambalo Litakusaidia kuweza kuondokana kabisa na Matatizo hayo.

K**a upo tayari na Unahitaji msaada huo...
..Basi nitumie ujumbe wako kwa njia ya WhatsApp kupitia namba hii +255625257681.

Jukumu langu ni kukusaidia wewe ili upate kumaliza kabisa aina zote za Matatizo ya Moyo au Presha ya Kupanda.

___________

PRESHA YA KUPANDA USILE VYAKULA HIVIWasiliana nasi 0625257581._______________________________________________Mgonjwa wa ...
15/06/2024

PRESHA YA KUPANDA USILE VYAKULA HIVI
Wasiliana nasi 0625257581.
_______________________________________________
Mgonjwa wa shinikizo la damu la kupanda (hypertension) anapaswa kuzingatia lishe bora ili kudhibiti afya yake. Kuna vyakula na tabia za kula ambazo mgonjwa wa shinikizo la damu anashauriwa kuepuka au kupunguza matumizi yake ikiwa inawezekana. Vyakula hivi ni pamoja na:

1. Chumvi nyingi: Ulaji wa chumvi nyingi unaweza kuongeza shinikizo la damu. Hivyo, ni muhimu kupunguza matumizi ya chumvi na badala yake kutumia viungo mbadala k**a vile viungo vya mimea au viungo visivyo na chumvi.

2. Vyakula vyenye mafuta mengi: Vyakula vyenye mafuta mengi hasa mafuta ya wanyama (trans fats) vinaweza kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo na kusababisha kuongezeka kwa shinikizo la damu.

3. Sukari nyingi: Ulaji wa sukari nyingi, hasa sukari iliyosindikwa, inaweza kusababisha kuongezeka kwa uzito na kuathiri afya ya moyo na mishipa ya damu.

4. Vyakula vyenye viwango vya juu vya cholesterol: Vyakula vyenye cholesterol nyingi k**a nyama nyekundu yenye mafuta mengi, vyakula vilivyosindikwa, na vyakula vyenye mayai mengi vinaweza kusababisha matatizo kwa watu wenye shinikizo la damu.

5. Vyakula vyenye caffeine nyingi: Caffeine inaweza kuwa na athari kwa shinikizo la damu kwa baadhi ya watu. Hivyo, unaweza kuhitaji kupunguza matumizi ya vinywaji vyenye caffeine k**a vile kahawa, chai, na vinywaji vya cola na hata soda hizi.

Kwa hiyo, mgonjwa wa shinikizo la damu anashauriwa kuzingatia lishe yenye afya kwa kula vyakula vyenye afya k**a matunda, mboga mboga, nafaka zisizo kobolewa k**a dona, protini zenye afya k**a samaki, kuku bila ngozi, maharage, na mlo wenye mafuta sahihi k**a vile mafuta ya mimea mfano mafuta ya mawese, n**i, mzeituni, na karanga, pamba n.k lakini nayenyewe yawekwe angalau kijiko kimoja tu kinatosha au k**a anaweza kula chupuchupu ni sawa pia.

✅İLİ KUONDOKANA NA CHANGAMOTO HII YA PRESHA BASI HAKIKISHA UMEFANYA HIVI👇

☎️Piga:0625257681.

🌳 *SHINIKIZO LA DAMU/BLOOD PRESSURE (BP)*0625257681 .  ✨Ni changamoto ya msukumo wa damu kutokuwa sawa katika mwili. 🌿 *...
15/06/2024

🌳 *SHINIKIZO LA DAMU/BLOOD PRESSURE (BP)*
0625257681 .
✨Ni changamoto ya msukumo wa damu kutokuwa sawa katika mwili.

🌿 *SABABU ZA PRESHA* 🌿
👉Ongezeko la sumu mwilini
👉Uwepo wa mafuta ya lehemu (Cholesterol) isiyohitajika kwenye mishipa ya damu
👉DNA genes ambazo mgonjwa anarithi kutoka kwenye ukoo mfano; Baba/mama amewahi ugua Presha.

✨1. ONGEZEKO LA SUMU
Ni moja ya vyanzo ambapo mgonjwa anakumbwa na ongezeko la sumu za vyakula, vinywaji (pombe,soda n.k) na matumizi ya dawa za kemikali kwa muda mrefu. Hizi sumu zote zinazuia msukumo wa damu (blood circulation) damu kutofikia vizuri Katika maeneo tofauti tofauti mwilini.

✨2. LEHEMU (Cholesterol)
Haya ni mafuta yanayopatikana kwa wanyama, mfano wa wanyama wenye kutoa haya mafuta ni nyama nyekundu k**a ng'ombe, mbuzi n.k. Cholesterol/Lehemu huathiri mzunguko wa damu kutokana na tabia ya kuganda na kubana mishipa ya damu, kupelekea damu kuto circulate vizuri na kufikia kwenye mishipa yote (mishipa midogo na mikubwa) hivyo huathiri mzunguko wa damu kutofikia kwenye mishipa midogo na mikubwa.

✨3 DNA/genes
Pia ugonjwa wa Presha ni tatizo la urithi endapo mgonjwa ana historia ya moja kati kana uko k**a Baba/mama kuugua tatizo hili, hivyo anapata izo genes tangu anazaliwa.

☘️ *ATHARI ZA PRESHA* ☘️
TATIZO LA PRESHA huathiri maeneo tofauti tofauti na kuleta complications/confusion mbalimbali kwa mgonjwa wa Presha. Mfano

👉KUSIKIA KELELE MASIKIONI; baadhi ya wahanga wa presha hupata tatizo la kusikia sauti mbalimbali masikio ambapo kadri linajitokeza linaweza kumsababishia kutosikia akifikia uzeeni

👉MAUMIVU YA VIUNGO; mgonjwa wa presha anaweza akapata changamoto ya maumivu ya mifupa k**a vile miguu kuwaka moto, maumivu ya mgongo, kiuno na kuhisi uchovu mara kwa mara.

👉MAUMIVU YA KICHWA/KIZUNGUZUNGU; mgonjwa wa presha ni rahisi kupata maumivu ya kichwa na hata kizunguzungu mara kwa mara, kupoteza uwezo wa kuona na mwili kufa ganzi.

Hivyo presha hupelekea complications tofauti tofauti kwa mgonjwa husika.
Hii ni kutokana na presha inaweza pelekea tatizo lingine kutokea, endapo mgonjwa akipatiwa tiba sahihi ya kuondoa presha hizi complications zinatoweka, msingi wa kuondoa izo complications ni kudhibiti presha ya mgonjwa.

Kwa ushauri na tiba za maradhi mbalimbali wasiliana nasi
What's app/call
+255 625257681.

Address

Buguruni Rozana
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when IJUE AFYA YAKO posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to IJUE AFYA YAKO:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram